Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Companero,

..unfortunately sina hicho kitabu.

..je, maudhui ya hiyo barua unayosema ilikuwa nzito yalikuwa ni nini?

..sehemu za kitabu hicho ambayo inapatikana kwa kutumia google search inaonyesha kwamba kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya kanisa na serikali kuhusu mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa ktk mfumo wetu wa elimu.

NB:

..hiyo barua inaweza kusaidia sana mjadala huu. lakini barua peke yake pia inaweza kuwa haitoshi. tunatakiwa kujua mazingira yaliyopelekea Mwalimu kuandika barua hiyo.

..kuna hotuba ya Mwalimu inaitwa "The Church and Society" ambayo aliitoa kwa wamisionary wa Maryknoll. Kuielewa hotuba ile unapaswa kwanza kuyaelewa mazingira yaliyopelekea Mwalimu kuitoa.
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi sana kuona nimeungana na watu wenye akili timamu werevu na wajuvi wa historia ya nchi yetu tuliokataa kuburuzwa na Shekhe Mohamed Said mwenye upeo wa kimadrasa, anaewaburuza waislamu wasio na hatia katika nchi hii.

Hakuna muislam yoyote ambaye anayeweza kukubaliana na wewe kwa kukejeli madrasa labda hawa unaowaita wajuvi na wenye akili. Acha kejeli kwa waislam jenga hoja tatizo unamajivuno kupita kiasi.
 
Companero,

..unfortunately sina hicho kitabu.

..je, maudhui ya hiyo barua unayosema ilikuwa nzito yalikuwa ni nini?

..sehemu za kitabu hicho ambayo inapatikana kwa kutumia google search inaonyesha kwamba kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya kanisa na serikali kuhusu mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa ktk mfumo wetu wa elimu.

NB:

..hiyo barua inaweza kusaidia sana mjadala huu. lakini barua peke yake pia inaweza kuwa haitoshi. tunatakiwa kujua mazingira yaliyopelekea Mwalimu kuandika barua hiyo.

..kuna hotuba ya Mwalimu inaitwa "The Church and Society" ambayo aliitoa kwa wamisionary wa Maryknoll. Kuielewa hotuba ile unapaswa kwanza kuyaelewa mazingira yaliyopelekea Mwalimu kuitoa.

Nyerere anawawakia Catholics Priests
 
Hakuna muislam yoyote ambaye anayeweza kukubaliana na wewe kwa kukejeli madrasa labda hawa unaowaita wajuvi na wenye akili. Acha kejeli kwa waislam jenga hoja tatizo unamajivuno kupita kiasi.

Madrasa ndio iliyokufanya wewe uwe unafikiri kinyumenyume. Mwenzenu MziziMkavu keshavutiwa na namna Wakatoliki wanavyowafundisha watoto wao Biblia kwa picha na Upendo badala ya mikwaju ya masab'uri mnayowakong'ota watoto wakishindwa kukariri kiarabu.

Shehe Sharif yeye aliweza kwa uwezo wa majini lakini sasa ameokoka anaitwa Michael Sewando na ana akili nzuri sasa baada ya kuacha uchawi. Jina la Bwana limihidiwe, ipo siku hata Shehe Yahya ataokoka naye ataacha uchawi. Hapo Wapemba hali zitakuwa mbaya kwani maduka ya ubani na mayai viza yatakosa wateja
 
Nashukuru mkuu mungu akuzidishie.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Mohamed Said sijui kama unatambua mchango wa Adam Sapi?

Kwa taarifa yako mkoa wa Iringa umeweka rekodi kwa kutoa maspika wawili wa nchi hii, mwingine akiwa ni spika wa sasa, Anne Semamba Makinda ambaye ni wa kabila la Wabena kutoka mkoani humo.
Sapi alikuwa spika wa bunge la Tanganyika tangu Desemba 27, 1962, akashikilia nafasi hiyo kwa ufanisi mkubwa hadi Aprili 25, 1994.
Mwaka 1973 hadi 1975 aliuacha wadhifa huo kwa muda baada ya kuteuliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Mji Mkuu (CDA).
Mtanzania huyo alivunja rekodi ya kushika wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi na alifanikiwa kufanya kazi yake bila matatizo kwani alikuwa akisimamia bunge la chama kimoja ambalo lilikuwa la watu ‘dugu moja'.
Akijulikana kama Mtwa (Chifu), Sapi alikuwa Mwafrika wa kwanza nchini kupewa cheo cha heshima cha Kepteni wa jeshi la wakoloni wa Uingereza la King's African Rifles (KAR) ambalo ‘Waswahili' walilitamka kama ‘KEYA' wakimaanisha ‘kei ei ara'.
Ni chifu Adam Sapi Mkwawa, aliyekuwa Mhehe wa Kalenga, muumini wa dini ya Kiislam ambaye alifariki dunia Juni 25, 1999 kutokana na shinikizo la juu la damu.

