Incredibo aly
Member
- Nov 24, 2010
- 48
- 1
Naihurumia jamii ambayo imelishwa hizi ngano za Mohamed Said kwa muda wa miaka 15 na yenyewe ikapokea hizo ngano kama zilivyo. Huyu mtu hana nukuu yoyote iwe ya John Sivalon, Andulwahid Sykes wala hiyo listi ndeeefu ya anaowaita wazee wake. Anayotetea yeye ni mawazo yake aliyokaa akayatunga kwa malengo maalum hasa pale alipowasoma aliowakusudia na kutambua mapema kuwa watayapokea mazima mazima bila hata kujiuliza.
Nina wasi wasi na hizo anazozitaja kama nyaraka za Abdulwahid Sykes kama zipo na anazinukuu kama zilivyo, watu wa aina yake ndivyo walivyo, wachochezi. Nikitoa mfano ameombwa alete nukuu ya kitabu cha Sivalon kama kilivyo kuthibitisha maneno anayodai kuyasoma humo lakini kashindwa...kama kawaida ya mbea amebakia kujiuma. Kama tusingepata hiyo hotuba ya Nyerere ambayo imemuumbua mchana kweupee, bado angekazania tu uongo wake kuwa Mwalimu hakuwataja wazee wake.
Kuhusu nyaraka za hao wazee wa Mohamed Said ambazo anadai anazo, hata siku moja hajawahi kuzitoa popote pale, ziko tu kichwani kwake na hakuna mtu amewahi kumdai sauti wala video kuzithibitisha. Uwezekano mkubwa upo kuwa aliziandika yeye mwenyewe na kwa njia aliyotaka. Yeye leo pamoja na kutolewa hotuba ya Mwalimu kwa Wazee wake bado anadai uthibitisho wa sauti na ikiwezekana video. Sasa na mimi leo namwomba na yeye atuletee hapa sauti za wazee wake wakisema na kutenda anayodai Mohamed Said.
Sasa maajabu ya hawa wazee wa Mohamed Said! Sisi tukiongelea wazee wetu Watanganyika wa sehemu zote kusini hadi kaskazini, magharibi hadi mashariki, yeye amekazania wazee wake wa Gerezani Dar es Salaam (ukanda), tukiwataja wazee wetu Watanganyika wa makabila yote makubwa kwa madogo, yeye amekazania wazee wake Manyema na Wazulu (ukabila) na tukiwaenzi wazee wetu Watanganyika wa dini zote pamoja na wasio na dini, yeye amekazania wazee wake wa Kiislaam (udini).
Mwisho nina ombi kwa jukwaa (hii ni JF)...imeonekana kitabu/vitabu alivyoandika Mohamed Said havina ukweli na kama upo ni asilimia kidogo sana, sasa tusiishie hapa...tuende next step...wapotoshaji kama yeye adhabu yao ipo. Their works have to be discredited as academic dishonesty...a deliberate attempt to falsify, fabricate data, records, or information. Taasisi, Waandishi na wachapishaji wote aliowawekea maneno mdomoni kwa nukuu zisizo sahihi, juhudi zifanyike wajulishwe hatua ziweze kuchukuliwa. Nawapa changamoto wana JF.
kanawe miguu ulale hoja yako nyepesi sana au izo post za juu hujaziangalia,, kwanza uko form ngapi?