Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rudia tena kuipost mkuu
tangu mjadala huu umeanza hujatoa hoja hata moja zaidi ya kubwabwaja ujinga wa kumuunga mkono huyo mzee wako muovu na zandiki mohamed saidi. Uovu wenu hautaleta tija yoyote katika nchi hii!
Naam huu ndio ujinga uliotamalaki ndani ya bichwa lako tupu!unataka hoja gani zaid ya hizo anazotoa ndugu yetu moh said??wewe umetoa hoja gani ya maana zaid ya matusi na kashfa dhidi ya waislam na moh said?
Hizi hasira na ghazabu zako ni ishara tosha ya kuumwa kwako kwa fikra na machungu ya kuumbuliwa na kuwekwa wazi kwa hii historia fichwa,
ndugu moh said namfananisha kama na simba dume mkali anaeng'ata kwa hoja.,amejitosheleza kila kona,hana hasira,hana jazba wala ghazabu,ama kwa hakika mmeshikwa pabaya safari hii.
naam huu ndio ujinga uliotamalaki ndani ya bichwa lako tupu!
Ajabu! na wewe chandimu unajiita mtu mzima? ebu ondoa uvundo wako hapa!unge-log out kwenye mjadala huu ungekuwa umefanya jambo la manufaa sana kuliko kutuongezea comments zisizo na tija,kwani umekosa la kufanya?
Watu wazima wanaongea mambo ya msingi humu ndani,hebu tuondolee vurugu zako.
Unafikiri wakati wote huu nilikuwa nikikufahamu wewe kama Mdanish?Nitashiriki kuandika historia ya nchi yangu kama mtanzania, hivyo nifahamu kama mtanzania.
Unataka kuandika Historia inayowahusu watu zaidi ya milioni 45 halafu huoni sababu ya msingi kujulikana wasifu wako mwandishi?!Yericko Nyerere said:Ikiwa kutakuwa na sababu za msingi za taifa kutujua wasifu wawashiriki wa uandishi huo basi itakuwa fursa kwako kunijua ndugu yangu
![]()
Safari ya UNO.
Mzee Mohamed,
Pengine unadhani uko daraja la peke yako katika kuifahamu historia ya nchi hii kwa kuwa tu wengine hatujaandika simulizi za wazee wetu tukaziegesha kwenye DINI zao. Unakosea sana. Huku kujikweza huku hata Mtume Mohamad (S.A.W) alikukataa sana asije akawa kama Issa bin Mariam.
Wewe Tanganyika unayoifahamu ni Kariakoo na sehemu chache za Wazee wako hawa. Historia unayoifahamu ni hii inayowazunguka wazee wako hawa. Sijui na wala sina hakika kama unamfahamu Mwalimu kuliko wale wazee wa MNF akina Butiko, SAS au akina Issa Shivji wa Kigoda cha Mwalimu.
Kaa utulie tukuwekee sawa historia ya nchi hii ambayo haitakuwa na UDINI kama hii ya kwako. Kaa utulie tukutafutie historia moja ya nchi hii ambayo wazee wako waliitengeneza kwa umoja wao bila kuingiza DINI na MAKABILA yao.
Mwalimu kaacha hotuba nzuri na nyingi sana zinaeleza kwa ufasaha tulikotoka. Hakuingia kichwakichwa kwenye harakati za kudai uhuru wa nchi hii. Aliingia kule kama msomi aliyekuwa amekamilika na M.A yake . Sielewi ni wangapi wakati ule ndani ya TAA na baadae TANU walikuwa na kiwango hiki cha ELIMU au sawa na hiki.
WC,
Umesema kweli.
Mimi historia ninayoifahamu kwa hakika kabisa ni hii ya wazee wangu hapo Kariakoo.
Hili umesema kweli kabisa.
Kwa kweli huwa nawaambia rafiki zangu kuwa dunia yangu ilikuwa pale Livingstone na Kipata kwa Bi Mkubwa wangu, kisha kwetu Kipata huku Swahili huku Nyamwezi basi.
Sikuwa najua nini kinatendeka nje ya hapo hadi nilipoanza shule darasa la kwanza.
Ni kweli Nyerere mimi simjui kama wanavyomjua akina Shivji, Butiku nk.
Lakini ukiniuliza chochote kuhusu Mzee OmariLondo, Saleh Muhsin, Abdu Sykes, Sheikh Hassan bin Amir, Titi Mohamed, Hawa biti Maftah, Bantu Group, TANU yenyewe, Rashid Sisso nitakupa habari.
Nyerere ni kweli aliwapita wenzake takriban wote kwa elimu.
Ila Nyerere hakuasisi TANU.
Ni hilo tunalogombania.
Mkuu Nguruvi3, kiukweli namheshimu sana Maalim Mohamed Said kwa kuwa ni great "orator" ila siku zote nimekuwa nikumuita ni "a man with a mission", tukishaisikia audio, kama ni kweli Nyerere aliyatamka maneno hayo, then nitaamini moja kwa moja kuwa MS had ill motives na nikamshauri kama aliteleza, atubu akingali hai kwa kitendo sio tuu cha kumzushia marehemu, bali kumsingizia uwongo, ni dhambi kubwa hapa dunuani na ahera!.
Kwa vile kitabu kiko published kwa miaka 15 sasa na kinasomwa kote, its about time ukweli halisi uandikiwe kitabu na kum denounce rasm Maalim Mahamed Said kama muongo, mzushi na mpotoshaji!, na hiyo truth ipelekwe kule kule alikopeleka uwongo na uzushi wake ili uwe scraped off toka katika literacy books!.
Pasco.
Ritz,
Ahsante sana kwa picha hii adhim.
Kutoka kushoto: Wa kwanza na wa pili siwafahamu.
Watatu Robert Makange, wanne aliyavaa tai Zuberi Mtemvu, wanne aliyavaa kanzu koti na tarbush Idd Faiz Mafongo (Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU), watano Julius Nyerere, wasita John Rupia, wasaba Bibi Titi Mohamed wanamsindikiza Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa (UNO) 1955.
Hii leo hakuna mtu anaemjua Idd Faiz Mafongo wala machango wake katika safari ya Nyerere UNO haijathaminiwa wala jasho alotowa katikakuijenga TANU hadi uhuru ukapatikana.
Idd Faiz ndiye alikabidhiwa jukumu la kutafuta fedha za kumpeleka Nyerere UNO kazi ambayo aliitimiza kwa ufanisi mkubwa.
Nawawekea wanaukumbi maelezo mafupi ya Idd Faiz Mafongo muamuwe wenyewe:
Idd Faiz the TANU treasurer died on 9th January, 1987, at the age of 75.
In 1959 he was elected TANU National Treasurer while serving as member of TANU National Executive Committee.
It was because of his honesty and diligence that he was nominated to manage TANU funds which became enormous, as independence was approaching.
Idd Faiz died a poor disillusioned man.
In his last days after retirement from TANU Press he used to spend most of his time reading the Holy Qur'an.
Upon his death, Mzalendo, the Party Sunday paper published by the firm which he helped to form and owned by the Party he helped to build, announced his death two days after his funeral.
The small article in the paper reported the death of a former employee of the printing company completely obscuring his political career.
At his funeral the Party was not represented.
What befell Abdulwahid befell Idd Faiz Mafongo; and what a coincidence, both had been leaders in Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika and TANU; and both of them had once been close to Nyerere.
Father James Lynch, the founder of St. Francis College, died in Britain only a few days before Faiz.
His death was announced by both the Party daily Uhuru (8 th January, 1987) and the government owned paper, the Daily News (8 th January, 1987).
The two papers highlighted his contribution to education to colonial Tanganyika.
Faiz, who founded TANU, supported Nyerere and fought for Tanganyika's independence, met his death in his humble house at Magomeni and not even the Party which he built, nor the government which he had helped to establish, were aware of his passing away.
