Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

The Big Show,
Sasa tufanye nini na kitabu nishaandika na kinasomwa?

Sheikh Mohammed,

Hata mimi nimestaajabu,maana naona kuna Mwanajamvi hapa anadai ati hii shughuli tayari ilishakwisha/ishakwisha!?

Baadhi yetu tuliyasema/tulishauri haya kitambo,tukaonekana "tunataka kukimbia" mnakasha.

Sasa inalazim labda wewe binafsi ushauriane na Yericko ili tujue khatma ya haya majambo.

Sisi huo "ugaidi,uchochezi na uhaini" bado asilan hatujauona!

Na kama wao wameuona sasa nini kifuatiacho!?...au siku hizi huko Tanganyika "wahaini,wachochezi na magaidi" huwa wanaletwa hapo Jf,khalafu wanafanziwa tashtit,kebehi na kuachiwa huru!?

Huu ni utoto mtupu.

Kama una "mipini" mingine tafadhali tumwagie hapa Al Akhiy...kelele za mpangaji/mlango hazimfanzi mwenye nyumba akose singizi nono!

Ahsanta.

C;Ritz
 
Hapa Yericko akifuatilia hotuba za Nyerere TBC ha ha haa... watu wanahojiwa VOA wewe TBC inakushinda
149331_552916038053633_107565525_n.jpg

Boko Haram,

Salaam Al Akhiy.

Najua wewe ni Multi-lingual... mbali na kile ki-Kongo chako,niliipenda pia ile methali yako ya ndugu zangu wa Kipare..."umgura afande udhuti" nafikiri!?ahaha!!

Hivi ni kweli huyu kwenye hii picha ndo huyo jamaa Yericko!?....ahahaa!! Kama ni kweli yaani huyu mtoto anataka kuchapwa viboko vingi saana,khalafu atafute kitanda akalale,sio kutuletea ile "pasua kichwa" hapa jamvini!

Ahsanta.
 
Sasa hivi ndugu zetu wanaomba maridhiano feki!

Hakuna asilan abadan anaeomba suluhu hapa...unachoshindwa kufahamu wewe ni kuwa kama umeshabitisha/mmeshathibitisha hayo madai na shutuma zenu za kitoto za "ugaidi,uchochezi na uhaini",ni kipi mnachotaka kufanza sasa!?

Au huyu "mtuhumiwa wenu" kwa sasa mnamwachia huru!?ahaha!! Si itakua bado zile nguvu na vurugu zoote tulizofanziana hapa jamvini zimekwenda bure,na pia hamtakua mmewatendea haki hao waliokutumeni!?ahaha!!
 
Kwakuwa tayari amekiri kiutu uzima, tunamtaka mtuhumiwa huyu ahuishe kitabu chake kama kweli anataka kiwe cha historia badala yakilivyo sasa ni cha tungo!

Hii itasaidia kuokoa kizazi kinachoendelea kupotoshwa kwa maandishi yake!

Kukiri huko, nyinyi wafia malimbuko hamtakuona, hivyo hamtaamini kuwa kiongozi wenu amekiri kupotosha jamii na kuchochea maasi ya kiroho!
 
Nilifahamu tu hapa wazee mnapiga nyago konzi tu maana hoja za kujisifia kuandika kitabu cha mradi wa USAID ilikuwa ni tosha kufahamu kuwa mna-deal na mtoto mdogo mwenye safari ndefu ya kujifunza.

Aisee unamatatizo kweli mkuu,

Kichwani unamawazo tofauti kabisa na unachokiandika!

Haya wanajamvi wanakusoma vizuri!
 
Wanajamvi,
Kinachonishangaza ni kuwa hata pale ninapowaambia kuwa
hiyo historia yenu nayo ni historia na mna haki ya kuiamini
bado hawaridhiki wanataka hii yetu ifutwe na ndiyo hivi sasa
bado tunavutana.

