Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Acha kudanganya watu mchana kweupe ndugu!

Lugha ya kiswahili ni moja tu,

Kamusi ya kiswahili ni moja tu,

Hapa tunatumia kiswahili sio Kizaramo au kimakua,

Acha kuharibu lugha yetu adhimu ya kiswahili!

Katika kamusi stahiki ya kiswahili hakuna neno "Ilmu" au "Darsa"

Elimu itatajwa kuwa ni Elimu hivyohivyo na Darasa litatajwa kuwa ni Darasa hivyohivyo!!
 

Wickama,

Woow!...Mr Wickama seems very hurt and angry,a lot of Paranoid going on over there!
How unfortunate...
 
Mohamed Said,

Logical ya historia ya UHURU wa Nchini huwa ni mitaa waliyoishi wapigania uhuru ama huwa ni WAPIGANIA uhuru hao?

Mitaa kwa historia ya nchi sio chaguo la kwanza, yaweza kuwa hitimisho tu au kunogesha/kuremba/kupamba NGANO lakini sio HISTORI ya NCHI

Mzee wewe wenzio wanakuita ni bingwa wa historia, lakini unawaangusha kwa hilo, Au hiyo ndio historia?
 

Napata raha sana kupata vitu adimu kama hivi, shukrani kwako gwiji la historia ya tanganyika/tanzania
 

Ahsantum Mohamed Said,

Hizo bayana zako zinathibitisha kuwa Wazee wa Mzizima ndiyo walikuwa waanzilishi wa harakati zote za uhuru hilo hata Nyerere mwenyewe amekiri.

Hebu ngoja nijaribu kiduchu kukumbuka mitaa ambayo Wazee walikuwa wanaendesha harakati zao.

Msimbazi, Congo, Narung'ombe, Raha, Nyati, Lumumba, Kipata, Lindi, Agrrey, Mchikichi, Maiwa, Muhonda, Magila, Tandamti, Chura, Muheza, Pemba, Livingstone, Manyema, Mafia, Swahili, Nyamwezi, Kariakoo, Uhuru, Likoma, Udowe, Mkunguni...ha ha haa kote huku kwa wazee wa madrassa.

Namalizia kwa haya maneno kutoka kwa Henry Ward Beecher 1813-1887 "Walo hatari kuliko wote ni wale wajinga"
 
Last edited by a moderator:
Kijana uko desperate sana. Nani kakudanganya kuwa mipaka ya somo la historia ni kujadili watu tu? Wapi unayaokota haya? Kijana una safari ndefu ya kujifunza na kwa mwendo huu ni wazi safari yako hata kuanza haijaanza.
 
Barubaru,
Kila ninapopita humu jamvini ndivyo ninavyozidi kumshukuru Allah.

Maryland Washington...
Nimekaa hapo.

Alhamdulilah.

Thanks na mimi nimetua hapa toka Ijumaa mosi na panapo majaaliwa naondoka Kesho kurudi Muscat, Oman.

Hapa wapo watoto zangu wanaosoma University.
 
Boko haram, mbona unarudia matusi yaliyokusababishia ban muda si mrefu! kwanini unaamini kuwa sisi tupo kama kasuku? Tumeshakuonesha udhaifu wa maandishi ya huyo nabii wako Mohamed Said yeye anayaita Historia! tumeshakuonesha uongo wa dhahiri aliouandika Mohamedi hii ni pamoja na uwongo wa hivi karibuni kwamba balozi wa Marekani alihutubia bunge la Tanzania! tumekuonesha kwamba Mohamed ameandika uchochezi na chuki na wala sio historia. Jukumu lako hapa ilikuwa sio kumushutumu Mag3 kwa kututaja sisi wala sio wewe kututukana sisi kuwa ni kasuku. Ulitakiwa ulete hoja kututhibitishia sisi kwamba kilichoandikwa na mchochezi Mohamed Said sio HISTOHISIA!! huwezi kutushinda kwa kututukana, utashinda kwa hoja ambazo naamini huna.
 

Samahani kama umeona ni matusi sisi watoto wa madrasa huwa tunanena kwa mifano kwahiyo kusema neno kasuku kwangu nimeona ni la kawaida na kama ni tusi basi tuanze na kitabu chetu QURAN KWA MFANO HUU HAPA;QURAN 62;5 The example of those who were entrusted with the Torah and then did not take it on is like that of a donkey who carries volumes [of books]. Wretched is the example of the people who deny the signs of Allah . And Allah does not guide the wrongdoing people.
 
Yericko,
Hapana ugomvi vile uonavyo wewe hakuna wa kukuzuia.

Hapa jamvini tunakimbilia sasa watazamaji 200,000 na
hawa ndiyo wanaonishughulisha mie.

Jumatano ilopita nimefanya kipindi live Radio Kheri kuhusu
Maisha ya Ally Sykes.

Ijumaa nimealikwa Radio Al Nur Zanzibar nikafanye kipindi
cha Maisha ya Ally Sykes na nimekifanya nacho kilikuwa live.

