Nguruvi,Nia yangu haijapata kuwa nikae humu kujibu maswali.
La hasha.Nimeingia humu kwa nia ya kukuelezeni upande wa Waislam.
Nia si kuwa mkubali kuwa lipo tatizo hapana.Nia ilikuwa kukufahamisheni la kwanza kuwa ipo historia nyingine
nje ya ile mliyofundishwa shule kwa zaidi ya miaka 50.
Hili naamini mshalijua. Pili ilikuwa kueleza mfumokristo.Hili mshalijua.
Kwetu nyie kuamini kuwa lipo tatizo si muhimu sana kwa sasa.
Tunaweza tukafanga mjadala ikiwa mtapenda.
Mjadala utajifunga wakati muafaka ukiwadia kwasasa subiri kidogo maana naona dalili za kukimbia nondo tulia kidogo bin mwekapopo.
Nasi pia kama wewe nia yetu si kuingia humu kumeza kila kitu hata ambacho hakihitaji elimu ya darasa la 5C.
Mohamed, wewe kakwambia nani unazungumza kama ''waislam''?
wewe zungumza kwa niaba ya wa Narung'ombe na Kipata, mchikikichi na Tandamti.
Hili la mfumo kristu hujaweza kulieza wala kulitetea kwa hoja au kwa mantiki.
Ni kwa sababu hizo hata watu wanaomeza ngano hii wameishia kuadhirika pale wanapoulizwa mfumo huo unafanyaje kazi.
Mfano, umesema kuwa uchaguzi uliopita waislam wamehimizana kumchagua mwislam.
Ukweli ni kuwa hawakuhamasishana hizo ni hisia zako.
Ingalikuwa hivyo basi asilimia 86 ya mwaka 2005 ingefikia 90 na ushee na badala yake imepungua na kufikia 60 hata kwa ulaghai! maana yake wale uliowashawishi wengine hawakukubaliana na ushawishi wako.
Lakini basi kama waislam wanauwezo wa kumchagua kiongozi wa nchi hii, nini kinawashinda kuvunja mfumo kristo unaoundwa pengine na makatibu kata au watendaji vijiji.
Siamini rais aliyewekwa na waislam angekuwa hana uwezo wa kuuvunja unless uniambie naye ni kafir kama BAKWATA.
Tumekusihi utupe specifics za jinsi gani mfumo huo unafanya kazi huna jibu. Jibu ulilotoa lisilo na chembe ya usomi ni kuhusu utafiti uliofanywa na warsha. Utafiti huo uliokuwa na majibu andalizi umeshindwa kabisa kuthibitisha kuwa tatizo la elimu lipo vyuo vya juu zaidi ya kutoa namba ambazo mpuuzi anaweza kuziamini.
Mohamed, sekomdari yenye watoto 250 na walimu 2 itatoa division 0 za nguvu, division 0 haziruhusu kwenda high school.
Asiyekwenda highschool anapunguza nafasi yake ya kuingia Chuo kikuu.
sasa unapoangalia chuo kikuu huangalii watu wanafikaje huko ni ulaghai wa kiwango cha Cambridge!
Tumekuomba utupe tafiti kuhusu mfumo wa elimu kuanzia msingi hadi sekondari, huna jibu bali unajibu la kuingia chuo kikuu kwa upendeleo. Mohamed, huwezi kupata mwanafunzi kama hajafanya mtihani.
Hapa ni lazima watu watumie akili za kuzaliwa tu haihitaji certificate au degree kubaini uzushi huu!
Shule ikifungwa maana yake hakuna wanafunzi na hakuna watahiniwa na hatima yake hakuna chuo kikuu.
Kama nilivyosema hapo awali historia ya nchii hii katika uvunjifu wa amani haitakamilika kama jina lako halitakuwepo.
Ukisoma habari ya njozi kuhusu rise of religious tension ni wazi kuwa wewe na yeye mna malengo dhidi ya watu fulani.
Kama ulivyomshambulia Mkapa wakati akiwa mhariri ndivyo njozi anavyomshambulia na kusahau kuwa kiongozi aiyekuwepo kabla ya Mkapa ni Mwinyi. Mnajifanya hamnazo katika kujua uvunjaji wa mabucha!!
Hatari kubwa ambayo haionekani ni jinsi unavyojenga chuki katika jamii.
Hatari kubwa ni jinsi unavyoipumbaza jamii ya waislam. Hakika siku wakibaini uzushi na upotoshaji wako watasikitika sana.
Kwa vijana wengi mnaosoma mijadala kama hii, labda niwaase kuwa lazima uwe na kibakuli kidogo cha kuweka nafaka na gunia tupu la kujaza pumba. Usichanganye maana utapata taabu mbele ya safari, kuna pumba zinang'aa kama nafaka.
Pili, labda niwagusie na kuwaibia siri ya jinsi gani mfumo kristo unafanya kazi
-Kama unakwenda kisutu kusikiliza kesi ya Ponda na kuacha darasa, mfumo kristo utakuumiza
- Kama unakaa barazani na kujadili majina ya watu na harakati zao mfumo kristo utakuumiza
- Kama utasoma takwimu na ukagoma kuzielewa bali kuzitamani, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huiangalii Tanzania na duni kwa upana wake unafikiri chuo kikuu kisichokuwepo, mfumo kristo utakuumiza
-Kama huangalii tatizo kama tatizo bali kutafuta namna ya kuficha ukweli, mfumo kristo utakuumiza
- Kama umeridhika kuwa wewe ni dhalili na dhaifu kwasababu kuna mtu kaazima akili zako na hatakikukurudishia, utaumia
-Kibaya zaidi ukishindwa kutumia chembe ya akili akaamua kuiweka rehani basi hilo ndilo tatizo kubwa kuliko yote hapo juu na mfumo kristo utaanza kukupiga bakora hapo hapo ulipokaa kitako,and guess what you will never recover