HOJA
Nimesoma maelezo ya Mohamed Said kuhusu Mshume Kiyate alivyomkirimu mwalim hadi kumpa pesa, chakula n.k.
Mohamed akaenda mbali zaidi na kusema Ditopile alipoelezea mchango wa Kiyate, Magazeti yalipotosha kwa kusema alimdhalilisha Nyerere kwa maneno ''kulishwa''. Hapa Mohamed anatuambia kuwa kuna kusoma habari na kupotosha habari kunakoweza kutokea. Fair enough!
Ukisoma maelezo ya vitabu tuhumiwa utaona kilichotokea ni kuchukua baadhi ya mistari na kupoteza dhana nzima.
Sina maana kila kinachosemwa hakikuandikwa, ninamaanisha kuwa kuna sehemu imechukuliwa sentensi tu na kuacha maudhui ya aya nzima.
Swali 1: Je, vitabu vya Bergen na Silvalon haviwezi kuwa vimefanyiwa upotoshaji kama ule uliofanywa kwa Ditopile?
HOJA
Ukisoma majibu kwa Yericko Nyerere kuhusu Mshume Kiyate, Mohamed ameelekeza tuhuma zake kwa Nyerere hasa pale anapodai kuwa kulikuwa na zipo hujuma za jina lake kutopewa mtaa. Kwamba Nyerere alifanya hivyo kama sehemu ya dharau na chuki kwa wazee wake.
Tangu Uhuru, madiwani wa jiji la Dar es Salaam kwa asilimia zaidi ya 80 hadi sasa ni Waislam wakiongozwa na Mameya Waislam tena wazee wake akina Kitwana Kondo, Sykes, Abouu n.k.
Swali 2:
a) Kuna ushahidi gani kuwa madiwani, mameya na viongozi wengine wa jiji walipigwa marufuku kutoa jina la mtaa wa Mshume Kiyate
b) Je, aliyebadilisha jina la bara bara kama UWT/Bibi titi ni Nyerere au ni madiwani wa jiji
c)Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani?
HOJA
Mambo yote yaliyotokea kati ya 1954 hadi 1985 yalimhusu Nyerere kama mtu.
Leo Mohamed anasema serikali ikae na Waislam iongee nao kuhusu tatizo.
Swali 3
a) Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali?
b)Mbona yaliyotokea nyuma hayatajwi kama ni matatizo ya serikali yanasemwa ni ya Nyerere na kwanini leo hayasemwi kama ya Kikweteyanasemwa kuwa ni ya serikali?
HOJA
Mohamed amekuwa analalmika dhidi ya dhulma kwa wazee wake na Waislam
Swali
a)Kwa vile tunatafuta muafaka wa kitaifa, yeye ana maoni yapi kuhusu suluhu ya duku duku hilo.
Nini suluhisho ili kuondoa dhulma anayoidai.Nini kifanyike
(i) katika kuleta uwiano wa madaraka
ii)uwiano wa elimu
iii) n.k.
HOJA
Mohamed ametoa madai kitabu cha Bergen kimepigwa marufuku kama kilivyopigwa marufuku kitabu chake kule UDSM
Swali 4
a)Kitabu cha Bergen Kimepigwa marufuku kwa tamko la nan na lini!
b) Kitabu cha Mohamed kilichozuiliwa kuwa reference UDSM, ni kwa tamko la nani na lilitoka lini