Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,061
Mohamed, katika uandishi unachekesha sana! Swali lilikuwa kwamba umetoa madai mazito ya Kanisa na Nyerere kuhusika na kifo cha EAMWS. Umekuwa unajinasibu kufanya utafiti katika kitabu chako. Kama ni hivyo utafiti wako umekuja na vithibitisho gani au logic gani za kuonyesha kuwa Kanisa lilihusika na kifo cha EAMWS?
Unapo quote mtu ukasema huo ni ushahidi ni soni na aibu kwa mwandishi wa miahadhara huko Harvard na Cambridge.
Nakuhakikishia wangelijua unachokifanya ni hicho na unaita utafiti huenda wangepiga na maganda ya mayai wanayokulisha usoni.
Mohamed hili usizilizungumzie tena maana tulikaa kimya tukusitiri naona umeamua kuvua hata ile iliyobaki.
Huna ushahidi wa uthibitisho wa kuaminika au kimazingira kuhusu kifo cha EAMWS.
Umeshindwa kuthibitisha kama ambavyo tulikuomba uthibitishe kuwa namba za mitihani zilianza kutumika wakati wa Profesa Malima, huweza na hadi leo kimyaa! hufunguwi kinywa kueneza upuuzi huo tena. Kama si upuuzi nithibitishie!
Umeshindwa kuthibitisha kuwa Abdul Sykes alimfundisha Nyerere siasa! Ushahidi wa maandiko yako umekusuta mchana kweupe! Mohamed, Moddy, MO! please
Umeshindwa kutuambia Nyerere alipotoa picha kwa Malima nini kiliendelea! huna jibu.
Unataka tuamini pale unapotaka wewe. Hilo si kwa wenye akili! never
Umeshindwa kuthibitisha kuwa Nyerere alikuwa anatembea kifua wazi hadi alipopewa suruali na wazee wako.
Tumekuuliza maswali unakimbia unasema hilo tuliache, hilo sina ujuzi nalo n.k.
Wewe unataka kusikilizwa tu ili ueneze chuki na husda!
Unafundisha jamii ulalamishi na wala huionyeshi njia.
Leo vijana wanakwenda kusikiliza kesi za Ponda badala ya kusoma Chemistry bado unatumaini utavunja daraja la udhalili.
Leo huwaambii watoto Kinondoni, masjid Quba, Thaqafa n.k. waache uhuni unawaambia NECTA inawaonea
Leo hujiulizi kwanini FEZA ni tofauti na Jabal Hilal, unatafuta mchawi NECTA
Leo, hujiulizi Ponda na BAKWATA wangombea nini unabaki kuwaaminisha kuhusu ngano ya EAMWS mwaka 1968
Leo tunakuuliza utupe nchi moja tu iliyojenga chuo kikuu wakati huo na sasa ni tofauti huna jibu.
Badala ya kufundisha jamii ijitambue, ione wapi wamejikwaa, ijifunze kutoka kwa wengine unashinda kutwa nzima ukiijaza uzushi na uongo kwa kutumia majina ya marehem na Nyakati ukiita historia.
Leo badala ya kuwaambi Kilwa wapeleke watoto shule, unaungana na sheikh Ilunga kuchochea mauaji ya maaskofu na mapadre!
Mohamed, MO! Uislam hausimami katika uzushi, uongo, fitna na mjungu.
Uislam ni ukweli amani na salama.
Muogope mola wako!
Sijui...huyo Bibi Titi katajwa wapi?Bibi Titi naye alikuwa Sheikh?
kabanwa kwenye kona tena??mohamed said naona umebanwa kwenye corner unajaribu kujinasua kwa rope a dope- opponents are going in for the kill-lets hope you get out of this in one piece-wachangiaji wote asanteni kwa somo hili
Mohamed Said ni Muhaini, na ni janga la kitaifa sasa, asiposhughulikiwa mapema taifa litakuja kujuta kesho!
Sisi hapa tunamuwashia taa nyekundu tu!
bwana nyerere huko tusende hakufai kabisa.
Vitisho hii leo?
Kujuta ndiko huku tayari tunajuta.
Wenye fahamu wanajiuliza hivi tumefikaje hapa?
Anaewashiwa taa nyekunda mchunguze.
Siyo mohamed said.
Yeye kakaa kitako hawezi kuogopa kuanguka.
Tuliza ubongo wako utaona taa nyekundu inamuwakia nani.
Kwa hakika si mohamed said.
Wala wa kujuta hatutakuwa siye.
Tujute kwa kipi tutakachopoteza?
Acha vitisho.
Marehemu sokoine angekuwa hai ningekwambia nenda kamuulize unamjua mohamed said?
Tuliandikiana barua.
Nilimwambia hana uwezo wala haki ya kuwakataza waislam kusomesha qur'an katika vibaraza.