JAMANI NA HIYO YENU NI HISTORIA MNA HAKI YA KUIAMINI.
MSISHIKILIE KUWA SIE TUFUTE YETU ILI YENU IPATE NGUVU
YA KUSIMAMA.

HII SI HAKI WALA UADILIFU.
Mohamed, nyie ni akina nani? Na sisi ni akina nani?
Nakuhakikishia kuwa yapo maelfu ya 'sisi'' wanakereka sana na hiyo historia.
Nani amekupa mamlaka ya kusema hiyo ni historia ya ''sisi''
Hayo ni mambo yako uliyoandika na wala hukushirikisha mtu.

Unapokwenda kwenye mihadahra huwakilishi kundi. Wewe hukutumwa kuandika historia na 'sisi''.
Unapofanya hivyo unawadhalilisha wale unaosema ni ''sisi'' kwasababu hata uongo unanasibishwa nao.

Hii ni hitsoria yako na Wamenyama, wazulu na na wanubi if you like, si historia ya kitu kingine.
Mohamed narudi tena kuna maelfu ya watu wanajisikia dhalili, wanakereka sana hivyo sema hiki ni kitabu cha utunzi wa historia yako si ya wewe na kundi lolote.

Hivi kuna''sisi'' ambaye angependa anasabishwe na dhalili kama ya Ibadan.
Tafadhali huu ni utunzi wako wewe na familia yako!wazulu, wanubi na wamanyema

Hizi ni chuki zako usizifanye chuku za taifa. Kama babu yako alikuwa bandari ukadhani unapaswa kuwa mkuu wa bandari na haikutokea hivyo, hizo ni personal failure.

Kama karume alilala mtaani kwenu ukadhani mtaa huo utakuwa sehemu ya Pemba hizo ni personal wish siyo za jamii.
Please, personal grudge, frustrations n.k. hazina uhusiano na jamii na ni vema ukazi handle nyumbani kwako si kuishirikisha jamii.

Huu ni ubunifu wako katika utunzi, kama kuna kundi basi unalijua wewe hapo nyumbani not in national stage!
 
Shariff Ritz,

Wallahi,nimecheka kuona bayana za huyu jamaa yako wa Ngaramtoni!ahaha!!

Unajua kwasasa nimepata picha khalis.

Nimecheka hiyo story yake ya huyo Komba!ahah!!

Lakini in a serious note,huyu jamaa ni disaffected/disgruntled majority ambayo ni reflection of cross section in our society.

Si unaona khadith zake anasema alipokua Shule,yakuwa alikua akibaguliwa kutokana na social status yake mbovu maskini,na ilikua taabu kwake hata kupata Gfs wa maana... Poor Nicholas!

Sasa kuna khatar ya watu wa aina hii ku-commit suicide maskini pale Chadema watakaposhindwa kuingia madarakani hiyo 2015 kama wanavyotaraji!?ahaha!!

Tuendelee na mnakasha.

Ahsanta.

Al Habiby gombesugu,

Waalahi ndugu yangu mimi kichwa changu kikiwa na madhila napenda kumsoma huyu jamaa huwa nacheka sana.

Huyu jamaa lazima atakuwa na matatizo katika mfumo mzima wa ubongo, mawasiliano baina ya moyo na ubongo.

Kuna kitu kinaitwa (Neurologically) kimekufa kwa kutumia homoni (Biochemicall) kinachotumia mawimbi ya mgandamizo wa hewa nacho kimekufa, halafu hata (Biophysically) nayo ina matatizo, halafu njia ya uvutano wa kisumaku (Energetically) nayo imekufa, ha ha haa, taendelea kuleta vichekesho vyake.

Wakati mwingine nikumsamehe tu tatizo lake anayeweza kulitatua ni Dr J. Andrew Armour.
 
Kwakuwa tayari amekiri kiutu uzima, tunamtaka mtuhumiwa huyu ahuishe kitabu chake kama kweli anataka kiwe cha historia badala yakilivyo sasa ni cha tungo!

