Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ni fikra pia.
Hapana tatizo.

Je ungependa kufahamu habari za Baraza la Wazee wa TANU
chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman Takadir lilivyotayarisha
safari ya UNO?

Au habari za mweka hazina wa safari ya UNO Idd Faiz Mafongo?

Umeridhika na ukweli kuwa watu hawa hawatambuliki katika historia
yake mwenyewe Nyerere na katika historia yspa TANU?

Au wewe umebaki na Nyerere na UNO hutaki kuwajua waliofanikisha
safari ile?
 
Ni fikra pia.
Hapana tatizo.

Je ungependa kufahamu habari za Baraza la Wazee wa TANU
chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman Takadir lilivyotayarisha
safari ya UNO?

Au habari za mweka hazina wa safari ya UNO Idd Faiz Mafongo?

Umeridhika na ukweli kuwa watu hawa hawatambuliki katika historia
yake mwenyewe Nyerere na katika historia yspa TANU?

Au wewe umebaki na Nyerere na UNO hutaki kuwajua waliofanikisha
safari ile?


Mohamed

1. Tunahitaji historia inayopepesa utanzania wetu sio ubaguzi wa wazee wako peke yake, huo ni ukabila na udini ndani yake.

2. Tunahitaji historia itakayojenga umoja wetu na siyo historia inayojenga fikra za kisasi na chuki miongoni mwetu kama watanzania

3. Huwezi kujenga historia bora kwa watanzania

-umeendekeza zaid udini nakuifanya historia yako kukosa uwiano wa kitaarifa (unbalanced history)

-Umejenga hoja nyingi za kumchafua nyerere kwa maana ya ukatoriki wake na kusahau kabisa uhalisia wa historia unayoiongelea

-umekuwa mwanahistoria wa pwani ya tanzanganyika wala historia ya jirani zako hutaki kuifahamu. (Coclusion must be poor, a point based conclusion cannot tell the reality and truth of a particular location)

Hunasifa ya kuendeleza historia zako za kichochezi na zinazolenga kutuweka watanzania matatani.

a) Huku unaongelea wazee wako

b) kule unaongelea mfumo kristo

c) Kwingine unamuheshimu Nyerere halafu kwingine unamwita muwongo na anaghiliba

d) Tena unaongelea mou ..........

e) mara unaongelea kodi za watanzania kutumiwa na wakristu peke yao

Na mengine mengi, unataka kutuaminisha nini Mohamedi?
 
Historia hii ndiyo nishaiandika huu mwaka wa 15
na kitabu kinakwenda toleo la tatu.

Dawa ni nyie kuja na kitabu chenu kipinge historia hii
ya wazee wangu.


Mohamed

Wakati wewe ukizani kuandika historia ya babu zako, sisi tutajifunza ya watanganyika wote siyo ya bagamoyo pekee. (Throughout the country not a point history)

wakati wewe unang'ang'ana na matoleo ujuwe kwamba, ulimwengu ulianza na zama za mawe ......steam

engine.....analogia...Digitali, kwa akili yako bado unaota watu kurudia zama za mawe? namaana hicho kitabu chako na matoleo

yake mwisho wa siku itakuwa takataka wala hakuna atakaye shughulika nacho we endelea mpaka yafike matoleo 200 halaf

tafakali nini kitafuatia! steam engine - diesel/petrol engine, solar .... nuclear.....wind.. nk wewe bado unagombana na ujima potofu! .
 
Kitabu hiki nakifahamu nakuachia wewe uwajuvye wasikizaji
nani kakiandika.

Waandishi wanazungumza kuhusu uhuru kuwa Nyerere kawaeleza
"colleagues" hawa "colleagues" ni akina nani? Hawajulikani?

Siwezi kusema yote.

Lakini mimi nimesoma nyaraka za Abdulwahid Sykes anazungumzia
TAA Political Sub Commiittee 1950.

1950 Nyerere hajafika Dar es Salaam.

Hii kamati ndiyo iliyoandika document alokwendanayo Nyerere UNO
1955.

Mbona kitabu hicho kipo kimya katika majina ya "colleagues?"

