Hizi ni dalili za kuishiwa hoja.
Nakushauri tu huu uzi unasomwa na watu 21,000.
Ficha Upumbuvu wako onyesha Hekima zako.
Zaidi ya apo utakuwa unawatukanisha wazazi wako...ni hiara yako kufuata au kupuuza.
Ritz,
Nilipokuwa mtoto wa miaka 12 nilijaribu masumbwi ''boxing.''
Ulingo ulikuwa unafungwa pale Mtaa wa Msimbazi na Aggrey
sasa Lindi.
Aliyekuwa akituingiza kupigana kijana mmoja akiitwa Hassan
Makwasukwasu.
Yeye kwa umri alikuwa katuzidi sisi ''mabondia'' wake.
Sikuziweza ngumi.
Kipaji changu kilikuwa kwenye mpira.
Nikarudi Makunguru kucheza mpira ni hapo hapo Msimbazi
kama unaelekea siku zile DMT baadae UDA Pugu Road sasa
Nyerere Road.
Hata hivyo nikampenda Cassius Clay kisha Muhammed Ali.
Ali katika biography yake ''The Greatest'' anasema baada ya
kutoka kifungoni aliponyang'anywa leseni ya kupigana na kurudi
tena ulingoni kuna kitu cha ajabu sana kilimjia katika hali yake.
Nacho ni huruma wakati anapombana na bondia ambaye yeye
anajua wazi hana uwezo wa kupigana na yeye.
Anasema kabla ya hapo yeye alikua yoyote aliye mbele yake
katika ulingo lazima apewe kipigo.
Hali ile ya Ali na mimi imeshanifika.
Hakika sijisikii raha kupambana na hawa jamaa zangu humu.
Hili nalisema kwa dhati ya nafsi yangu.
Huruma na simanzi imeniingia moyoni.