Mama Nuru, Shamma na Shufaa. Aaah Sheikh Mohamed Said, unanipeleka nyumbani kabisa, hakuna ambae alikuwa hamjui mwenzake Kariakoo yetu, Kuanzia Gerezani Mpaka Kisutu mpaka Jangwani nani asiyemjuwa mwenzake? halafu hawa kina Yericko leo wanakuja humu badala ya kukaa na wapate faida wanaleta za kuleta? Namkumbuka Sharrif Saggaf na wanawe au watoto wa nduguze kina Ali "ndimu", kina Mzee Ali Awadh wa Mchikichi, "Gordon Scott", na wale mabulushi ambao baba yao alikuwa na dawa za kihindi (ayuverdic medicine) kina Marehem Shamim.
Tahiya ana uhusiano wowote na kina Tewa Saidi Tewa? kuna kijana pale kwao siku hizo alikuwa mdogo akiitwa Tewa.
Nasubiri kwa hamu kubwa habari za Nyerere ndani ya Sheikh Kassim.
Umenikumbusha Mnazi mmoja ya kweli hiyo na siku za sikukuu ya Eid. Amma kweli siku zinapita.
Turudi kwenye mada, maana hapa kina
Yericko Nyerere na kikundi chake hawaambulii kitu.