Unataka wahehe nao waje na historia yao ya Uhuru wa Tanganyika?
Kwani ndugu yangu hairuhusiwi kwa Wahehe au kabila lolote lile kuandika historia yao?

Pokea nyongeza ya Chief Adam Sapi Mkwawa:

Maisha ya Chifu Adam Sapi Mkwawa yalitokeaa katika ''Baragumu'' Aprili 12, 1956.

Alisoma Tabora na Makerere alikokwenda kusomea udaktari.
Hakumaliza masomo yake na alilazimika kurudi nyumbani kuchua nafasi ya Uchifu wa Wahehe.

Alichaguliwa mjumbe wa Baraza la Kutunga sheria mwaka 1947 akiwa na umri wa miaka 27. Mwaka 1955 Abdulwahid na Dossa walialikwa na Chifu Adam Sapi kwenda Kalenga kwenye sherehe za kukabidhiwa fuvu la Chifu Mkwawa aliyejiua katika vita vya Wahehe na Wajerumani.

Chifu Adam Sapi Mkwawa aliingizwa kisirisiri ndani ya TANU na Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz alipowaalika katika sherehe ya kupokea fuvu la babu yake.

Chief Mkwawa alikuwa mmoja wa machifu wa wachache sana waliounga mkono TANU.
Kwa maelezo ya Machifu waliounga mkono TANU angalia Sauti ya TANU No. 22 ya tarehe 28 Februari, 1958.

Sasa tuingie kwenye historia ya mbali kidogo ya babu yake Abdulwahid Sykes na babu yake Chief Mkwawa. Katika jeshi la Wajerumani waliokwenda Kalenga kupigana na Mkwawa alikuwa babu yake Abdulwahid Sykes Sykes Mbuwane.

Sykes Mbuwane alikuwa Mzulu mamluki aliyeingia Tanganyika na Mjerumani Hermann Von Wissman akitokea Kwalikunyi Mozambique.
Jeshi hili la Wazuu lilikwenda Kalenga kupigana na Mkwawa baada ya kumshinda Abushiri bin Salim wa Pangani.

Hii illikuwa miaka ya mwisho ya 1800.

Sasa wazalendo hawa Abdu na Adam Sapi ambao wazee wao walikuwa maadui katika miaka 1800.

Mwaka 1955 Abdu na Adam Sapi wakiwa marafiki wa karibu sana na wana udugu wa damu Abdu akamkatia Adam Sapi kadi ya TANU nyumbani kwake Kalenga.
 
Fanya utaratibu utuwekee hapa hata baadhi ya nukuu . Vitu kama hivi mohamed said huwa havioni.

Nilijaribu kunukuu nikashindwa, kila mstari ni mwako wa nguvu tu wa Mwalimu Nyerere kwa Wakatoliki wenzake - inabidi mtu aisome barua yote na jibu la Father Rweyemamu.
 
Labda mantiki ya mjadala huu tulikuwa hatujaelewana mkuu,

Mimi sipingi kila mmoja (mtanzania)kuandika historia yake, na ingekuwa fahari kila familia ya Kitazania kuwa na Kitabu chake cha historia,

Ninachopinga tena kwa nguvu zote ni kuiita

"Historia ya uhuru wa Tanganyika Upande wa Pili" na zaidi kusema kitabu hicho ndicho chenye dhamana ya masimulizi ya uhuru,

Hilo tu halikubaliki na linadhihaki uhalali na uhalisia wa nchi yetu!
 
Bahati mbaya natumia simu, nitajitahidi kesho niilete hapa mkuu, na nitaifafsiri kabisa ili waswahili wenzangu wote tufaidi.
 
sijawahi kusoma upumbavu wa kifikira wa kutunga .... very sorry ... wajaze ujinga majuha wenzio

you are dangerous in any how

Upumbavu, Ujinga, Majuha...

Mbona unanitukana ndugu yangu?
JF ni mahali pa kushindanisha hoja.

Haya matusi ya nini?
Hivi na mimi nikakuvurumishia matusi

Si ukumbi utajivunjia heshima yake?

Jitulize ili tushindanishe hoja.
Matusi hayajengi.
 
