Huu ni uongo mkubwa sana maana hakuna nchi hata moja ya kiarabu ilochukua watumwa kutoka mashariki yetu. sasa hawa walikwenda kulima nini jangwani ama huko Oman kuna zao gani ama kazi gani walizofanya kukuza uchumi wa waarabu maana wao wenyewe walikuwa wakisifika kwa umachinga (merchant).. Au unachukulia swala la Utumwa pasipo kuelewa kwa nini biashara ile ilifana?..Mkandara sijasema uongo.
Wazungu walichukua utumwa sana nchi za Magharibi mwa Afrika kwani ilikuwa rahisi kusafirisha kwenda Amerika na Ulaya, kumbuka kipindi hicho Suez Canal ilikuwa haijajengwa ili kuwezesha meli za Ulaya kuja Pwani yetu kirahisi. Hapakuwa na haja ya kuchukua watumwa Afrika Mashariki ilihali palikuwa na wengi tena wenye nguvu na miili mikubwa Afrika ya Magharibi. Kumbuka biashara ya Utumwa ya Atlantiki (Atlantic Slave Trade).
Waarabu hawakua madalali tu, madalali walikuwa baadhi ya machifu kama Mkwawa,Mirambo n.k hawa waliwauza watumwa kwa waarabu, waarabu wakawapeleka Zanzibara kisha wakapelekwa nchi za Kiarabu. Watumwa waliopelekwa nchi za Amerika na Ulaya wapo hadi leo hii vizazi vyao lakini waliopelekwa nchi za Kiarabu ni wachache sana na kuna sababu mbalimbali zimetolewa katika hili. 1) walihasiwa (castration) ili wasije wakazaa na mabinti wa hao mabwana (masters) zao. 2) Hawakuruhusiwa kuoa mabinti wa masters zao. Lakini walipelekwa wengi tu huko. Tip Tip ni muarabu pia.
Kanisa la Angalikan la hapo Mkunazini lilijengwa siku za baadae wakati Uingereza ikiwa imepitisha sheria ya kuzuiz Biashara hiyo ya utumwa, hivyo walijenga kanisa maksudi ili kuwasaidia kupambana na biashara ya Utumwa.
Mkandara soma historia vema, ukitaja wakoloni pasi na kuwataja waarabu utakuwa bado hujawataja vema hao wakoloni.
Waarabu ndio walikuwa na access ya kwenda bara hadi Kongo (wakitutawala) na hata huko Magharibi ni waarabu ndio walikuwa wakiwauza watumwa kwa wazungu kutokana na kwamba wana access ya kuingia ndani barani kama wachuuzi..Kazi yao ni kukusanya watumwa kuja kuwauza sokoni pwani ktk makanisa ya Mombasa na Zanzibar. Pale kulikuwa na wazungu wanaonunua watumwa na ndio maana Sultan alikuwa protected na wazungu halafu jiulize hivi ilikuwaje kanisa lijengwe Zanzibar na Mombasa (fort Jesus) na ndio liwe soko la kuuzia watumwa kama biashara ni yao wao? hawakuhitaji kupeleka watumwa kupitia kanisani ikiwa wao ndio wahitaji na wao ndio wanatawala.