Hii itasaidia kuokoa kizazi kinachoendelea kupotoshwa kwa maandishi yake!

Kukiri huko, nyinyi wafia malimbuko hamtakuona, hivyo hamtaamini kuwa kiongozi wenu amekiri kupotosha jamii na kuchochea maasi ya kiroho!

Creative and funny! I do hope Wanajamvi are able to see the humour....

Don't let your idiocy insult your intelligence!
 
Wickama,

Mbona hujiamini ndugu yangu,huna haja ya kujibu post mara mbili. Lile jibu lako la awali japo ni duchu lakini nilikufahamu uzuri tu.

Hizo stories zoote unazoniambia,mimi tayari nilishazungumzia kwenye wiki yangu ya mwanzo tu tangia najiunga hapa Jf...nilikhis vingi mapema mno!

Hizo khabar za Wanajamvi waliokua wana-quote Ayat...kumbuka wewe binafsi na Mwanakijiji ni wamojawapo. Sasa unaposema "wanagwaya" nashindwa kukufahamu,nawe pia yatakiwa uwemo kwenye mkumbo huo!?

Nafikiri tuachie kwa hapa.

Ahsanta sana.

Ndugu yangu Al Habiby gombesugu,

Bahati nzuri Uislam huwa unatabia ya kujisimamia wenyewe, Uislam ndiyo dini yenye nguvu yenye ubavu wa kusimama dhidi ya mawimbi ya upagani na ukiburi wa kutomwamini Mungu na tabia za kejeli na dhihaka Wislam haupendi mtu dhahifu, Uislam umeanza kutukanwa na kukejeliwa toka karne 7 lakini bado unakata mbunga hakuna wa kuushinda Uislam.

Uislam unawavutia wasomi wengi kati ya wahitimu wa vyuo hasa hasa wale waliochoshwa na hoja zisizo na mantiki. Nadhani umenipata ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:
Kizazi cha leo kimebadilika ndugu yangu, itabu havisomwvi kama unavyofikiria!

Mitandao ya kijamii ndio uwanja sawia kwa kizazi cha leo kusoma na kupata habari mpya!

Huoni mfano hapahapa jf kuwa Watanzania wengi kwa zaidi ya miaka 15 sasa walikuwa hawakijui kitabu cha Mohamed Said wala kitabu cha TANU, lakini kupitia ulimwengu wa dotikomu leo wanasomeshwa watu zaidi ya 200000 ndani ya miezi sita tu!

Hivyo sioni umuhimu wa kitabu kwa leo hii, lakini nimechukua fursa ya kulala jf, kukesha jf, kushinda jf ili kuwazidua walipotea kama wewe!

Juu ya kumuona Mama yetu mpendwa Mama Maria Nyerere kwalengo lakupata "ushahidi" wa ayasemayo Mohamed Said, sioni sababu,

Kwakuwa haya niliyonayo yanatosha kumbomoa kabisa kama ilivyo sasa uchochezi wake upo wazi kwa Watanzania zaidi ya 200000

Nakueleza tena wewe na Mohamed Said, kuwa mimi naijua vema historia ya Uhuru wa nchi hii na nina HAZINA kubwa ya vielelezo vya uhuru wa Tanzania huenda kuliko kijana yeyote wa kizazi hiki cha dotikomu!

Ndiomana nazungumza kwa starehe kabisa kuwa Mohamed Said ni MUONGO tu, MZUSHI na laghai wa kijahidina anataka kulifarakanisha taifa kwa maslahi yake!

Tumeamua sasa kumdhibiti, tumeanza kwa maandishi ya hoja kisha tutaingia kwa vitendo hatua kwa hatua mpaka uzandiki wake ukome kabisa na awe mtu mwema kabisa kwa taifa hili takatifu!

Yericko,

Labda nikuulize je unajua idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote huko Tanzania? Linganisho na watu 200,000 unaosema.
Je hao watu 200000 ni asilimia ngapi dhidi ya wasomi wote wa Tanzania ni duniani kote?