Tulimalizana kwa heshima.
Alinielewa.
Mimi si mtu wa kutishika ndiyo maana unaona naandika na jina langu halisi naweka.
Hakuna asiyenijua.
Kuwa na adabu kidogo.
PLEASE,please do us a favor,vaa sucide belt ukakutane na ma bikra 20 mbele ya safarikabanwa kwenye kona tena??
Kweli sikio la kufa haliskii dawa?pamoja na nondo zote hizo bado unaukumbatia ububusa?
Kweli mapenzi ni mabaya sana,basi unapozungumza ujaribu kuonesha nawewe ni sehemu ipi aliyobanwa na yeye anapojitahid kujinasua ndugu,usiwe mwepesi kuendeshwa endeshwa na upepo,pia usiwe mwepesi kuchagua upande pasi na kutambua credibility ya upande huo as far as this mnakasha is concerned.
asante wakuu wangu najivunia contents zenu na mmenisaidia kujua msamiati wa histohisia; na hivyo imepelekea mie nami kujua tofauti kubwa kati;
historia vs
-based on fact
-rules of writing history are followed
histohisia
-based on fulfilling person feelings
-mostly rules of writing arent followed e.g mzee said book
- for pressure n pride e.g wazee wangu wa gerezan
- praising some groups within community "group interests" e.g sie waislamu ndio haswa tuligombania uhuru
- developed from chuki mf: Mzee moh'd anaonyesha wazi kuwa anachuki na nyerere pamoja na dini yake; la angekuwa muislamu ngano mnakasha huu usingekuwepo
please,please do us a favor,vaa sucide belt ukakutane na ma bikra 20 mbele ya safari
Mohamed Said naona umebanwa kwenye corner unajaribu kujinasua kwa rope a dope- opponents are going in for the kill-lets hope you get out of this in one piece-WACHANGIAJI wote asanteni kwa somo hili
Kiswahili kingi ndio kilicho stagnant maendeleo yenu,kiswahili kingi kinasababisha mtu uwe na upeo wa "small holding" ghafla ikipatikana a bigger holding mnanyanganyana matonge mdomoni-hii ndio tatizo la jamii yenuHivi haitoshi mimi peke yangu natoa darsa kwa nyie nyote?
Mnapokuwa wengi na mimi ndipo bongo langu linavyofunguka.
Nimesimama Univeristy of Ohio wakati wa maswali na majibu.
Bingwa mmoja wa masuala ya Afrika anatoa data anasema kuwa
Tanzania Waislam ni wachache ukilinganisha na Wakristo.
Kamwaga takwimu kwa kujiamini.
Ukumbi umesisimka.
Hawa ni Neocons.
Hawapendi Waislam
Walinialika lunch nikawasoma katika mazungumzo yao.
Mie hasikiza sana nasema kidogo.
Sura zao kama vile zinanisuta.
Tabasamu zimetawala kwenye nyuso.
Wanasubiri jibu.
Nikitoa data kinzani nitakuwa sijapata ushindi na mimi lazima niwashinde
hawa Waamerika.
Jibu likaja sijapata kulifikiri hata siku moja.
Nikasema:
''Ushahidi kuwa Waislam ni wengi hautaki takwimu.
Ushahidi wetu ni huu.
Nionyesheni katika historia ya dunia ambako wachache katika nchi walisimama
kupigana na mavamizi a nchi yao.
Waislam ndiyo walionyanyua silaha kupambana na ukoloni wa Wajerumani.
Wangekuwa wachache wangwaachia jukumu hili wale waliokua wengi walifanye.
Nionyesheni tena katika historia wachache katika nchi walisimama kudai uhuu wa nchi
yao.
Waislam ndiyo waliosimama kuupinga ukoloni wa Waingereza Tanganyika.''
Ukumbi ulikuwa kimyaaaaaaaaaa.
Tabasamu zimetoweka katika nyuso zao.
Nyuso zimevaa sura za mashangao.
Hapo nilikuwa nazungumza na baadhi ya wanahistoria wa Afrika na wameandika sana.
Halikjuja swali.
Nilikuja kujua liliwekwa mwisho hili swali kwa makusudi.
Liliwekwa mwisho kunikata ngebe yangu.
Ikawa mimi ndiye niliyekata ngebe yao.
mwanaharakati, pamoja na kwamba hujaomba msamaha kijana, nimekusamehe kwani hujui ulitendalo. Ungekuwa unafuatilia mjadala huu kimakini, hungekosa kuona kejeli, dhihaka na matusi ya kimtaani anayopewa baba wa taifa, mwalimu julius kambarage nyerere. Lakini hebu shuhudia wazee wa mohamed walivyoupokea ujio wa mwalimu mwaka 1952 dar es salaam.
