Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu zako waislamu wenyenye ni kama hawa akina Ritz, The big show, kichwangumu na wengine?

Kama ni hawa wala siumizi kichwa kuwauliza!

Tuendelee kuchambua ngano zako mkuu japo hupendezwi tukiita "NGANO" wakati ndio uhalisia stahiki.

Tumekuzoea kwa maneno yako wala utupi shida. Sijui wewe unawasemea Waislam gani. Unakumbuka ulishamwambia Mohamed Said ana akili za kimadrassa...kejeli zako dhidi ya uislam zipo wazi Waislam wanakusoma.
 
Hakuna watu rahisi kwa sasa DUNIANI kuburuza na kudanganya kama WAISLAM. Ili mradi uwe na maneno makali dhidi ya UKRISTO na WAKRISTO kama Mwalimu.

Watu rahisi kudanganyika wanakutoa povu hivyo...au mmeamua kujifariji na kujiliwaza.
 
Bwana Nyerere hajui kama si madras nisingekuwa
na fahamu hii.

Hajui kama madras imetufunza "power of retention."
Kuhifadhi sura na sura.

Hapa jamvini naona udhaifu wa jamaa zetu.
Atakuuliza swali hilo hilo tena na tena.

Naona udhaifu katika adab wepesi kutumia matusi.
Wepesi kughadhibika.

Wazito kusoma kitu kipya nk.
 
Ukisoma kitabu cha John IIiffe, utajua kuwa mwanachama wa kwanza wa TANU kisesa alikuwa Zacharia Madilla, mkulima wa pamba na mwenyekiti wa chama cha ushirika. Madilla alilipia mchango wake kupitia mjane wa Lameck Bogohe. Utajua kuwa huko Rungwe ilijulikana kuwa hauwezi kuwa mwanachama wa chama cha ushirika bila kuwa mwanachama wa TANU. Juhudi hizo zilifanywa na wakina Mwakangale. Utangundua kuwa huko Bukoba, Ali Migeyo alipotoka jela, mwenyekiti wa TANU wa wakati huo Herbert Rugizibwa alim-suspend kwa kuhofia kuwa TANU itafungiwa. Lakini Mwalimu Nyerere (yule aliyekuwa na chuki na waislamu) alipotembelea Bukoba alimsema mmisheni mwenzake na kumuamuru amuachie Ali aendelee na shughuli za chama.

Utajua kuwa kwa wasambaa, ni chama cha Shambaa Citizen Union kilichoongozwa na Petro Njau ndicho kilichokuwa kitovu cha TANU. Utafahamishwa kuwa kule Kondoa ambako uongozi serikalini ulishikwa na waislamu ni walimu wakatoliki wa Haubi ndio walioibeba TANU.

na mengine mengi.

Leo hii, huyu mchochezi anataka kutuaminisha kuwa ni ndugu zake wa Gerezani peke yao ndio waliotuletea uhuru! hata aibu hana?

Amandla..........
 
Watu rahisi kudanganyika wanakutoa povu hivyo...au mmeamua kujifariji na kujiliwaza.
Ninyi mliobahatika kusomeshwa na mfumokristo mmekuwa kama mwenye jicho moja kwenye kundi kubwa la vipofu( sorry, wasioona). Mnawaburuza wenzenu mtakavyo!
 

asante
 

Hapana, kuwataja si kuwa enzi. Kwani wakina Sykes hawajatajwa katika historia? Kama unavyodai sisi tunafanya kwa wakina Sykes, ndivyo unavyofanya kwa wakina Mwanjisi. Ungetambua na kuheshimu mchango wao usingediriki kung'ang'ania centrality ya uislamu katika harakati za kugombea uhuru. Ukisimama katika mihadhara hauwazungumzii. Hauwezi kudai kuwa ni wakina Sykes ndio waliompa ulaji Mwalimu, na kuwasahau wakina Rupia na Kyaruzi. Mpaka uchokozwe ndio unawakumbuka. Kama ulivyofanya sasa.