Kumbuka alichoandika Mohamed Said sio kitabu cha kawaida bali ni kitabu cha kitaaluma ndio maana anapata mialiko mbalimbalu duniani katika vyuo vikuu kutoa mihadhara.

Wewe na kijitabu chako cha UGAIDI sidhani kama unaweza kupata nafasi ya kualikwa katika vyuo vikuu maarufu kutoa muhadhwara wowote ule na nafikiri sababu utakuwa unazifahamu.

Kumbuka kuwa nii wangapi kati ya watu laki mbili wenye uwezo wa ku print mnakasha mzima na kuusoma post by post na ku digest kile kilichoandikwa na kuweza kujua nini kilicho bora.

Mimi kama msomi nimegundua umejawa na USHABIKI na KUPENDA KUJINASIBISHA NA NASABA MAARUFU na ndio maana unakuwa mgumu sana wa kutaka ku PROVE KILE ALICHOANDIKA MOHAMED SAID. Ulitakiwa umuulize Mama Maria kuwa unamfahamu Mshume Kihate? au Sharif Attas na hata wakina Sykes akupe kidogo kuhusu watu hao . Hapo ungepata mashiko hata ya kusema UONGO au UKWELI wa Mohamed Said kwani yeye amemchambua mpaka mama yake Nyerere na wengine wake wa karibu.

Kumbuka huko nyuma niliwahi kukwambia mimi naifahamu vizuri sana familia ya Nyerere na nilianza kukupa hata historia zao kidogo niligusia upande wa Ilmu zao lakin.

Lakin kikubwa katika mjadala huu katika JF utafungwa au hata mada kupotea kwa si zaidi ya miaka miwili lakin kitabu tena cha kitaaluma kitabakia na kufundishwa na kusomwa na vizazi kwa vizazi.

JF ni sehemu ndogo tu ya kupata info na kisha mtu kufatilia kwa kusoma vitabu. Mfano mdogo mimi binafsi kutokana na mnakasha huu umenifanya nitafute vitabu vya Mohamed said na kuvisoma na vile vile kutafuta kitabu cha historia ya uhuru kilichotungwa na chuo cha kivukoni. Hivyo kwangu mimi na naamini kwa wengi JF ni kichocheo cha kupata habari na kuzifuatilia in detail katika vitabu husika na ndio maana kila unachoandika ndani ya JF lazima useme na REf

naomba nikupe Pole sana kwa mtazamo wake kwani hilo limenifanya kukumbuka msemo mmoja ukitaka kumfichia kitu mTz basi ficha kwenye kitabu.

Pole sana kwa mtazamo wako.
 
Wickama,

Hebu pumzika na hii:

We have seen many times that the question of Zanzibar revolution is associated with
"Arab slave trade."

The origin of this paradigm stems from not knowing the actual source of the revolution.

The most telling problem was to perceive that the revolution in Zanzibar had to take
place because of the oppressive regime of the Zanzibaris of Arab descent.

It was not necessary that the invasion of Zanzibar should take place.

It was a special plot by one country invading another and hiding that hideous fact which
gave Zanzibar sleepless nights for forty nine years.
Mohamed Said,

..lakini Znz kulifanyika chaguzi tatu na mara zote ASP walikuwa wakifanyiwa mizengwe.

..sheria za uchaguzi za Znz , na ukizingatia UBAGUZI uliokuwepo dhidi ya Mwafrika, zilikuwa zina-guarantee kwamba ASP[chama kilichokuwa kikiwakilisha Waafrika] hakitoweza kushika madaraka.

..tuhuma kwamba ASP ilikuwa inashinda kwasababu ya kukusanya wapiga kura toka Tanganyika hazina mashiko. Muingereza, Waarabu, na Sultani, walikuwa pamoja ktk kuikomoa ASP. Muingereza, Waarabu, na Sultani, ndiyo waliokuwa na dola, sasa haiyumkiniki ASP wa-rig chaguzi tatu mfululizo.

