1968 serikali inashutumiwa kushiriki katika uanzishwaji wa BAKWATA na hivyo chombo hicho pamoja na kuongozwa na Waislaam, wachochezi wanadai si cha Waislaam lakini
2013 serikali ikiwateua Makadhi wa mahakama ya Kadhi Visiwani, wachochezi wale wale kimyaa! I am just thinking out loud...hivi ingekuwaje kama Raisi wa Tanzania wakati huo angekuwa Muislaam, je wachochezi wangelalamika! Mwaka 1961 namuona shujaa wa harakati za uhuru Abdulwahid Sykes anaapishwa kuwa Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru, wazee wa Gerezani mpo? Oops! nilikuwa naota tu...kumbe huu ni mwaka wa hamsini toka tupate uhuru! Mbona uchochezi uko pale pale hali watoto waliorithi chuki na fitina za wazee wao sasa wamekua. Kwamba sasa uongozi wameukamata si hoja, malamishi bado yako pale pale, ni bahati ilioje Mwalimu hayupo! Kwa kweli tatizo nadhani si dini, dini inatumiwa tu kama kibwagizo...tatizo ni watu wenye donge rohoni wakiteka hisia za wale wenye uelewa finyu. Yaani mwananchi na matatizo yote, unakubali kutumiwa na mtu anayefisadi matunda ya ngano zake, wewe huyoo ukikesha kwa mihogo ya kuchemsha! Kweli duniani ujanja kupata...hujafa hujaumbika! Naambiwa hata hilo Baraza la Mapinduzi si halali kwani lilitokana na mapinduzi haramu. Kwamba
Mohamed Said anapofika Unguja asiye na mwana hueleka jiwe! Watu hujazana na kupigana vikumbo kuwahi maudhui ya kuwalaani walompindua Sultani tarehe 12 Januari 1964.