Julius quickly gained leadership and was elected president of taa. He began by educating his followers to think about independence. Chief patrick kunambi who knew him well said that his leadership was not based on what julius promised "because julius practically never promised anything.
Because of this goal of independence nyerere and his colleagues reorganized taa as a political party, the tanganyika african national union, on july 7, 1954. It became better known as tanu and the date of it founding, the seventh day of the seventh month became saba saba (in swahili "seven-seven").
His colleagues unanimously elected julius as president of tanu. He was 32 years old at the time. One of the founding members of tanu.
mwanaharakati, amua mwenyewe, hayo ni maandishi ya hao wazee...mohamed said anadai wazee wake ndiyo walimwingiza katika siasa na kumfundisha ustaarabu wa kuvaa suruali mwalimu nyerere...kuna kejeli na tusi kuliko hilo.
kama oxford,cambridge na havard wanafikia hatua ya kuyapa heshima maandiko hayo,utakua wewe?Hakuna wa kuweza kukukataza kuyaita histohisia ama ngano,ama historia fake and whatsoever,,
umeshindwa kuupokea ukweli kwa kuwa umekuwa una ukakasi na mgumu kumezeka kwako,pole sana na ujaribu tuh kuvumilia kama unachomwa na ukweli huo,haki hii itaendelea kusemwa tuh,hadi akili ziwakae sawa,na bila shaka zishaanza kuwakaa sawa sasa.
Kiswahili kingi ndio kilicho stagnant maendeleo yenu,kiswahili kingi kinasababisha mtu uwe na upeo wa "small holding" ghafla ikipatikana a bigger holding mnanyanganyana matonge mdomoni-hii ndio tatizo la jamii yenu
narudia kusema kuwa sijapata mimi kusema kuhusu mambo ya kaptula kwa kweli inaniuma sana jina langu kuhusishwa na matusi na kejeli hasa kwa mtu mzima makamu ya kunizaa.
Mohamed acha unafiki, katika posti yako umemnanga nyerere kama muwongo na ....... kwanini useme hutukani au hii hapa chini
sio post yako? hebu isome kisha useme roho inakuuma kwasababu hujawahi kutukana.
By Mohamed Said
Umeingiza mambo mengi sana.
Kuna Zanzibar, elimu ya Waislam, matokeo mabaya ya shule za Kiislam, kuchinja.
Itakuwa tabu kufanya mjadala uliokuwa hauna mwelekeo ulionyooka.
Lakini kwa mukhtasari ukitaka historia ya Zanzibar na maendeleo yake itabidi tuanza kwa kuvamiwa
kwa Zanzibar na jeshi mamluki la Wamakonde kutoka Kipumbwi wakifadhiliwa na utawala wa Nyerere.
Kuanzia hapa tutaingia katika tatizo la Muungano na kwa nini leo Wazanzibari wanadai nchi yao.
Kuhusu elimu ya Waislam itatubidi tuje katika njama za Nyerere kuhujumu chuo kikuu cha Kiislam
kilichokuwa kijengwe Dar es Salaam mwaka 1968 na jinsi alivyotumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS
na kuunda taasisi kibaraka BAKWATA.
Vipi shule za Waislam hazifanyi vyema inabidi tuje katika hujma ya NECTA kwa wanafunzi wa Kiislam na
tuupitie waraka wa marehemu Prof. Malima kuhusu yale aliyoyakuta Wizara ya Elimu mwaka 1987.
Wizara ya Elimu na NECTA vimegeuzwa vigango vya kanisa.
Kubwa zaidi ni kuwa Waislam kwa muda mrefu hatukuruhusiwa kujioganaizi nje ya BAKWATA kibaraka
wa serikali.
Makanisa mnaendelea kwa kupendelewa na serikali iliyojaza watendaji Wakristo sisi tungepewa hayo
mabilioni ya MoU kati ya Makanisa na Serikali tusingekuwa kama hivi.
Yapo mengi sasa chagua tuanze na lipi katika hayo hapu juu niliyokugusia.
Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.
Kwenye ghetto hakuna maji wala misala sasa watu wafanyeje?
Mnatusimanga kwa hospitali mnazoendesha kwa hela ya kodi ya serikali kodi inayolipwa na raia
wote.
Tunabanwa na mfumokristo kisha mnatulaumu hatuna maendeleo
Nimesema ''muongo.''
Hilo lipo na naweza nikalirudia wala sijalisema nikiwa siko hadhir.
Mimi nalalamika kuhusu ''kaptula.''
Naona mnakasha unatoka ladha.
Labda tuupumzishe.
Uchovu umeingia.
Labda tuupumzishe huu mnakasha.
Watu wanasema yasiyokuwapo.
Wengine wanatukana.
Mnasemaje wanaukumbi?