Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Unakasirika bure ndugu yangu.

Si kama hivyo umewaeleza wazalendo kutoka bara na juhudi zao?
Nao hao si walisahauliwa?

Lakini mstari mmoja hautoshi.
Ufanyike utafiti makini habari zao zitolewe kitabu.

Itakuwa tumewaenzi wazee wetu hawa.


Wazee wetu au wazee wako? unasimamia wapi? maana ya wazee wetu inahusisha watanzania wote wa wakati huo (watanganyika)

Tumekukariri mara kadhaa ukisema wazee wako, na mara kadhaa umekataa maswali yanayouliza watanzania wengine nje ya

wazee wako, na umejenga hoja kwamba wazee wako walitengwa na kufanyiwa dhulma ndio sababu ya kuwahuwisha kwa kitabu

chako.
 
Hapana, kuwataja si kuwa enzi. Kwani wakina Sykes hawajatajwa katika historia? Kama unavyodai sisi tunafanya kwa wakina Sykes, ndivyo unavyofanya kwa wakina Mwanjisi. Ungetambua na kuheshimu mchango wao usingediriki kung'ang'ania centrality ya uislamu katika harakati za kugombea uhuru. Ukisimama katika mihadhara hauwazungumzii. Hauwezi kudai kuwa ni wakina Sykes ndio waliompa ulaji Mwalimu, na kuwasahau wakina Rupia na Kyaruzi. Mpaka uchokozwe ndio unawakumbuka. Kama ulivyofanya sasa.

Amandla.......

Si kweli ndugu yangu kama kweli nimekuchoma kwa kuwataja the
Sykes brothers na baba yao kwa upande mwingine ungechukia
kuona mchango wao umeondolewa katika historia.
 
Wazee wetu au wazee wako? unasimamia wapi? maana ya wazee wetu inahusisha watanzania wote wa wakati huo (watanganyika)

Tumekukariri mara kadhaa ukisema wazee wako, na mara kadhaa umekataa maswali yanayouliza watanzania wengine nje ya

wazee wako, na umejenga hoja kwamba wazee wako walitengwa na kufanyiwa dhulma ndio sababu ya kuwahuwisha kwa kitabu

chako.

adolay,

Hivi unamchukuliaje Nyerere kama mtume au binadamu?
 
Last edited by a moderator:
hili nalo ni swali mkuu!

Kibaraka wa kwanza niwewe, nitathibitisha.

Umekubaliana na maelezo ya mohamedi said kila siku, sihitaji ushahidi mwingi wa huko nyuma nikupoteza muda(kila mtu kachagua upande hilo liko wazi kabisa,na hakuna alielazimishwa kuchagua upande na yeyote yule,kila mtu amepima upande wa mleta mada yericko,,na upande wa mshutumiwa ndugu moh' said,kama ulivyoamua wewe kuchagua upande wa yericko na kuungana nae kuuthibitishia umma ya kwamba ndugu moh' said ni kibwetele na kwamba wanaoziafika hoja zake ni vibaraka wake,ndio nikakuuliza je hiyo lugha ni lugha ya hoja au lugha ya viroja na kushindwa?ni wapi umeskia yericko ama wale wanaompa backup wakihusishwa na majina ya fedheha na kukashifiwa mfano wa hilo la kibwetere?
Ngoja tuwe wawazi hapa,hizo hoja zako za mou,necta,bakwata n,k..,zimesatolewa ufafanuzi na zimeshaeleweka,au labda kama wewe hujaufuatilia huu mjadala,
kwa ufupi mimi nakubaliana na maelezo yake moja kwa moja bila kuacha hata nukta,sababu sijaona ukija na hoja za uhalisia za kumpinga zaidi ya kumkejeli kama ulivo mkejeli kwa kumwita kibwetere.






unatakaka mungu ambaliki mohamedi kwa dalsa la posti yake hapo juu?

A) kwa kumwita nyerere muwongo na mwenye ghiliba unaweza thibitisha uwongo wa nyerere na ghiliba bila kuwacha mashaka?

