zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Ndio ukweli sahihi wa mambo ambao Mohamed Said anakesha jf kuufuta lakini haufutiki
Wewe saa hizi unalo la kuongea? Unasikitisha sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio ukweli sahihi wa mambo ambao Mohamed Said anakesha jf kuufuta lakini haufutiki
Ni kosa dogo tu. Abdulwahid alifariki Oktoba 1968. (naweza kusahihishwa mwezi)Si kweli. Rudia vitabu vyako vya historia, hapo unapotosha kama kawaida yako.
Ni kosa dogo tu. Abdulwahid alifariki Oktoba 1968. (naweza kusahihishwa mwezi)
Jasusi, mwanzoni nilitaka niendelee kudai kua Abdulwahid alifariki 1969.. lakini nilijua toka mwanzo wachache wangenipatga vizuri na huyu bwana alivyoingia na kudakia ndio kabisa nikajua point yangu haitaeleweka. Fikiria kama ningeendelea kudai kuwa Abdulwahid alifariki 1969?
Kwa mfano, nikiwaambia kuwa EAMWS ilivunjwa mwaka 1966 sidhani kama watakubali.
Ni kosa dogo tu. Abdulwahid alifariki Oktoba 1968. (naweza kusahihishwa mwezi)
Wewe si ulijidai hunijibu? Imekuwaje?
Mjuzi wa historia asiyejuwa miaka!
Nakuuliza, ni lini Vasco da Gama, alikanyaga Ardhi hii ya Tanganyika?
Na huu ndiyo mfano wa dhihaka kutoka kwa "typical" muumini wa Mohamed Said aliokusudia...Baba wa Taifa hakuwa na akili kama Wazee wa Gerezani...
Walimkaribisha Dar es Salaam, wakamfunda na kumwingiza kwenye siasa, wakaasisi TANU na kumkabidhi akiongoze, wakamsaidia hela za kununulia mboga, wakamchangia hela za safari UNO, wakamwandikia hotuba ya kusoma akifika huko, wakamnusuru dhidi ya baadhi ya wazee wa Dar es Salaam waliotaka kumng'oa...
Baadaye akaanza ubaguzi wa Ujinga, akawanyima elimu, akawazuia kujenga chuo, akavunja jumuiya yao (EAMWS) na kuwasweka ndani, akawaundia BAKWATA bila hiari yao, akafuta historia yao, akajikweza kama mtakatifu...naam, Mohamed Said, malengo yanaonekana kutimia na ma zomba wanaongezeka kwa kasi, hongera sana.
Najua sana; na zote zinamuonesha Nyerere kama kipenzi cha Waislamu. Wakati wote wa maisha yake mamilioni ya Waislamu walikuwa na mapenzi naye. Maandishi yako yanashuhudia hili. Binafsi naamini kitabu chako kinapaswa kusomwa na kila na kila mtu ili wajue ni jinsi gani Baba wa Taifa alivyokuwa muungwana, mkweli, mwenye heshima na aliyependwa na watu wa kila rika. Kwa kile nilipokisoma kitabu chako na kuondoa zile "inasemekana" na "huenda" na "ilisemwa" basi kuna mambo matamu na manono kweli kweli mle. Masimulizi mengine of course yanakuja na ndimu na limau lakini kwa vile mtu wa pwani wewe natarajia lazima kuwe hivyo si ndivyo inavyokuwa kwa wote ambao tumekulia pwani.
Usisite kutuwekea visa hivi vya uungwana, heshima aliyokuwa nayo Mwalimu kwa wazee wote - bila kuwabagua na ukarimu wao kwake muda wote wa maisha yake na utumishi wake wa umma. Asante sana mzee kwa kutuonesha yale ambayo hatukuyajua kuhusu Baba wa Taifa. Kwa hili ubarikiwe sana.
Naomba uniruhusu swali moja hapa: Katika utafiti wako wote na katika mazungumzo na wazee wako wote kuna yeyote ambaye aliyemfahamu Nyerere kwa karibu amemtaja Nyerere kama mtu asiye na heshima, aliyekosa uungwana, na katili?
Jasusi, mwanzoni nilitaka niendelee kudai kua Abdulwahid alifariki 1969.. lakini nilijua toka mwanzo wachache wangenipatga vizuri na huyu bwana alivyoingia na kudakia ndio kabisa nikajua point yangu haitaeleweka. Fikiria kama ningeendelea kudai kuwa Abdulwahid alifariki 1969?
Kwa mfano, nikiwaambia kuwa EAMWS ilivunjwa mwaka 1966 sidhani kama watakubali.
Na huu ndiyo mfano wa dhihaka kutoka kwa "typical" muumini wa Mohamed Said aliokusudia...Baba wa Taifa hakuwa na akili kama Wazee wa Gerezani...
