Ni rahisi sana kubomowa, si rahisi kujenga. Ikiwa nyumba inayomchukuwa mtu miaka 2 kuijenga unaweza kuibomowa kwa siku moja tu, sasa piga hesabu nchi iliyobomolewa kwa miaka 44 mfululizo, itachukuwa muda gani kuijenga? Nakwambia miaka 44 kwa kuwa Nyerere 24, chaguo lake la kwanza 10, chaguo lake la pili 10.
Nchi hii ndio kwanza Kikwete kaanza kuijenga ipasavyo, kumbuka kuwa yeye tu hakuwa chaguo la Nyerere na yeye ndiye tunashuhudia akileta mabadiliko ya kweli ya utawala mpaka ya uchumi.
Hata wapigania Uhuru waliosahauliwa na Nyerere na vikaragosi vyake kwa miaka 44 tumeona wakikumbukwa rasmi kwa mara ya kwanza kwenye awamu hii ya uongozi.
Mkuu wangu wewe unaishi nchi gani?... siku hizi nyumba najengwa kwa muda mfupi sana na ikisha sii huyo huyo kigaragosi cha pili ndiye mnayemsifia kwa kabomoa mfumo wa Nyerere wa siasa za
Ujamaa na kujitegemea?... mbona mliweza kubomoa Ujamaa siku moja huko Zanzibar na mkarudisha mashule na Hospital kwa Wajarumani mnashindwa vipi leo kuanza hata ujenzi mpya ili waislaam nao wafaidike?... Leo vipi mnashindwa hata kubomoa msingi wa Utawala wa Nyerere ikiwa kazi ya kubomoa ni rahisi?..
Halafu usiovyokuwa na aibu unataka kuwaambia watu ya kwamba JK ndiye pekee anayejenga wakati unajua wazi hata kubomoa kashindwa japo miye nasema alojenga alorudisha mfumo wa kikoloni ni Mwinyi. Mbali na haya huyo Mohammed said mwenyewe anafahamu njinsi Mwinyi kikaragosi mwenzenu alivyotusumbua BALUKTA hadi yeye mwenyewe kwa amri yake akauawa Sheikh Kassim bin Jumaa!
Na nitasema tena na tena ya kwamba hata siku moja usitake kumfanya mtu MUISLAAM sana kwa sababu kazaliwa ndani ya ukoo wenye kujiita Waislaam. Uislaam sio sawa na kabila bali Uislaam ni IMANI na IBADA hivyo kama ibada (matendo) yake ni kinyume cha tulivyoamrishwa - hakuna Uislaam bali jina tu..huwezi kuwa na imani (kukiri kwa moyo) na usifanye ibada ni kumdhihaki Mwenyezi Mungu..
Nne na mwisho, hakuna mtu aliyeogopwa kama mnafiki, na nitasema hivi viongozi wote wa CCM ni wanafiki wakubwa maana ni wao walotuahidi mengi sana iwe ktk elimu, Afya, Umeme, maji, kilimo lakini hakuna hata moja ambalo wamelifanya. Kwa mfano, ni Kikwete aliyesema kwa ulimi wake mwenyewe kuwa tatizo la Umeme nchini litakwisha mwaka 2008, kumbe badala yake akatuletea Richmond kutubomoa zaidi... Na waswahili husema dalili za mnafiki ni zipi?..
Yote mnayoyaandika humu ni unafiki mkubwa sana maana ni nyie mlokuwa CCM na nyie ndio mnaolalamikia mfumo kristu ambao mliuasisi wenyewe. Kama mngekuwa wakweli wa nafsi zenu basi nanyi mngeondoka CCM kama walivyoondoka Hassan bin Amir na Takadir chama cha TANU mkaanzisha chama chenu cha waislaam na kujenga sera za kiimani na sio za sera za Kibepari na ukoloni mamboleo. Huu ni unafiki mkubwa mnaufanya kuitumia dini kwa manufaa yenu kisiasa, ili mradi watu waichukie Chadema kwa kuwa Dr.Slaa ni mkristu..