Mohamed Said,shikamoo sijawahi kuona mtu anayejua kufanya mjadala wa kiungwana kama wewe,Ni kwa vile unajua nini unachosema,aliyeanzisha mjadala na wanaomsapoti wameshindwa kutuonesha ushahidi wapi uchochezi wako,zaidi ya kulalamika na kutoa maneno ya kichokozi.Kutojibu upuuzi wao umefanya kuonekane tofauti kubwa ya uelewa wa mambo,akili,hekima,busara na uungwana baina yako na yao.Huyu aliyeanzisha post hii bila shaka hakujui vizuri umahiri wako wa hoja na ushahidi mwanana wa historia ya nchi yetu.Wengi huko nyuma walijaribu lakini waliishia kukimbia mjadala au kutoa kashfa. Mungu akulipe kila la kheri kwa kutuelimisha historia iliyofichwa kwa makusudi.
 
Mkuu naomba unionyeshe majibu ya Mohamed Said hasa yaliyojibu hoja stahiki?

Ukiweka iitikadi ya kidini hutauelewa mjadala huu utakuwa mpiga makofi tu hata pasipostahili ndugu yangu!

Soma kwa makini uzi huu kisha fuatilia hatua kwa hatua majibu ya hoja!
 
Last edited by a moderator:
Kwa kile ninachojua, historia huwekwa vitu muhimu vya kusaidia jamii fulani. Hii historia ya 'Uhuru wa Tanganyika upande wa pili' kama alivyosema mwandishi alipenda tuwatambue wazee wa kiislamu ambao walishiriki kwenye kupigania ila juhudi zao kwa bahati mbaya au kwa makusudi hazikutambuliwa. Sikufurahishwa na alivyosema 'watu hawapendi kusikia kuwa uhuru ulipiganiwa na waislam', sidhani kama hili ni kweli kwa sababu hata bila kuambiwa naamini watanganyika kwa kipindi hicho walikuwepo wakristo wengi pia. Kwenye siasa kuna mambo mengi, hata vikiandikwa vitabu vingapi vya tukio la kuonekana moja bado utabaki ukweli uliojificha kwa maslahi ya wahusika. Kama ambavyo Abul Sykes alishindwa kuweka bayana na Nyerere alivyoshindwa kusemea vizuri na mwandishi kukiri kutosema kabisa aloambiwa au alosoma katika kutafuta habari hizi. Si rahisi kwa gafla watu waliokaa pamoja kufanya mambo wasisemeshane na aliyeonewa au aliyeguswa na tatizo kulinyamazia.
Pamoja na hayo, miaka hamsini sasa imepita na zaidi ya miaka kumi mshutumiwa afariki. Leo kiongozi mwingine jamii moja na wanaoonewa akiri si yeye anayeongoza serikali na tatizo limedumu kwa miaka hata baada ya mshutumiwa kuondoka madarakani na kufariki na viongozi wengine kushika. Inawezekana kabisa si wazo binafsi lililompelekea kutenda kwa uonevu bali kuna nguvu ya nyuma kama inavyoonekana sasa na kwa viongozi wengine waliopita. Nadhani juhudi zingelekezwa huko kuliko kuishia kuwaona hawa wasaliti pengine tungepewa sisi ingekuwa hivyo.
Kupambana na adui kwa hitaji maandalizi ya kikosi vizuri, nadhani wakati waislam wanajiandaa kudai haki yao ni bora wangeanza juhudi za kujijenga ndani kwanza katika matatizo yao ya ndani, umoja na elimu nadhani ni vitu muhimu kufikia hili.
Kwa uzoefu binafsi kutoka shule mbili za serikali za jinsia moja, tuliishi vizuri katka shule ambayo jamii ilipana kwa uwezo binafsi na si dini na nilikuwa kati ya wanyonge katika shule ambayo dini na dhehebu, kabila, uwezo wa kifedha viliweka nafasi yako katika jamii bila kujali uwezo wako. Si vizuri kuzipa dini zetu nguvu kutawala mawazo ya jamii tunaharibu juhudi za maendeleo. mi ni kati ya wenye bahati ya kuwa na ukoo wenye dini mchanganyiko pande zote mbili, heshima na upendo ndio vinatulea.
 
Ahsante kwa fikra zako.

Ukikataa kuwa Waislam ndiyo walioongoza mapambano ya uhuru tunarudi palepale tulipoanzia
na mimi ikabidi niandike kitabu hiki ambacho leo ndiyo kimezua yote haya humu JF.

Hili la Waislam kuwa mstari wa mbele dhidi ya ukooni sikulisema mimi.

Kleist Sykes aliandika kumbukumbu zake vipi alianzisha African Association 1929.

Kumbukumbu hizi zikaja nyambuliwa na mjukuu wake Daisy Aisha Sykes zikatiwa
katika kitabu alichohariri John Iliffe ''Modern Tanzanians,'' ''Kleist Sykes ''The Townsman.''

Ndani ya kitabu hiki Kleist anasema kuwa viongozi wa African Association walikuwa Waislam
kwa kuwa Wakristo walionywa wasijiingize katika siasa.

