Kimsingi kilichobadilika ni jina la mmiliki tu uongozi na malengo ya shule yalibaki vile vile. Ndiyo maana hakuna mtu yoyote aliyethubutu au atakayethubutu kudai eti kwamba ukienda katika shule zilizotaifishwa mfano, Pugu, Minaki, Tambaza, Zanaki, Jangwani, Kibasila, Ilboru, Weruweru, Tosamaganga, Msalato, Umbwe, Ndanda n.k, utakuta idadi ya kuridhisha ya wanafunzi Waislamu wanaosoma huko. Lakini hata katika shule za sekondari chache mpya ambazo serikali ilijenga au kujengewa mwishoni mwa miaka ya 70, kama vile: Kibiti, Ruvu, Karatu, Bagamoyo n.k , kote walimu, wafanyakazi na wanafunzi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80.
Watoto wachache wa Kiislamu wanaosoma huko huonekana kama wakimbizi wanaosaidiwa katika nchi ya ughaibuni. Kuhusu kuingia sekondari kwa kigezo cha kuchaguliwa na mpango wa quota system, watendaji Wakristo waliojazana katika mfumo wa elimu nchini wamekuwa wakihakikisha kwamba Waislamu hawasomi kutokana mbinu zifuatazo:-
i. Kufanya matokeo ya darasa la saba kuwa ni siri hivyo kuweza kuibadili nafasi walizoshinda Waislamu na kuwapa wengine. Tazama ushahidi mzito uliotolewa na Njozi mwaka 2000; katika kitabu cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania uk. wa 62 -70. Hapa vijana wa Kiislamu waliofaulu darasa la saba walinyimwa nafasi kuingia sekondari na wale waliofaulu kidato cha nne walinyimwa kuingia kidato cha tano. Kazi hii ya kuwakwamisha vijana wa Kiislamu ilifanywa vyema na mawakala wa Mfumokristo waliojazana katika mfumo wote wa elimu nchini.
ii. Kuhamisha wanafunzi Wakristo kutoka maeneo yenye ushindani mkubwa kwenda Mikoa iliyokuwa na alama ndogo za kuchaguliwa kama Pwani, Dar, Lindi, Mtwara na Tanga ambayo pia ni maeneo ya Waislamu . Tazama Malekela 1983 in Access to secondary education in Sub- Sahara Africa
Katika jedwali la ruzuku sio sahihi kwa sababu kiwango kinachotolewa kwa makanisa kimeonekana kuwa ni kikubwa sana kuliko kinachotolewa kwenye Hospitali zote za serikali. Mbona haujaonyesha n kiasi gani cha fedha kilienda kwenye hospiltali za wilaya na mikoa na zahanati na vituo vya afya vya serikali ndipo ulinganishe fedha ngapi ilienda hospitali za makanisa? Baada ya kuchukua idadi kamili kiasi cha fedha kinachokwenda kwenye mahospitali yote ya serikali na kiasi cha fedha kinachokwenda kwenye mahospitali ya makanisa utakuta kwamba hospitali za makanisa zinapata kiasi kidogo sana cha fedha za serikali tofauti na takwimu hizo hapo juu. Kama unaweza kutoa takwimu zisizo sahihi ulizochakachua nadhani pia habari zingine ulizotoa huenda zinaweza kuwa za uongo.
Shule ulizotaja hapo juu ni za zamani za wakristo je, mbona haujataja shule za kiislamu zilizotaifishwa na serikali?
Hapo penye rangi nyekundu: kama matokeo ya darasa la saba yalikuwa ni siri wewe ulijuaje kwamba waislamu waliofaulu walikuwa wanaachwa na wanachukuliwa wakristo waliokuwa wamefeli ili waende sekondari na kidato cha tano; ikiwa matokeo yalikuwa ni ya siri na hao unaosema walikuwa wanachagua walikuambia??
wanafunzi Wakristo kutoka maeneo yenye ushindani mkubwa kwenda Mikoa iliyokuwa na alama ndogo za kuchaguliwa kama Pwani, Dar, Lindi, Mtwara na Tanga ambayo pia ni maeneo ya Waislamu . Hii inamaanisha kwamba uwezo wa kielimu, au kufaulu mitihani ulikuwa mdogo sana na kwamba ufaulu wa waislamu uko chini ukilinganisha na ufaulu wa wakristo kwenye mikoa anayodai ina ushindani sana. Kwa hiyo hao wakristo walipokwenda kwenye mikoa hiyo wakawa wanapeta kwenye mitihani. Lakini cha ajabu ni kwamba mimi nilikuwa natumia jina la kiislamu; JUMA HASSAN na nilifaulu nikaenda sekondari nikitumia jina hilo. Maelezo yako ni ya uongo, hakukuwa na upendeleo wowote.
Nitajie uislamu ulipokuja ulileta shule gani ya msingi, sekondari, au chuo cha uganga na hospitali? Waislamu wamewahi kujenga wapi chuo cha nursing wakasomesha wauguzi? Mahali pengine nimeshasema swala la elimu ni la ukristo. Ukristo umeleta elimu, na mahospitali Uislamu umeleta madrasa na misikiti tu. Waambieni watu wenu Elimu hiyo mnayodai ni ya wakristo. Wao wamewahurumia wakawapatieni. Niambie katika elimu mchango wa waislamu katika ugunduzi wowote Scientific invention, haupati majina ya waislamu katika elimu. Hakuna lolote katika elimu lililoletwa na waislamu, tulieni tuwafundishe aliyekwisha tangulia ametangulia.