Watu wanapenda kusikia historia hii hakuna haja ya kutoleana
ufedhuli kwa jambo linalopendeza.
 

Kwangu hilo halina uzito mkuu,

Lakini nikujuze kuwa hivyo vyombo vya habari vyote unavyodai kuhadhiri pamoja navyo havina tofauti na WEWE kimlengo!

Ni sawa na mimi ningeibuka na kukutangazia wewe kuwa nimehadhiri Tv Tumaini au Redio Tumaini,

Bila shaka ungepaza sana sauti kudhihaki!

Mimi nakuambia kuwa kundi lako lote la Radical Muslims msomi ni wewe tu japo hujapevuka na hutapevuka!

Akina Ilunga,Ponda,Basale na wengine wote wanakutegemea wewe!

Wewe umekuwa mratibu wa vipindi na mwanamikakati wa mda mrefu wa redio ya kichochezi iliyofungwa pale Morogoro (redio heri).

Unadhani vituo vingine vyenye misimamo ya kichochezi kama yako hawatakualika?
 

Gwalihenzi,
Nabii wa Mwisho kwa mujibu wa Uislamu ni Nabii Muhammad(SAW) sasa kumnasibisha Mohamed Said na unabii ni kuidhihaki dini ya Kiislamu! naomba tujadiliane kuhusu uchochezi wa MS na dhihaka kwa wapigania uhuru kama alivyosema Yericko Nyerere tuache kashfa za kidini!
 
Hivi ni nani kakuambia kila anayeshiriki mnakasha huu ni muumini wa QURANI?
 
Mbona humkemei ndugu yako Boko haram aliyetuita Kasuku sisi tusiekubaliana na huyo mzee wenu Mohamed? na kwanini unataka kunihusisha na imani yako? Kama wewe unaamini nguruwe ni haramu kwangu mimi ni kitoweo safi kabisa!
 
Mbona humkemei ndugu yako Boko haram aliyetuita Kasuku sisi tusiekubaliana na huyo mzee wenu Mohamed? na kwanini unataka kunihusisha na imani yako? Kama wewe unaamini nguruwe ni haramu kwangu mimi ni kitoweo safi kabisa!

Sijakuhusisha na Imani yangu! kila mtu ana Dini yake! lakini usimhusishe MS na unabii hilo tu! yeye sio nabii! nakama BH kakuita Kasuku ni vipi tena MS anaingia ktk Unabii?
 
Sijakuhusisha na Imani yangu! kila mtu ana Dini yake! lakini usimhusishe MS na unabii hilo tu! yeye sio nabii! nakama BH kakuita Kasuku ni vipi tena MS anaingia ktk Unabii?
Tabu yako unatoka mapovu bila kutumia busara, rudi kasome huyo jama yako Boko haram aliandika nini kunihusu mimi. Mohamed Said mwenyewe anasoma maoni yangu, ndie ajibu kama anasitahili au hastahili heshima hiyo. Mbona mnaitana mawalii n.k. hapa JF, nani kawakataza?
 

Yericko,
Iko siku watu watataka uandike maisha ya baba yako.

Hudhani haya ninayokueleza hayatakusaidia kujenga haiba na hali ilivyokuwa wakati mzee
anafika Dar es Salaam na kujiunga na TAA?

Hebu pitia tena yale niliyoandika:

Tuanze na Kipata.

Kipata na Msimbazi nyumba ya kwanza ilikuwa ya Abdallah Matimbwa.
Huyu ni mmoja wa wanachama wa mwanzo TANU.

Abdallah Matimbwa
ni mmoja wa waliochangia ujenzi wa kujenga Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam.

Baada ya uhuru alitoa gari yake kuanzisha ushirika wa CORETCO.

Bado tupo Kipata.
Kipata na Congo.

Nyumba ya kona kwa Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association
1929.

Kipata na Nyamwezi.
Nyumba ya Mama Nambaya na mama yake Shabaka.

Nyumba ya mbele no. 32.
Hapa ndipo alipozaliwa Mohamed Said.

Kipata na Sikukukuu nyumba ya Mohamed Clement Mtamila katibu wa TAA wakati
wa Vita Vya Pili ni katika nyumba hii Nyerere aliwasilisha barua kutoka kwa Father
Walsh
akishauriwa asomeshe au aache siasa.

Halmashauri Kuu ya TANU Mzee Mtamila akiwa mwenyekiti mmoja wa wajumbe
akiwa Bi Tatu Biti Mzee walikutana ndani ya nyumba hii na uamuzi ukapita Nyerere
ajiuzulu aje Dar es Salaam atakaa kwa Abdu Sykes hadi TANU itakapomtafutia nyumba.

Kipata huku Livingstone huko New Street.
Nyumbani kwa Kleist Sykes na wanae.

Hapa ndipo ulipokuwa umefichwa mtambo wa kuchapa makaratasi ya "uchochezi" na
mchapaji alikuwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab.

Hapa yapo mengi na Nyerere alikuwa hapungui nyumba hii.
Mkabala na nyumba hii akiishi babu yangu.

