Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Son of Alaska, Ulinidhania ninapomchekea Yericko sijiwezi? Si kataka mwenyewe akogwe? Sasa unategemea nini kama nitamkoga? Nanawa uso basi?!
oh....kweli JF kuna raha.....kuna logic za duniani nyingine..Logic hizi ukimpa hata fisi anaweza kufa njaa.Masikini wee...kumbe wanafanya haya kwa kutojua wafanyalo... Akikuambia mwenyewe akogwe unamkoga?Akikuambia umtumie kuchamba?Akikuambia umuue?.....akikuambia umloge...?
 
Yericko,
Bora nikakuoga.

Si unajua sisi huwa tuna kazi nyingine na maji achilia mbali kuoga.
Sidhani kama utafurahi kama wewe ukiwa maji nitakufanya hivyo.

Ninabaki kuwa mimi ni maji kwako, huwezi kunikwepa,

Mimi ni pumzi kwako ya uzima na haki, huwezi kukaa saa moja bila kuja jf kuniona!

Nimekuhamishia makazi jf bila kutaka!

Na zaidi nimeisimamisha ngano yako na kuichanachana kabisa!

Nimeruhusu fikra mpya magwiji wa historia wamekuhukumu mchana kweupe kabisa!

Kwamara yakwanza katika historia ya wanahistoria umekuwa mtu wa kwanza unaejiita mwanahistoria kuchambuliwa na kubezwa juu ya tungo zako kwanjia ya majukwaa huru ya mitandao ya kijamii na "ukakiri" wazi na kulialia mbele ya umma!

Katika hilo tu umevunja rekodi ya dunia, hakuina mwandishi wa vitabu aliyewahi kubanwa na mitandao ya kijamii na akalia mbele ya hadhila kama wewe!

Wengi hujibia hoja kwanjia hadhila za jumuiya za kisomi!

Lakini sisi tumekumwaga uswahilini tu na tukakuchangua changua na kukuvua nguo hadharani!

Pole sana hukutegemea yaliyokukuta!

Ulidhani hapa ni Ibadan ulipotapika sumu bila watu kukuhoji sababu za matapishi hayo!
 
Wickama kwa mujibu wa hadithi ya Mohamed, aliyeanzisha AA ni K.Sykes na kisha ikaenda enda kwa namna namna mara Abdul Kaibukia TAA, na hapo ndipo mambo yalipoanza kupamba moto ikiwa ni pamoja na kumuingiza katika siasa Nyerere kwa maraya kwanza walipoonana. Narudia ni kuwa mujibu wa maandiko na majidiliano ya Mohamed Said.

Kuna wanajamvi werevu wamesema hapa AA ilianzishwa na akina Matola kama Rais wake, Ramadhani Ali(kama sikosei) makamu na K.Sykes kama katibu. Ilikuwa ni kundi na si mtu. Wakaendelea kuhabarisha kuhusu D.Cameron alivyokuwa " anaunga'' mkono jitihada za kisiasa na hadi kutoa Jengo.

Jengo hilo likafanyiwa maarifa na wazee na vijana wa mjini nakugeuzwa kuwa mali ya familia.
Ingekuwa zama hizi tungesema ufisadi lakini nyakati hizo neno hilo lilikuwa halija wekwa katika mafaili au maandishi na tuseme ilikuwa sehemu ya matendo ya kisiasa.

Hapo kati kati wakawepo akina Mtamilwa na kuna nyakati V.Kyaruzi alikuwa rais wa TAA lakini haisemwi.
Huyu hakuwa sehemu ya wazee na ushiriki wake una walalkini. Anyway, tuendelee na Abdul, huyu kakiongoza chama hadi alipomuachia Nyerere kwa uchaguzi mkali sana ambao ulipangwa matokeo kabla.
Tafadhali usiniulize mkali halafu kupangwa maana yake ni nini.

Kuanzia AA hadi TAA ya Abdul chama kilikuwa cha kisiasa kwa matendo hadi Nyerere alipoandika katiba na kuanza kukidhoofisha. Nyerere ndiye alipendekeza chama kibadili mwelekeo lakini tayari chama kilikuwa na brain child kutoka Burma ambaye alishafikiria siku nyingi sana uhusu hilo kwa matendo na si nyaraka au faili.

Sijui kama nimekidhi haja na matarajio, naoba uniwie radhi kama kuna sehemu yenye mapungufu! huenda nilifyonza vibaya
 

Hapo hapo wanalia kuwa nchi ni ya mfumo kristu,

Je wanafanya juhudi gani kubadili hali hiyo?

Utawasikia wakisema nikupata mahakama ya kadhi,

Hivi ukiweka mahakama ya kadhi na ukamteu kafiri kuwa kadhi mkuu utakuwa umewatatulia tatizo au umewafunga kilemba cha ukoka?

Mungu awape ufahamu wa kuona hawa maamuma!
 

Hahaahaaa nimecheka sana,

Mpaka mke wangu amehoji kama ninaota au ninaumwa?

Hahahaa kweli Mohamed ni Scholar wa historia!

Uongo huwa haujisimamii hata kwa dakika moja! Lazima ushikiliwe ndipo usimame!
 

Uongo Mwingine huu hapa,

TANU ianzishwe mwezi wa saba mwaka 1954,

Kisha 1955 japo haitajwi mwezi gani,Dome Okochi Budohi akamatwe nakurudishwa kwao Lamu Kenya nakufungwa jela!

Kumbukeni wanajamvi, mashirikiano ya karibu kati ya TANU na KANU ya Jomo Kenyatta yalianza mwaka 1958 baada ya ule uchaguzi wa kura tatu pale Tabora

Baada ya uchaguzi ule wajumbe wa TANU wakiongozwa na Julius Nyerere na Bibi Titi walikwenda Nairobi kushinikiza kuachiwa kwa Kenyatta,

Sasa jiulize Dome Okochi Budohi alishiriki vipi akiwa jela zaidi ya miaka 5 nyuma?

Wanajamvi chambueni wenyewe!
 


Yericko,
Ungekuwa unachukua muda wa kufanya utafiti hata kiduchu kabla ya kuandika.
Wanajamvi chambueni wenyewe.

Huyu mtoto anachekesha sana ni Launcelot Gobbo wa JF.

Yericko
,
Hebu nisome kwanza hapa chini:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] My family was acquainted with one Dome Budohi, a Kenyan nationalist who was in Dar es Salaam during the struggle. Budohi helped in the founding of TANU and his membership card was no.6 issued to him in July, 1954. He was arrested in 1955 by the colonial government on charges of being a member of Mau Mau, a peasant uprising in Kenya against the British.

I have many recollections of visiting Budohi in his cell at the Central Police Station building which now houses the headquarters of the Tanzania Railway Corporation (TRC). I was at that time a child of not more than four years old. My first recollection of Budohi was that whenever we went to visit him we always found him reading a newspaper. Budohi was later deported to Kenya and detained on Lamu Island. On being released from detention just before Kenya's independence in 1963, Budohi went to Uganda and worked with The Uganda Argus. I now understand why I always found him immersed in newspapers whenever we went to visit him in his cell during his period in remand in Dar es Salaam.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] I was able, through the assistance of one Maxwell, probably a Luo and an old friend of his who remained in Tanganyika, to trace Budohi in Nairobi in 1972. I visited him in Nairobi. At that time he was staying at Ruiru a few miles from the city. Budohi had a portrait of Nat King Cole hanging in his sitting room. In 1974 I visited him again this time at his Ngei Estate house. Budohi became my primary source of information on the early history of Tanganyika's struggle against the British. At that time, however, I had no intention of writing a book.
Yericko,
Soma tena na hapa chini:

There were also patriots from nearby Kenya such as Dome Okochi Budohi and Patrick Aoko who had been exposed to the problems of colonial settler politics of grabbing land from the people. From them, Abdulwahid received very attentive ears and admiration for his ideas of transforming TAA into a more robust political organisation. Soon after the formation of TANU the two Kenyan nationalists were arrested by the government. For six months they were interrogated and kept in remand at the Central Police Station chained in their cells.

Yericko,
Hapa napenda kukufahamisha kuwa Dome Budohi akifahamiana vyema na baba yako Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Soma hapa chini wapi walikutana:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]

The composition of the TAA leadership showed East African solidarity that existed during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid talked to Nyerere seriously about forming an open political party to replace TAA.


Yericko,
Bado una hoja bado mie ni muongo?[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Nimecheka sana wewe ndiyo unasema kijana peke ambaye unaijua historia ya Tanganyika kuliko vijana wengine, masikini mpaka unatia huruma hujui chochote kuhusu Dome Okochi Budohi? Ngoja nikupe darsa kidogo.

Mahusiano ya Tanganyika na Kenya wala hayakuanza mwaka 1958 kama unavyodanganya wala hayakuanza na TANU, jitihada za kuunganisha nguvu zimeanza 1950 TAA na KAU, mwaka huo Adulwahid Sykes alisafiri kwenda kukutana na Jomo Kenyatta ili kuanzisha uhusiano na Kenya wakati huo Nyerere hayupo tena walitumia nafasi ya kombe la Gossage.

Hauwezi kusema unaijua historia ya TANU halafu hujui habari za Dome Okochi Budohi na Patrick Aoko, kwa kukusaidia tu Budohi aliwahi kucheza sinema ya kiswahili na Kawawa iliyoitwa "Mgeni Mwema" huyu jamaa alifika mpaka Handeni.
 

