Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,061
typical mswahili,wewe lazima ulikuwa mteja mzuri wa kitonsa hapo livingstoneHakuna kitu kama hicho, kuna mkate wa kumimina.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
typical mswahili,wewe lazima ulikuwa mteja mzuri wa kitonsa hapo livingstoneHakuna kitu kama hicho, kuna mkate wa kumimina.
Kila siku nakuambia wewe ni mtupu sana kwenye historia ya Tanganyika.Mnamo 1929 sir Cameron aliamua kuwaweka pembezoni mwa starehe za weupe na hasa baada yakuona anakereka kuwaona weusi hao wakiwa jirani sana na maeneo yao muhimu ya burudani na starehe,
Katika kuwaweke mbali aliamua kuwaanzishia kikundi/chama chao cha kushughulikia starehe zao, na Matola akawa ndie kiongozi wao wa kwanza mpaka 1933 alipofariki,
Mwaka 1933 ndipo vibaraka wa mjerumani akina Klest Sykes ambao ni wazamiajia wa Afrika ya kusini waliingia ndani ya chama hiki nao wakaja na malengo yao ambayo ni kudai haki katik himaya za muingereza, katika kuhakikisha dai lao linatiwa nguvu, waliazimia kubadili jina la chama/kikundi liendanena malengo yao na kuwa TAA.
Mwalimu Nyerere alipojiunga na TAA nae akaja na filosofia yake toka chama chake cha TAWA ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Ndilo chimbuko la kubadili jina la TAA na wakaanza kupendekeza majina na kuangukia TANU jina lililotolewa na Abdul aliyekuwa nalotangu akiwa Burma vitani,
Swali tusilokuwa na jibu mimi na wewe ni je Abdul alikuwa na ndoto ya chama chenye filosofia gani kabla ya makutano yae na Nyerere?
typical mswahili,wewe lazima ulikuwa mteja mzuri wa kitonsa hapo livingstone
typical mswahili,wewe lazima ulikuwa mteja mzuri wa kitonsa hapo livingstone
Nawe ukishindwa kujibu hoja unalazimisha kicheko.
Hakuna kitu kibaya kama utumwa wa kiakili...kwa hiyo wewe typical mzungu.
Sivalon aliongopa sana tu kuhusu composition ya Bunge letu. Hakuna wakati tangu uhuru Bunge letu limewahi kuwa na 70% ya Wabunge Wakatoliki. Majimbo yapi hayo nchi hii? Allegation hii pia iliwahi kusemwa kuhusu Cabinet mojawapo ya Mwalimu kwamba kajaza Wakatoliki mle. Mwalimu alipowatuma watu kuchunguza akakuta Wakatoliki ni yeye na Sir George Kahama ambaye hata hivo alikuwa amefanya maendeleo kama yangu. Ana wake wawili!
Mzee Mohamed Mohamed, Press conference ya Mwalimu pale Kilimanjaro Hotel, mwaka 1995, uliisikia?
kuna "stigma" attached ukiitwa mswahili ambayo siyo nzuriHajui kama ni sifa kubwa kuwa Mswahili.
Mohammed baada ya kusoma hii post kasema Mnh,Nimekusoma.Halafu kajiondokea zake.Napenda kujibu swali la mheshimiwa Mzee Said kama ifuatavyo. Kwa vile swali lake linadhania mambo kadha wa kadha naomba niainieshe mambo ambayo ni ya msingi na ya tofauti baina yetu kuhusiana na maandishi yake (points of contention)
a. Ulichoandika wewe kwanza siyo historia; ni histohisia. Umetumia matukio ya historia kuelezea hisia zako. Sasa kila mwanadamu ana hisia zake na hivyo hakuna mtu mwingine anayeweza kuwaangalia watu wale wale wa kihistoria (historical figures) na akatoa tafsiri ile ile hasa kama kuna tofauti kubwa ya hisia baina ya watu.
b. Kwa vile hukufuata kanuni za uandishi wa kihistoria (historical method) basi uandishi wako wa aina ya simulizi, vijembe, na kukisia hauwezi kuandikwa na mtu mwingine yeyote. Ukisoma John Illife aliyeandika kwa kufuata kanuni za historia na uandishi wako wewe tofauti ni kama bahari na mlima. Yeye aliandika kitabu cha historia kweli kweli.
c. Kwa vile umeamua kutumia dini kuangalia historia na kuilezea ni wazikuwa mtu mwingine asiyetumia dini anaweza kuangalia matkio yale yale unaoyaona wewe na akayapa tafsiri nyingine kabisa. Mimi niliposoma kitabu chako cha Sykes kwa kweli nilivutiwa na masimulizi ya majina ya watu mbalimbali. Lakini sikuvutiwa kabisa na ushawishi wa hoja. Katika kujenga hoja kwa kweli una udhaifu mkubwa mno kwani badala ya kutumia reason kujenga hoja unatumia 'emotional appeal' na ndio maana umewapata wengi kwa kugusa dini, imani yao.
d. Kwa vile matukio mengi unayoyasimulia yanatokana na yale unayodai ni mang'amuzi yako binafsi (personal experience) au ya kuambiwa (hearsay) na hivyo vyanzo unavyotumia haviwezi kuhojiwa na wanataaluma wengine ni wazi kuwa hicho unachodai ni historia kitabakia cha kwako peke yako. NInaamini udhaifu wako mkubwa kabisa katika uandishi wako ni hili - the failure to make it possible for other scholars to access the sources you claim to have used to get some information - for either these sources are dead, hidden or exclusively known to you.