Mkunguni na New Street.
Hapo unamkuta Hawa Biti Maftah unaijua nyimbo "Hongera Mwanangu?"

Huyo mwana anaepongezwa ni baba yako Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa akiimbisha
nyimbo hii mikutanoni ni Bi Hawa Biti Maftah.

Hapo hapo mbele ni nyumba ya Idd Tosiri.
Tosiri ndiye aliyempeleka Nyerere Bagamoyo kwenda kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramia.

Yericko,
Usitudharau wala kujaribu kuwadhalilisha wazee wetu.
Hawa wameacha alama katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Unataka kuidhalilisha mitaa hii alokuwa akikanyaga Baba wa Taifa mitaa ambayo akiitembea
na wazee wetu?

Unataka kuifanya kichekesho Mtaa wa Kipata na Mkunguni ilhali mitaa hii ndiyo iliyomfikisha
Nyerere juu kileleni?

Jitulize na fikiri kabla hujaandika.
Ujuvi haukufai kijana.

Una miaka mingi ya kuishi Allah akipenda.

Yericko,

Katika haya yote huna la kudadisi wala kutaka kujua historia hii?
Historia hii ndiyo inawavuta watu hapa jamvini hawapungui...

Mimi ninapata mialiko kote kwa ajili ya historia hii wewe unasema kuwa wenye kunialika ni mfano
wa mie...

Je, nao Northwestern University, Marekani ni kama mimi?
Vipi Chuo Kikuu cha Johannesburg, Kenyatta wote hawa ni mfano wangu?

Nimefanya mahojiano ya zaidi ya saa moja mara mbili na Al Jazeera hawa nao ni mfano wa mie?
Vipi vipindi kadha nilivyopata kufanya na VOA, DW, BBC...

Nao ni kama mimi?
Narejea tena jitulize na fikiri kabla ya kuandika.

Kumbuka hapa tunasomwa sasa na watu wanakimbilia 200,000.
Naambiwa na wenyeji wa JF kuwa hii haijapata kutokea.
 
Yericko Nyerere,

Wakati mwingine ukikaa kimya ni bora zaidi kuliko kuropoka.

Lakini nikujuze kuwa hivyo vyombo vya habari vyote unavyodai kuhadhiri pamoja navyo havina tofauti na WEWE kimlengo!
Wanajamvi haya magazeti hapa chini nayo yanaandika habari za Mohamed Said, nayo yana mlengo kama wake Mwananchi ndiyo gazeti linalo ongoza kwa kutoa nakala nyingi.
 
Yericko Nyerere,

Wakati mwingine ukikaa kimya ni bora zaidi kuliko kuropoka.


Wanajamvi haya magazeti hapa chini nayo yanaandika habari za Mohamed Said, nayo yana mlengo kama wake.

Shariff Ritz,
Ahsante sana.

Nakuongezea na magazeti mengine - The East African (Nairobi), New African (London), Africa Analysis (London), Daily News (Dar es Salaam), Rai (Dar es Salaam), Raia Mwema (Dar es Salaam)...

Nimeandika vitabu vitatu na Oxford University Press (Nairobi), Abantu Publications (Nairobi na Dar es Salaam), Phoenix Publishers (Nairobi), Minerva Press (London)...

Nimepewa reviews mbili kwenye Cambridge Journal of African History, na nyingine Marekani na Ulaya.
Nimezungumza Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

Ndiyo humwambia mdogo wangu Yericko, kabla hajaandika afikiri kwanza.
Haya yote tungeyaepuka.

Ahsante tena Shariff.
 
Mag3,
Umeandika maneno mingi sana lakini mimi tadadavua kiduchu hizo bayana zako.
Hapa CCM ni mmoja tu chama, hao wengine wote ni wafuasi wa Chadema halafu ni Wakirsto, isipokuwa Mkandara, tu kwenye hii orodha yako Waislam ni wawili tu chama, na Mkandara, hawa wawili toka mwezi wa kwanza ameachana na huu mnakasha baada ya kuona kumbe ni vita vya kidini kati ya Waislam na Wakirsto.
Kwanza tambua Uislam na Uarabu ni vitu viwili tofauti hapa hakuna mtu anayetetea ushenzi wa waarabu, hebu Wanajamvi tusome hapo chini kuhusu habari za utumwa Mag3, anatuambia utumwa wa mwanzo ulikuwa karne ya tisa.
Nadhani wanajamvi mmejionea wenyewe habari za utumwa, ngoja kiduchu tuendelee kudadavua bayana za kaka yetu.
  1. Naona hapa unatuaminisha kuwa Waislam wapo CCM halafu nyie Wakirsto mpo Chadema.
  2. Mfumo Kristo umeanza baada ya uhuru wa Tanganyika soma hapa chini kazi ya Nyerere.
  3. @Mag3, kila siku mnawatukana Waislam lakini hao hao wanawasaidia katika chama chenu, hebu angalia hapa Mzee Sabodo anayowapa hundi kwa dharau anatia sahihi kwa mkono wa kushoto lakini kutokana na njaa yenu amna jinsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…