B) kwakusema necta ni vigango vya makanisa? Unaweza kututhibitishia necta wanaongoza na kufanya maombi ya wakatoliki kila siku na ndiyo majukum yao ya kiutendaji kila siku?

C) kwa kusema mou inawafaidisha wakristu? Je waislam mmezuiwa na nani kuweka mou yenu kama anavyolalama mohamedi

d) kwamba pale necta mnafelishwa, kunakumbukumbu za matokeo miaka mingi tu, je mshafatilia kuona jinsigani mnafelishwa ukiachana na lilekosa la islamic ambalo kulikuwa na makosa ya ukokotoaji (improper formula)?(usinimezeshe maneno yako kinywani mwangu,nataka mungu ambarik ndugu moh' said kwa moyo wake na muda wake alioutumia kuyaeleza yale ambayo yalikuwa yanataka kufutwa kwa makusudi za wazi wazi katika historia ya nchi hii,na sio histohisia kama unavotokwa povu,,
amefanya kazi kubwa ambayo anastahili pongez za hali ya juu,na sisi kwa heshima na taadhima tunampa pongezi zake.






katika maelezo yako hapo juu yanaakisi msimamo wako na wala sio tatizo ni mfuasi wa mohamedi(you can decide to call me whatever according to your perception,ila mimi nitabakia kushikilia msimamo wa kujibishana kwa nguvu za hoja,na sio hoja za nguvu kama zako,kwa namna yoyote ile nitakuwa upande wa ndugu moh' said na si kwa sababu ya uislam wangu,la hasha,ila kwa sababu ya hoja zilizopo upande huo.

je wewe siyo mfuasi wa kibwetele (mohamed)? unaweza kunijibu hapo juu maswali yangu tuhamie hoja nyingine utakayo ichaguwa katika maelezo yangu?
(nilishakuambia kabla hatujaenda kwenye hoja zako,unamwomba radhi ndugu moh' said kwa kumwita kibwetele?unamwomba radhi yericko kwa kumwaribia hoja yake kuu katika huu mjadala?unawaomba radhi wana jf wanaofuatilia huu mnakasha au huombi radhi??
 
adolay,

Hivi unamchukuliaje Nyerere kama mtume au binadamu?


Ninamchukulia nyerere kama mwanadamu mwingine yoyote, hata wewe kama itatokea mtu mwingine akakutusi, kukuchafua bila

sababu za msingi nitakutetea. nikawaida yangu. masimamo wangu ni ukweli bila kupakana matope pasi na sababu.

Nje ya uanadamu wake ni waziri mkuu wa kwanza, rais wa kwanza wa tanzania na mmoja kati ya wapigania uhuru

wengi ambao taifa litawakumbuka kwa ushujaa wao. Hivyo siyo sahihi kumtusi kumkejeli na kulundikia lawama nyingi zisizo na

msingi wala ukweli.
 
Huenda kweli hukuwa na taarifa.
Waislam takriban wote walisahau vyama vyao wakampigia Kikwete.

Iko siku utafanyika utafiti na hiyo "pattern of voting itadhihirika."
Hapa ndipo tulipoifikisha nchi.

Nimeshangaa kuwa wewe umekuja kujua sasa.
Mohamed una data gani za kuthibitisha hilo ndugu yangu?
Kwanini unapenda kuongea kama wewe ni Waislam? Vipi ilikuwaje JK akapata 60% mwaka 2010.

Huyu mzushi anataka kujenga hisia miongoni mwa watu kuwa waislam wanauwezo wa kumchagua Rais peke yao.
Anatumia propaganda hapa akiwa hana data wala nini.

Ukimuuliza maswali mengine anasema hana ujuzi wa mambo ya waislam
Mohamed wewe ni mwislam si Waislam, usitake jamii ionekane kwa mfano wako maana si kila mmoja angependa kunasabisha na wewe, Ponda au Ilunga kwa tabia, kauli au fikra. Si kila mmoja anapenda awe mwovu, mhalifu na kufur

Kuna waislam wengi sana wanakereka na hoja zako, Ponda na za Ilunga!
Acha uzushi na uongo! kama huna data au uthibitisho stop open you big mouth Mohamed.
Umekuwa mtu wa majungu tuu kila jambo!
 
