Pasco
Pole sana kwa kukwazika..Ila nadhani ambaye alipaswa kukwazika zaidi alikuwa ni Mzee Nyerere..yeye kwenye kitabu kile ametajwa kwa jina na yooote aliyoyafanya yamaorodheshwa. Haya yalifanyika yeye akiwa hai. Sasa wewe Paco, kaka yangu Mgosi Nguruvi3, Mzee wa Uhamishoni Mwanakijiji, Yericko n.k.n.k ...hivi mtakuwa na ukweli upi kumshinda mwalimu Nyerere..au unataka kufurahisha baraza tu kaka?Kikwebo.
Siyo Nyerere tu, Abdul Sykes alifariki bila kusema neno hadi anaingia kaburini kwa mujibu wa Mohamed.
Lakini lazima ia utambue kuwa Nyerere na Mohamed Said ni vitu viwili tofauti. Nyerere alisimama katika utaifa na ni mwanadiplomasia, ndugu yangu Mohamed yeye ni mchochezi, mzushi na muongo.
Ingekuwa jambo la kusikitisha sana endapo Nyerere angesimama kumjibu Mohamed.
Nikupe mfano mzuri utakaokupa picha Mohamed ni wa daraja gani.
Siku zote amekuwa anasema 'wazee wake'' akimaanisha wazee wa kiislam.
Katika hotuba ya kuwaaga wazee Nyerere alitumia neno wazee wa Dar es Salaam.
Nyerere alisema hayo kwasababu wazee ni pamoja na wale waliomsomea dua na wale waliofanya matambiko.
Kuna vitu viwili hapo, waliomsomea dua na waliofanya matambiko.
Kwahiyo Nyerere alitambua kuwa kutumia neno waislam kunaweza kutoeleweka kwa baadhi (kama Mohamed) na hivyo kuwadhalilisha wazee wa kiislam waliofanya dua na wasioamini tambiko, au wazee wa jadi waliofanya tambiko lakini si waumini.
Kwa msingi huo Nyerere anawaita wazee wangu ili kuwalindia heshima zao, Mohamed anawaita na kuwavunjia heshima bila kudhamiria au kwa kutojua tu
Kwa upande mwingine Mohamed anawaita wazee kama waislam. Hilo halina tabu, tatizo ni kuwa inapofika mahali pa tambiko tayari amewashawaondoa wote katika Uislam kwa vile dini ya Uislam hairuhusu tambiko za jadi.
Kw vile anaongozwa na ushabiki, mara nyingi hujifunga magoli yasiyo ya lazima na hata kuiweka jamii wakati mgumu.
Sasa huyu ndiye alihitaji kujibiwa na Nyerere! real! Mo!
Mody Said Salum Abdallah Myukwa Mwekapopo Samtungo, tete a tete with Nyerere! real!