Ajabu! na wewe chandimu unajiita mtu mzima? ebu ondoa uvundo wako hapa!
Mohamed Said,
Umetupa habari nzito kuhusu huyu mzee Mzalendo Idd Faiz Mafongo.
Hao wazee wamepambana siku nyingi lakini historia imewatupa mkono.
Yericko, aliandika humu kuwa mchango mkubwa wa pesa alitoa Maliale, Nyerere kwenda UNO Bahati mbaya huyu mzee Idd Faiz Mafongo hajawahi kumsikia wala hajui mchango wake kwenye harakati za kupigania uhuru. Hii picha muhimu sana.
Mbaya zaidi akijitokeza mtu akawaelezea watanzania mchango wao anaonekana anamkejeli Nyerere.
Thanks for the information.
Naihurumia jamii ambayo imelishwa hizi ngano za Mohamed Said kwa muda wa miaka 15 na yenyewe ikapokea hizo ngano kama zilivyo. Huyu mtu hana nukuu yoyote iwe ya John Sivalon, Andulwahid Sykes wala hiyo listi ndeeefu ya anaowaita wazee wake. Anayotetea yeye ni mawazo yake aliyokaa akayatunga kwa malengo maalum hasa pale alipowasoma aliowakusudia na kutambua mapema kuwa watayapokea mazima mazima bila hata kujiuliza.
Nina wasi wasi na hizo anazozitaja kama nyaraka za Abdulwahid Sykes kama zipo na anazinukuu kama zilivyo, watu wa aina yake ndivyo walivyo, wachochezi. Nikitoa mfano ameombwa alete nukuu ya kitabu cha Sivalon kama kilivyo kuthibitisha maneno anayodai kuyasoma humo lakini kashindwa...kama kawaida ya mbea amebakia kujiuma. Kama tusingepata hiyo hotuba ya Nyerere ambayo imemuumbua mchana kweupee, bado angekazania tu uongo wake kuwa Mwalimu hakuwataja wazee wake.
Kuhusu nyaraka za hao wazee wa Mohamed Said ambazo anadai anazo, hata siku moja hajawahi kuzitoa popote pale, ziko tu kichwani kwake na hakuna mtu amewahi kumdai sauti wala video kuzithibitisha. Uwezekano mkubwa upo kuwa aliziandika yeye mwenyewe na kwa njia aliyotaka. Yeye leo pamoja na kutolewa hotuba ya Mwalimu kwa Wazee wake bado anadai uthibitisho wa sauti na ikiwezekana video. Sasa na mimi leo namwomba na yeye atuletee hapa sauti za wazee wake wakisema na kutenda anayodai Mohamed Said.
Sasa maajabu ya hawa wazee wa Mohamed Said! Sisi tukiongelea wazee wetu Watanganyika wa sehemu zote kusini hadi kaskazini, magharibi hadi mashariki, yeye amekazania wazee wake wa Gerezani Dar es Salaam (ukanda), tukiwataja wazee wetu Watanganyika wa makabila yote makubwa kwa madogo, yeye amekazania wazee wake Manyema na Wazulu (ukabila) na tukiwaenzi wazee wetu Watanganyika wa dini zote pamoja na wasio na dini, yeye amekazania wazee wake wa Kiislaam (udini).
Mwisho nina ombi kwa jukwaa (hii ni JF)...imeonekana kitabu/vitabu alivyoandika Mohamed Said havina ukweli na kama upo ni asilimia kidogo sana, sasa tusiishie hapa...tuende next step...wapotoshaji kama yeye adhabu yao ipo. Their works have to be discredited as academic dishonesty...a deliberate attempt to falsify, fabricate data, records, or information. Taasisi, Waandishi na wachapishaji wote aliowawekea maneno mdomoni kwa nukuu zisizo sahihi, juhudi zifanyike wajulishwe hatua ziweze kuchukuliwa. Nawapa changamoto wana JF.