Mbona kimeruka taarifa muhimu ya Nyerere nini ilikuwa na nani waliompa
nguvu ilhali yeye mgeni Dar es Salaam?

Fedha za kuanzisha TANU kapata wapi?
Wanachama kafanya uchawi gani kuwapata?

Alikuwa anakutana na wanachama wa TANU wapi kabla na baada ya TANU kuasisiwa?

Haya ni machache.

Iallah nitaweka barua ya Kleist ya 1933 alomwandikia Mzee bin Sudi rais wa AA inayozungumza
kuhusu kuendeleza harakati na kudai uhuru.

Hawa ni wazee wangu nimepokea kwao mengi.
Wametuachia hazina ya nyaraka.

Sina uchoyo urithi huu ni wetu sote.


H
 
Mbona nimekupa jibu pitia utaona.

Babu yangu hakuwapo.
Alikuwapo Mashado, Saleh Muhsin na wengineo.
 
Mbona nimekupa jibu pitia utaona.

Babu yangu hakuwapo.
Alikuwapo Mashado, Saleh Muhsin na wengineo.

Nyerere alikuwa amewakosea nini hawa hata wamchukie kwa dini yake lakini hawakumchukia Dr. Kyaruzi Mkristu kabla yake au kina Mhando? Why Nyerere?
 
Hiyo historia uitakayo si mpaka iwepo?

Aliyekwambia haipo nani? au unadhani ukipika ugali mbichi basi nawengine watapika mbichi! watapika uloiva na bora kuliko wako.

au kabla yako hapakuwa na historia wala waandishi mpaka ulipozaliwa wewe? bado unathibitisha kujifungia ndani ya bagamoyo.

Maandishi yalibuniwa mwakagani hata ukayakuta na kuyatumia kuandika historia yako ya uzushi? ujuwe ilikuwepo na utaiacha
 
... Abdulwahid, Nyerere, Ally, Dossa Aziz, Mhando, Rupia, Dunstan Omar na wengine walikuwa wakikutana kila Jumapili nyumbani kwa Dossa Aziz Congo Street au nyumbani kwa Abdulwahid, Stanley Street.

Hizi ndizo zilikuwa baraza mbili ambazo wazalendo walikuwa wakikutana kujadili mustakabali wa Tanganyika. Mijadala mizito sana ilijitokeza katika vile vikao vya kila Jumapili wakati akili na ujuzi wa siasa wa Abdulwahid vilipopambana na uhodari wa majadiliano wa Nyerere.

Vijana wenzake wa mjini aliowakuta katika siasa pale Dar es Salaam kama Abdulwahid na mdogo wake Ally, na Dossa Aziz walikuwa watu wenye uwezo wao na wakiishi ndani ya mji wao ukilinganisha na yeye mgeni, tena amekulia kijijini.

Uongozi wa TAA ulimpendekeza Julius Nyerere ili kukiimarisha chama kwa kuwa na Waafrika wenye elimu ya juu ndani yake. Ilibakia kwa Nyerere kukubali au kukataa.

Abdulwahid pamoja na viongozi wenzake wa TAA waliamini kwamba kuwa na Mwafrika aliye na elimu ya juu kama rais wa chama kungeimarisha uongozi wa TAA na kutoa sura nzuri machoni mwa serikali ya kikoloni na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukitembela Tanganyika.

Miaka mingi baada ya Tanganyika kupata uhuru, Abdulwahid aliulizwa kwa nini hakuliondoa jina lake kwenye ule uchaguzi wa mwaka 1953 ili kumpalilia njia Nyerere achukue uongozi bila kupingwa.

''Kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya Nyerere wakati huo na baadhi ya wanachama ndani ya kamati yangu mwenyewe ya utendaji walikuwa wakinishinikiza nisikubali kushindwa hivi hivi. Nilikuwa mgombea niliyependwa na kuondoa jina langu kungevuruga uchaguzi. TAA kilikuwa chama cha kisiasa chenye nguvu kilichokuwa kikiamini katika uchaguzi wa kidemokrasia. Uongozi wa chama ulikuwa upatikane kwa ushindani wa uwezo na sifa njema za uongozi. Tulimchagua Nyerere kugombea kwa sababu tulikuwa na imani naye nami nilikuwa mmoja katika wale walioamua hivyo, alijibu Abdulwahid.''

