Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Unajua maana halisi ya KIZAZI cha NYOKA?

Uliza mkuu usikimbilie kulaumu tu!

Kizazi cha nyoka ni binadamu wote wakizazi baada ya Eva/Hawa kula Tunda la mti wa mema na mabaya!

Hivyo mimi, wewe na yule ni kizazi cha nyoka.

Mkuu unajitahidi sana kumtetea Nyerere lkn mbaya zaidi huna USHAHIDI wowote unaoutoa ktk Maelezo yako, nakuomba nikuulize kitu kile chama chenu cha CATHOLIC OLD BOYS ASSOCIATION (COBA) BADO KIPO???
 
Na mika 25kabla ya uhuru mambo yalikuaje?

Tulikuwa nchi ya kwanza duniani kusafirisha baadhi ya mazao ya kilimo Mkonge, Korosho, tulikuwa nchi ya kwanza Afrika katika kusafirisha mazao ya kilimo, baada ya kuingia "janga" kwa miaka 7 tu, tukawa nchi ya kwanza duniani kwa kuomba chakula cha msaada na tukawa masikini wa mwisho duniani na tukaendelea kuwa hivyo kwa miaka 40. Soma.
 
But thats what you did sir... you accuses others of doing what you yourself are doing... incredible double standard.

Hata mpande mshuke, Mohamed Said kaandika kuhusu Waislaam walivyokuwa mstari wa mbele na walivyoasisi kupigania uhuru wa Tanganyika.

Jee, unaweza tuambia nyumba ilipozaliwa TANU ilikuwa ya nani?
 
mimi naomba uniwekee kitabu kilichowataja Mzee Waikela, Sheikh Hassan Bin Amir, Sheikh Nurdin Hussein and Sheikh Abdallah Chaurembo,Jaffari Idd, Ramadhani Abdallah Singo, G. B. Somji, Elias Kissenge, Julius Mwakasanyangi, Idd Tosiri, Hadari Mwinyimvua, Idd Tulio.n.k

Hakujibu hilo, anajuwa atamtaja mbaya wao!
 
Umeona kumbe mzee huyu anaugomvi na waandishi wa chuo cha Kivukoni, sasa kaamua kuliangamiza taifa kwa uzushi wake!

Na nyinyi mna ugomvi na Mohamed said kwa kuuonesha ulimwengu ukweli wa wapigania Uhuru wa Tanganyika.
 
hata mpande mshuke, mohamed said kaandika kuhusu waislaam walivyokuwa mstari wa mbele na walivyoasisi kupigania uhuru wa tanganyika.

Jee, unaweza tuambia nyumba ilipozaliwa tanu ilikuwa ya nani?

good question zomba,
good question,,

huyo mzee mwanakiji na hulka zake za kidini kwa hakika hawezi kulijibu hilo abadan asilani...!
 
Tulikuwa nchi ya kwanza duniani kusafirisha baadhi ya mazao ya kilimo Mkonge, Korosho, tulikuwa nchi ya kwanza Afrika katika kusafirisha mazao ya kilimo, baada ya kuingia "janga" kwa miaka 7 tu, tukawa nchi ya kwanza duniani kwa kuomba chakula cha msaada na tukawa masikini wa mwisho duniani na tukaendelea kuwa hivyo kwa miaka 40. Soma.
Na sasa tupo wangapi?
 
Hiyo ni name calling and I hope Moderator analiona hilo na atatimiza wajibu wake.

Nyerere si muasisi wa kupigania uhuru tanganyika, alipopokelewa na kina Sykes na kuwekwa nyumbani kwao, tayari harakati zilishaanza, au hilo linakupa shida?

Ni nani ambae amemfanya kuwa nyerere ndio pekee mpiganiaji uhuru kwenye historia? jiulize. Msome kidogo Mohamed Said anasemaje hapa ili ujijuwe kuwa wewe, kama wenzako, ni wazushi tu:
Mkuu Zomba, I am realy sorry, it was typically a typing error, it was not my intention to distort your name! Back to the debate, i don't take Mohamed Saidi's stories to be authentic source of historical facts, what he has done is to put his historical opinions into writings he calls history of his 'wazee'.
 
