zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Katika hotuba ya kitaifa huwezi kuanza kusimulia yaliyojiri,
Mwalimu alilitambua hilo ndiomaana alisimamia hapo!
Alisimamia wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika hotuba ya kitaifa huwezi kuanza kusimulia yaliyojiri,
Mwalimu alilitambua hilo ndiomaana alisimamia hapo!
Nataka unijuze, amma wewe, amma Yericko Nyerere, amma Juliasi Nyerere, yupi tukubali ndio mkweli kama nilivyoainisha kwenye post #5300 . Kuna japo mmoja atakuwa si mkweli. Fafanuwa.
zomba,
Hakuna cha kujadili hapo. Msioufahamu UKATOLIKI mnadhani URAIS wa Mwalimu katika Tanganyika na baadae Tanzania ndio utakaompatia utakatifu. Actually, kazi hii ya Urais itamchelewesha au kumnyima kabisa utakatifu kwa kuwa kuna watu alitia saini wanyongwe kwa mfano.Naona umejikita zaidi kujadili picha, vipi hayo maandishi hutaki kuyajadili.
Ungeandika ya wazee wako tu bila kumbambikia Mwalimu tuhuma za UDINI, uasisi wa MfumoKristo, yeye kutokuwa muasisi wa TANU wakati yeye ndie RAIS wa KWANZA wa chama hiki, kuwachukia Waislamu wote,..., wengi tusingehangaika nawe. Ungeweka ushahidi wa wazi juu ya tuhuma hizi, wenye akili timamu tusingehangaika nawe.
Wewe mimba yako ilikuwa tayari?zomba,
Uhuru wa Tanganyika unapatikana mwaka 1961( sijui kama mzee wetu anaikubali tarehe hii, atakwambia uhuru tulikuwa nao vichwani na TANU yetu tangu mwaka 1929!) Mag3 alikuwa sekondari. Wewe kwa kukusoma humu unavyoandika, hata mimba yako haikuwepo! Hauwezi kujilinganisha naye. Endelea kuwa mfuasi mtiifu tu wa mzee wetu.
zomba,
Uhuru wa Tanganyika unapatikana mwaka 1961( sijui kama mzee wetu anaikubali tarehe hii, atakwambia uhuru tulikuwa nao vichwani na TANU yetu tangu mwaka 1929!) Mag3 alikuwa sekondari. Wewe kwa kukusoma humu unavyoandika, hata mimba yako haikuwepo! Hauwezi kujilinganisha naye. Endelea kuwa mfuasi mtiifu tu wa mzee wetu.
Ndio wimbo wako huu "nina mengi mengine, hamtaki kuyasikia?" Halafu hayaji! Au unataka kuyaleta kama tafiti na simulizi? Hauna na hautakuwa na jipya hadi upate wasimulizi wapya.
amewataja baadhi
ya wazee wako wa kiiislam waolivyojiingiza katika siasa vilevile kama
Shehe Mohammed Ramia? Naona kama kawaida yako unahamisha magoli. Umesema
ati baadhi ya wazee wako walikuwa hawajawahi kutajwa katika siasa za
Tanzania kuwa hadi wewe ulipokuja ndio kina Shehe Ramiya wanatajwa
katika siasa. Sasa umehamisha magoli na kudai haijawahi kuandikwa
historia ya TANU kama ulivyoandika wewe.
Sasa hiyo si uamuzi tu wa mtunzi? Kila mtunzi ana namna yake ya
uandishi. Wallahi nikiamua miiye kuandika haitofanana na wewe vile
vile.
Hakuna cha kujadili hapo. Msioufahamu UKATOLIKI mnadhani URAIS wa Mwalimu katika Tanganyika na baadae Tanzania ndio utakaompatia utakatifu. Actually, kazi hii ya Urais itamchelewesha au kumnyima kabisa utakatifu kwa kuwa kuna watu alitia saini wanyongwe kwa mfano.
KASUMBA YA MKOLONI
Ndugu zangu kwanza niwasalimieni - Aslaam aleikum na Amani iwe juu yenu..
Nawaomba sana mnaposoma maandishi yangu haya mtafakari sana juu yenu na kuzihoji nafsi zenu ktk UTAIFA wenu maanake hili neno kasumba ya mkoloni lilitumika sana zamani zama zetu za ujana, sasa hivi limepotea sana kutokana na kwamba ile kasumba imekuwa sehemu ya maisha ya kila Mtanzania (utamaduni)..
Labda niwakumbushe kidogo tu juu ya harakati za Uhuru wa nchi yetu na pengine baadhi yenu mtajikuta katika kundi mojawapo la hawa watu nitakaowataja...Ni hivi, wakati harakati za UHURU zinaendelea kulikuwa na makundi matatu moja likiwa lile la UMOJA wetu, jingine la Kidini na la tatu la Kikabila na makundi haya yote yalitumika ktk siasa za mwanzo ktk kuutafuta Uhuru kutokana na ile kasumba ya mkoloni..
Sasa ifanmike tu ya kwamba Mkoloni alitumia sana ujanja wa kugawa watu ili apate kutawala na nyie wadhungu mnaita devide and rule ambayo kwa ajabu kabisa mnaijua sana athari zake lakini kwa sababu ya kasumba ile tulilishwa na imekuwa genetic ktk bongo zetu. K
Kila napowasoma hua nacheka sana maana kasumba hiyo hutafsiri kila neno mnaloandika humu JF..na ajabu ya Mungu mtu kama Mohammed Said, msomi na mtu alolaani sana kasumba ile ndiye wa kwanza leo hii kuendelea kuisheheneza kama vile ilikuwa sifa pasipo kuelewa ya kwamba wale anaowataja leo hii na kuwapa sifa zote za Uzawa wao ama Uislaam wao ndio walopinga vikali kasumba ile ya mkoloni halafu anajirudi na kuwavuta tena wale wenye kasumba ya mkoloni na kuwaweka kundi moja - Nitamwambia kwa nini?
Wote wanachanma wa TANU toka Abdul Wahid Sykes na wengine wote hata baada ya Nyerere alipojiunga wakaunda TANU na wakabakia TANU hadi UHURU wetu, ni wale waliotaka UMOJA wa Mtanganyika isipokuwa kundi la wachache waliojichomoa uanachama kwa sababu ya kasumba ya mkoloni walojazwa ujinga. Hao ndio pamoja na kina Hassan bin Amir, kina Takadir ambao waliona kwa nini waislaam wawe bega kwa bega na mkristu ambao mkoloni aliwapa nafuu zote maisha na hawa ndio endelezo la kizazi hiki cha kina Mohammed Said.
Wapo pia wale walochukia kwa nini wakristu wanajiunga na waislaam kuutafuta Uhuru wakati wao hawana shida yoyote wakaunda vyama vyao vile vile na hawa ndio kizazi hiki cha kina Mtikila, mchungaji Munisi na wengineo. Wote hawa kama utakuwa na kasumba kama yao hutayaona makosa isipokuwa utawapa sifa zao kwa kile ambacho wewe mwenyewe umeuziwa kasumba hiyo na kuona tu njia pekee ya kujijenga ktk makundi yetu ya dini ama makabila...
Maadam kasumba ile ipo kichwani utajikuta tu unawasifia watu kama Mojammed Said ama Mtikila kwa sababu wewe mwenyewe umerithi kasumba ile..Sasa kinachonishangaza miye ni kuwasoma watu wakitaka kuona sifa ziliwafikia baadhi ya watu kwa sababu ya jitihada zao ktk kuutafuta UHURU wetu wakati sisi wenyewe tunashindwa kuzitunza ama kuzienzi historia zetu wenyewe. Sisi Wadanganyika hata historia za ukoo ama kizazi chetu hatuna naweza kusema hata makaburi ya mababu na mabibi zetu hatujui yalipo.
Mohammed Said kwa jeuri kabisa anadiriki kutumia majina ya watu ambao wao walikubali kubakia TANU wakajitenga mbali kabisa na sifa zile walozitaka AMNUT za Uislaam kuwa nguzo ya uanachama na malengo ya ukombozi, halafu anawatumia hawa kuuzungumzia Uislaam?. Kwani unataka kunambia kweli kina Sykes hawakujua kama AMNUT ni chama cha waislaam? na kama walijua na wao Waislaam kwa nini hawakujiunga na wenzao ama wao alikuwa wakristu pindi walipobakia TANU pamoja na kina Nyerere..
Na kwa wale waliokuwepo ktk masiba wa AbdulWahid watakwambia hawakuwahi kumwona Nyerere mnyonge na akilia kama mtoto mdogo isipokuwa siku alokufa AbdulWahid Sykes, Nyerere alikuwa mdogo na hakika marehemu alizikwa!..Sasa wewe unayempenda sana Marehemu Abdul Sykes ni mara ngapi umewahi kulitembelea kaburi lake ama hata kuuliza liko wapi na ukaenda kuweka hata shada la maua?.Huyo Mwinyi ama Kikwete ameweza kuwaenzi watu hao kwa nini iwe Nyerere tuu ndioye mwenye kmakosa lkn wale walopewa dhamana sawa na ile ya Nyerere wasifanye pia wasiwe na makosa yale yale?..
Sidhani kuna sababu isipokuwa Ndivyo tulivyo. sisi wote ni mazao ya kasumba ya mkoloni, ndani ya vichwa vyetu bado kasumba hiyo ipo isipokuwa tumeshindwa tu kujiyambua..Kina Sykes hawakupendwa na baadhi yenu kwa misimamo yao tena baadhi walimwona kama mnafiki wakahoji hadi Uzawa na Utanganyika wake kwa sababu ya kuwachia Nyerere kuwa mwenyekiti hata baada ya uchaguzi wa kwanza akiwa yeye ameshinda kwa kura chache..Hao kina Takadir mnaowasifia ndio walokuwa na kasumba maana sidhani kama Mohammed Said umewahi kuuliza kwa nini Dr. Kyaruzi hakuenziwa ama kusifiwa kama muasisi wa chama?..Na hata ukichukua list nzima ya wazee wote walokuwepo TANU utakuta hakuna mwenye kubebeshwa sifa iwe Muislaam ama mkristu - hakuna, sasa iweje watu mchague baadhi ya majina ya watu kuyatolea mifano?
Nadhani imetosha kwa leo, ila nawaomba sana jaribuni kuifuta hiyo kasumba ya mkoloni akilini mwenu...maana unapoandika lolote kuhusu Nyerere kisha ukautumia Ukristu wake kuwa sababu ya kuijengea hoja fahamu ya kwamba wewe pia una KASUMBA maana Nyerere hakujitenga na TANU ilojaa waislaam bali aliungana nao na kuifanya TANU kuwa chama kisichokuwa na dini wala kabila...Pia ukiandika lolote juu ya AbdulWahid ukautumia Uislaam wake basi jua wewe pia una kasumba ya mkoloni maana Sykes hakujitenga na wakristu ktk jitihada za kuutafuta Uhuru wetu bali aliungana nao na kushikamana nao wakaunda katiba ya chama. Na huu ndio Ushindi wa TANU kuvishinda vyama vyote na wale wote walojazwa UJINGA maana unapojiona wewe kwa imani ama uzawa wako, ndivyo mkoloni alivyotaka uwe na kawapata wengi tu ambao ujinga huo wanauendeleza hadi kizazi hiki.
Ni rahisi sana kuandika neno - Devide and rule kama mkakati wa mkoloni ukashindwa kujitambua mwenyewe kuwa ni zao la kasumba hiyo hasa pale unapoandika hoja inayokutenga wewe na Watanzania wengine. Sisi ni WAMOJA na tulijiunga na TANU kwa sababu hiyo kwanza acha hizi habari za siasa za leo hii. Hivyo kama wewe unajiona tofauti na hutaki UMOJA ina maana wewe ni ktk kundi la wale kina Hassan Amir ama kina Mtenvu....ambao kwa hakika walijazwa Ujinga - Kasumba ya mkoloni.
Nawasilisha.
Kwa nini yanatokea sasa miaka 14 baada ya kifo cha Mwalimu? Haya ni matokeo halisi ya UDINI ulioachwa kuhubiriwa na akina Mzee Mohamed kwa muda mrefu sasa. Mkristo anajiuliza: Kwanini Muislamu achinje tule sote lakini mkristo akichinja ale mwenyewe?Siku zote huwezi ficha pembe la ng'ombe.
haya sasa yale yaliokuwa yamefichikana sasahivi yapo dhwahir shahir. Je umesikia yale ya kule Buseresere na katoro?
ndicho alichopanda kwa kificho JKN. sasa kipo hewani.
Kwa nini yanatokea sasa miaka 14 baada ya kifo cha Mwalimu? Haya ni matokeo halisi ya UDINI ulioachwa kuhubiriwa na akina Mzee Mohamed kwa muda mrefu sasa. Mkristo anajiuliza: Kwanini Muislamu achinje tule sote lakini mkristo akichinja ale mwenyewe?
Haya, kulikuwa na haja kuivamia bucha ile ya nyama iliyochinjwa na Mkristo? Tatizo la kuelewa tu!
Mimi mzee Ritz. Hata keyboard nadonyoa herufi mojamoja.Wewe mimba yako ilikuwa tayari?
Ndio wimbo wako huu "nina mengi mengine, hamtaki kuyasikia?" Halafu hayaji! Au unataka kuyaleta kama tafiti na simulizi? Hauna na hautakuwa na jipya hadi upate wasimulizi wapya.
Mimi mzee Ritz. Hata keyboard nadonyoa herufi mojamoja.
Kumbe hapa ni "nepotism" ya Kikariakoo na kidini inaendelea. Kuhusu lugha hata wewe zomba? Umesahau ile ya Abdu kumuweka ndani Mwalimu? Hongera kama mafundisho ya Maalim Haruna yamekuokoa.Pitia tena nyuzi utaukuta umri wangu humuhumu, inaonesha unarukaruka. Nimezaliwa kabla ya kuzaliwa TANU wacha Uhuru.
Mie nyumbani kwetu ni nyumba ya tatu kutoka ilipozaliwa TANU. Usione nakesha humu, wazee wengi wanaoelezewa humu nami ni wazee wangu amma wao nawafahamu amma watoto zao amma wajukuu zao ni marafiki zangu na tumekuwa pamoja Kariakoo. Labda huelewi mshikamano uliokuwa Kariakoo enzi za wazee wetu, wote walikuwa ni wazee wetu na sisi sote tulikuwa amma watoto zao amma wajukuu zao.
Hawakututofautisha nasi hatukuwatofautisha, kwa kabila zetu wala kwa rangi zetu wala kwa huyu wa fulani yule wa fulani, hili likumbuke na ujiulize, kwanini?
Kuhusu hili la mimba nadhani si lugha njema, na hapa tumepewa darsa na Maalim Mohamed Said aliyoakifundishwa na Maalim wake, Maalim Haruna nasi imetuingia vizuri sana, vipi wewe basi hata kidogo haijakuingia?
Weka picha ya Ali Hassan Mwinyi akiwa na Papa hapa Ikulu yetu. Hii ya Mwalimu ilipigwa Vatican. Kwa miaka yote 24 alioongoza nchi hii hakuna Papa aliyetembelea hapa kwetu.
Mohamed Said, kabla sijafanya reference na kucomment, Je historia iliyoandikwa katika kitabu hiki ni sahihi au nayo imepotoshwa??????? Maana imezungumzwa sana hii historia iliyopotoshwa lakini vitabu vilivyopotosha havitajwi. Ila nachokiona from your side ni kwamba you have freedom to choose anywhere ku-cite references zako iwe Tanzania, Cambridge Uni Press, Amazon.com, Marekani u name it. A freedom I suspect is somehow limited to some of us thru branding na unguided limitations.
"Voices from Tanganyika: Great Britian, the United Nations and the decolonization of a Trust Territory, 1946-1961" By Ullrich Lohrmann
Nyambala, Tafadhali tuelewane. Kitabu ambacho si sahihi katika historia ya TANU ni hiki:
"Kivukoni Ideological College, Historia ya Chama Cha TANU 1954-1977, DaresSalaam,1981."
Ikiwa umefuatilia makala zangu katika Mwananchi na ukaja kusomakitabu hicho utapigwa na butwaa maana hiyo yao si historia ya TANU. Hayumo Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz, Sheikh Hassan Bin Amir, Sheikh Suleima Takadir, Mshume Kiyate, Bibi Titi Mohamed, Bi Tatu Bint Mzee nk. Hiyo si historia ya TANU ni kitu kingine kabisa.
Hicho kitabu ulichotaja kwa bahati mbaya sijakisoma kwa hiyo siwezi kusema kitu. Ilani hivi vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusu historia Tanganyika na kugusia"nationalist politics" haya niliyoandika hayamo ingawa wemeeleza mengikwa kupitia kijuujuu tu ukiondoa The Making of Tanganyika cha Judith Listowel,1965.
Asante sana Mohamed Said kwa kuliweka hili wazi kuhusu kitabu hiki cha "Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981." Kusema ule ukweli jina tu la hicho kitabu linanifanya hata nisiwe na hamu ya kukisoma au kukitafuta. Kitabu nilichokielezea hapo juu nimekikuta kwenye makabrasha flani na nimekisoma fasta fasta maana sikuwa na muda. Weekend hii nikipata nafasi ntakipitia tena mstari kwa mstari maana kuna vitu interesting ningependa tujadili.
Lakini pia kwa kukumbusha umewahi kutuhumu kwamba vitabu vinavyotumika mashuleni kusomeshea historia navyo vimepotosha unaweza kututajia mifano tafadhali ukiondoa huki cha CCM.
Kabla sijaendelea nawaomba wana JF mpitie hivi vipande vifuatavyo, myasome kwa umakini muweze kujua angalau kwa kifupi tu EAMWS East African Moslem Welfare Society anayodai Mohamed Said kwamba ilivunjwa na Mwalimu Nyerere ilikuwa ni nini hasa na ilianzishwa na nani halafu -
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Aliyeandika haya anaitwa Ulrich Lohrmann.
- baadaye tutaendelea............
Mag3
Please usituletee data za kutengenezwa, TUMEZICHOKA; KWA SABABU ZIMETENGENEZWA. Tunataka credible sources please!!
Jasusi, Habari nilizoelezwa na wazee wangu naziamini kuliko vitabu elfu vya wanahistoria ambao hawakuwapo wakati wazee wangu wanapambana na ukoloni wa Waingereza.
Nionyeshe jipya lolote la mzee wetu huyu mbali na nukuu za vitabu na machapisho yake mwenyewe na Padre Sivalon.Unaonesha huusomi uzi, unakurupuka, anza mwanzo uone mtiririko wa nyundo zinavyoshuka, kila moja inaishinda iliopita, kila Mohamed Said akiuliza niishie hapa, watu kimyaaaa. Huoni? basi hata husikii?