Huenda kweli hukuwa na taarifa.
Waislam takriban wote walisahau vyama vyao wakampigia Kikwete.

Iko siku utafanyika utafiti na hiyo "pattern of voting itadhihirika."
Hapa ndipo tulipoifikisha nchi.

Nimeshangaa kuwa wewe umekuja kujua sasa.
Mohamed,
Labda unaweza kutufafanulia zaidi. Ikiwa Waislamu takriban wote walisahau vyama vyao wakampigia Muislamu mwenzao Kikwete, iweje kura za Kikwete zipungue kutoka asilimia 80 hadi 60? Hilo unalielezaje?
 
(nilishakuambia kabla hatujaenda kwenye hoja zako,unamwomba radhi ndugu moh' said kwa kumwita kibwetele?unamwomba radhi yericko kwa kumwaribia hoja yake kuu katika huu mjadala?unawaomba radhi wana jf wanaofuatilia huu mnakasha au huombi radhi??


Mkuu niombe radhi kwalipi tena

-Umetaka nithibishe wewe ni mfuasi wa Kibwetele (mohamed) umekubali kabisa kwamba wewe ni mfuasi wake hili halina shida

-Ili niombe radhi yakupasa ukanushe uzushi, uchochezi na ubaguzi katika mchango wangu kuonesha kwamba mohamed anachokifanya ni amani. Nionavyo mimi ni mmoja kati ya watu hatari kabisa anayetumia kalamu yake vibaya kufarakanisha watanzania. (kufarakanisha maana yake kutupeleka machafukoni yaani katika maafa kama alivofanya kibwetele original wa uganda, kwa maana hiyo basi huyu naye anastahili kuitwa kibwetele maana final goal ni machafuko kwa maana ya maafa.

Ukikanusha haya mafundisho yake kwamba nisahihi na ukanishinda kwa hoja nitaomba msamaha la huwezi

Wewe na Mohamed (kibwetele) itawalazimu kuwaomba radhi watanzania wote (waislam, wakristu, wahindu, wanaoamini na wasioamin) kwa kuwafarakanisha kwa kutumia hoja dhaifu mkijenga chuki na ubaguzi kutoka uchochezi wenu.


Hili nalo ni swali mkuu!

Kibaraka wa kwanza niwewe, hili umekubali halina utata.


Unatakaka mungu ambaliki mohamedi kwa dalsa la posti yake hapo juu?

a) kwa kumwita nyerere Muwongo na mwenye Ghiliba unaweza thibitisha uwongo wa nyerere na ghiliba bila kuwacha mashaka?

b) kwakusema Necta ni vigango vya makanisa? unaweza kututhibitishia Necta wanaongoza na kufanya maombi ya wakatoliki kila siku na ndiyo majukum yao ya kiutendaji kila siku?

c) kwa kusema Mou inawafaidisha wakristu? Je waislam mmezuiwa na nani kuweka mou yenu kama anavyolalama Mohamedi

d) kwamba pale Necta mnafelishwa, Kunakumbukumbu za matokeo miaka mingi tu, je mshafatilia kuona jinsigani mnafelishwa ukiachana na lilekosa la islamic ambalo kulikuwa na makosa ya ukokotoaji (improper formula)?


unaweza kunijibu hapo juu maswali yangu tuhamie hoja nyingine utakayo ichaguwa katika maelezo yangu?
 
Mohamed Said, Jasusi, Mzee Mwanakijiji, THE BIG SHOW,

..nimepata kipande cha hotuba ya Mwalimu wakati akiwaaga wazee wa D'Salaam.

..bahati mbaya sijapata hotuba nzima. sijui kama miongoni mwenu yuko aliye na hotuba nzima.

..ile mjadala uwe mzuri basi tuwe na utaratibu wa ku-quote the original source.