Je wanajamvi Abdulwahid Sykes aligombea uongozi wa TANU au hakugombea? Kama aligombea matokeo yalikuwaje kwani inaonekana kwa sifa ya uongozi, akili na kupendwa alimzidi Nyerere (mgeni aliyetoka kijijini, mbishi na asiye na uzoefu wowote kisiasa wala kiuongozi) kwa mbaali!

Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi lakini kwa nini huyu mchochezi anaruhusiwa kumtukana ovyo Baba wa Taifa? Je nchi hii hauna uongozi? Je Kikwete umebariki haya?

Mwaka 1955 chama kilichoanzishwa kilikuwa Tanganyika Railway African Union (TRAU) babu yangu Salum Abdallah akiwa Mwenyekiti muasisi na katibu wake Kassanga Tumbo.
Mohamed
Je Mwenyekiti na muasisi wa AA mwaka 1929?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TAA mwaka 1950?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TANU mwaka 1954?

Wanajamvi, I rest my case...nitabakia msomaji tu.
 
Nimesema ''muongo.''
Hilo lipo na naweza nikalirudia wala sijalisema nikiwa siko hadhir.

Na hayo yote mengine naweza nikayarudia tena na tena na tena.
Ila hilo la "kaptula"

Mimi nalalamika kuhusu ''kaptula.''

Naona mnakasha unatoka ladha.
Labda tuupumzishe.

Uchovu umeingia.
Labda tuupumzishe huu mnakasha.

Watu wanasema yasiyokuwapo.
Wengine wanatukana.

Mnasemaje wanaukumbi?
Kabla hatujapumzisha mnakasha ningependa kwanza uonyeshe ni wapi Nyerere alisema uwongo. Tupe na quote kabisa isiwe mambo ya kufikirika. Ahsante.
 
pamoja na kuendelea kutoa maneno ya kejeli,
kila unapojisikia kufanya hivyo,mwalimu Mohamed Said bado hajachoka kufundisha.
Anafundisha historia ya uhuru wetu,pia adabu kwa wale wasiofunzwa na wazazi wao.
wakati mwingine tabia ya mtoto hutoa picha ya walivyo wazazi wake.
wamesema maji hufata mkondo ati
Hii ni dalili ya uchovu na kuishiwa,
mfa maji 'heshi' kutapatapa
Ukirusha jiwe gizani,ukisikia mguno ujuwe limempata
cc @barubaru @Rizt @kichwakigumu @THE BIG SHOW @mv butiama
Mohamed Said ni Muhaini, na ni janga la kitaifa sasa, asiposhughulikiwa mapema taifa litakuja kujuta kesho!

Sisi hapa tunamuwashia taa nyekundu tu!
 
Last edited by a moderator:
pamoja na kuendelea kutoa maneno ya kejeli,
kila unapojisikia kufanya hivyo,mwalimu Mohamed Said bado hajachoka kufundisha.
Anafundisha historia ya uhuru wetu,pia adabu kwa wale wasiofunzwa na wazazi wao.
wakati mwingine tabia ya mtoto hutoa picha ya walivyo wazazi wake.
wamesema maji hufata mkondo ati
Hii ni dalili ya uchovu na kuishiwa,
mfa maji 'heshi' kutapatapa
Ukirusha jiwe gizani,ukisikia mguno ujuwe limempata
cc @barubaru @Rizt @kichwakigumu @THE BIG SHOW @mv butiama

Dos Santos,

Naogopa hata kumuonya na hatari za kauli yake.
Bora mumtahadharishe nyinyi.

Mfahamisheni ni vibaya sana kumtishia mtu maisha.

Huyu anaishi katika dunia yake mwenyewe anadhani bado
wana uwezo wa kutisha Waislam.
 
Kabla hatujapumzisha mnakasha ningependa kwanza uonyeshe ni wapi Nyerere alisema uwongo. Tupe na quote kabisa isiwe mambo ya kufikirika. Ahsante.

