Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said,

Kuna huyu mtu anaitwa Dome Okochi Budohi, raia wa Kenya mmoja wa viongozi wa TAA na muasisi wa TANU.

Kuna mwanabodi yeyote anayejua habari zake.

Huyu mtu muhimu sana kwenye historia ya Tanganyika.

Kama unacho kitabu changu tazama utaona nimepiganae picha nyumbani kwake
Ruiru Nairobi mwaka 1972.
 
mm binafsi sijalewa mada hii,naona udini,mchango wa waislam kama taasisi katika uhuru wa nchi yetu,matatizo ya zanzibar na nyerere,mwislam mmoja mmoja katika harakati za uhuru wa tanganyika.naomba nisome kwanza mada ya said mohamed
 
Samahani kidogo Mzee Mohamed Said, naomba tujadiliane hili kwa faida ya wanajavi:

Unafahamu harakati za Mwalimu Nyerere akiwa mwanafunzi pale Chuo kikuu cha Makelele nchini Uganda?

Bada ya kuanza kufundisha pale Pugu sekondari jijini Dar harakati zake za ukombozi zilikuwaje mpaka kufikia uamuzi wa kuacha kazi yenye mshahara?
 
Hii haingii akilini, sasa serikali imemtupa D Aziz,ina maana na mwanae wa kumzaa Hamza Aziz nae alimtupa baba yake-how there is something being hidden from the world- baada ya kufariki wanae wakaanza kugombania nyumba zake kariakoo-sasa mtasemaje alikuwa hajiwezi AU mlitaka fadhila ilipwe mara 100

Huyu Hamza Azizi kuna kipindi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) na Mwl.Nyerere.Bila shaka ilikuwa ni kulipa fadhila kwa niaba ya Baba yake.Kwa cheo hiki alishindwaje kumtunza Baba yake?.
 
Haya lete hili kosa lolote lile unaloliona lipo kwenye Quran.

Si mimi bali ni Quran yenyewe ndiyo inayowapa changamoto hii zaidi ya miaka 1400 iliyopita ili uingilie na kutafuta kosa kama utaliona
Quran 4:82. Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi"

Mmeshindwa na Mohamed Said wenye Historia ya Tanganyia sasa mnataka kuingilia Quran! haya karibuni.

Haya Mufti, twende huku https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/386657-nakaribia-kusilimu.html#post5486976 hapa tumuachie Yericko na Mudi Side
 
mm binafsi sijalewa mada hii,naona udini,mchango wa waislam kama taasisi katika uhuru wa nchi yetu,matatizo ya zanzibar na nyerere,mwislam mmoja mmoja katika harakati za uhuru wa tanganyika.naomba nisome kwanza mada ya said mohamed

Kaka! Tupo post #44 ungeanzia mwanzo post #1 nadhani utaelewa.
 
HOJA
Nimesoma maelezo ya Mohamed Said kuhusu Mshume Kiyate alivyomkirimu mwalim hadi kumpa pesa, chakula n.k.
Mohamed akaenda mbali zaidi na kusema Ditopile alipoelezea mchango wa Kiyate, Magazeti yalipotosha kwa kusema alimdhalilisha Nyerere kwa maneno ''kulishwa''. Hapa Mohamed anatuambia kuwa kuna kusoma habari na kupotosha habari kunakoweza kutokea. Fair enough!

Ukisoma maelezo ya vitabu tuhumiwa utaona kilichotokea ni kuchukua baadhi ya mistari na kupoteza dhana nzima.
Sina maana kila kinachosemwa hakikuandikwa, ninamaanisha kuwa kuna sehemu imechukuliwa sentensi tu na kuacha maudhui ya aya nzima.

Swali 1: Je, vitabu vya Bergen na Silvalon haviwezi kuwa vimefanyiwa upotoshaji kama ule uliofanywa kwa Ditopile?

HOJA
Ukisoma majibu kwa Yericko Nyerere kuhusu Mshume Kiyate, Mohamed ameelekeza tuhuma zake kwa Nyerere hasa pale anapodai kuwa kulikuwa na zipo hujuma za jina lake kutopewa mtaa. Kwamba Nyerere alifanya hivyo kama sehemu ya dharau na chuki kwa wazee wake.

