Sasa hapa ndio ukweli wa kwanini kazi yako huwezi KABISA kuiita ni kazi ya kihistoria. Katika uandishi wa historia kuna kitu kinaitwa "historical method" yaani namna ya kuandika au kusimulia tukio la kihistoria. Hii ni tofauti na mtu anapofanya kile kinachojulikana kama "scientific method". Sasa historical method kwa mujibu wa Wikipedia (unaweza kupata sources nyingine nzuri zaidi) ni:
comprises the techniques and guidelines by which historians use primary sources and other evidence to research and then to write histories in the form of accounts of the past.
Sasa, mwandishi wa historia anatakiwa aende karibu zaidi na primary sources kabla ya kwenda kwenye secondary sources. Unapoenda kwenye primary sources you are close to credibility of your information kuliko kwenda kwenye secondary or tertiary sources.
Sasa what constitutes a primary source? hiyo hiyo Wikipedia inaeleza hivi na kutoa mfano:
Primary sources are original materials.[SUP][1][/SUP] Information for which the writer has no personal knowledge is not primary, although it may be used by historians in the absence of a primary source. na inaendelea na kusema
In the study of history as an academic discipline, a primary source (also called original source or evidence) is an artifact, a document, a recording, or other source of information that was created at the time under study.
Bahati mbaya sana katika maandishi yako unawataka wasomaji wako waamini kuwa documents ulizoziona wewe ndivyo zilivyo! Unasema ulioneshwa barua na familia ya Sykes na watu wengine lakini kwenye kitabu chako hujathubutu kuweka hata moja hadharani. Umedai kuwa Nyerere alidai kuwa hakufahamu cheo cha Abdul wakati anajiunga TAA lakini hujathubutu kuweka sehemu ya hotuba hiyo (unawataka wasomaji wakatafute TBC).
Sasa mzee mwenzangu hiyo siyo historia ndio maana nimeiita 'histohisia' yaani unaandika historia kwa kuongozwa na hisia. Historia ni taalum ambayo ina kanuni zake na misingi yake. Kuandika mambo yaliyotokea huko nyuma na ukayaelezwa kwa kirefu haitoshi kufanya historia. HIstoria ni pale ambapo unaweza kuonesha ushahidi wa kile kilichotokea kwa kutumia vyanzo vya msingi (primary sources).
Hili si kweli; kazi ya kusomi ili iweze kukosolewa kisomi inahitaji kuandikwa kisomi vile vile. Na ili iandikiwe kisomi ni lazima basi ifuate kanuni za taalum. Ya kwako siyo kazi ya kihistoria kwa hiyo ukosoaji wowote utakuwa ni kama huu unaofanyika ambao kwa kweli ni ukosoaji wa fasihi (literature review/criticism). Kwa sababu tayari tumeonesha kwa muda mrefu sasa kuwa kazi yako siyo ya kisomi na haifuati misingi ya uandishi wa kihistoria kilichobakia ni kukosoa uandishi wako tu kama kazi ya fasihi.
Randal Saldeir anaandika kwa kirefu juu ya kitabu chako -
UNAWEZA KUSOMA KWA KIREFU HAPA - na anakutana na matatizo haya. Yeye anaeleza hivi katika review yake:
Lakini unaweza kusema huyu mtu aliwajua vipi: Well aliishi Tanganyika/Tanzania kuanzia 1943 hadi 1973 na anajielezea hivi kwenye hiyo review:
Huyu bwana tungeweza kumuita kwa uhakika kabisa kuwa ni "primary source" na maneno yake ni mazito. Katika hitimisho lake anasema hivi:
Sasa huyu mzee wakati anaandika review hii ilikuwa ni 1999 naamini ilikuwa ni baada ya toleo lako la kwanza; anasema hujaweza kumshawishi kuwa Nyerere alikuwa na chuki dhidi ya Waislamu au serikali na kanisa vilikuwa na njama dhidi ya Uislamu. Anasema case not proven! Na anasema akiwa mtu aliyeishi na kuwafahamu karibu wahusika wote wakuu wa kitabu chako. Sisi leo tunapohoji haya haya tunaangalia methodology uliyotumia ndio maana tunakukatalia kwua siyo kitabu cha historia. Ulichoandika huwezi kupeleka kwenye mahakama ya watu na ukawashawishi kwani kote wataulize 'show us your evidence"... so far you have failed miserably!