Hapana Ritz, mama yangu kabla ya kuolewa na baba yangu alikuwa muislam, aliolewa na baba ambaye alikuwa sio muumini wa dini yeyote, sasa sijui kama alipoteza uislam wake au vipi! nijuavyo, ikitokea baba akitaka kuchinja ng'ombe(baba alikuwa mfugaji) alilazimika kumuuita mzee wa kiislam amchinje ng'ombe kwa kitoweo.
Sijui alikfanya hivyo kumheshim mama au vipi sina uhakika. Nilichokiandika hapa ni kulaani mgawanyiko unaoletwa na nyie ambao mnaligawa taifa hili katika mapande ya WAO wakristo na NINYI waislam! hii ni hatari sana.
Kwamba wazazi wangu wanilaani kwa kuwa ATHEIST, haina maana kwani mtu ukisha kuwa na umri wa miaka 18, unahaki ya kujiamulia mambo yako! au wewe hulijui hilo? watoto wako wakiukana uislam utawalaani?