Amandla.......
 
Lakini na wewe majibu na maelezo yako ni yaleyale tangu ile thread yako mwenyewe. Ungekuwa umefika 65 tungesema umeanza kuwa "senile".
 
Ninyi mliobahatika kusomeshwa na mfumokristo mmekuwa kama mwenye jicho moja kwenye kundi kubwa la vipofu( sorry, wasioona). Mnawaburuza wenzenu mtakavyo!

Hivi Bishop Joseph Kibwetele alikuwa anawaburuza kina nani? Achilia mbali kina Kakobe, Mama Rwakatale, Mzee wa Upako.

Tujikite kwenye munakasha wa historia ya TANU tuyaache hayo.
 
Hivi Bishop Joseph Kibwetele alikuwa anawaburuza kina nani? Achilia mbali kina Kakobe, Mama Rwakatale, Mzee wa Upako.

Tujikite kwenye munakasha wa historia ya TANU tuyaache hayo.

Lakini haonsi 'wabaya' wenu. Wabaya wenu ni kanisa katoliki.
Hao uliowataja wanaweza kuingia vizuri sana kwenye kundi la msingi la kuburuzwa na chongo.
 
Hivi Bishop Joseph Kibwetele alikuwa anawaburuza kina nani? Achilia mbali kina Kakobe, Mama Rwakatale, Mzee wa Upako.

Tujikite kwenye munakasha wa historia ya TANU tuyaache hayo.
Hawa wote uliowataja hawawaburuzi wenzao kushambulia na kuwachukia watu IMANI na DINI tofauti. Wanawaburuza kuwakamua tu kwa kutumia jina la Yesu. Wanajikita zaidi kwenye Biblia na Miujiza kama ya Yesu. Wao wanajifanya kiungo kati ya wafuasi wao na Yesu.

Tunakoelekea sasa kubaya. Si umesikia masuala ya kuchinja kule Mwanza yanaleta taabu? Mchango wa mzee Mohamed ni mkubwa tu katika haya.
 

Moh Said na yeyote anayekubaliana nawe:
Hiyo statement in blue, ni maneno yako mwenyewe kwenye kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)"

Ni statement nzito sana.

Hivi hiyo TRUTH uliipatapataje? Ni kwa kutegemea maandishi ya Sivalon aliyokuwa ameandika several years before?
HIvi ni kweli kuwa hali za waislam (na waislam pekee) wakati ulipooandika kitabu, au wakati Nyerere alipotoa ile speech, zilikuwa mbaya kama wakati wa ukoloni? Je katika utafiti wako (kama ulifanya utafiti) uliwaangalia waislam na wasio waislam wa mijini na vijijjini na kufanya mlinganisho?
 

Nini maana ya kuwaburuza.
 
Nini maana ya kuwaburuza.
Unamburuza mtu pale anapokuwa ameacha kufikiri na kuamua kila jambo nawe unafanya hivo kwa niaba yake. Hahoji, hadadisi wala hashtuki. Ntakupa mfano unaotokana na huu mjadala wetu hapa. Waislam wengi tu sasa hivi wanaamini yote anayoyasema na kuyaandika Mzee wetu Mohamed juu ya Mwalimu na utawala wake ni ya kweli.

Imefika mahala huyu mzee kalewa sifa hii. Anajiita "mimi ni authority" juu ya hili au lile. Cambridge, Havard,..., kote huko wamemkubali!
 

Waislamu na Wakristo wote ni kama viatu tu, mnatumiwa kwa kuvaliwa na kisha viatu vikiisha vinatupwa, vinanunuliwa vingine na kuanza kazi ile ile tena na kamwe mwenye kiatu hawezi kukumbuka thamani ya kiatu alichokitumia na kukitupa kama kilimsaidia wakati wakati wa mvua na jua kali, kwa maana ana kiatu kingine kipya! Kwa kifupi wote MATAKATAKA TU!
 
Unashauri nini kifanyike?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…