Jasusi,

Mimi sikuingia humu ndani kuja kufanya maskhara.
Mambo niandikayo ni mambo ninayoyafahamu na kufanya utafiti wa kina.

Watu ninaowashutumu kwa dhulma ni watu wakubwa wenye heshima zao.
kwa hiyo basi niandikapo kwanza natunguliza ''Bismilliah Rahman Rahim.''

Sitanii.
Chini ya kumtanguliza Allah siwezi kulinajisi jina lake kwa uongo.

Angalia hii na kwa kweli hiyo nukuu inatoka katika ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes...'' na si ngeni:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Betrayal of Ideals
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] On 5 th November, 1985, before he stepped down as president, Nyerere delivered an emotional speech to elders of Dar es Salaam.

Most of them were former members of TANU-the townsman who supported Nyerere during the struggle for independence
[1] Nyerere acknowledged the role of Muslims in those difficult days.

Nyerere told his audience that the imbalances between Muslims and Christians which his government had inherited from the British were rectified under his rule:
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
''And they (Muslims) gave us chance through our education policies, to correct the imbalances which we have done.

I am now in the happy position of sometimes not knowing whether a new member of Parliament, a Minister, or a Principal Secretary in our government ministries, is a Muslim or a Christian or neither unless their first name happens to give it away. And even that is not a sure guide in Tanzania, for we have Christians with Muslim names, Muslims with Christian names. This religious tolerance and freedom is your creation; what I have done is to speak up for those values on your behalf.''
[2]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] The speech was a farce.

The truth is that three decades after independence Muslim are not better off than they were under colonialism.

Sivalon has revealed that the Church has been able to create its own lobby which controls 75% of the seats in the parliament.

Among these seats 70% are held by Catholics and the rest are divided among Muslims and Christian denominations.
[3][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1] See footnote no.19.

[2] Daily News, 6 th November, 1985

[3] Sivalon, op.cit. p. 49.


Kwa kukumbusha tu ni katika hotuba hii Nyerere alisema kuwa alipoingia TAA Dar es Salaam aliwakuta vijana wenzake Dossa na Abdul. Akasema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo gani.

Hotuba hii inaogopwa.
Hairudiwi katika radio.
 
Je wanajamvi Abdulwahid Sykes aligombea uongozi wa TANU au hakugombea? Kama aligombea matokeo yalikuwaje kwani inaonekana kwa sifa ya uongozi, akili na kupendwa alimzidi Nyerere (mgeni aliyetoka kijijini, mbishi na asiye na uzoefu wowote kisiasa wala kiuongozi) kwa mbaali!

Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi lakini kwa nini huyu mchochezi anaruhusiwa kumtukana ovyo Baba wa Taifa? Je nchi hii hauna uongozi? Je Kikwete umebariki haya?


Je Mwenyekiti na muasisi wa AA mwaka 1929?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TAA mwaka 1950?
Je Mwenyekiti na muasisi wa TANU mwaka 1954?

Wanajamvi, I rest my case...nitabakia msomaji tu.

Ndugu yangu Mag3,

Nitakujibu tena huku nimetulia.

Kwanza umekosea kuuliza hilo swali.
Swali lako lingekuwa hivi:

Je, Mwenyekiti na muasisi wa AA mwaka 1929?
Je, Mwenyekiti wa TAA mwaka 1950?
Hapo nimeondoa neno ''muasisi'' kwa sababu 1950 TAA haikuasisiwa tayari ilikuwapo.

Je, Mwenyekiti na muasisi wa TANU mwaka 1954?

Mwenyekiti wa AA 1929 Cecil Matola.
Mwenyekiti wa TAA 1950 Dr Vedasto Kyaruzi
Mwenyekiti muasisi wa TANU 1954 Julius Kambarage Nyerere

Lakini je hiyo ndiyo historia yote?
Hutaki kujua ilikuwaje AA ikaasisiwa?

Hutaki kujua mchango wa Dr Aggrey na Kleist Sykes katika kuunda AA?
Hutaki kujua Dr Aggrey alimwambia nini Abdu 1924 alipokutananae Dar es Salaam?