..kwa mtizamo wangu chanzo cha mapinduzi ni mbinu chafu walizokuwa wakifanyiwa ASP[waafrika]. Yupo kiongozi mmoja, sina uhakika kama ni Mohamed Shamte, au Ali Muhsin, aliyejiapiza kwamba asingeweza kuunda umoja na Karume/ASP hata kama angelazimishwa na MTUME MOHAMMED!!

..zaidi nakuomba hebu soma hapa chini Ahmed Rajab anasema nini kuhusu Ali Muhsin.

Ahmed Rajab said:

" Nilipokuwa mlangoni tukiagana nilimuuliza[Ali Muhsin]: '
Ikiwa historia itajirejea tena, ni kosa gani kubwa kati ya makosa yako ambalo hutolirejelea?' Mwenzangu mmoja niliyekuwa naye aliniambia baadaye kwamba swali langu lilikuwa la utovu wa adabu.Mimi sikuhisi hivyo. Ala kulihali swali lilikuwa likichezacheza kwenye ulimi wangu na lilinidondoka. Nilipoliuliza Ali Muhsin "Zaimu" aliganda. Baada ya muda niliouhisi kama wa kufika mbinguni na ambao pingine ulikuwa wa sekunde chache tu, Sheikh Ali alitazama chini, halafu kama aligutuka hivi na akanijibu kwa msisimko: ‘Lakini sikufanya makosa yo yote.'

Ukweli ni kwamba juu ya ugwiji wake wa kisiasa kufanya makosa alifanya. Moja ni kupoteza dira ya zile siasa zake za awali na kujiachia akatekwa na wahafidhina na mabwanyenye waliokuja baadaye kukikalia kichwani chama cha ZNP.

Kosa jingine ni kushikilia katika enzi za ukoloni kuwa Sheikh Abeid Amani Karume, kiongozi wa ASP, ashtakiwe kwa madai kwamba si mzaliwa wa Unguja.
Sheikh Karume alishinda kesi hiyo. Angalishindwa asingaliweza kusimama kwenye uchaguzi na pengine hatima yake katika siasa za Zanzibar ingekuwa nyingine.

Juu ya hayo nafikiri kuna haja ya kuyatathmini upya maisha ya kisiasa ya Ali Muhsin na kukumbusha jinsi huyu jogoo wa uhuru alivyokuwa akiwika Zanzibar na Afrika kwa jumla. " -- Ahmed Rajab

NB:

..linapokuja suala la historia ya Zanzibar binafsi nakiri kumuamini mwandishi asiye Mzanzibari.

..nasema hivyo kwasababu Wazanzibari karibu wote wanapoandika wanakuwa na agenda nyuma yao, ama kumpamba Sultani, au kuyapamba Mapinduzi.

..ni mara chache sana huacha propaganda zao, na "kuchoropokwa" na ukweli.

cc: Wickama, gombesugu, Mag3, Nguruvi3, Ritz
 
Yericko,

Labda nikuulize je unajua idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote huko Tanzania? Linganisho na watu 200,000 unaosema.
Je hao watu 200000 ni asilimia ngapi dhidi ya wasomi wote wa Tanzania ni duniani kote?

Kumbuka alichoandika Mohamed Said sio kitabu cha kawaida bali ni kitabu cha kitaaluma ndio maana anapata mialiko mbalimbalu duniani katika vyuo vikuu kutoa mihadhara.

Wewe na kijitabu chako cha UGAIDI sidhani kama unaweza kupata nafasi ya kualikwa katika vyuo vikuu maarufu kutoa muhadhwara wowote ule na nafikiri sababu utakuwa unazifahamu.

Kumbuka kuwa nii wangapi kati ya watu laki mbili wenye uwezo wa ku print mnakasha mzima na kuusoma post by post na ku digest kile kilichoandikwa na kuweza kujua nini kilicho bora.

