1974 Nimewawekea bandiko zima Sivalon anasema Kanisa Katoliki linautizama Uislam kama adui. Wamemkana Sivalon.Nimeweka taarifa kadhaa. Wanataka ushahidi wa kimahakama....
Mohamed, katika uandishi unachekesha sana! Swali lilikuwa kwamba umetoa madai mazito ya Kanisa na Nyerere kuhusika na kifo cha EAMWS. Umekuwa unajinasibu kufanya utafiti katika kitabu chako. Kama ni hivyo utafiti wako umekuja na vithibitisho gani au logic gani za kuonyesha kuwa Kanisa lilihusika na kifo cha EAMWS?
Unapo quote mtu ukasema huo ni ushahidi ni soni na aibu kwa mwandishi wa miahadhara huko Harvard na Cambridge.
Nakuhakikishia wangelijua unachokifanya ni hicho na unaita utafiti huenda wangepiga na maganda ya mayai wanayokulisha usoni.
Mohamed hili usizilizungumzie tena maana tulikaa kimya tukusitiri naona umeamua kuvua hata ile iliyobaki.
Huna ushahidi wa uthibitisho wa kuaminika au kimazingira kuhusu kifo cha EAMWS.
Umeshindwa kuthibitisha kama ambavyo tulikuomba uthibitishe kuwa namba za mitihani zilianza kutumika wakati wa Profesa Malima, huweza na hadi leo kimyaa! hufunguwi kinywa kueneza upuuzi huo tena. Kama si upuuzi nithibitishie!
Umeshindwa kuthibitisha kuwa Abdul Sykes alimfundisha Nyerere siasa! Ushahidi wa maandiko yako umekusuta mchana kweupe! Mohamed, Moddy, MO! please
Umeshindwa kutuambia Nyerere alipotoa picha kwa Malima nini kiliendelea! huna jibu.
Unataka tuamini pale unapotaka wewe. Hilo si kwa wenye akili! never
Umeshindwa kuthibitisha kuwa Nyerere alikuwa anatembea kifua wazi hadi alipopewa suruali na wazee wako.
Tumekuuliza maswali unakimbia unasema hilo tuliache, hilo sina ujuzi nalo n.k.
Wewe unataka kusikilizwa tu ili ueneze chuki na husda!
Unafundisha jamii ulalamishi na wala huionyeshi njia.
Leo vijana wanakwenda kusikiliza kesi za Ponda badala ya kusoma Chemistry bado unatumaini utavunja daraja la udhalili.
Leo huwaambii watoto Kinondoni, masjid Quba, Thaqafa n.k. waache uhuni unawaambia NECTA inawaonea
Leo hujiulizi kwanini FEZA ni tofauti na Jabal Hilal, unatafuta mchawi NECTA
Leo, hujiulizi Ponda na BAKWATA wangombea nini unabaki kuwaaminisha kuhusu ngano ya EAMWS mwaka 1968
Leo tunakuuliza utupe nchi moja tu iliyojenga chuo kikuu wakati huo na sasa ni tofauti huna jibu.
Badala ya kufundisha jamii ijitambue, ione wapi wamejikwaa, ijifunze kutoka kwa wengine unashinda kutwa nzima ukiijaza uzushi na uongo kwa kutumia majina ya marehem na Nyakati ukiita historia.
Leo badala ya kuwaambi Kilwa wapeleke watoto shule, unaungana na sheikh Ilunga kuchochea mauaji ya maaskofu na mapadre!
Mohamed, MO! Uislam hausimami katika uzushi, uongo, fitna na mjungu.
Uislam ni ukweli amani na salama.
Muogope mola wako!