Kaka si tupo kwenye munakasha tunapeana darsa.
Ok. Nawe chukua hili darsa halafu utanieleza kama Mwalimu aliwasahau Waislam. Nakupa Cabinet ya KWANZA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar:
-Rais- Julius Kambarage Nyerre;
-Makamu wa Kwanza wa Rais- Abeid Amani Karume;
-Makamu wa Pili wa Rais- Rashid Mfaume Kawawa;
-Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Nsilo Swai, Mohamed A Babu, Amir Jamal;
-Waziri wa Nchi Makamu wa Kwanza wa Rais-Aboud Jumbe;
-Mawaziri wa Nchi Makamu wa Pili wa Rais- Lawi Sijaona, Bhoke Munanka;
-Waziri Kilimo, Misitu na Mifugo-Said Ali Maswanya;
-Waziri Biashara na Ushirika-Jeremiah Kasambala;
-Waziri Uchukuzi na Ujenzi-Sir George Kahama;
-Waziri Fedha-Paul Bomani;
-Waziri Mambo ya Nje- Oscar Kambona;
-Waziri Mambo ya Ndani-Job Lusinde;
-Waziri Ardhi, Makazi, Maji-Tewa Said Tewa;
-Waziri Viwanda, Migodi-Abdullah Kassim Hanga;
-Waziri Elimu- Solomon Eliufoo;
-Waziri Afya- Dereck Bryceson;
-Waziri Kazi- Michael Kamaliza;
-Waziri Maendeleo ya Jamii, Utamaduni-Sheikh Amri Abeid;
-Waziri Serikali za mitaa-Austin Shaba;
-Waziri Sheria-Hassan Nassoro Moyo;
-Waziri Habari, Utalii- Idrissa A Wakil.
Hapo haikuangaliwa DINI ya mtu, KABILA ya mtu wala Ukanda. Humo kuna Waafrika, Wahindi, Waarabu na Mzungu. Leo hii wanazuka watu wanasema kuna Waislam walisahaulika.
-