Tangu Uhuru, madiwani wa jiji la Dar es Salaam kwa asilimia zaidi ya 80 hadi sasa ni Waislam wakiongozwa na Mameya Waislam tena wazee wake akina Kitwana Kondo, Sykes, Abouu n.k.

Swali 2:
a) Kuna ushahidi gani kuwa madiwani, mameya na viongozi wengine wa jiji walipigwa marufuku kutoa jina la mtaa wa Mshume Kiyate
b) Je, aliyebadilisha jina la bara bara kama UWT/Bibi titi ni Nyerere au ni madiwani wa jiji
c)Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani?

HOJA
Mambo yote yaliyotokea kati ya 1954 hadi 1985 yalimhusu Nyerere kama mtu.
Leo Mohamed anasema serikali ikae na Waislam iongee nao kuhusu tatizo.

Swali 3
a) Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali?
b)Mbona yaliyotokea nyuma hayatajwi kama ni matatizo ya serikali yanasemwa ni ya Nyerere na kwanini leo hayasemwi kama ya Kikweteyanasemwa kuwa ni ya serikali?

HOJA
Mohamed amekuwa analalmika dhidi ya dhulma kwa wazee wake na Waislam

Swali
a)Kwa vile tunatafuta muafaka wa kitaifa, yeye ana maoni yapi kuhusu suluhu ya duku duku hilo.
Nini suluhisho ili kuondoa dhulma anayoidai.Nini kifanyike
(i) katika kuleta uwiano wa madaraka
ii)uwiano wa elimu
iii) n.k.

HOJA
Mohamed ametoa madai kitabu cha Bergen kimepigwa marufuku kama kilivyopigwa marufuku kitabu chake kule UDSM

Swali 4
a)Kitabu cha Bergen Kimepigwa marufuku kwa tamko la nani na lini!
b) Kitabu cha Mohamed kilichozuiliwa kuwa reference UDSM, ni kwa tamko la nani na lilitoka lini
 
a)Kitabu cha Bergen Kimepigwa marufuku kwa tamko la nan na lini!
b) Kitabu cha Mohamed kilichozuiliwa kuwa reference UDSM, ni kwa tamko la nani na lilitoka lini
Kitabu kimetoka na waandishi wake hawajasema kuna tatizo la upotoshaji.

  1. Uwezekano ni mdogo sana
  2. (a) Katika mambo ya hujuma shida kupata ushahidi isipokuwa watendaji wanakuwa hawafanyi kinachotakiwa.

(b) Sijui
(
3 (a) Sijui hilo swali wanaweza kujibu viongozi wa Waislam
(b) Sijui waulizwe viongozi wa Waislam

Dukuduku ni kwanza serikali ikubali lipo tatizo

Hayo mengine matatu ni Waislam wanyewe waseme uwiano nk.
Kitabu kuzuiwa hilo haliwekwi dhahir ila wanafunzi wa historia wanaambiwa hivyo
 
Mohamed Said,

Unayo ile picha ya waasisi wa TANU iliyopigwa tarehe 7 Julai, 1954 na mpiga picha maarufu wakati ule Gomez.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Hamza Azizi kuna kipindi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) na Mwl.Nyerere.Bila shaka ilikuwa ni kulipa fadhila kwa niaba ya Baba yake.Kwa cheo hiki alishindwaje kumtunza Baba yake?.

Dossa Aziz na Hamza ni watoto wa Aziz Ali.
Dossa mkubwa na Hamza ni mdogo.
 
Mohamed Said,

Unayo ile picha ya waasisi wa TANU iliyopigwa tarehe 7 Julai, 1954 na mpiga picha maarufu wakati ule Gomez.

.
Afj0YTQ35eu9AAAAAElFTkSuQmCC
 
Mohamed Said,

Rudia kuiweka vizuri hiyo picha haionekana au Mods watusaidie kuiweka vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Samahani kidogo Mzee Mohamed Said, naomba tujadiliane hili kwa faida ya wanajavi:

Unafahamu harakati za Mwalimu Nyerere akiwa mwanafunzi pale Chuo kikuu cha Makelele nchini Uganda?