Kutokana na hayo basi ni vigumu na haiwezekani mtu mwingine kuandika kuhusu wazee wako namna hiyo. Hata hivyo, inawezekana kabisa mtu kuandika historia ya Tanganyika kwa umakini mkubwa na kutaja baadhi ya majina uliyonayo vizuri zaidi.
Pamoja na hayo ni ukweli pia kuwa umejitahidi kuweka kumbukumbu ya wazee wako na kuyaacha majina yao yatajwe katika historia. Haya ni mafanikio yako makubwa - hata kama ndani yake umeweka limau, pilipili, mdalasini, tangawizi na pilipili manga.
0
Kituko kingine Mwanakijiji na Uislam au Waislam wapi na wapi jamani lini kwako Muislam hakawa na jema bahati nzuri mabandiko yako yapo mengi sana fikra zako kuhusu Waislam zipo wazi kabisa.
Ushawataja mpaka "Mkapa" eti wamemkolimba. Sasa unajidai unachojuwa not fit for print. Usilete utani kwenye mambo ya kitaifa, unajuwa sisi tuna uchungu sana wa kuondokewa na Nyerere.
kuna "stigma" attached ukiitwa mswahili ambayo siyo nzuri
Ukumbuke pia kuwa litmus test ya Mohammed na wengine wanaoshabikia simulizi lake ni kuwa Muislamu siyo Muislamu kama anapingana na 'wazee wake' Bw. Said au yule ambaye hakubaliani na the revisionist narrative ambayo Mohammed Said ameitengeneza. Ukimsoma sana ni kuwa Waislamu hawawezi kuwemo BAKWATA; na Waislamu ni lazima wakubaliane na kina Ponda na Farid, na lazima waamini uwepo wa dubwasha liitwalo Mfumo Kristu. Muislamu yeyote asiyekubaliana na kumkejeli, kumdunisha au kumbeza baba wa taifa hawezi kuwa Muislamu.
Kwa mtazamo wa hawa Uislamu siyo tena Kumwamini Mungu Mmoja na Mtume wake na haihusiani tena na kujisalimisha kwa Mnyezi Mungu. Kwao Uislamu umegeuzwa kuwa suala la nani anakubaliana na masimulizi ya Mohammed Said nani hakubaliani. Utaona kuwa katika wale wanaokubaliana na masimulizi haya wote wana alama zile zile:
- a. Kejeli kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (hawawezi kamwe kujenga hoja bila kumdunisha Nyerere)
- b. Chuki dhahiri dhidi ya Wakristu (hata kama ni ndugu zao wa damu)
- c. A revisionist outlook ya historia yetu (Sykes ndiye muasisi wa taifa, Waislamu ndio wapigania uhuru pekee, na Dar-es-Salaam ndio mahali pekee walikotaka uhuru; na Wakristu hawakutaka Uhuru isipokuwa baada ya kukaribishwa na Waislamu wa Dar)
- d. Wengi (kama siyo wote) bado ni watu wa CCM; chama kile kile kinachodaiwa kuendesha dhulma dhidi ya Waislamu ndicho hicho hicho kinakumbatiwa; serikali ile ile 'iliyounda BAKWATA' ndio hiyo hiyo inatarajia itatue matatizo ya "Waislamu". Utaona pamoja na malalamiko yao yote hutawasikia wanataka kuiondoa CCM madarakani!
Hizo ndizo alama zao...
Bahati mbaya wapo Maelfu kama sio mamilioni ya Waislamu ambao hawajalazimishwa kukubali alama hizi na wanaendelea kunufaika na kulitumikia taifa lao kwa uadilifu mkubwa; bado wanamuenzi Baba wa Taifa na bado wanatambua ushiriiiano wa wazee wote - bila kuwabagua kwa mahali, dini, au rangi - katika kupigania uhuru wa Taifa letu na umoja wetu.
Ndugu hebu nipe darasa wewe uijuae historia ya Tanganyika, Matola na Plantan nani aliingoza AA na kwa vipindi vipi?Kila siku nakuambia wewe ni mtupu sana kwenye historia ya Tanganyika.
Rais wa kwanza wa African Association ni mwalimu Thomas Plantan.
Hivi kuna kitabu ama maelezo yoyote yanayoonyesha mchango wa WAKRISTU ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika? - Kiasi kwamba wewe Mohammed Said umeona haikuwa haki kutowazungumzia Waislaam!Shwari,
Ahsante kwa yote.
Swala halikuwa ''credit'' na halitapata kuwa hili katika maandishi yangu.
Wala sitapenda kuzungumza kuhusu mchango wa Waislam katika uhuru
wa Tanganyika.
Kila mnakasha unavyosonga mbele ndivyo unavyopoteza kiini cha kitabu
changu.
Kwa mukhtasari kitabu changu kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British
Colonialism in Tanganyika.''
Kitabu kimeeleza ule mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika, mchango
ambao haukupatwa kuandikwa popote.
Hii ndiyo ''theme'' ya kitabu changu.
Kitabu kimewaudhi na kuwaumiza wengi.
Nimezungumza mengi humu na naamini wengi wamefaidaka kwa kusoma yale ambayo
hawakupata kuyajua au kuyasikia hata siku moja.
Hilo ndilo linalotusikitisha tuluo wengi tukimuona ndugu huyu akieneza sumu ya udini usio na tija kwa taifa.Hivi kuna kitabu ama maelezo yoyote yanayoonyesha mchango wa WAKRISTU ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika? - Kiasi kwamba wewe Mohammed Said umeona haikuwa haki kutowazungumzia Waislaam!
Mimi nakusoma sana lakn najaribu kuunganisha hoja yako sipati jibu...Maana hata huyo Nyerere aliyeandikwa vitabu vingi hazungumziwi kwa kusifiwa kwa Ukristu wake.
Hivi kuna kitabu ama maelezo yoyote yanayoonyesha mchango wa WAKRISTU ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika? - Kiasi kwamba wewe Mohammed Said umeona haikuwa haki kutowazungumzia Waislaam!
Mimi nakusoma sana lakn najaribu kuunganisha hoja yako sipati jibu...Maana hata huyo Nyerere aliyeandikwa vitabu vingi hazungumziwi kwa kusifiwa kwa Ukristu wake.
Dada hujui kuwa Mkandara alikuwepo na alichangia sana siku za mwanzo za uzi huu?
Mkandara kadandia daladala linaloelekea Tabata, kaingia ndani kabisa na kukaa siti ya nyuma na kuanza kusoma gazeti lake huku anakunywa COCACOLA!
Abiria wanazidi kuingia na kujaza sehemu ya mbele! basi linaendeshwa na kukaribia Tabata, ghafla Mkandara anakurupuka na kumuuliza abiria mwenzake hivi basi laelekea wapi? anajibiwa kwani wewe wenda wapi? Mkandara anajibu Kimara! duh! mwenzake anaanza kucheka na kumshangaa Mkandara yaani umekaa ndani ya gari na kustarehe muda wote huo na nauli umelipa lakini hujui gari laelekea wapi!
Ushauri kwa Mkandara: anza kusoma topic hii tangu mwanzo ndipo uje kuchangia!
Mkuu wangu naona umerudia uchafu ule ule wa mkoloni na kuupamba tu. Sasa kama unajua mkoloni alitugawa ili atutawale kwa nini leo wewe unataka tugawanyike?.. Ebu fikiria Kenya leo wajaluo waliokuwa wamemezwa na Wakikuyu wakianza nao kuandika kitabu juu ya harakati za Wajaluo kupigania Uhuru watafika kweli....kama ulivyobainisha hapo nilipo BLUE.
wazungu walitumia Divide and Rule katika kuitawala East Africa na athari zake mpaka leo zinaonekana japo tanganyika mumejitahidi kuzificha.
Kifupi Kenya alitumia ukabila. jambo ambalo mpaka leo linawapeleka.
Uganda alitumia ukabila , jambo ambalo mpaka leo linajidhihirisha na wanalissema wazi wazi.
Tanganyika alitumia UDINI na sababu kubwa nchi ilikuwa na makabila mengi sana lakin dini kuu zilikuwa mbili tu. Na hili japo lilikuwa linafichwa japo akina Dr Silvalon na akina Mohamed said kulibainisha lakin sasa ndio limejitokeza kabisa hadhwarani. Je umesikia yale ya Buseresere?
haya siku zote huwezi kuficha ukweli hata siku moja.
Ni kweli TANU haikuwa ya Nyerere peke yake. Lakini Nyerere personified TANU and you cannot talk about TANU without mentioning Nyerere, whether you like it or not. Hao wengine wote walikuwa na supporting roles tu. Huwezi leo kuwaelevate na kuwa star of the movie.Jasusi,
Sina haja ya kusema mengi katika hayo ulosema ila nitakupa
moja tu.
Hiyo fikra kuwa TANU ilikuwa Nyerere ndiyo imefanya historia
ya uhuru iingie katika farka kubwa mpaka leo.
TANU haikuwa ya Nyerere peke yake.
Walikuwapo miamba walioisimamisha TANU hadi uhuru ukapatikana.
Mashujaa hawa nimewataja katika kitabu changu.
Hili na wewe halikupendezi.