Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mohamed, unapomuasa Yericko ajitulize na kufikiri kabla ya kuandika ningependa uiangalie kauli hiyo na kuona kama si muhimu sana kwako.Yericko,
Hudhani haya ninayokueleza hayatakusaidia kujenga haiba na hali ilivyokuwa wakati mzee
anafika Dar es Salaam na kujiunga na TAA?
Kipata na Nyamwezi.
Nyumba ya Mama Nambaya na mama yake Shabaka.
Usitudharau wala kujaribu kuwadhalilisha wazee wetu.
Hawa wameacha alama katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Unataka kuidhalilisha mitaa hii alokuwa akikanyaga Baba wa Taifa mitaa ambayo akiitembea
na wazee wetu?
Unataka kuifanya kichekesho Mtaa wa Kipata na Mkunguni ilhali mitaa hii ndiyo iliyomfikisha
Nyerere juu kileleni?
Jitulize na fikiri kabla hujaandika.
Historia hii ndiyo inawavuta watu hapa jamvini hawapungui...
Je, nao Northwestern University, Marekani ni kama mimi?
Vipi Chuo Kikuu cha Johannesburg, Kenyatta wote hawa ni mfano wangu?
Kumbuka hapa tunasomwa sasa na watu wanakimbilia 200,000.
Naambiwa na wenyeji wa JF kuwa hii haijapata kutokea
Mohamed, si kweli kuwa Nyerere alijiunga na TAA alipokuja Dar es Salaam. Tumekuonyesha kuwa alikuwa katibu wa Tawi Tabora. Unless useme TAA ilikuwa New street peke yake, kauli yako inaunga mkono hoja yangu ya usahaulifu''amnesia''.
Pili, mitaa ya kipata, mkunguni n.k haikumfikisha Nyerere kileleni! Tanganyika ni zaidi ya Narung'ombe na kirk street.
Unaposema hayo unadhalilisha wazee wetu wengine waliopigania uhuru wa nchi hii eti kwasababu hawakuwa karibu na Kipata, mkunguni au Jang'ombe.
Tatu, Nimeshangaa uliposema Nyerere ni baba wa taifa! nadhani umelenga kumsema kwa njia isiyo sahihi.
Wewe ndiye muasisi wa neno baba wa kanisa, leo unasema baba wa taifa! real.
Nne, unapokataa wazee wasidhalilishwe basi anza na kauli hiyo kwako, usiwadhalilishe wazee!
Hili la Nyerere kuishi kwa Sykes umelisema ukilenga kumdhalilisha. Haina taabu lakini usije amsha jazba pale mwingine atakapousema ukweli unaodhalilisha.Hivi siyo wewe ulichukia Amir kuitwa mnafiki hata kama ilikuwa ni hivyo?
Tano, hawa 200,000 si kuwa wanasoma historia yako, wapo wanaotoa machozi baada ya kugundua kuwa walichokisoma, kukiamini na hata kukihadithia sicho, ndiyo maana kwa umaarufu simulizi linaitwa ngano mubashara.
Sita,Katika orodha umesahau chuo kikuu cha Ibadan
cc al-khyi wote,Talib, Swahib, shariff, Mag3, JokaKuu, Jasusi,Mkuu wa chuo, Wickama, Prishaz,wanajamvi