Japo mnakasha umefungwa lakin nilitaka niweke sawa maneno yako niliyo BLUE.
Mkandara

Kama umesoma vizuri Qur'an au Uislam kijumla utagundua kuwa kuna waislam na waumini (walioamini) ambao wamebainishwa wazi wazi. Utagundua kuwa hao wote uliobainisha juu ni waislam na wana haki kabisa ya kujinasibu kwa nasaba, mavazi na mengine yote kama ulivyobainisha kuwa ni WAISLAM, lakin waumini nao wamebainishwa katika mambo maalum. Mfano suala la kufunga ramadhwani, hapa hawakutajwa waislam bali wametajwa WAUMIN ndio waliofaradhwishiwa kufunga wmezi wa ramadhwani. na kama unazitaka swifa za waumini zimebainishwa katika Surat Al baqara 2:4 -7.

Lakin siku zote ukweli unasimama na uongo unajitenga kwani hata siku moja Batwil haiwezi kuishinda haki.

Ahsantum Al Akhiy Mohamed Said kwa kutubainishia haki dhidi ya Batwil. Alllah akuzidishie zaidi na zaidi katika umri, hekima, busara , Ilmu ili uweze toa darsa muruwa kama hili.
Mkuu wangu umezungumzia Surat Baqara, unajua ilishuka kwa sababu gani? unajua maana ya neno Baqara! hadi ukalijengea hoja kuwa ndio waumini?. ( Mfano suala la kufunga ramadhwani, hapa hawakutajwa waislam bali wametajwa WAUMIN ndio waliofaradhwishiwa kufunga wmezi wa ramadhwani.) Tafadhali ikiwa hujui jambo ni bora ukae kimya...
- Unawezaje kuwa Muislaam pasipo kuwa muumini?..
 
Mkuu Zomba, I am realy sorry, it was typically a typing error, it was not my intention to distort your name! Back to the debate, i don't take Mohamed Saidi's stories to be authentic source of historical facts, what he has done is to put his historical opinions into writings he calls history of his 'wazee'.

Mention a single thing that Mohamed Said wrote about his "wazee" which is not a fact.
 
Yani nyie mna ndoto za kuona Abdul Sykes ana beba nembo ya uasisi?

Hilo halitatoke kamwe katika ardhi hii ya Tanganyika/Tanzania!

Tangu aliposhindwa uchaguzi wa Urais wa TAA pale Anartogulo Mnazi mmoja mwaka 1953 chini ya Jemadari na mwanazuoni mbobevu Julius Kambarage Nyerere, nyota ya Abdul Sykes kuwa kiongozi wa uasisi iliyeyuka na kuwa sehemu tu ya waasisi wa Taifa leytu!

Hilo litasimama wima daima, Historia ipo na haitabadilika kwa NGANO za Maulamaa kama Mohamed na wafia dini wengine!

Nawashauri wajikite zaidi kutafiti mambo ya kiroho waache kulivuruga taifa!
 
Kimsingi mimi na wengine tunaozipinga ngano zako kuzihalalisha kuwa histori ya watanganyika hatuna shida ya video au audio ya hotuba hiyo ya Mtakafu Julius Nyerere,

Wenye hofu ni wewe na wenzio ndio mlistahili kuja na audio ama video kuipinga hiyo hotuba niliyoiweka hapo juu!

Mimi na wenzangu tumeridhika kuwa hotuba hiyo ni sahihi, na iimefuta uongo wako kuwa Mwalimu alisema hamfahamu/hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na CHEO gani, kumbe mwalimu alisema wazi kuwa alikuwa katibu wa TAA.

Kwanza lete hapa hiyo hotuba uliyoinukuu kuwa mwalimu alisema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo gani, hiyo itasaidia kuipinga hotuba niliyoiweka pale juu, kisha nitaleta AUDIO kuthibitisha ZAIDI uongo na uchochezi wako mzee wewe!
Nyerere this is not fair!
Ni wewe uliyesema utaleta audio jumatatu.
Tukasubiri kwa hamu mpaka leo hujaileta na sasa unamgeukia Mohamed kuhusu audio?
Mimi sio mshabiki wa Mohamed lakini nataka kujua pia upande wa pili wa shilingi kwani nimeona hoja za Mohamed tu ambazo kaziweka bayana either kwa kuwahoji au kuchukua Info kwa hao waanzilishi.
Wewe ulichotuwekea ninini?
Ingekua vizuri na wewe kwa upande wako ukatuwekea audio tuchambue kipi ni kweli na kipi sio kweli.
 