Mimi kama msomi nimegundua umejawa na USHABIKI na KUPENDA KUJINASIBISHA NA NASABA MAARUFU na ndio maana unakuwa mgumu sana wa kutaka ku PROVE KILE ALICHOANDIKA MOHAMED SAID. Ulitakiwa umuulize Mama Maria kuwa unamfahamu Mshume Kihate? au Sharif Attas na hata wakina Sykes akupe kidogo kuhusu watu hao . Hapo ungepata mashiko hata ya kusema UONGO au UKWELI wa Mohamed Said kwani yeye amemchambua mpaka mama yake Nyerere na wengine wake wa karibu.

Kumbuka huko nyuma niliwahi kukwambia mimi naifahamu vizuri sana familia ya Nyerere na nilianza kukupa hata historia zao kidogo niligusia upande wa Ilmu zao lakin.

Lakin kikubwa katika mjadala huu katika JF utafungwa au hata mada kupotea kwa si zaidi ya miaka miwili lakin kitabu tena cha kitaaluma kitabakia na kufundishwa na kusomwa na vizazi kwa vizazi.

JF ni sehemu ndogo tu ya kupata info na kisha mtu kufatilia kwa kusoma vitabu. Mfano mdogo mimi binafsi kutokana na mnakasha huu umenifanya nitafute vitabu vya Mohamed said na kuvisoma na vile vile kutafuta kitabu cha historia ya uhuru kilichotungwa na chuo cha kivukoni. Hivyo kwangu mimi na naamini kwa wengi JF ni kichocheo cha kupata habari na kuzifuatilia in detail katika vitabu husika na ndio maana kila unachoandika ndani ya JF lazima useme na REf

naomba nikupe Pole sana kwa mtazamo wake kwani hilo limenifanya kukumbuka msemo mmoja ukitaka kumfichia kitu mTz basi ficha kwenye kitabu.

Pole sana kwa mtazamo wako.

Maneno yako yoooooote hayana mafaa,

Najibu hilo la kwanza tu,

Kwanza nikujuze kuwa hakuna chuo cha Tanzania kinachotumia maandishi ya Mohamed Said kama rejea!

Hata kama Waziri wa elimu ya juu angekuwa Shehe Ilunga bado naamini hangeruhusu maandishi ya Mohamed Said yatumike vyuoni!

Ndiomana mahali sahihi pakupata kitabu cha Mohamed Said ni misikitini na sio maktaba za vyuo vya Tanzania hii!
 
Wickama,

Mbona hujiamini ndugu yangu,huna haja ya kujibu post mara mbili. Lile jibu lako la awali japo ni duchu lakini nilikufahamu uzuri tu.

Hizo stories zoote unazoniambia,mimi tayari nilishazungumzia kwenye wiki yangu ya mwanzo tu tangia najiunga hapa Jf...nilikhis vingi mapema mno!

Hizo khabar za Wanajamvi waliokua wana-quote Ayat...kumbuka wewe binafsi na Mwanakijiji ni wamojawapo. Sasa unaposema "wanagwaya" nashindwa kukufahamu,nawe pia yatakiwa uwemo kwenye mkumbo huo!?

Nafikiri tuachie kwa hapa.

Ahsanta sana.

Umenichekesha sana Ustadh, mwenzio nilirushiwa Aya usoni na ma-baunsa!!!! ili nitiwe adabu ndio maana nacheka..... sasa katika kukaa sawa ndio nikatafuta japo kiji-aya cha kujishikiza (hahahahahah)

kazi njema bwana ngoja tu-enjoy kidogo, ya Kipumbwi na Zenj na ASP inaelekea " BWANA KATWAA"
 
Km wewe hutoweza switch millions time bila kutoka kwenye mstari..ndio maana hamjaweza mtazama huyu mzee vyema na ngano zake...

Kuna Hadithi za kutunga zinaweza husisha characters wa kweli,scene za kweli, ha hata matukio fulani ya kweli na bado zikabaki hadithi za kubuni...ndio maana huwa wanaweka anaglizo..kuwa inagwa wahusika wanaweza kuwa ni "Historical People..." na "Mazingira ni ya kweli" kazii inabaki kuwa hadithi ya kutunga.

Siku hizi hata ktk computer games, kuna characters wa kweli....na mechi za kweli ila matokeo na matukio si ya kweli...Mfano..NI FIFA SOCCER.

Mkuu Nicholas,Mwanahistoria wetu Sheikh Mohamed ametutajia majina mengi ya wazee wetu na baadhi bado wako hai kwa nini hamuendi kuhakiki ukweli wa aliyoandika?Mzee Bilali Waikela,Tewa Saidi Tewa,Selemani Ngozi wote wapo hai mkuu nendeni mkahakiki mje mtujuze,msitokwe na mapovu tu bila ushahidi wowote.

Mwezi wa sita huu tupo tunafuatilia mtuonyeshe uchochezi uko wapi lakini hatuoni bali tunashuhudia mnavyodhihirisha chuki zenu dhidi ya uislamu na waislamu.
 
Mohamed, nyie ni akina nani? Na sisi ni akina nani?
Nakuhakikishia kuwa yapo maelfu ya 'sisi'' wanakereka sana na hiyo historia.
Nani amekupa mamlaka ya kusema hiyo ni historia ya ''sisi''
Hayo ni mambo yako uliyoandika na wala hukushirikisha mtu.

Unapokwenda kwenye mihadahra huwakilishi kundi. Wewe hukutumwa kuandika historia na 'sisi''.
Unapofanya hivyo unawadhalilisha wale unaosema ni ''sisi'' kwasababu hata uongo unanasibishwa nao.

Hii ni hitsoria yako na Wamenyama, wazulu na na wanubi if you like, si historia ya kitu kingine.
Mohamed narudi tena kuna maelfu ya watu wanajisikia dhalili, wanakereka sana hivyo sema hiki ni kitabu cha utunzi wa historia yako si ya wewe na kundi lolote.

Hivi kuna''sisi'' ambaye angependa anasabishwe na dhalili kama ya Ibadan.
Tafadhali huu ni utunzi wako wewe na familia yako!wazulu, wanubi na wamanyema

Hizi ni chuki zako usizifanye chuku za taifa. Kama babu yako alikuwa bandari ukadhani unapaswa kuwa mkuu wa bandari na haikutokea hivyo, hizo ni personal failure.

Kama karume alilala mtaani kwenu ukadhani mtaa huo utakuwa sehemu ya Pemba hizo ni personal wish siyo za jamii.
Please, personal grudge, frustrations n.k. hazina uhusiano na jamii na ni vema ukazi handle nyumbani kwako si kuishirikisha jamii.

Huu ni ubunifu wako katika utunzi, kama kuna kundi basi unalijua wewe hapo nyumbani not in national stage!

Wewew unamuuliza Mohamed Said, nani kakupa mamlaka ya kusema, hapo kwenye bold na wewe nani kakupa mamlaka ya kusema...ha haa haaa.
 
Mkuu Nicholas,Mwanahistoria wetu Sheikh Mohamed ametutajia majina mengi ya wazee wetu na baadhi bado wako hai kwa nini hamuendi kuhakiki ukweli wa aliyoandika?Mzee Bilali Waikela,Tewa Saidi Tewa,Selemani Ngozi wote wapo hai mkuu nendeni mkahakiki mje mtujuze,msitokwe na mapovu tu bila ushahidi wowote.

Mwezi wa sita huu tupo tunafuatilia mtuonyeshe uchochezi uko wapi lakini hatuoni bali tunashuhudia mnavyodhihirisha chuki zenu dhidi ya uislamu na waislamu.

Uthman,

Ndugu yangu hawa jamaa hawana kitu.

Mie nimewashauri mara nyingi sana waandike kitabu cha historia hiyo
ambayo wao wataridhikanayo.

