Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

jmushi1
Ulikuwa wapi? Hujaonekana kwa muda sasa.
Nipo mkuu,ni shughuli so nakuwa busy sometimes.Mkuu nawashangaa sana ndugu zetu wengine watanzania.Wanasahau kuwa endapo makao makuu ya mkoloni na ikulu yake ingekuwa Tanga ama Arusha sijui wangepata sababu gani ya kumnanga Nyerere.

Kupewa kipaumbele kulikofanyika kwa Dar ni sababu hiyo(makao makuu ya mkoloni).Lakini haina maana kuwa Dar peke yao ndiyo waliogombea uhuru wa Tanganyika.Ndiyo maana mwalimu na wengine wengi walisafiri na kwenda Dar.However hata mwalimu alipojiuzulu aliamuwa kurudi Butiama licha ya kuwa na nyumba pale Msasani.

Kuna dalili mbaya sana za ubaguzi kwenye hoja zao.
 
Wakuu nadhani kuna jambo ambalo halijazungumziwa hapa.Kilichofanya Nyerere aende Dar ni kwasababu ndipo yalipokuwa makao makuu ya mkoloni na hata ikulu na ofisi zote na uongozi ulikuwepo Dar.

Kwahiyo wale wanaodai sijui wazee wa gerezani mimi naona ni kwamba kilichotokea ni wao kuwa wenyeji wa makao makuu ya mkoloni.

Na wanaodai kwanini asingewaondoa wakoloni akiwa Butiama wana dalili za kutoelewa vyema,na wanapotosha either kwa makusudi ama kwa bahati mbaya.

Mangi....heshima yako mkuu......karibu tena mkuu...
 
Naam; na hapa ndio ugomvi ulipo. Historia ya Gerezani imekuwa ni historia ya Tanganyika nzima. Lakini siyo hivyo tu, Bw. Said kwa makusudi kabisa (na ameashiria kukubali hilo) ameamua kuwaweka pembeni wazee wengine wote walioshiriki katika harakati za Uhuru hasa kama a. Ni Wakristu (hawa hawaiti wazee wake) na b. Wako nje ya Dar (wapo wenggine wa nje ya Dar anawaita wazee wake kwa sababu ni Waislamu). Hivyo majina mengine anayataja kwa kupita tu hata kama wana mchango mkubwa sana.

Mimi matumaini yangu ni kuwa vijana na hata watu wengine ambao wametusoma toka mwanzo watakuwa wameelewa namna ya KUTOKUJENGA hoja na vile vile namna ya KUTOKUANDIKA HISTORIA. Nimepata bahati ya kusoma waandishi wengi walioandika kuhusu Tanganyika na mwamko wa Uislamu katika Tanganyika na karibu wote wametaja majina makubwa ya wakati ule katika Waislamu. Lakini hawa walitajwa zaidi katika Uislamu wao kuliko katika siasa zao.

Sasa ukiamua kuangalia kwa mwanga wa Uislamu tu utakosa mengi kwa sababu ni lazima unachoangalia kifit kwenye paradigm yako uliyotengeneza. Bw. Said kaamua kutengeneza prism ya Uislamu na hapo basi watu wote katika historia yetu wanahukumiwa kupitia hapo. Ukipingana na Sheh Amir basi uko kinyume ya Uislamu na Muislamu ukimuunga mkono Nyerere basi wewe siyo Muislamu mzuri.

Sasa hivi kwa kweli niko tempted sana kuamua kuchambua maandishi ya Bw. Said na kuyamegua megua kuyaonesha how absurd some of the claims are, and why some facts as claimed by the author have no historical bearing - and they are quite plentiful. Mimi sasa hivi wala sihitaji majibu ya Bw. Said tena kwani hana majibu hayo; ninachofanya ni kuwapa wasomaji wetu maswali wajiulize wanapomsoma.

MM,

Nakuwekea hapa yoye niliyoandika yakusaidie.
Kitabu nakala hii ya Kizungu ina kurasa 358.

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Table of Contents
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 1. Dedication[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 2. Acknowledgements[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 3. Table of Contents[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 4. Introduction[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part One
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Abdulwahid Sykes 1924-1968
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 1. The Sykes: Origins 1894-1929[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Old Town of Dar es Salaam and its Elites[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Kleist Sykes, Pioneer and Man of Ideas: 1894-1949[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · World War One 1914-1918[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Founding of the African Association and Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association of Tanganyika), 1929-1933[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 2.The Second World War and Tanganyika’s Political Foundation, 1938-1945
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Burma Infantry, 1942[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 3. Dar es SalaamDockworkers Movement 1947-1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Dar es Salaam Port, 1947[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Erika Fiah[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Dockworkers’ Union, 1948[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 4. The Genesis of Open Politics in Tanganyika 1950 -1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Tanganyika African Association, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TAA Political Subcommittee, 1951[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanganyika as a Mandate Territory[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Kenyan Nationalists in the Struggle of Tanganyika,1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TAA and KAU: Attempts at Linkage and Solidarity, 1950 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Meru Land Evictions, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 5. Julius Kambarage Nyerere [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Story of Julius Nyerere, 1952[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanganyika African National Union (TANU)-The Party of Independence, 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 6. The Pan African Congress of Northern Rhodesia, 1953[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Ally Kleist Sykes[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part Two
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Mass Mobilisation and Independence 1954-1961
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 7. Mass Mobilisation 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Elders’ Council and Nyerere’s Visit to the United Nations, New York, 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Idd Faiz Mafongo [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The African Press-Ramadhani Mashado Plantan, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Ahmed Rashad Ali-Radio Free Africa (Radio ya Afrika Huru), 1952 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Propagandists-The Bantu Group,1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Incorporation of Swahili Women’s Societies into the Struggle, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Football As a Political Weapon[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 8. The Formation of the Party in the Provinces[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Central Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Southern Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Western Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanga Province, 1956[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TANU in Mombasa, Kenya, 1957[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 9. The Tabora Conference-The Road to Independence, 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Tanga Strategy, 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Debate for Tripartite Voting[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Pan-African Movement of East and Central Africa (PAFMECA), 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Independence, 1961[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part Three
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Conspiracy Against Islam 1961-1970
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 10. The Muslim Factor in Post-Independence Tanzania 1961-1970[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Islam: The Ideology of Colonial Resistance[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The First Muslim Congress, 1962[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Resistance to Change[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Second Muslim Congress, 1963[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Proposal for an Islamic University, 1964[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Politics of Islam, Church, State and the African Christian[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 11. The East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ‘Crisis’[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Fomentation of the BAKWATA ‘Crisis’[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Nyerere, Tewa, Bibi Titi Encounter, 1968[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Islamic National Conference, 1968[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Omissions Analysed[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Betrayal of Ideals[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Conspiracy Theory[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Epilogue [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Bibliography[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mkuu wangu; swali hili liko at the core of the allegations za mzee wetu huyu. Hakuna kiongozi mwenye hisia za ubora wa dini, rangi, au nasaba yake ambaye hajawahi kuzisema hadharani na watu wakajua. Hitler alitukuza rangi yake -siyo sirini bali hadharani kabisa; Kina Milosevic walitukuza nasaba yao ya Kiserbia dhidi ya non-Serbs wa Serbia na Bosnia.. Idi Amin alitukuza Uafrika wake dhidi ya watu wengine wote hawa walifanya hadharani. Kaburu Botha na wabaguzi wa Deep South huko Marekani walitukuza rangi zao hadharani na haikuwa kificho.

Hakuna mtu yeyote kiongozi aliyeetukuza dini au rangi yake ambaye alifanya hivyo kwa kificho. Ahmedinajad na wenzie wote hawana siri. Hisia hii ya ubora haifikichiki kwa aliyonayo. Hata hapa unaweza kuona watu wanavyozungumza kwa ubora (superiority complex) inayotokana na dini.

Sasa, Nyerere kama kweli - NA TUMPE BENEFIT OF THE DOUBT Bw. Said...basi asingeweza kujificha kwa miaka zaidi ya 25 aliyokuwa akiongoza (miaka 31 tangu achukue uongozi wa TANU). Kungekuwepo angalau na barua, hotuba, mazungumzo ya sirini ambapo Nyerere ameusema vibaya Uislamu, au Waislamu.

Kama kuna mtu kasoma maandishi ya Bw. Said na mimi nimesoma maandishi yake mengi mno - HAKUNA MAHALI HATA PAMOJA - ambapo Bw. Said anamnukuu mzee wake YEYOTE (siyo Abdul, Rashad Ali, Dossa, Mshume Kiyate n.k) akisema amewahi kumsikia Nyerere akiutukana Uislamu, akiwakejeli Waislamu au akisema neno lolote baya kuhusu vyote viwili. HAKUNA.

Lakini jambo la pilli ambalo huwezi kuliona ni ushahidi wa aina yoyote wa agizo, amri, maelekezo yoyote ya Baba wa Taifa kwa mtu yeyote ambayo yalihusiana na kutowatendea haki Waislamu kwa misingi yoyote ile ya kidini.

Lakini la tatu ambalo kihistoria ni zito zaidi ni kuwa - HAKUNA jambo lolote ambalo Bw. Said anadai liliwatokea wazee wake wa Kiislamu ambalo halikuwatokea wazee wengine wasio Waislamu. Mfano mzuri ni uamuzi wa Nyerere kuvunja Baraza la Machifu ambao tunaweza kusema waliwakilisha watu wengi zaidi kuliko Waislamu na Wakristu. Watu wa jadi wangeweza (labda kwa haki) kudai kuwa Nyerere anawabagua katika uongozi na kuthibitisha hilo alivunja Baraza la Machifu.

Chief David Kidaha Makwaia kwa mfano alitupwa Tunduru. Kitu ambacho labda wengi hawakumbuki ni kuwa alizaliwa katika Uislamu na kukulia katika Uislamu. Alikuja kuingia ukatoliki baadaye ukubwani. Ukweli ni kuwa Waingereza walimfikiria Makwaia kama Rais wa kwanza wa Tanganyika kuliko Nyerere. Huyu amekufa juzi tu hapa (2007) lakini kwa vile hakuwa tena Muislamu basi hakumbukwi. Ana historia yake nchini lakini ni wachache sana wanajua baadhi ya mambo ambayo alifanikiwa kuyafanya.

Sasa Bw. Said ameamua kuimega historia na kutengeneza "sub-history' ambayo haifungi na matukio mengine ya historia. Anaangalia kwa jicho moja tu nalo ni la Uislamu. Sasa hili ni zuri kuvutia hisia lakini kwa mtu mwenye hekima ni lazima wahoji. Mifano miwili inatosha hapa:

Maasi ya Jeshi ya 1964 yalisababisha kamatakamata itokee; miongoni mwa watu waliokamatwa walikuwa ni mashehe na wengine wapinzani wa muda mrefu wa Mwalimu kuanzia 1958 na kabla. Sasa kama ingekuwa ni kamata kamata ya Waislamu tu basi hoja ni rahisi kujengwa lakini ni kweli walikamatwa Waislamu watupu? Kama walikamatwa na wasio Waislamu ni vipi basi kamata hiyo ionekane ni dhidi ya Uislamu unless kama wale wengine nao walishukiwa kushirikiana na Waislamu.

Tukio jingine ambalo huwa linatajwa sana ni kesi ya Uhaini ya 1969 ambapo mmojaa wa waliohusishwa ni Bi. Titi Mohammed. Kwa wengine hili lilikuwa ni dhidiya Waislamu. Ingekuwa kweli kama hawakukamatwa wengine. Lakini tuwakumbushe majina ya wale watu saba waliofikishwa mahakamani Juni 8, 1970 mbele ya Jaji Mkuu T. Georges

Bi. Titi Mohammed (Muislamu) (Muasisi wa TANU na mpigania Uhuru)
Michael Kamaliza (Waziri wa zamani wa Kazi - Mkristu)
William Chacha (Mwambata wa Kijeshi, Peking - Mkristu)
Grey Mattaka (mhariri gazeti la The Nationalist - Mkristu)
Oscar Kambona (mpigania Uhuru na Waziri wa zamani wa Ulinzi na Mambo ya Nje - Mkristu)*
John Chipaka (kiongozi wa chama cha ANC- Mkristu)
Eliya Chipaka (Kapteni wa JWTZ - Mkristu)
Alfred Mulinga (Luteni wa JWTZ - Mkristu)

* Kambona hakuhesabiwa kama miongoni mwa wale saba waliofikichwa mahakamani mwanzoni. Kambona alikuwa ameshatoroka kwenda Uingereza kabla ya kesi kuanza.

Sasa, kati ya wote hao saba ni mmoja tu Muislamu - Bi. Titi Mohammed. Lakini Bw. Said anaandika kana kwamba Nyerere alikuwa na baya dhidi ya Waislamu japo mtu angeweza kusema ilikuwa dhidi ya watu wa Kambona (wanne ya watuhumiwa walikuwa wanausiana na Kambona).

Sasa, vijana wanaosoma hapa natumaini wanapata mwanga kidogo wa kuelewa kwanini wengine tunachukulia hoja nyingi za Bw. Saiid ni za kutengeneza na zimeandikwa mahsusi kuvutia watu wasiotaka kutafuta ukweli.

Mag3,

Ukitaka mwanga wa yaliyotokea baada ya uhuru soma ''Conspracy
Theory'' katika nakala ya Kizungu ikiwa una kitabu changu hicho.

Tatizo si kama Nyerere alitukana au hakutukana Uislam.
Nia ni dunia nayo ijue upande wa Waislam.

Kwa takriban miaka 50 iliyokuwa ikijulikana ni historia rasmi.

Sasa Waislam wanajua Sheikh Hassan bin Amir hakuwa na njama
za kuisaliti serikali.

Tatizo lilikuwa EAMWS kutaka kujenga chuo kikuu wakati Kanisa
Katoliki halijaweka vyema mikakati yake ya mfumokristo.

Waislam sasa wanajua kila kitu.

Sasa vijana wa Kiislam wanaijua historia ya babu zao vyema kabisa.

Ndiyo joto hili unalosikia likivuma sasa...NECTA nk.

Chief Kidaha Makwaia yupo katika kitabu bora unisome kabla hujaandika:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Chief Kidaha Makwaia of Shinyanga and others were regular visitors to Abdulwahid's house.

This was the high society of Dar es Salaam. Abdulwahid's house soon became a center of political debates and at times, depending on the background of the invited guests, a center of very radical political thought on the future of Tanganyika.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] It was about this time that Abdulwahid and the TAA leadership approached Chief Kidaha Makwaia and invited him to the leadership of the Association as president.

Abdulwahid told Chief Kidaha that his assumption of the leadership of the African people through TAA would make him a pioneer of change in Tanganyika because all the other chiefs would follow him.

Chief Kidaha was the favourite chief of the colonial government and did not, therefore, accept the invitation. In spite of the statement he had made demanding that African civil servants be allowed to participate freely in politics, which was probably why the TAA leadership invited him to lead the Association, Chief Kidaha believed in the system of chiefdoms and close cooperation with the British government through indirect rule.

He was not the kind of person to jeopardize his position and that of his people by supporting TAA's radical nationalism.

He only came to realise when it was too late that he had let pass his only chance of becoming president of Tanganyika's first open political party and probably of becoming the first Prime Minister when Tanganyika became independent in 1961.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Nimesoma darasa moja na mtoto wa Chief Kibaha na tulikuwa marafiki sana katika utoto wetu.
Najua mengi sana kuhusu Chief Kidaha na nilikutananae.
 
Bw. Said kitabu chako nimekisoma chote. Mapungufu ninayoyaanisha hapa ni sehemu tu ya mapungufu ya maandishi yako. Hiyo table of contents haijibu kabisa maswali ambayo mimi na wengine tumekuuliza. Utakuwa muungwana kama utatoa majibu badala ya kuzungusha watu kujinukuu wewe mwenyewe. '
 
Mag3,

Tatizo si kama Nyerere alitukana au hakutukana Uislam.
Nia ni dunia nayo ijue upande wa Waislamu...

Mzee Said tafadhali uwe mkweli basi. Hoja yako nzima dhidi ya Baba wa Taifa imejengwa kwenye nadharia kuwa Nyerere alikuwa na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na alifanya kila awezalo kuukandamiza Uislamu (dhulma). Umewaaminisha mashabiki wako kuwa Nyerere alikuwa mtumishi wa kanisa akitumikia kuujandamiza Uislamu na hawa wamekuamini. Sasa unageuka na kusema kuwa hilo siyo tatizo? Kuwa sasa tatizo ni historia?

Nyerere alisema nini dhidi ya Uislamu, Waislamu au Mtume Mohammed kiasi cha kumfanya awe adui wa Waislamu? Au alitoa agizo gani lililowalenga Waislamu pekee yao na kutishia dini na ibada yao?
 
...uliulizwa hivi, ni nani alikutuma uje kuwasemea waislam?

kumbe ndo maana ukiulizwa maswali majibu yako ni kama haya, waulizeni wao..., soma kitabu changu,.... etc

historia ya wazee wako? na kila mtu akiweka historia ya wazee wake jinsi walivyopigania uhuru wa nchi hii zitakuwa historia ngapi nje ya hiyo tuliyofundishwa miaka 50?

kwenye utetezi wako mwingi sana hili neno naona unalitumia mno, kila kitu unasema tushaakijua, hii ni jibu la hoja mufilisi kabisa.

umeulizwa toa mfano wa mfumo kristo hujibu, hivi kweli kungekuwa na mfumo kristo ungekuwa hai kweli wewe na huu upotoshaji wako unaojenga ufa wa kidini kwenye jamii ya mfumo kristo?

nimeshajua lengo lako, kumbe lengo lako ni maelfu ya watu wasome na kusikia ngano zako ndo raha yako?

Baba katika jina la Yesu lipitalo majina yote naamuru pepo la vita, pepo la uchonganishi litoke kwa mtu huyu amani yako ipate kutawala tena kwa watu wako, aaamen.

Z,

Nimeandika historia ya wazee wangu kwa kuwa kilikuwapo cha kuandika.

Ikiwa nawe unacho katika historia cha kusema kuhusu wazee wako hapana
ubaya ukaandika nasi tukasoma.

Hayo mengine sina haja ya kuyasemea.
 
Mzee Said tafadhali uwe mkweli basi. Hoja yako nzima dhidi ya Baba wa Taifa imejengwa kwenye nadharia kuwa Nyerere alikuwa na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na alifanya kila awezalo kuukandamiza Uislamu (dhulma). Umewaaminisha mashabiki wako kuwa Nyerere alikuwa mtumishi wa kanisa akitumikia kuujandamiza Uislamu na hawa wamekuamini. Sasa unageuka na kusema kuwa hilo siyo tatizo? Kuwa sasa tatizo ni historia?

Nyerere alisema nini dhidi ya Uislamu, Waislamu au Mtume Mohammed kiasi cha kumfanya awe adui wa Waislamu? Au alitoa agizo gani lililowalenga Waislamu pekee yao na kutishia dini na ibada yao?

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"] [h=2]Betrayal of Ideals[/h] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] On 5 th November, 1985, before he stepped down as president, Nyerere delivered an emotional speech to elders of Dar es Salaam. Most of them were former members of TANU-the townsman who supported Nyerere during the struggle for independence[1] Nyerere acknowledged the role of Muslims in those difficult days. Nyerere told his audience that the imbalances between Muslims and Christians which his government had inherited from the British were rectified under his rule:

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] ''And they (Muslims) gave us chance through our education policies, to correct the imbalances which we have done. I am now in the happy position of sometimes not knowing whether a new member of Parliament, a Minister, or a Principal Secretary in our government ministries, is a Muslim or a Christian or neither unless their first name happens to give it away. And even that is not a sure guide in Tanzania, for we have Christians with Muslim names, Muslims with Christian names. This religious tolerance and freedom is your creation; what I have done is to speak up for those values on your behalf.'' [2]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] The speech was a farce. The truth is that three decades after independence Muslim are not better off than they were under colonialism. Sivalon has revealed that the Church has been able to create its own lobby which controls 75% of the seats in the parliament. Among these seats 70% are held by Catholics and the rest are divided among Muslims and Christian denominations.[3] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[1] See footnote no.19.
[2] Daily News, 6 th November, 1985

[3] Sivalon, op.cit. p. 49.

Hivi nina hitaji mie kusherehesha hii yaani kutia maelezo?
 
Bw. Said kitabu chako nimekisoma chote. Mapungufu ninayoyaanisha hapa ni sehemu tu ya mapungufu ya maandishi yako. Hiyo table of contents haijibu kabisa maswali ambayo mimi na wengine tumekuuliza. Utakuwa muungwana kama utatoa majibu badala ya kuzungusha watu kujinukuu wewe mwenyewe. '

MM,

Mie ndiye niliyefanya utafiti nimeandika vitabu na kutoa paper kadhaa.

Sasa kama sikueleza niliyoyaona kwa kunukuu kutoka maandishi yangu
nimnukuu nani?

Sikuingia humu kujibu maswali.

Kubwa lililonileta hapa ni kubandikwa kwa tamko la maaskofu na Bwana
Nyerere kisha akatuhamishia hapa.

Nilitaka na nyie msikie upande wa Waislam.
Vipi wanayaona haya mambo.

Salama yenu msinione mie wapumzisheni Waislam na matamko ya maaskofu.
 
Nguruvi,Nia yangu haijapata kuwa nikae humu kujibu maswali.
La hasha.Nimeingia humu kwa nia ya kukuelezeni upande wa Waislam.
Nia si kuwa mkubali kuwa lipo tatizo hapana.Nia ilikuwa kukufahamisheni la kwanza kuwa ipo historia nyingine
nje ya ile mliyofundishwa shule kwa zaidi ya miaka 50.
Hili naamini mshalijua. Pili ilikuwa kueleza mfumokristo.Hili mshalijua.

Kwetu nyie kuamini kuwa lipo tatizo si muhimu sana kwa sasa.

Tunaweza tukafanga mjadala ikiwa mtapenda.
Mjadala utajifunga wakati muafaka ukiwadia kwasasa subiri kidogo maana naona dalili za kukimbia nondo tulia kidogo bin mwekapopo.

Nasi pia kama wewe nia yetu si kuingia humu kumeza kila kitu hata ambacho hakihitaji elimu ya darasa la 5C.
Mohamed, wewe kakwambia nani unazungumza kama ''waislam''?
wewe zungumza kwa niaba ya wa Narung'ombe na Kipata, mchikikichi na Tandamti.

Hili la mfumo kristu hujaweza kulieza wala kulitetea kwa hoja au kwa mantiki.
Ni kwa sababu hizo hata watu wanaomeza ngano hii wameishia kuadhirika pale wanapoulizwa mfumo huo unafanyaje kazi.
Mfano, umesema kuwa uchaguzi uliopita waislam wamehimizana kumchagua mwislam.

Ukweli ni kuwa hawakuhamasishana hizo ni hisia zako.
Ingalikuwa hivyo basi asilimia 86 ya mwaka 2005 ingefikia 90 na ushee na badala yake imepungua na kufikia 60 hata kwa ulaghai! maana yake wale uliowashawishi wengine hawakukubaliana na ushawishi wako.

Lakini basi kama waislam wanauwezo wa kumchagua kiongozi wa nchi hii, nini kinawashinda kuvunja mfumo kristo unaoundwa pengine na makatibu kata au watendaji vijiji.
Siamini rais aliyewekwa na waislam angekuwa hana uwezo wa kuuvunja unless uniambie naye ni kafir kama BAKWATA.

Tumekusihi utupe specifics za jinsi gani mfumo huo unafanya kazi huna jibu. Jibu ulilotoa lisilo na chembe ya usomi ni kuhusu utafiti uliofanywa na warsha. Utafiti huo uliokuwa na majibu andalizi umeshindwa kabisa kuthibitisha kuwa tatizo la elimu lipo vyuo vya juu zaidi ya kutoa namba ambazo mpuuzi anaweza kuziamini.

Mohamed, sekomdari yenye watoto 250 na walimu 2 itatoa division 0 za nguvu, division 0 haziruhusu kwenda high school.
Asiyekwenda highschool anapunguza nafasi yake ya kuingia Chuo kikuu.
sasa unapoangalia chuo kikuu huangalii watu wanafikaje huko ni ulaghai wa kiwango cha Cambridge!

Tumekuomba utupe tafiti kuhusu mfumo wa elimu kuanzia msingi hadi sekondari, huna jibu bali unajibu la kuingia chuo kikuu kwa upendeleo. Mohamed, huwezi kupata mwanafunzi kama hajafanya mtihani.

Hapa ni lazima watu watumie akili za kuzaliwa tu haihitaji certificate au degree kubaini uzushi huu!
Shule ikifungwa maana yake hakuna wanafunzi na hakuna watahiniwa na hatima yake hakuna chuo kikuu.

Kama nilivyosema hapo awali historia ya nchii hii katika uvunjifu wa amani haitakamilika kama jina lako halitakuwepo.
Ukisoma habari ya njozi kuhusu rise of religious tension ni wazi kuwa wewe na yeye mna malengo dhidi ya watu fulani.

Kama ulivyomshambulia Mkapa wakati akiwa mhariri ndivyo njozi anavyomshambulia na kusahau kuwa kiongozi aiyekuwepo kabla ya Mkapa ni Mwinyi. Mnajifanya hamnazo katika kujua uvunjaji wa mabucha!!

Hatari kubwa ambayo haionekani ni jinsi unavyojenga chuki katika jamii.
Hatari kubwa ni jinsi unavyoipumbaza jamii ya waislam. Hakika siku wakibaini uzushi na upotoshaji wako watasikitika sana.

Kwa vijana wengi mnaosoma mijadala kama hii, labda niwaase kuwa lazima uwe na kibakuli kidogo cha kuweka nafaka na gunia tupu la kujaza pumba. Usichanganye maana utapata taabu mbele ya safari, kuna pumba zinang'aa kama nafaka.

Pili, labda niwagusie na kuwaibia siri ya jinsi gani mfumo kristo unafanya kazi
-Kama unakwenda kisutu kusikiliza kesi ya Ponda na kuacha darasa, mfumo kristo utakuumiza
- Kama unakaa barazani na kujadili majina ya watu na harakati zao mfumo kristo utakuumiza
- Kama utasoma takwimu na ukagoma kuzielewa bali kuzitamani, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huiangalii Tanzania na duni kwa upana wake unafikiri chuo kikuu kisichokuwepo, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huangalii tatizo kama tatizo bali kutafuta namna ya kuficha ukweli, mfumo kristo utakuumiza
- Kama umeridhika kuwa wewe ni dhalili na dhaifu kwasababu kuna mtu kaazima akili zako na hatakikukurudishia, utaumia

-Kibaya zaidi ukishindwa kutumia chembe ya akili akaamua kuiweka rehani basi hilo ndilo tatizo kubwa kuliko yote hapo juu na mfumo kristo utaanza kukupiga bakora hapo hapo ulipokaa kitako,and guess what you will never recover
 
Indeed it is, doing business with Allah your capital is you. Doing business with your fellow humans your capital is material. Someone told me if you are not a good contributor forget about the front row, is it true?
Kwa kweli hapa umeongea zomba. Sasa hii WAISLAMU kupigania UHURU wa TANGANYIKA sielewi inatoka wapi! Sio kazi ya UISLAM kupigania uhuru wa nchi. Uislam ni "doing business with ALLAH your capital is you". Shukrani sana zomba.
 
Ha ha haaaaa....sipati picha ikatokea mtoto wa kike wa Mzee Mohamed Said kafall in love na mvulana wa kigalatia na wanataka kuona kwa masharti ya binti wa kike(mtoto wa Mzee Mohamed Said) abadili dini na kuwa mgalatia ili wafunge
ndoa ya kikristu kanisani. Duuh yaani sipati picha hilo timbwili litakalotokea hapo!...hebu nisaidieni jamani.
 
kesho tutaambiwa wazee wetu wamesaulika kupewa vitambulisho
Tena huyu Alhad Musa Salum ni kipenzi cha Mufti na MfumoKristo. Nadhani ndie anaandaliwa kumrithi. Huyu ni kati ya maadui wakubwa wa UISLAM wa Mzee Mohamed, Sheikh Ponda, Sheikh Ilunga,...
 
Mjadala utajifunga wakati muafaka ukiwadia kwasasa subiri kidogo maana naona dalili za kukimbia nondo tulia kidogo bin mwekapopo.

Nasi pia kama wewe nia yetu si kuingia humu kumeza kila kitu hata ambacho hakihitaji elimu ya darasa la 5C.
Mohamed, wewe kakwambia nani unazungumza kama ''waislam''?
wewe zungumza kwa niaba ya wa Narung'ombe na Kipata, mchikikichi na Tandamti.

Hili la mfumo kristu hujaweza kulieza wala kulitetea kwa hoja au kwa mantiki.
Ni kwa sababu hizo hata watu wanaomeza ngano hii wameishia kuadhirika pale wanapoulizwa mfumo huo unafanyaje kazi.
Mfano, umesema kuwa uchaguzi uliopita waislam wamehimizana kumchagua mwislam.

Ukweli ni kuwa hawakuhamasishana hizo ni hisia zako.
Ingalikuwa hivyo basi asilimia 86 ya mwaka 2005 ingefikia 90 na ushee na badala yake imepungua na kufikia 60 hata kwa ulaghai! maana yake wale uliowashawishi wengine hawakukubaliana na ushawishi wako.

Lakini basi kama waislam wanauwezo wa kumchagua kiongozi wa nchi hii, nini kinawashinda kuvunja mfumo kristo unaoundwa pengine na makatibu kata au watendaji vijiji.
Siamini rais aliyewekwa na waislam angekuwa hana uwezo wa kuuvunja unless uniambie naye ni kafir kama BAKWATA.

Tumekusihi utupe specifics za jinsi gani mfumo huo unafanya kazi huna jibu. Jibu ulilotoa lisilo na chembe ya usomi ni kuhusu utafiti uliofanywa na warsha. Utafiti huo uliokuwa na majibu andalizi umeshindwa kabisa kuthibitisha kuwa tatizo la elimu lipo vyuo vya juu zaidi ya kutoa namba ambazo mpuuzi anaweza kuziamini.

Mohamed, sekomdari yenye watoto 250 na walimu 2 itatoa division 0 za nguvu, division 0 haziruhusu kwenda high school.
Asiyekwenda highschool anapunguza nafasi yake ya kuingia Chuo kikuu.
sasa unapoangalia chuo kikuu huangalii watu wanafikaje huko ni ulaghai wa kiwango cha Cambridge!

Tumekuomba utupe tafiti kuhusu mfumo wa elimu kuanzia msingi hadi sekondari, huna jibu bali unajibu la kuingia chuo kikuu kwa upendeleo. Mohamed, huwezi kupata mwanafunzi kama hajafanya mtihani.

Hapa ni lazima watu watumie akili za kuzaliwa tu haihitaji certificate au degree kubaini uzushi huu!
Shule ikifungwa maana yake hakuna wanafunzi na hakuna watahiniwa na hatima yake hakuna chuo kikuu.

Kama nilivyosema hapo awali historia ya nchii hii katika uvunjifu wa amani haitakamilika kama jina lako halitakuwepo.
Ukisoma habari ya njozi kuhusu rise of religious tension ni wazi kuwa wewe na yeye mna malengo dhidi ya watu fulani.

Kama ulivyomshambulia Mkapa wakati akiwa mhariri ndivyo njozi anavyomshambulia na kusahau kuwa kiongozi aiyekuwepo kabla ya Mkapa ni Mwinyi. Mnajifanya hamnazo katika kujua uvunjaji wa mabucha!!

Hatari kubwa ambayo haionekani ni jinsi unavyojenga chuki katika jamii.
Hatari kubwa ni jinsi unavyoipumbaza jamii ya waislam. Hakika siku wakibaini uzushi na upotoshaji wako watasikitika sana.

Kwa vijana wengi mnaosoma mijadala kama hii, labda niwaase kuwa lazima uwe na kibakuli kidogo cha kuweka nafaka na gunia tupu la kujaza pumba. Usichanganye maana utapata taabu mbele ya safari, kuna pumba zinang'aa kama nafaka.

Pili, labda niwagusie na kuwaibia siri ya jinsi gani mfumo kristo unafanya kazi
-Kama unakwenda kisutu kusikiliza kesi ya Ponda na kuacha darasa, mfumo kristo utakuumiza
- Kama unakaa barazani na kujadili majina ya watu na harakati zao mfumo kristo utakuumiza
- Kama utasoma takwimu na ukagoma kuzielewa bali kuzitamani, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huiangalii Tanzania na duni kwa upana wake unafikiri chuo kikuu kisichokuwepo, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huangalii tatizo kama tatizo bali kutafuta namna ya kuficha ukweli, mfumo kristo utakuumiza
- Kama umeridhika kuwa wewe ni dhalili na dhaifu kwasababu kuna mtu kaazima akili zako na hatakikukurudishia, utaumia

-Kibaya zaidi ukishindwa kutumia chembe ya akili akaamua kuiweka rehani basi hilo ndilo tatizo kubwa kuliko yote hapo juu na mfumo kristo utaanza kukupiga bakora hapo hapo ulipokaa kitako,and guess what you will never recover

Naona umeamua kujifariji na kujiliwaza hakuna nondo za kumkimbiza Mohamed Said, hujui kama watu walikuwa wanatafuta hii nafasi ya kueleza haya.

Wewe upo hapa kutetea Ukirstu wako na Mohamed Said yupo hapa kutetea Uislam hakuna haja ya kutishana wasomaji ndiyo wataamua.

Mohamed Said kaamua kula JF, kulala JF, kushinda JF, halafu unasema bado kidogo akimbie wakati yeye kaamua kutoa dasra.

Watu wanatamani huu munakasha uendelee hata mwaka.
 
Last edited by a moderator:

Hana hoja huyo, ana viroja.
 
Z,

Nimeandika historia ya wazee wangu kwa kuwa kilikuwapo cha kuandika.

Ikiwa nawe unacho katika historia cha kusema kuhusu wazee wako hapana
ubaya ukaandika nasi tukasoma.

Hayo mengine sina haja ya kuyasemea.
Ungeandika ya wazee wako tu bila kumbambikia Mwalimu tuhuma za UDINI, uasisi wa MfumoKristo, yeye kutokuwa muasisi wa TANU wakati yeye ndie RAIS wa KWANZA wa chama hiki, kuwachukia Waislamu wote,..., wengi tusingehangaika nawe. Ungeweka ushahidi wa wazi juu ya tuhuma hizi, wenye akili timamu tusingehangaika nawe.
 
Tena huyu Alhad Musa Salum ni kipenzi cha Mufti na MfumoKristo. Nadhani ndie anaandaliwa kumrithi. Huyu ni kati ya maadui wakubwa wa UISLAM wa Mzee Mohamed, Sheikh Ponda, Sheikh Ilunga,...

Siyo adui wa Mohamed Said ni adui wa Waislam Tanzania.

Kama anapendwa mwambie aende basi kwenye misikiti tofauti na Bakwata.
 
Siyo adui wa Mohamed Said ni adui wa Waislam Tanzania.

Kama anapendwa mwambie aende basi kwenye misikiti tofauti na Bakwata.
Kumbe na misikiti mmegawana! Ndio nafuu yetu hiyo tusiohangaika na DINI. Anavyoandika Mzee Mohamed humu ni kama vile anamiliki WAISLAM wote wa NCHI hii! Anasikilizwa na Waislam wote wa nchi hii!
 
Siyo adui wa Mohamed Said ni adui wa Waislam Tanzania.

Kama anapendwa mwambie aende basi kwenye misikiti tofauti na Bakwata.
Hivi kwenye misikiti ya Bakwata huwa anasali peke yake tu au kuna waumini wengine pia?
 
Kumbe na misikiti mmegawana! Ndio nafuu yetu hiyo tusiohangaika na DINI. Anavyoandika Mzee Mohamed humu ni kama vile anamiliki WAISLAM wote wa NCHI hii! Anasikilizwa na Waislam wote wa nchi hii!

Kugawana misikiti unayasema wewe Bakwata siyo chaguo la Waislam.
 
Back
Top Bottom