Mohamed Said,

Kila siku nakuambia mzee wangu huyu kijana hana alijualo kuhusu historia ya Tanganyika eti na yeye anawasomesha wanaukumbi anawambia uongo mwingine huu, ha haa haaa JF kuna vituko.
 
Last edited by a moderator:


Shariff Ritz,
Hawa jamaa tumewachukua kama abiria wetu katika safari ambayo
hawakuwahi hata kuiwaza.

Nchi tuliyowafikisha hawajawahi kufika hata siku moja.
Ndiyo maana wamepigwa na butwaa kuu.

Ukiwatajia Budohi kisha ukamuunganisha na TANU na Nyerere kwao ni maajabu.
Historia waliyosoma wao haina mambo haya.

Historia yao ni hii ya Nyerere mwanzo.
Historia yao ni ile ya Nyerere mwisho.
 
Wanajamvi wakati AA na TAA ikiwa under serious scrutiny nawarudisha kwenye Mapinduzi ya Zanzibar kidogo.
Mnakumbuka Mohamed Said alileta vipande viwili na kimoja ni hicho hapo juu kama majibu japo hayakuwa majibu.

Wickam aliomba reference na haraka Mohamed akaomba radhi kuwa hawaweza kutoa hizo reference.
Ikumbukwe kuwa suala la Kipumbwi si geni na amelishaliandikia na kuslisema sana huko nyuma. Kwahiyoo excuse ya kuwa source ni siri ima kwa kuzuia uandishi unaoendelea kama upo au kumkinga mtu si kweli na haina mashiko.

Nimeleta vkpengele hivyo kwasababu ukisoma kwa makini sana hiyo ni 'self quote' na hakuna mahali Mohamed amenukuu. Ni kawaida ya yeye kuji-quote na kusema ni reference. Narudia tena hiyo ni "self-quote''

Soma nukuu nambari moja between he lines kuna kitu kipo hapo ambacho kinaonyesha maandiko aliyonukuu si siku nyingi, pengine ni ya jana.

Natoa changamoto kwa Mohamed Said kufanya haya
Asitaje jina la mtu wala makala, kitabu, gazeti au paper na asitaje title.
Na wala asitaje mwaka, tunamuomba atoe muda (range) kwamba maneno hayo yalisemwa kati ya (mfano 1976-1986) basi

Kinyume chake iliombe radhi jamvi!
 
Mohamed Said,

Kila siku nakuambia mzee wangu huyu kijana hana alijualo kuhusu historia ya Tanganyika eti na yeye anawasomesha wanaukumbi anawambia uongo mwingine huu, ha haa haaa JF kuna vituko.

Shariff,
Yericko ni mtu muhimu sana kwetu.

Kama si yeye wapi mie ningepata nafasi ya kushuka na huo mpini wa Budohi?
 

Sheikh Mohamed Said,

Kituko kingine Yericko anawasomesha wanaukumbi kuwa TANU wameanza mahusiano na KANU mwaka 1958 baada ya kula tatu, ha haa haa, sijui anamdaganya nani masiki hajui chochote anaropoka tu.
 
Last edited by a moderator:

Mbona watu wengi tu humu ukumbini wanaleta mabandiko bila kuonyesha source na wewe unayagongea Like na kuyasifia, ha haa ha jamaa yako Mag3, ndiyo bingwa wa kuleta quote bila source lakini hata siku moja haujahoji akileta Mohamed Said, unawashtakia wanajamvi ha haa haa.

Vipi lile bandiko la Mag3, la kina Jamal Amir, Lawi Nangwanda Sijaona, ulisema limetamalaki ulihoji chanzo au ulimeza kama mamba, vipi hotuba ya Okello na Karume ya kiingereza ulihoji au ulimeza kama mamba, haa haa haa. Kunya anye bata...

Maandiko ya Yericko Nyerere, yote hayana source lakini hata siku moja sijakusikia ukiomba source hata siku moja unameza tu kama mamba.

CC: gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
Shariff,
Yericko ni mtu muhimu sana kwetu.

Kama si yeye wapi mie ningepata nafasi ya kushuka na huo mpini wa Budohi?

Huu mbini wa Budohi hatari unanikumbusha world cup Mexico 1986 Maradona alikuwa anachukuwa kijiji kuanzia katikati ya uwanja kisha anafunga goli kwa style anayotaka anawaacha mabeki wanatizama hakuna wa kumlaumu mwenzake wote masikini walikuwa hawana uwezo wa kumkaba Maradona, ha ha haa ha.
 

Wewe kweli ni maji na watu wameamua kukuoga...ha haa ha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…