‘Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAWA

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

WAZEE NA MSIMAMO

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

WAINGEREZA WAONGO

Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.


Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

TWAININGI AMEKWISHA

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.’

 
Last edited by a moderator:
@Mohamed Said, Jasusi, Mzee Mwanakijiji, THE BIG SHOW,

..nimepata kipande cha hotuba ya Mwalimu wakati akiwaaga wazee wa D'Salaam.

..bahati mbaya sijapata hotuba nzima. sijui kama miongoni mwenu yuko aliye na hotuba nzima.

..ile mjadala uwe mzuri basi tuwe na utaratibu wa ku-quote the original source.



Unaona hapa anavyosutwa Mohamed? Ametuambia katika hotuba hii Nyerere alisema hajui au hakujua Abdul alikuwa na cheo gani. And sometimes it makes me wonder, why didn't Mohamed attempt to get a word from Nyerere when he started writing his book? Was it bias, was it hatred? Angetuwekea quote kama hii kitabu chake kingekuwa more authentic and balanced. But no.
What a shame!
 
Mohamed,
Labda unaweza kutufafanulia zaidi. Ikiwa Waislamu takriban wote walisahau vyama vyao wakampigia Muislamu mwenzao Kikwete, iweje kura za Kikwete zipungue kutoka asilimia 80 hadi 60? Hilo unalielezaje?

Waliwezaje kuamua kwamba Kikwete ndiye mwislamu mwenzao na Prof. Lipumba sio?

Second, au the point here is waislamu ni wengi,ni zaidi ya 60% ya dini nyingine zote, na kwamba, waktristo walimpigia Dr. slaa na kura hazikutosha kwasababu hao wakrusto ni wachache sana.

Huyo ndo Mr. Researcher.
 
Unamburuza mtu pale anapokuwa ameacha kufikiri na kuamua kila jambo nawe unafanya hivo kwa niaba yake. Hahoji, hadadisi wala hashtuki. Ntakupa mfano unaotokana na huu mjadala wetu hapa. Waislam wengi tu sasa hivi wanaamini yote anayoyasema na kuyaandika Mzee wetu Mohamed juu ya Mwalimu na utawala wake ni ya kweli.

Imefika mahala huyu mzee kalewa sifa hii. Anajiita "mimi ni authority" juu ya hili au lile. Cambridge, Havard,..., kote huko wamemkubali!
Walioandika historia ni watu wengi sana. Ukimuacha mzee MS je ulipata kumhoji yeyote katika waandishi hao? Kama ndio ni nani? Na kama sio kwa nini?
 
Unaona hapa anavyosutwa Mohamed? Ametuambia katika hotuba hii Nyerere alisema hajui au hakujua Abdul alikuwa na cheo gani. And sometimes it makes me wonder, why didn't Mohamed attempt to get a word from Nyerere when he started writing his book? Was it bias, was it hatred? Angetuwekea quote kama hii kitabu chake kingekuwa more authentic and balanced. But no.
What a shame![/QUOTE Mohamed Said nilikwambia vultures are circliing overhead tayari kuchukua a soon to be mzoga-hotuba ya NYERERE imewekwa na Sykes katajwa cheo chake-what more have you to say???sooner or later your book will be consigned where it belongs-THE dustbin
 
Last edited by a moderator:
Mohamed una data gani za kuthibitisha hilo ndugu yangu?
Kwanini unapenda kuongea kama wewe ni Waislam? Vipi ilikuwaje JK akapata 60% mwaka 2010.

Huyu mzushi anataka kujenga hisia miongoni mwa watu kuwa waislam wanauwezo wa kumchagua Rais peke yao.
Anatumia propaganda hapa akiwa hana data wala nini.

Ukimuuliza maswali mengine anasema hana ujuzi wa mambo ya waislam
Mohamed wewe ni mwislam si Waislam, usitake jamii ionekane kwa mfano wako maana si kila mmoja angependa kunasabisha na wewe, Ponda au Ilunga kwa tabia, kauli au fikra. Si kila mmoja anapenda awe mwovu, mhalifu na kufur

Kuna waislam wengi sana wanakereka na hoja zako, Ponda na za Ilunga!
Acha uzushi na uongo! kama huna data au uthibitisho stop open you big mouth Mohamed.
Umekuwa mtu wa majungu tuu kila jambo!
Unamyooshea kidole MS kumbe vidole vingine unajinyooshea mwenyewe. Ziko wapi data za kuthibitisha hayo uyasemayo?
 
1974 Kinshasa.
Muhammad Ali yuko ulingoni na George Foreman.

Foreman alikuwa na record.
Mpinzani havuki duru ya tatu.

Anakuwa keshawekwa chini flat.

Ilipofika raundi ya tatu handlers wa Foreman wakawa kwa sauti
wanamwambia Foreman.

George finish him off.

Ali anasikia.

Daktari wa Ali Dr Pacheco akamgeukia Ali anamuuliza vipi unasikia
maneno hayo?

Ali akamjibu Dr Pacheco akamwambia mimi huyu nampiga.

Pacheco akasema fanya haraka basi.
Ali akamwambia sitaki kumfanyia haraka nataka nistarehe na yeye kwanza.

Naam.
Ali ulipofika wakati akampiga Foreman kwa nockout.

Katika kitabu cha maisha yake The Greatest Ali anasema.

Kuanzia pale round ya tatu alimchukua Foreman katika njia ambayo kabla yeye
Foreman hakuwahi kutia mguu.

Mimi hawa sina papara nao mimi ni mtoto na mjukuu wa watu walioanzisha TANU.
Ndiyo maana unaona humu natamba.

Mawanda haya yote wazee wangu wamepita na mimi wakanipitisha.
Siyo kwenye mbeleko.

Wamenipitisha mtu mzima na akili zangu natembea mwenyewe kwa miguu yangu.

Niliwawekea tuvuti ya Baba wa Taifa inasema TANU kaasisi Nyerere Pugu.
Wameikataa.

Nimewawekea bandiko zima Sivalon anasema Kanisa Katoliki linautizama Uislam kama
adui.

Wamemkana Sivalon.

Nimeweka taarifa kadhaa.
Wanataka ushahidi wa kimahakama...

Lakini hapa kwa nyakanga.
Nyimbo hazishi.

Insha Allah kuanzia hapa nataka nimchukue Bwana Nyerere katika safari ya masafa marefu
hajapatapo kwenda.

Hajui njia.
Mohamed,
Ukinukuu uwongo kuthibitisha hoja zako na wewe unakuwa muwongo. Nimekwambia, na narudia tena, baba wa taifa amefariki bila kuwacha tovuti yake. Hiyo tovuti unayoisema na kuinukuu hakuianzisha Nyerere. In fact nitakaporudi Dar-es-Salaam nina mpango wa kuonana na wakuu wa Nyerere Foundation niwashauri waanzishe tovuti authentic ya Nyerere siyo hii bandia unayotuzungumzia hapa. Kwa hiyo ukiendelea kuinukuu tovuti hiyo ambayo unajua, na mimi najua, hyaijaanzishwa na Nyerere na haina baraka ya Nyerere Foundation au familia ya Nyerere unazidi kuendeleza uwongo.
 
Mohamed Said,where are you????unajua watu tumeacha kuangalia thread zote humu JF kupunguza distractions-mpaka hatma ya hii thread itakapojulikana!! staying silent unakuwa hututendei haki
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, Jasusi, Mzee Mwanakijiji, THE BIG SHOW,

..nimepata kipande cha hotuba ya Mwalimu wakati akiwaaga wazee wa D'Salaam.

..bahati mbaya sijapata hotuba nzima. sijui kama miongoni mwenu yuko aliye na hotuba nzima.

..ile mjadala uwe mzuri basi tuwe na utaratibu wa ku-quote the original source.



Mkuu nikushukuru sana kwakkuleta hotuba hii inayotupa mongozo sasa wa nini cha kujadili kwa undani hizi ngano za Mohamed Said
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom