Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said,huu msikit wa maamur,upanga ndio upi au ndio wa tambaza?? Upanga ipi hasa ilikuwa mali ya tambaza,maana in many places upanga kuna nyumba za kijerumani which my take could not have belonged to Tambaza

Kwa kukuongezea mpaka eneo la Muhimbili Hospital lilikuwa mali ya Tambaza.

Unauliza kubisha au unauliza kufahamishwa.
 
Last edited by a moderator:
Mmmmmh nabaki kushangaa tu! Sawa mkuu tusonge mbele mwanaharamu apite!

Ehee kitabu hicho kinaandikwa na nani?

Sahib yangu Yericko Nyerere,

Mbona unaniangusha?

Baba yetu anaandikiwa kitabu na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ndiyo
wafadhili wewe huna habari hii muhimu...

Mbona ilitangazwa kwenye Kigoda Cha Mwalimu Nyerere na wanaoshughulikia
hiyo ni Prof. Saida Othman Yahya na Prof. Issa Shivji.

Kitabu kipo njiani ndugu yangu.

Huenda nami nikafanyiwa mahojiano maana wameambiwa nina nyaraka na taarifa
nyingi kuhusu siku za awali za Nyerere Dar es Salaam.

Ndiyo nakuambia sahib wangu jitulize usome kwanza kisha ndiyo uingie katika mnakasha.
 
Kwa kukuongezea mpaka eneo la Muhimbili Hospital lilikuwa mali ya Tambaza.

Unauliza kubisha au unauliza kufahamishwa.
nauliza kufahamishwa,kabla ya kuitwa muhimbili,hospital iliitwa sewa haji,baadaye ikaitwa princess margerat-sasa huyo TAMBAZA itakuwa mwaka gani?maana years dont add up
 
Sahib yangu Yericko Nyerere,

Mbona unaniangusha?

Baba yetu anaandikiwa kitabu na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ndiyo
wafadhili wewe huna habari hii muhimu...

Mbona ilitangazwa kwenye Kigoda Cha Mwalimu Nyerere na wanaoshughulikia
hiyo ni Prof. Saida Othman Yahya na Prof. Issa Shivji.

Kitabu kipo njiani ndugu yangu.

Huenda nami nikafanyiwa mahojiano maana wameambiwa nina nyaraka na taarifa
nyingi kuhusu siku za awali za Nyerere Dar es Salaam.

Ndiyo nakuambia sahib wangu jitulize usome kwanza kisha ndiyo uingie katika mnakasha.

Kama ni hicho na washarika ni hao, sina neno kwakuwa taarifa ninayo,

Nilidhani ni wakujitegemea kama ulivyofanya wewe na ngano/simulizi za wazee wako!
 
Bw. Said, mke wa marehemu Abdul aliwahi kumsikia mumewe akimtuhumu Nyerere kuwa alikuwa na njama dhidi ya Uislamu au Waislamu?
 
Naona umeamua kujifariji na kujiliwaza hakuna nondo za kumkimbiza Mohamed Said, hujui kama watu walikuwa wanatafuta hii nafasi ya kueleza haya.

Wewe upo hapa kutetea Ukirstu wako na Mohamed Said yupo hapa kutetea Uislam hakuna haja ya kutishana wasomaji ndiyo wataamua.

Mohamed Said kaamua kula JF, kulala JF, kushinda JF, halafu unasema bado kidogo akimbie wakati yeye kaamua kutoa dasra.

Watu wanatamani huu munakasha uendelee hata mwaka.
Ritz kama mkakati ulikuwa fursa ya kueleza, nadhani ni mkakati mbovu sana maana hata wale waliokuwa na shaka sasa hawana shaka tena!

Ame adulterate kila kitu na kufanya watu wasome wakiwa na macho mawili. Hizi ndizo mbinu za ajabu sana halafu huyo mwenye mbinu hizi ndiye kiongozi wa waislam kwa mujibu wake. Please Waislam deserve better than that!
 
wonders will never cease,yaani mohamed Said anaona Kissinger na Prof Mazrui wanampaka Nyerere siagi!!

"Dr. Henry Kissinger, an arrogant intellectual, acknowledged Nyerere's brilliance and was even outwitted by him during the Rhodesian crisis as documented by the author (see Appendix IV). He also got a potent "dose of African nationalism," as David Ottaway wrote in The Washington Post, when he met President Nyerere in Tanzania in 1976 to discuss the Rhodesian crisis. They differed on how to resolve it, prompting reporters to ask Nyerere if he thought Kissinger's mission to Africa was a failure. As David Ottaway who covered the event wrote in The Washington Post: "Nyerere responded professorially by saying, 'A mission of clarity is not a mission of failure.' " Kissinger, a former professor at Harvard, got a good lecture on African nationalism and the Rhodesian crisis from Nyerere, a man of immense intellect Africa will always be proud of. He was indeed a colossus who did bestride this narrow world, as Kenyan Professor Ali Mazrui put it in his moving tribute to one of the giants of this century.
 
Last edited by a moderator:
nauliza kufahamishwa,kabla ya kuitwa muhimbili,hospital iliitwa sewa haji,baadaye ikaitwa princess margerat-sasa huyo TAMBAZA itakuwa mwaka gani?maana years dont add up

Ukitulia kwaumakini utagundua mengi sana yaliyopandwa bila kuwa halali katika historia ya nchi hii,

Mzee Mohamed Said amewapanda watu katika mkkumbo wa wapigania uhuru hata ambao hawakkushiriki tu, ilimradi tu walikuwepo enzi za harakati basi waiitwe wapigania uhuru!

Baadhi ya wazee anaowalilia Mohamed Said hawakusikika wala kuhisiwa kuwepo kwenye mbio za kuusaka uhuru, alichokifanya Mohamed ni kuwakusanya wale mashekhe waliokuwepo enzi za harakati na kuwachanganya na kundi la ukombozi kwamgongo wa dini tu!
 
Ritz kama mkakati ulikuwa fursa ya kueleza, nadhani ni mkakati mbovu sana maana hata wale waliokuwa na shaka sasa hawana shaka tena!

Ame adulterate kila kitu na kufanya watu wasome wakiwa na macho mawili. Hizi ndizo mbinu za ajabu sana halafu huyo mwenye mbinu hizi ndiye kiongozi wa waislam kwa mujibu wake. Please Waislam deserve better than that!

Nguruvi,

Siwezi kukupinga.
Kwa nini nikupinge na kila mtu ana fikra zake?
 
Ukitulia kwaumakini utagundua mengi sana yaliyopandwa bila kuwa halali katika historia ya nchi hii,

Mzee Mohamed Said amewapanda watu katika mkkumbo wa wapigania uhuru hata ambao hawakkushiriki tu, ilimradi tu walikuwepo enzi za harakati basi waiitwe wapigania uhuru!

Baadhi ya wazee anaowalilia Mohamed Said hawakusikika wala kuhisiwa kuwepo kwenye mbio za kuusaka uhuru, alichokifanya Mohamed ni kuwakusanya wale mashekhe waliokuwepo enzi za harakati na kuwachanganya na kundi la ukombozi kwamgongo wa dini tu!

Karibu sahib yangu karibu.
 
wonders will never cease,yaani mohamed Said anaona Kissinger na Prof Mazrui wanampaka Nyerere siagi!!

"Dr. Henry Kissinger, an arrogant intellectual, acknowledged Nyerere's brilliance and was even outwitted by him during the Rhodesian crisis as documented by the author (see Appendix IV). He also got a potent "dose of African nationalism," as David Ottaway wrote in The Washington Post, when he met President Nyerere in Tanzania in 1976 to discuss the Rhodesian crisis. They differed on how to resolve it, prompting reporters to ask Nyerere if he thought Kissinger's mission to Africa was a failure. As David Ottaway who covered the event wrote in The Washington Post: "Nyerere responded professorially by saying, 'A mission of clarity is not a mission of failure.' " Kissinger, a former professor at Harvard, got a good lecture on African nationalism and the Rhodesian crisis from Nyerere, a man of immense intellect Africa will always be proud of. He was indeed a colossus who did bestride this narrow world, as Kenyan Professor Ali Mazrui put it in his moving tribute to one of the giants of this century.

Son...

Sijapata kuthubutu kushusha uwezo wa Nyerere hata siku moja.

Ninachosema ni kuwa katika hili la kuasisi TANU...panahitaji
maelezo.

Hili la EAMWS na Sheikh Hassan Bin Amir pana hitaji maelezo.

Mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika ipo historia
nyingine ya wazee wangu.

Ni hayo tu ndugu yangu.

Umesoma taazia niliyomwandikia Nyerere ilichapwa na Mtanzania.
Itafute Insha Allah.
 
Bw. Said, mke wa marehemu Abdul aliwahi kumsikia mumewe akimtuhumu Nyerere kuwa alikuwa na njama dhidi ya Uislamu au Waislamu?

MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Wewe umekuwa kichwa cha gramafoni na santuri yenye shimo?

Nyerere, Nyerere, Nyerere...
 
Bw. Said, mke wa marehemu Abdul aliwahi kumsikia mumewe akimtuhumu Nyerere kuwa alikuwa na njama dhidi ya Uislamu au Waislamu?

MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Wewe umekuwa kichwa cha gramafoni na santuri yenye shimo?

Nyerere, Nyerere, Nyerere...
 
Ame adulterate kila kitu na kufanya watu wasome wakiwa na macho mawili. Hizi ndizo mbinu za ajabu sana halafu huyo mwenye mbinu hizi ndiye kiongozi wa waislam kwa mujibu wake. Please Waislam deserve better than that!

Kusema ukweli binafsi nasikitika kuona vijana wa Kiislamu ambao wana nia njema kwelii na wanataka kujua sana wanaamini habari za Mohammed Said bila kuzihoji. Wanaamini si kwa sabbau wanajua ni kweli bali kwa sababu mzee anaonekana anautetea Uislamu na hivyo kumuuliza au kumkatalia kunawafanya wajihisi kama hawautendei haki Uislamu. Hii si sahihi kwa sababu ni mbinu ya 'sympathy' ambayo kwa kweli kwenye ukweli haina nafasi.

Maandishi ya mzee Said yanahitaji kuangaliwa kwa mwanga wa kisomi tu; hoja zake hata zingetolewa na mpagani bado zingeangaliwa kisomi. Ni jukumu la mtu yeyote mwenye akili kuuliza maswali mbele ya mtu anayetoa madai. Lengo si kumdhalilisha mtoa hoja bali kumsaidia mtoa hoja kuelezea vizuri hoja zake, kuzisahihisha na hata kuzitetea vizuri. Binafsi naamini Waislamu na hasa wale mashabiki wa Bw. Said waanze kumuuliza maswali ya akili ili kuupata ukweli vizuri.
 
MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Wewe umekuwa kichwa cha gramafoni na santuri yenye shimo?

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu kama uaminivyo,

Kuna hoja ya nera sana ndani ya fikra huru za Mwanakijiji

Tulia rafiki yangu, tulia ujibu, tulia ujisomeshe, tulia upembuke mwana wa Hajir
 
Sahib yangu Yericko Nyerere,

Mbona unaniangusha?

Baba yetu anaandikiwa kitabu na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ndiyo
wafadhili wewe huna habari hii muhimu...

Mbona ilitangazwa kwenye Kigoda Cha Mwalimu Nyerere na wanaoshughulikia
hiyo ni Prof. Saida Othman Yahya na Prof. Issa Shivji.

Kitabu kipo njiani ndugu yangu.

Huenda nami nikafanyiwa mahojiano maana wameambiwa nina nyaraka na taarifa
nyingi kuhusu siku za awali za Nyerere Dar es Salaam.

Ndiyo nakuambia sahib wangu jitulize usome kwanza kisha ndiyo uingie katika mnakasha.
Ha ha haaaaaaaaaaaaaa mzee Mohamed umenifurahisha umemwambia bwana mdogo atulize baal kabla kuingia kwenye mnakash
 
MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Ooh pole sana mzee mwenzangu; ninafahamu nina kawaida ya kuwachosha watu kwa udadisi wangu. Vumilia tu ninajua ulizoea mawazo rahisi rahisi yasiyochosha.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Ala! Sasa mbona wewe huachi kusema "wazee wangu, wazee wangu, wazee wangu"? Ukiacha nami nitaacha... vinginevyo tuendelee kubanana humo humo.

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Hujaichambua lolote; nilitaka kusema na kukuuliza maswali lakini najua ungepeperuka tena kama kipepeo anayetafuta maua... Ungekuwa unaujasiri wa kujibu maswali basi santuri hii isingekwama.
 
MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Wewe umekuwa kichwa cha gramafoni na santuri yenye shimo?

Nyerere, Nyerere, Nyerere...
haya majibu,haya majibu -inabidi ujue tofauti ya kariakoo shimoni na JF,street wise answers humu si mahali pake-lazima unajua kwamba watu wanafuatilia sana-either kaa kimya au jibu kiungwana,kebehi za kimjini hapa si mahali pake
 
Back
Top Bottom