Bada ya kuanza kufundisha pale Pugu sekondari jijini Dar harakati zake za ukombozi zilikuwaje mpaka kufikia uamuzi wa kuacha kazi yenye mshahara?

Habari za Nyerere za Makerere sizifahamu.

Uamuzi wa kuacha kazi ya kufundisha nafahamu kilichotokea.
Soma hapa chini niliyoandika katika kitabu cha Abdu Sykes:

Nyerere ambaye alikuwa akiogopa kuchukua uongozi wa TANU tangu 1953 alikuwa amefarajika sana na mshikamano huu ulioonyeshwa na wananchi.

Sasa ilikuwa dhahiri kwake kwamba rafiki yake Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na uongozi mzima wa TANU pamoja na lile Baraza la Wazee lilikuwa limemsafishia njia kuongoza harakati kwa niaba yao.

Lakini Padri Walsh na Wamishionari katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, walitazama harakati hizi kwa mtazamo mwingine kabisa. Wamishionari hawakuweza tena kumvumilia Nyerere kuwa mmoja wa walimu katika shule yao.

Hatima ile ile iliyowasibu wazalendo wengine kabla yake sasa ilimkabili Nyerere.

Aliambiwa ama abakie mtumishi mtiifu wa kanisa au ajiuzulu.

Kanisa halikuweza kukaa kimya na kumuangalia Nyerere akiwatumikia mabwana wawili.

Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU.

Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee.[1]

Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu.

Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi.

Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu.

Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena.

Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake.

Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley.

Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma.
 
Wanajamvi, hapo nyuma kidogo nimechokoza tu mjadala kwa kuuliza maswali mawili nayo ni;

  1. Naomba yeyote mwenye ufahamu anitajie kwa majina viongozi wakuu wa AA toka iundwe mwaka 1929 mpaka inabadilika na kuwa TAA na viongozi wakuu wa TANU toka iundwe mwaka 1954 mpaka tunapata uhuru mwaka 1961.
  2. Je hawa viongozi walipatikanaje...walichaguliwa ? Na kama walichaguliwa, sifa kuu zilikuwa zipi?
Kama kawaida bingwa wa hadithi anayejulikana kama Mohamed Said, haraka haraka, akadakia kwa kutoa majibu na nanukuu tu sehemu ya simulizi ambazo anadai alipewa na wazee wake wa Gerezani.

Mohamed Said said:
Nakuwekea hapa historia ya kuasisiwa AA kwa muhtsari kama nilivyoandika katika kitabu changu:

Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Kleist akiwa katibu muasisi...
Hilo hapo juu ndilo jibu la Mohamed Said kuhusu viongozi wakuu walioiongoza AA toka kuasisiwa kwake mwaka 1929 hadi ilipobadilika na kuwa TAA na badaye kuundwa TANU mwaka 1954. Kwa hilo jibu peke yake Mohamed Said anathibitisha hila zake za kichochezi na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika (na Zanzibar?) kama mtoa hii mada alivyoainisha.

Je ni kitu gani kimejificha katika hili jibu la Mohamed Said? Ukilisoma hili jibu kwa haraka haraka utadhani AA haikuwa na Kiongozi Mkuu. Kwa nini hataji kuwa AA ilikuwa na Raisi aliyeiongoza? AA haikuwa kikao kama cha wanywa kahawa ambapo watu wanapasishana kikombe bila kujali "protocol" yoyote. Je huyo Kleist anayetajwa mara mbili, ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa AA?

Mwalimu Cecil Matola, myao ambaye nyumbani kwake ndiko kulikofanyika mkutano wa kwanza wa TAA yeye akiwa ndiye Raisi wa kwanza, mbona anatajwa mwisho kama vile hana umuhimu wowote? Je baada ya kufariki kwake mwaka 1933, kwa nini AA ilizorota na hakuweza kupatikana kiongozi mwingine wa kuiongoza AA hadi alipoingia kijana msomi kutoka Makerere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Raisi wa kwanza wa TAA?