Kwa hali hii hata TAA ilipokuja kubadilishwa kuwa TANU 1954 Waislam walikuwa ndiyo wanachama
wa mwanzo wa TANU.

Hiyo pembeni wanachama wa mwanzo wa TANU walikuwa wanachama wa Al Jamiatul Islamiyya fi
Tanganyika (Muslim Association of Tanganyika).

Hata viongozi wa mwanzo wa TANU walitoka Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akina Idd Faiz Mafongo,
Ali Mwinyi Tambwe na wengine wengi.

Ilibidi viongozi wa TANU Jimbo la Kusini Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Masudi Mnonji, Yusuf Chembera
na Salum Mpunga waweke mkakati maalum kuivunja fitna ya Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini ili wawaachie
Wakristo kuingia TANU.

Kitabu changu kimeeleza hili kwa kirefu.
Najua historia hii hapendezi sana kwa baadhi ya watu na wangependa isisemwe.

Juu ya hilo huo ndiyo ukweli.
Sina haja ya kueleza zaidi katika hili.

Pili historia hii anuani yake siyo ''...upande wa pili...'' hayo ni maneno kajiaandikia
Nyerere wa humu JF usiyatie maanani.

Hakika kulikuwa na Wakristo katika TANU lakini hawakuwa katikati ya jukwaa.

Fanya utafiti wako hili utalitambua.

Sitokujibu yote uliyoandika.

Lakini ikiwa unapenda kujua historia ya uhuru wa Tanganyika soma kitabu cha maisha ya
Abdu Sykes.
 
Labda mantiki ya mjadala huu tulikuwa hatujaelewana mkuu,

Mimi sipingi kila mmoja (mtanzania)kuandika historia yake, na ingekuwa fahari kila familia ya Kitazania kuwa na Kitabu chake cha historia,

Ninachopinga tena kwa nguvu zote ni kuiita

"Historia ya uhuru wa Tanganyika Upande wa Pili" na zaidi kusema kitabu hicho ndicho chenye dhamana ya masimulizi ya uhuru,

Hilo tu halikubaliki na linadhihaki uhalali na uhalisia wa nchi yetu!

Mimi sina tatizo kwa wewe kupinga kitabu changu.

Mimi nimekipinga kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na Kivukoni College
sasa iweje mimi nikukataze wewe kukipinga kitabu changu?

Tofauti yetu mimi na wewe ni moja tu.

Mimi nimepinga kwa kuandika kitabu na kueleza historia ya TANU kwa kutumia nyaraka
halisi za wenyewe waliounda African Association na TANU.

Wewe mwenzangu unapinga mikono mitupu, maneno matupu na kwa bahati mbaya sana
na huu ndiyo msiba niuonao kwako unaandika kwa kejeli na ujuba.

Sasa wasomi wanapokhitilafiana katika jambo hupambanisha hoja kwa hoja basi.
Hawabughudhiani wala hawatukanani.

Iwe itakavyokuwa narudia kusema kuwa sina tatizo kwako au kwa yoyote yule kupinga
kitabu changu.

Sababu ni moja tu.

Wanaoamua ukweli wa kitabu si mtu mmoja au wawili au kikundi cha watu.
La hasha.

Wanaotoa uamuzi ni wasomi na wanafunzi wa somo uloandikia pamoja wa wanajamii
kwa ujumla.

Kitabu changu kimefungua mlango mwingine si kwangu mie binafsi bali kwa watafiti katika
vyuo vingi duniani vinavyosomesha African History kuitupia jicho upya historia ya Tanganyika.

Hili mimi limenitosha.
Kitabu sasa kina umri wa miaka 15.

Kuwa juu ya kipindi hicho bado kitabu tunakijadili humu JF kama kimetoka jana kwangu mimi ni
ushindi na faraja kubwa.

Hivi tuandikavyo humu JF kitabu kinakwenda toleo la tatu.

Kitabu cha Kivukoni College bado kipo kwenye toleo la kwanza na sidhani kama kuna mpango wa
kukichapa tena kwa kuwa hakina wasomaji.
 
Nashukuru kwa maelezo yako ndugu yangu.

Unaposema mimi napinga kitabu chako mikono mitupu ni kweli, sijaandika kitabu chakupinga kitabu chako na hili naamini lingekuwa la furaha kwako.

Lakini si mwiko kupinga kitabu chako kwa majadiliano ya hoja hapa jamvini kabla ya kutunga kitabu hicho.

Nimetumia hoja nyingi zilizozaliwa kutokana na kitabu chako ambazo kimsingi wewe unadhamana ya kuzijibu,

Kwa mafaa ya wasomaji wetu hapa jamvini, ungewatendea uungwana kwa kujibu hoja kama zilivyosimama ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom