Mohamed Said;6553341]Wild Card,Nasema mmeshtushwa kwa sababu mnavyohangaika humu kujaribu
kuibomoa historia hiyo.... Hivi nyie hamjiulizi kwa nini mimi sijapinga historia yenu wala sikuulizeni
mswali, wala situkani au kutumia lugha chafu na kali.
Mohamed Said;6559104]
Uthman, Ndipo nilipoamua kuandika historia hii iwe jibu kwa historia ya Chuo Cha
Kivukoni.
Nicholas, usije sema nimevamia Jugular!
Mohamed, hakuna mwenye historia ya TANU, historia ni mali ya nchi na wananchi.
Hakuna aliyesema kuwa ile ya kivukoni ilikuwa kamili.
Watu wapo hapa kuhakikisha kuwa kizazi kijacho hakiingii katika mtafaruku na tafran zingine.
Ulichokifanya wewe ni sawa na mfano wa mtu atukanaye kwa kusema ''mshenzi'' halafu mwingine amjibu kwa lile tusi la mama!
Unachikifanya wewe pengine ni kibaya kuliko historia ya kivukoni. Ile kama ilikuwa na mapungufu si kama yako.
Abdul Sykes(Mohamed Said) alisema yeye na wenzake wanafanya jitihada za kumkomboa Mwafrika.
Hakusema kundi la watu fulani. Wewe unasema ''ninyi'' na ''sisi'' kuwatenga Waafrika wa Tanzania kinyume na Abdul, halafu unatuambia kuwa unamsemea Abdul
Kwa wale wanaouliza uchochezi, basi ndio huo maana hakuna mahali Abdul na wazee wenzake waliwahi kusema ''sisi'' na ''ninyi'' haya kayaleta Mohamed. Hakuna mahali Abdu na wenzake walisema sisi wazulu, sisi wamanyema au sisi wanuvi, hayo kayaleta Mohamed. Hata pale alipoamua kumwagia hamira bado aliumbuka, ''sisi wamanyema ni waislam watupu''
Walipomchangia Nyerere kwenda UNO hawakusema ''sisi au ninyi'' na hata akina Maryknol walimchangia Nyerere kwa kusema Tanganyika si kwa wewe au sisi au ninyi.
Hatari kubwa zaidi ni ile ya kuchomeka chembe za dini. Hadi leo hakuna mahali ulipoonyesha kuwa wazee wako walifanya hivyo kuwakomboa watu wa imani fulani. Endapo ingelikuwa hivyo basi wasingekubali Nyerere awaongoze.
Tena kuna ushahidi kuwa wazee wetu walikataa udini kwa kukataa AMNUT, sijui udini unaotoa wapi maana ukisoma historia yako mwenyewe inaonyesha jinsi wazee walivyoongozwa kupinga dhulma tena wakisema kwa Mwafrika.
Historia yako ndiyo imeingiza udini na hakuna shaka wewe ni masalia ya AMNUT!
Umeandika paper ikiwa ni mwendelezo ili kuonyesha kuwa waliopigania uhuru wameachwa.
Huku ukichagua kwa makabila na dini umeacha wazee wetu wa sehemu nyingine kwa kosa lile lile unalolilaumu.
Kitabu chako kinatumika huko wasikoijua Tanganyika, hapa Tanganyika hakitaingia katika mtaala hata siku moja.
Na bahati njema nyuzi hii imefichua kila kilichojificha na hakika ukisimama mbele ya kadamnasi ya werevu unaweza bububujikwa na maji ya puani. Leo kila mmoja anajua kuwa yapo usiyoyasema kwasababu za hila na si historia.
Toleo linalofuata sina uhakika kama utauza tena maana credibility ya maandishi yako imefinyangwa sana.
Unaposhauri watu wasome wasiulize unatupa ujumbe kuwa wewe unakosa element za scholar.
Scholar hupenda kutoa ufafanuzi na wala si kuorodhesha majina.
Hakika kama utaandika kuhusu wazee wako, vinyozi n.k. si haki kukuhoji, lakini ukishatumbukiza Tanganyika tutaingia kwa nguvu kunusuru sehemu ya jamii iliyobaki na inayokuja kuingia katika mtego huu mbovu, dhalili na usio na tija achilia mbali maana.
Leo unakwenda toleo la nne, unachosema ni kuwa usipingwe kwasababu hujapinga, tunashukuru hatusikii tena neno historia ya kweli. Mnakasha unasaidia kila mmoja ati