Bravo Nguruvi3! you have made my day! i hail you intellectuality.

G,

Hivi nyie JF ndiyo kipimo chenu?
Nimekuwekea hapa wewe ili msaidiane nyote wawili mkamilishe hesabu lau kwa uchache sana.

Kuna hili nilikwishaliweka la kuandikwa kwa historia ya Nyerere.
Hii kazi ya kuandika sio siri imetangazwa katika Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.

Mimi hamtaki kuniamini.

Hebu fanyeni uchunguzi na nyie mjue nini chanzo cha kazi hiyo kisha rejeeni kwangu Insha Allah.

Saida Othmann Yahya (mke wa marehemu Prof. Haroub Othman) na Prof. Issa Shivji wanaandika
hivi sasa maisha ya Nyerere.

Wameshahoji watu Zanzibar.

Hili la kwanza sasa.

La pili hebu fikeni na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia waulizeni fikra zao kuhusu kitabu
changu.

Nakala ya Kizungu iko Maktaba ya Chuo Kikuu East Africana.
Waulizeni hivi siku hizi East Africana mnaweka vitabu vya ngano?

Hapo ndipo kitovu cha taaluma na utafiti msikalie JF, JF, JF, JF, hapa ni mpata mpatae ndiyo maana
hata Yericko na yeye yumo.

Msitambe kwa kuuliza maswali JF...
Humu kila ''msomi'' ni uwanja wake hata wale wasomi chekechea.

La tatu mbona hamtii kidole katika ''reviews'' za kitabu?
Ingieni na humo nami nikusomeni huo ndiyo usomi.

Nyie JF, JF, JF...
Imekuwa kisa cha kipofu na tembo.

Hebu basi ingieni kwenye ''serialisation'' zangu tatu katika The East African.
Hamna la kusema?

Zitafuteni hizo ''series'' mtazipata zilichapwa December 1998.

Maofisa ofisi za serikali walikuwa wanachekea chooni gazeti la The East African
wanapasiana kama timu ya Brazili 1970 iliivyokuwa wanapeana pasi.

Ukipenda wanapasiana The East African kama kitabu cha Barzanji.

Nakupeni home work hiyo fanyeni uchunguzi kisha rudini hapa mnambie kuwa
bado mnaamini kuwa John Iliffe, Jonathan Glassman, James Brenan na wengineo,
wasomi hawa mabingwa wa African History waliokifanyia ''review'' kitabu changu
walikuwa wanareview ngano na Cambridge Journal of African History walichapa ngano.

Rudini hapa mnambie The East African katika ''serialisation,'' iliyodumu wiki tatu walikuwa
walikuwa wanafanya kichekesho katika ''serialisation'' ya ngano.

Halikadhalika mje mseme hawa nao Amazon, WH Smith, Africa House (London) hawa wote
waliokuwa wakiuza kitabu changu walikuwa wakiuza unga wa ngano na kuwa waliuziwa mbuzi
ndani ya gunia.

Na hawa wasomaji wa kitabu hiki kinachokwenda toleo la tatu ni watu wasiojua kitu.
Hebu piteni humo na jengeni hoja zenu humo.

Basi nyie mmekuwa kazi muijuayo ni kuuliza, kuuliza, kuuliza, ubishi, ubishi, ubishi...
Kujipongeza na kutaka ushindi mwepesi.

Hii haiwezekani.
Ilm sharti usome, upinde mgongo, usome na uandike mambo ya maana yenye tija.

Mwisho nakupeni tanbihi acheni lugha za mitaani za ''JF hapendwi mtu nk. nk...''
Inachusha.

Kama ni hizo lugha zingekuwa za maana kutumia mimi ni aula zaidi kuzitumia kwa kuwa sikuzaliwa
kijijini wala kuja kutoka popote.

Nafungua macho niko Dar es Salaam.
Na Dar es Salaam ni bingwa wa kuzua maneno.
 
G,

Hivi nyie JF ndiyo kipimo chenu?
Nimekuwekea hapa wewe ili msaidiane nyote wawili mkamilishe hesabu lau kwa uchache sana.

Kuna hili nilikwishaliweka.
Hii kazi ya kuandika sio siri imetangazwa katika Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.

Mimi hamtaki kuniaini.

Hebu fanyeni uchunguzi na nyie mjua nini chanzo cha kazi hiyo kisha rejeenikwangu Insha Allah.

Saida Othmann Yahya (mke wa marehemu Prof. Haroub Othman) na Prof. Issa Shivji wanaandika
hivi sasa maisha ya Nyerere.

Hili la kwanza sasa hebu fikeni na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia waulize fikra zao
kuhusu kitabu changu.

Hapo ndipo kitovu cha taaluma na utafiti msikalie JF, JF, JF, JF, hapa ni mpata mpatae ndiyo maana
hata Yericko na yeye yumo.

Msitambe kwa kuuliza maswali JF...
Humu kila ''msomi'' uwanja wake hata wale wasomi chekechea.

Mbona hamtii kidole katik ''reviews'' za kitabu?
Ingieni na humo huo ndiyo usomi.

Nyie JF, JF, JF...

Hebu basi ingieni kwenye ''serialisation'' zangu tatu katika The East African.
Hamna la kusema?

Zitafuteni hizo ''series'' mtazipata zilichapwa December 1998.

Maofisa ofsis za serikali walikuwa wanachekea chooni gazetila The East African
wanapasiana kama timu ya Brazili 1970 iliivyokuwa wanapeana pasi.

Ukipenda wanapasiana The East African kama kitabu cha Barzanji.

Nakupeni home work hiyo fanyeni uchunguzi kisha rudini hapa mnambie kuwa
bado mnaamini kuwa John Iliffe, Jonathan Glassman, James Brenan na wengineo,
wasomi hawa mabingwa wa African History waliokifanyia ''review'' kitabu changu walikuwa
wanareview ngano na Cambridge Journal of African History walichapa ngano.

Rudini hapa mnambie The East African katika ''serialisation,'' iliyodumu wiki tatu walikuwa
walikuwa wanafanya kichekesho katika ''serialisation'' ya ngano.

Halikadhalika mje mseme hawa nao Amazon, WH Smith, Africa House (London) hawa wote
waliokuwa wakiuza kitabu changu walikuwa wakiuza unga wa ngano na kuwa waliuziwa mbuzi
ndani ya gunia.

Na hawa wasomaji wa kitabu hiki kinachokwenda toleo la tatu la kitabu ni watu wasiojua kitu.
Hebu piteni humo na jengeni hoja zenu humo.

Basi nyie mmekuwa kazi muijuayo ni kuuliza, kuuliza, kuuliza, ubishi, ubishi, ubishi...
Kujipongeza na kutaka ushindi mwepesi.

Hii haiwezekani.
Ilm sharti usome, upinde mgongo, usome na uandike mambo ya maana yenye tija.

Mwisho nakupeni tanbihi acheni lugha za mitaani za ''JF hapendwi mtu nk. nk...''

Kama ni hizo lugha zingekuwa za maana kutumia mimi ni aula zaidi kuzitumia kwa kuwa sikuzaliwa
kijijini wala kuja kutoka popote.

Nafungua macho niko Dar es Salaam.
Na Dar es Salaam ni bingwa wa kuzua maneno.

Unakosema tukapate ushahidi sio kule kunakohalalisha ukweli wa historia ya Uhuru Tanganyika!

Kitabu chako hakifundishiwi na chuo chochote katika ardhi ya Tanzani na kwakukidhibiti zaidi serikali imekiita ni kitabu cha KUFIKIRIKA tu (conspiracy Book)

Unauhadaa ulimwengu kwakusema ni kitabu cha Historia ya Uhuru wa Tanganyika wakati mamlaka zinazo ratibu mambo ya historia kwa nchi yetu wameshatuthibitishia kuwa ni NGANO tena za vuli?

Niambie hapa ni chekechea, shule ama chuo gani katika ardhi ya Tanzania ambao kitabu chako kinatumika kama rejea kwa wanafunzi?

Hata hivyo vyuo huko ughaibuni wanaokualika ukawadanganye huenda wanajua kuwa unadanganya ila wanapenda NGANO zako tu huku wewe ukijinasibu umtu muhimu wa historia!
 
Hata hamu ya kujibu sina.
 
Back
Top Bottom