Ukisoma kitabu cha John IIiffe, utajua kuwa mwanachama wa kwanza wa TANU kisesa alikuwa Zacharia Madilla, mkulima wa pamba na mwenyekiti wa chama cha ushirika. Madilla alilipia mchango wake kupitia mjane wa Lameck Bogohe. Utajua kuwa huko Rungwe ilijulikana kuwa hauwezi kuwa mwanachama wa chama cha ushirika bila kuwa mwanachama wa TANU. Juhudi hizo zilifanywa na wakina Mwakangale. Utangundua kuwa huko Bukoba, Ali Migeyo alipotoka jela, mwenyekiti wa TANU wa wakati huo Herbert Rugizibwa alim-suspend kwa kuhofia kuwa TANU itafungiwa. Lakini Mwalimu Nyerere (yule aliyekuwa na chuki na waislamu) alipotembelea Bukoba alimsema mmisheni mwenzake na kumuamuru amuachie Ali aendelee na shughuli za chama.
Utajua kuwa kwa wasambaa, ni chama cha Shambaa Citizen Union kilichoongozwa na Petro Njau ndicho kilichokuwa kitovu cha TANU. Utafahamishwa kuwa kule Kondoa ambako uongozi serikalini ulishikwa na waislamu ni walimu wakatoliki wa Haubi ndio walioibeba TANU.
na mengine mengi.
Leo hii, huyu mchochezi anataka kutuaminisha kuwa ni ndugu zake wa Gerezani peke yao ndio waliotuletea uhuru! hata aibu hana?
Amandla..........