Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wewe Mzee unataka kutudanganya kweupe!.Huu mjadala umekuwa mrefu kutokana na wewe kurudia maswali na Mohammed kujaribu kujibu kila kitu na kukitolea ufafanuzi.Bado wewe unarudia suala hilo hilo kuwa anakwepa kujibu.Mzee Said hakuna hata mahali hata pamoja ambapo miye naleta viroja. Viroja ninavyoona ni vile vya kwako. Unazungumza kama unataka utambulike kwa utafiti ulioufanya. Baati mbaya sana wenzako wakikuuliza kuhusu "utafiti" huo unaruka. Unatoa madai tunakuuliza utujuze unakwepa; una kile ambacho naweza kukiita ni intellectual arrogance ya kuamini kuwa ulichosema wewe ni neno lisiloulizwa, lisilohojiwa, na lisilopingwa. Umejiaminishha kichwani mwako kuwa ulicohsema ni 'kweli' na kuwa ni kweli si kwa sababu ya ushahidi uliopo bali ni kwlei kwa sababu wewe umesema. Hivyo, watu hawahitaji kukuulizwa, hawahitaji kufafanuliwa, na hawahitaji kukusahihisha. Unaamini kuwa ukikubali kusahihishwa au kusahihisha histohisia yako au lugha unayotumia basi unajidhalilisha.
Mchango wako ni mkubwa sana katika kuelewa kwa kiasi harakati za Uhuru; kwa kweli miye nimekipenda kitabu chako (na nimekisoma) kwa sababu moja kubwa. Kinathibitisha kuwa Nyerere ndiye alikuwa kinara wa harakati za Uhuru. Mashujaa wengine wote ambao unawataja walimzunguka shujaa huyu.
Ungekuwa unabishana na mimi