Kama barua hizo zipo, onyesha angalau nakala moja tu. Unazificha za nini wakati kitabu chako ndicho chanzo cha yote haya? Sikuachii kabisa Mzee Mohamed hata kama utanipuuza!
Mwalimu alikupuuza wewe hivo sitoshangaa nawe ukipata mtu wa kupuuza. Madhara na madhila ya kitabu chako hiki na unayoendelea kuyahubiri kwa Waislam wenzako ndicho chanzo cha chokochoko zote hizi nchini.
Naapa tena, sikuachii hata kidogo.
Nguruvi,
Hii post yangu hapa chini hukuiona?:
Kwenye hotuba ya kuaga Nyerere alimuadhimisha vizuri sana
Abdulwahid Sykes.
Nyerere akaeleza vipi uchaguzi wao ulivyokwenda na yeye juu
ya ugeni wake Dar es Salaam alimshinda mwenyeji wake na
kuchukua uongozi.
Wala nyumba ya TAA haukujengwa kwa kujitolea kila Jumapili
kama Abdu Sykes alivyoeleza na kuwa yeye akiwa mtoto alikuwa
akifuatana na baba yake kwenye ujenzi wa nyumba ile.
Abdu Sykes ni mwongo nyumba kajenga Gavana na itakuwa vyema
kama semina paper aloandika binti yake Daisy Aisha Sykes mwaka
1968 "The Life of Kleist Sykes" akisimamiwa na John Illife ikaondolewa
Maktaba ya Chuo Kikuu kwa kuwa ni kazi ya kugushi.
Hotuba ya Waikela kwa Nyerere "Moto wa Waislam" haikusomwa
katika mkutano wa EAMWS wala Waikela hakuwekwa kizuizini nk. nk.
Yote niliyoandika ni mambo ya kutunga tu hakuna ukweli wowote.
Kitabu changu lau kama kimepata reviews mbili Cambridge Journal
of African History hao waandishi John Illife na Jonathan Glassman ni
wapuuzi kama mimi.
Hawana maana yoyote.
Hiyo kunialika kwenye vyuo vyao US kuhadhir ni magumashi tupu
wamepoteza fedha zao zilizokuwa zinawawasha.
Historia ya uhuru ilishaandikwa na wasomi mabingwa wa TANU 1981
wakiongozwa na Dk. Mayanja Kiwanuka.
Naamini ubishi sasa umekwisha.