Walimkaribisha Dar es Salaam, wakamfunda na kumwingiza kwenye siasa, wakaasisi TANU na kumkabidhi akiongoze, wakamsaidia hela za kununulia mboga, wakamchangia hela za safari UNO, wakamwandikia hotuba ya kusoma akifika huko, wakamnusuru dhidi ya baadhi ya wazee wa Dar es Salaam waliotaka kumng'oa...
Baadaye akaanza ubaguzi wa Ujinga, akawanyima elimu, akawazuia kujenga chuo, akavunja jumuiya yao (EAMWS) na kuwasweka ndani, akawaundia BAKWATA bila hiari yao, akafuta historia yao, akajikweza kama mtakatifu...naam, Mohamed Said, malengo yanaonekana kutimia na ma zomba wanaongezeka kwa kasi, hongera sana.
Atakuambia hilo swali aliwezi kukusaidia.
Ni mbinu zao za kuchomokea kwenye kona.
zomba,
Kuna watu humu wanalamika eti Mohamed Said anakesha JF.
Wakati anaaga wote walivaamia huu uzi na kuanza maneno kuwa amekimbia hii ndiyo JF watu hawakubali ngano zake.
Baada ya hayo maneno Mohamed Said akarudi jamvini kama kazaliwa upya sasa wanalalamika tena anakesha JF kwani imeandikwa wapi kwenye sheria na kanuni za JF ni marufuku kukesha.
Uzuri kaishawafahamu na anajua kila mtu muda wake wakuja jamvini.
Hao wanajidai tu, Mohamed Said amewapa ilmu waliokuwa hawana. Na mimi nafurahi sana kila wanapokuja na munkar, Maalim Mohamed Said, tartiiib anawapa darsa mpaka wanachanganyikiwa.
Màandiko ya Maalim Mohamed Said yametufaidisha sana kujuwa wapi tumetoka, wapi tupo, wapi tunaelekea.
Leo hii nani asiyejuwa kuwa TANU ni ubunifu wa wazee wa uswahilini?
Wenzetu hawa ukweli unawaumiza sana.
Mohamed Said,
Huu munakasha umeleta habari mpya huku mitaani kuna sehemu nilikuwa jana maeneo ya Upanga kuna watu walikuwa wanajadili huu munakasha. Kuna mmoja akasema amesoma na wewe chuo cha IFM ni kweli umeishawahi kusoma IFM.
Mbona Nyerere alishasema wazo la jina TANU walikuwa nalo akina Abdu Sykes!
hapo tatizo lipo wapi? Lakini si kweli kuwa Nyerere ndiye kiongozi wa kwanza wa TANU!
Upande wa Sheikh Amir mbona hatujausikia! maana tumesoma yeye kuwekwa ndani na jinsi alivyoshiriki katika harakati.
Je, hayo yanatosha kusema kuwa Nyerere alikuwa mwendawazimu kumuonodoa bila sababu?
Sijui kama unakumbuka radical muslim katika kitabu chako na majaribio ya kumuondoa Nyerere katika uongozi mara mbili kwasababu tu ni mkristu. Je hilo kiongozi gani angelivumilia tena wakati wa kuongoza mapambano na baada ya uhuru?
Kuhusu mawazo yako na ukweli wa vitabu vyako, hayo yanabaki kuwa maoni yako. Nisichokubaliana nacho ni wewe kuyafanya kama ni ukweli na kuushindilia miongoni mwa wachache wasiobahatika kupata ufahamu wa kutosha, au wale walioamua kuweka akili zao rehani ikiwa ni pamoja na manazi, mashabiki na wapenzi wako.
Nisichokubaliana nawe ni kuzua maneno, kufinyanga ukweli na kuficha ukweli ulio wazi ili kujenga chuki na farki miongoni wa wananchi. Unafanya hivyo ukielewa kuwa maandiko yako yasiyo na kina (details na specific) yataamsha hisia hasa kwa wasiobahatika na hivyo kuzua vurugu.
Kibaya zaidi ni wewe kujivika joho la kuandika historia ya waislam wa Tanganyika kama ulivyosema hapo juu.
Lini waislam walikaa kitako na kukubaliana nawe kuwa mawazo yatokanayo na simulizi kutoka kwa wahenga na malenga wako ndio msimamo wa waislam.
Kwa vile ni maoni yako na yaheshimiwa, basi heshimu wengine kwa kuepuka na pengine kuacha kutumia maneno ''sisi waislam'' au kwa ''upande wetu''. Upande wako na nani?
Upande gani huku ukiita wengine wasaliti, wanafiki na wenye husda, vijiba na vijuha! wale wa upande wako ni wapi?
Ni nani amekwambia kuwa waislam wanakubaliana na vitabu vyako hivyo usimamie hoja zako kama zao.