Wanakesha JF kupambana na kitabu abacho kipo sokoni huu sasa mwaka
wa 16 na tunaingia toleo la tatu.

Sisi tulikaa kimya miaka kadhaa wakati ikitamba historia ya TANU ile ya
Kivukoni College iliyowatoa wazee wetu wote.

Mimi sikutokwa povu hata siku moja.

Niko pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwanafunzi nasikiliza kebehi
za walimu wangu na nikizijibu kwa makini sana.

Wakati mwingine nauliza, ''Jamani mmepata kumsikia Mshume Kiyate,
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir nk. nk.''

Nawaeleza hadi kuwatajia namba zao za kadi za TANU hazizidi digit 2.

Kwanza walimu wakinipuuza lakini baada ya kuona yale niliyokuwa yote
nikyamwaga pale yalikuwa mageni kwao baadhi ya walimu zangu wakawa
sasa wananisikiliza kwa utuvu chembelecho Gombesugu.

Ndipo nilipoamua kuandika historia hii iwe jibu kwa historia ya Chuo Cha
Kivukoni.

Kama wasemavyo Wazungu ''the rest is history.''

Sasa halazimishwi mtu kuamini haya nisemayo wala hii haiwezi kuwa sababu
ya sisi kutukanana.

Ikiwa unataka kuamini kuwa Nyerere kakutana na Abdu Sykes na Nyerere kaja
pale ana TANU yake sawa.

Mimi nani nimkatalie?

Lakini iwepo nafasi vilevile ya kuieleza TANU kwa mwelekeo usio huo.
Msiktukataze kuaianza TANU 1929 na Kleist Sykes.

Ikiwa mtu anataka Sheikh Hassan bin Amir na TAA Political Subcommittee asitajwe
katika historia ya TANU sawa hapana ugomvi lakini asizuiwe mtu mwingine kueleza
historia ya TANU Jimbo la Kusini akamtaja Sheikh Mohamed Yusuf Badi na Masoud
Mnonji
na Bi Shariffa biti Mzee.

Hii ni nchi huru alazimishwi mtu chochote kile uhuru wa mawazo unahakikishwa.

Ukitaka kuianza historia ya TANU kutoka Musoma ruksa, ukitaka kuanza historia ya
TANU Burma ruksa!

Mwasemaje wanajamvi wenzangu?
Wakati umefika wa kuanua jamvi au tuendelee na mieleka?
 
Ndugu yangu kwa jinsi unapiga makonde mazito...nadhani km ungekuwa Simba aliyeshika mnyama sasa anakwenda ktk Jugular vain "pale shingoni". Km ni Box basi unatandika ngumi nzito za kumalizia game.

Ohhhh boy; this is funny!!!!!!! A jugular vein. Wajua this type of approach kwenye debate huwa ni nzuri kuondoa classes
 
Wewew unamuuliza Mohamed Said, nani kakupa mamlaka ya kusema, hapo kwenye bold na wewe nani kakupa mamlaka ya kusema...ha haa haaa.

Shariff Ritz,

Kinachowauma ni kuwa kila wanapogusa anawakuta wazee wetu.

Hakika Karume siku ile ya mapinduzi si alikuwa kalala mtaani kwetu.
Kalala kwenye nyumba mojawapo ya wazee wetu.

Na haukuwa usingizi siku ile...
Masikio yote yalikuwa Zanzibar.

Walikesha na kutokea hapo safari ilikuwa Kunduchi kupanda boti ya
Mzee Shebe kurudi Zanzibar.

Shariff,
Hawa wanaumwa kwa kuwa hawana historia ya kueleza yote
yaliwapita.

Wanatuonea wivu sisi hapa tukitamba mpaka na madokumenti ya zaidi
miaka 60 tunayamwaga humu mwaaaaaaaaa!

Wao wanani?
Hawana chochote ila kuuliza maswali ya kuchokonoa.
 
Back
Top Bottom