Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Yericko,
Anajiliwaza wakati wewe hii nafasi ya kufundisha JF miaka mingi umeitafuta, hajui kwa tutakaa na kulala JF hata miaka mitano. Nani angewafahamu kina Mshume Kiyate. Ha ha ha.
Shariff Ritz,
Nani angelikujamjua ''The Sweet Abdulwahid.''
Stanley alikuwa Mzungu akifanya kazi Dar es Salaam Municipal Council.
Alifahamiana na Abdu Cosy Cafe ambako Abdu alipenda kwenda kwenda.
Alipokufa Abdu alimwandikia Ally Sykes barua kumweleza jinsi alivyojuana
na Abdu.
Barua hii imo kwenye file maalum la taazia alizopokea Ally Sykes baada ya kifo
cha kaka yake 1968.
Hili file lilipotea lakini likaja kuonekana.
Siku Ally Sykes alipoliona akanambia nende nikalichukue nisome.
Niliyokuta mle ni mazito.
Allah ameumba watu na akawajaalia ukarimu.
Ndipo nilipoelewa kwa nini alipewa jina ''The Sweet Abdulwahid.''
Akiingiza mkono mfukoni kinachotoka ndicho hicho hicho harejeshi
kupunguza.
Mungu mlipe kheri huyu mja wako na mjaalie Firdaus.
Amin.