Dr. Kyaruzi aliiongoza TAA kwa miaka miwili hadi 1951 na hata alipohamishiwa mikoani na kushindwa kumudu kuiongoza TAA kwa nini hakupatikana Kiongozi mwingine hadi mwaka 1953 alipoingia kijana mwingine msomi kutoka Edinburgh, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere? Kwa nini wazee wa Mohamed ambao anadai ndio walikuwa vinara wa mwamko wasimchague mmoja wao kuwa Raisi?

Je ni kweli kuwa chombo cha kwanza kilichowaunganisha waafrika kilianzia Dar es Salaam? Vipi Msomi Martin Kayamba aliyeanzisha TTACSA (Tanganyika Territory African Civil Service Association) huko Tanga mwaka 1922? Je si kweli kuwa TAA iliasisiwa kwa kufuata unyayo na misingi iliyoanzishwa na TTACSA? Ni TTACSA iliyowawezesha wafanya kazi kukutana pamoja bila kubaguana kikabila, kirangi wala kidini.

Tuendelee na mjadala...
 
Mohamed Said,

Rudia kuiweka vizuri hiyo picha haionekana au Mods watusaidie kuiweka vizuri.

Picha ya Waasisi wa TANU ndiyo hiyo lakini hii imechakachuliwa.
Kisa chake nitakieleza Insha Allah siku nyingine.

Kassela Bantu amepachika picha yake kati ya Abdu na Chief Kunambi.

Hiyo ofisi ya TAA ndiyo hilo jengo lililojengwa na baba yake Abdu Sykes Mzee Kleist.

TANU FOUNDER MEMBERS 1954.jpg
 
Habari za Nyerere za Makerere sizifahamu.

Uamuzi wa kuacha kazi ya kufundisha nafahamu kilichotokea.
Soma hapa chini niliyoandika katika kitabu cha Abdu Sykes:

Nyerere ambaye alikuwa akiogopa kuchukua uongozi wa TANU tangu 1953 alikuwa amefarajika sana na mshikamano huu ulioonyeshwa na wananchi.

Sasa ilikuwa dhahiri kwake kwamba rafiki yake Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na uongozi mzima wa TANU pamoja na lile Baraza la Wazee lilikuwa limemsafishia njia kuongoza harakati kwa niaba yao.

Lakini Padri Walsh na Wamishionari katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, walitazama harakati hizi kwa mtazamo mwingine kabisa. Wamishionari hawakuweza tena kumvumilia Nyerere kuwa mmoja wa walimu katika shule yao.

Hatima ile ile iliyowasibu wazalendo wengine kabla yake sasa ilimkabili Nyerere.

Aliambiwa ama abakie mtumishi mtiifu wa kanisa au ajiuzulu.

Kanisa halikuweza kukaa kimya na kumuangalia Nyerere akiwatumikia mabwana wawili.

Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU.

Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee.[1]

Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu.

Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi.

Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu.

Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena.

Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake.

Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley.

Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma.

Asante sana kwa maelezo, japokuwa yanahitaji masahihisho ya dhana kwa ujumla!
 
Kitabu kimetoka na waandishi wake hawajasema kuna tatizo la upotoshaji.

  1. Uwezekano ni mdogo sana
  2. (a) Katika mambo ya hujuma shida kupata ushahidi isipokuwa watendaji wanakuwa hawafanyi kinachotakiwa.

(b) Sijui
(
3 (a) Sijui hilo swali wanaweza kujibu viongozi wa Waislam
(b) Sijui waulizwe viongozi wa Waislam

Dukuduku ni kwanza serikali ikubali lipo tatizo

Hayo mengine matatu ni Waislam wanyewe waseme uwiano nk.
Kitabu kuzuiwa hilo haliwekwi dhahir ila wanafunzi wa historia wanaambiwa hivyo

Naona ujanja wako ni kum frustrate mtu unapojibu hoja zake ili asikuulize tena. Jaribu kukaa chini basi ujibu kiutu uzima kama ulivyomuamba aandike maswali yake. Nimesikia uzee ukishika kasi saa nyingine akili zinakuwa kama za kitotokitoto hivi.
 
Back
Top Bottom