Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #16,061
Yericko; Shukran
Naona tunarudi main stream kwenye mada. Nipo kwenye hawa wanaoitwa Wamakonde wa Kipumbwi walioipindua serikali ya sultan zenj kwa msaada wa Julius Nyerere. Hofu yangu ni kuwa likiachwa kama lilivyo, mabwana hawa (Wamakonde)wataonekana kama wahuni tuu waliovamia nchi ya watu na kuiondoa serikali yao madarakani kumbe wao walikuwa askari tuu. Hii haitakuwa haki ukizingatia mchango wao katika kuleta historia mpya Zenj. Kwa kiwango cha chini kabisa inatakiwa kutowaonyesha aina yoyote ya dharau kutokana na nasaba zao.
Sasa, kwa vile sio kila "Makonde aliyeshiriki Kipumbwi" ataandika "kitabu" cha kuinasua nafsi yake na tuhuma au dharau zinazolundikwa juu yao, na ikizingatiwa kuwa wamiliki wa mapinduzi haya kikubwa ni ASP (hawajawahi kukana mapinduzi haya na bado wanayaenzi) na inaelekea Nyerere alijitolea kuwapa msaada wa kujikwamua na dhiki yao (yeye na Karume walijua kwa nini wasaidiane kwenye hili) hapa nina maswali yatakayohitaji majibu;
(i) Hivi, ASP waliomba au walilazimishwa msaada na Julius Nyerere kuhusu mapinduzi haya? Hii ni muhimu kujua nani mwenye dhamana nayo.
(ii)Nani aliyejenga sababu za mapinduzi haya huko Zenj na kwanini? Iwekwe wazi pia na ushahidi tunauomba
(iii)SMZ wanawachukulia vipi washiriki/askari waliweka maisha yao hatarini kwenye mapinduzi haya?
(iv) Kuna yeyote anayesema haikuwa halali wao ASP kupinduwa ile serikali ya sultan? atoe msimamo wake na sababu ili utafutwe msaada hata wa SMZ tujibiwe
(v)jee nasaba ya askari aliyeshiriki kupinduwa ina umuhimu? (km, askari wangekuwa ni wagunya/wacomoro ingeleta ahueni?)
Hii naiona ni muhimu kwa vile moja kati ya dondoo zako za tuhuma umeeleza kuwa Mzee MS hayuko bayana juu ya Mapindizi haya
cc Mohammed Said
Mkuu umenena,
Tunahitaji kuyachambua haya na kuyaeleza bayana kisha tupate maadhimio ya pamoja!