Je wanajamvi Abdulwahid Sykes aligombea uongozi wa TANU au hakugombea? Kama aligombea matokeo yalikuwaje kwani inaonekana kwa sifa ya uongozi, akili na kupendwa alimzidi Nyerere (mgeni aliyetoka kijijini, mbishi na asiye na uzoefu wowote kisiasa wala kiuongozi) kwa mbaali!
Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi lakini kwa nini huyu mchochezi anaruhusiwa kumtukana ovyo Baba wa Taifa? Je nchi hii hauna uongozi? Je Kikwete umebariki haya?
Je Mwenyekiti na muasisi wa AA mwaka 1929?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TAA mwaka 1950?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TANU mwaka 1954?
Wanajamvi, I rest my case...nitabakia msomaji tu.
Ndugu yangu Mag3,
Nitakujibu tena huku nimetulia.
Kwanza umekosea kuuliza hilo swali.
Swali lako lingekuwa hivi:
Je, Mwenyekiti na muasisi wa AA mwaka 1929?
Je, Mwenyekiti wa TAA mwaka 1950?
Hapo nimeondoa neno ''muasisi'' kwa sababu 1950 TAA haikuasisiwa tayari ilikuwapo.
Je, Mwenyekiti na muasisi wa TANU mwaka 1954?
Mwenyekiti wa AA 1929 Cecil Matola.
Mwenyekiti wa TAA 1950 Dr Vedasto Kyaruzi
Mwenyekiti muasisi wa TANU 1954 Julius Kambarage Nyerere
Lakini je hiyo ndiyo historia yote?
Hutaki kujua ilikuwaje AA ikaasisiwa?
Hutaki kujua mchango wa Dr Aggrey na Kleist Sykes katika kuunda AA?
Hutaki kujua Dr Aggrey alimwambia nini Abdu 1924 alipokutananae Dar es Salaam?
Hutaki kujua vipi Dr, Kyaruzi alichaguliwa 1950 na yale yaliyopelekea kuchaguliwa kwake?
Hutaki kujua Nyerere aliingiaje TANU?
Hutaki kuijua ile Kamati ya Ndani ya Kuasisi TANU iliyokuwa nje ya TAA Political Sub Committee?
Hutaki kujua hadhi na nafasi ya Sheikh Hassan bin Amir na Abdulwahid Sykes au Hamza Mwapachu, Stephem Mhando, Dr Kyaruzi, John Rupia, Said Chaurembo katika Political Sub Committee?
Basi wewe unachotaka kusikia kikisomeshwa ni kuwa Nyerere kakalia kiti cha TANU basi.
Hutaki kujua vurugu Schneider Abdillah Plantan aliyowafanyia maofisa wa Kiingereza pale Arnauotoglo
hadi uchaguzi 1950 ukaitishwa?
Hutaki kujua Schneider alikuwa anapigana kaka yake Mwalimu Thomas Sauti Plantan aliyekuwa rais wa TAA avuliwe uongozi?
Haya yote wewe huna haja nayo?
Wala hutaki kujua ''politics'' za Dar es Salaam ya 1950 kuwa Wakristo walikuwa hata wakija kutaka kupanga nyumba Kariakoo wanaambiwa nenda Mission Quarter vipi wanachaguliwa katika TAA pamoja na Abdu?
Wala hutaki kujua nguvu ya Waislam katika siasa za Dar es Salaam ya 1950?
Wewe ni Nyerere, Nyerere, Nyerere.
Hasira zako ni za kujifanya.
Sijamtukana Nyerere.
Kwa hiyo huna haja ya kuninasibisha mimi na Rais Kikwete.
Si kitu chema mimi na wewe kufanyiana.
Ningekuwa namtukana Nyerere heshima yangu ingedondoka siku nyingi na hao wanaonialika katika vyuo na mikutano yao
wangekuwa washanidharau sina maana yoyote.
Ila wewe kinachokuchoma ni kuona kuwa historia niliyoandika mimi inaweka alama ya kuuliza kwa Nyerere.
Ni hilo tu.
Abdulwahid hakugombea nafasi yoyote 1954.
Abduwahid atakumbukwa na wale waliokuwanaye katika harakati kwa ukarimu wake.
Yeye hadi pale alikuwa ametimiza ndoto yake ya kuasisi TANU.
Fedha nyingi za mkutano ule zilitoka mfukoni kwa Abdulwahid, Ally, Dossa na Rupia.
Abdu amekwenda kaburini hakunufaika binafsi na TANU wala siasa.
Ila yeye kaifadhili sana TANU na hili Nyerere analijua sana.
Sasa hatuwezi kuacha kuwaenzi watu hawa.
Kadi 1000 za kwanza alizitengeneza Ally Sykes kwa fedha zake na kadi na. 1 ya Nyerere aliitoa Ally na ina sahihi yake.
Kadi na, 2 Ally Sykes, kadi na 3 Abdulwahid Sykes na kadi na 4 Dossa Aziz.
Ningeeleza mengi lakini haya kwa sasa yanatosha.
Ukweli ni kuwa Nyerere asingeliweza kupata uongozi wa TANU kama si kuungwa mkono na Abdulwahid Sykes.
Waulize wazee waliokuwapo wakati ule watakueleza.