Hutaki kujua vipi Dr, Kyaruzi alichaguliwa 1950 na yale yaliyopelekea kuchaguliwa kwake?
Hutaki kujua Nyerere aliingiaje TANU?

Hutaki kuijua ile Kamati ya Ndani ya Kuasisi TANU iliyokuwa nje ya TAA Political Sub Committee?

Hutaki kujua hadhi na nafasi ya Sheikh Hassan bin Amir na Abdulwahid Sykes au Hamza Mwapachu, Stephem Mhando, Dr Kyaruzi, John Rupia, Said Chaurembo katika Political Sub Committee?

Basi wewe unachotaka kusikia kikisomeshwa ni kuwa Nyerere kakalia kiti cha TANU basi.

Hutaki kujua vurugu Schneider Abdillah Plantan aliyowafanyia maofisa wa Kiingereza pale Arnauotoglo
hadi uchaguzi 1950 ukaitishwa?

Hutaki kujua Schneider alikuwa anapigana kaka yake Mwalimu Thomas Sauti Plantan aliyekuwa rais wa TAA avuliwe uongozi?

Haya yote wewe huna haja nayo?

Wala hutaki kujua ''politics'' za Dar es Salaam ya 1950 kuwa Wakristo walikuwa hata wakija kutaka kupanga nyumba Kariakoo wanaambiwa nenda Mission Quarter vipi wanachaguliwa katika TAA pamoja na Abdu?

Wala hutaki kujua nguvu ya Waislam katika siasa za Dar es Salaam ya 1950?
Wewe ni Nyerere, Nyerere, Nyerere.

Hasira zako ni za kujifanya.
Sijamtukana Nyerere.

Kwa hiyo huna haja ya kuninasibisha mimi na Rais Kikwete.
Si kitu chema mimi na wewe kufanyiana.

Ningekuwa namtukana Nyerere heshima yangu ingedondoka siku nyingi na hao wanaonialika katika vyuo na mikutano yao
wangekuwa washanidharau sina maana yoyote.

Ila wewe kinachokuchoma ni kuona kuwa historia niliyoandika mimi inaweka alama ya kuuliza kwa Nyerere.
Ni hilo tu.

Abdulwahid hakugombea nafasi yoyote 1954.
Abduwahid atakumbukwa na wale waliokuwanaye katika harakati kwa ukarimu wake.

Yeye hadi pale alikuwa ametimiza ndoto yake ya kuasisi TANU.
Fedha nyingi za mkutano ule zilitoka mfukoni kwa Abdulwahid, Ally, Dossa na Rupia.

Abdu amekwenda kaburini hakunufaika binafsi na TANU wala siasa.
Ila yeye kaifadhili sana TANU na hili Nyerere analijua sana.

Sasa hatuwezi kuacha kuwaenzi watu hawa.

Kadi 1000 za kwanza alizitengeneza Ally Sykes kwa fedha zake na kadi na. 1 ya Nyerere aliitoa Ally na ina sahihi yake.
Kadi na, 2 Ally Sykes, kadi na 3 Abdulwahid Sykes na kadi na 4 Dossa Aziz.

Ningeeleza mengi lakini haya kwa sasa yanatosha.

Ukweli ni kuwa Nyerere asingeliweza kupata uongozi wa TANU kama si kuungwa mkono na Abdulwahid Sykes.
Waulize wazee waliokuwapo wakati ule watakueleza.
 
Aliyekwambia haipo nani? au unadhani ukipika ugali mbichi basi nawengine watapika mbichi! watapika uloiva na bora kuliko wako.

au kabla yako hapakuwa na historia wala waandishi mpaka ulipozaliwa wewe? bado unathibitisha kujifungia ndani ya bagamoyo.

Maandishi yalibuniwa mwakagani hata ukayakuta na kuyatumia kuandika historia yako ya uzushi? ujuwe ilikuwepo na utaiacha

Kama ipo kama usemavyo mimi siwezi kupinga.
Ikiwa ipo iwekwe hadharani ili sote tuisome.
 
Back
Top Bottom