Mgogoro uliopo baina ya serikali na waislamu kuhusu kuwekwa kipengelel cha dini haukuanza ghafla tu. Waislamu wameshiriki sensa zisizo na kipenghelel cha dini pasina malalamiko yoyote tangu ile 1978, 1988 na 2002. Hatukuw ana sababu yoyote kudai kiwekwe kipengele cha dini katika sense pamoja na kutambua kwamba takwimu za mwaka 1967 zilichakachuliwa na pia kuna takwimu feki juu ya idadi ya waislamu na wakristo zipo katika machapisho mbalimbali na mitandao mbalimbali.
Mtazamo wetu ulianza kubadilika tulipoanza kuona kalenda zenye nembo na bendera ya taifa zikiwemo zilizotiolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Takwimu za Bodi ya Utalii, shajara (diary) ya mwaka 2010 iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Ndani n.k. zikionesha kwamba idadi ya wakristo nchini ni kubwa kuliko ya waislamu. Takwimu hizi zilimaanisha jambo moja tu- kwamba takwimu hizi zinatambulika kiserikali.
Mgongano wa kwanza kati ya waislamu kwa upande mmoja na serikali na Makanisa kwa upande mwingine kuhusu suala hili la sensa ya mwaka huu ni uliotokea katika mkutano ulioitishwa na idara ya takwimu White Sands Hotel Dar es Salaam ambapo viongozi wa Kikristo na Kiislamu walikutana kujadili maandalizi juu ya sensa.
Waislamu waliitaka idara ya ya takwimu kuthibitisha kama takwimu zilizotolewa na TBC1 siku ya tarehe
26 Aprili, 2012 kwamba wakristo ni wengi kuliko waislamu ambapo wakristo 52% na waislamu 32% na wapagani 16% ni sahihi au la. Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu akasema takwimu hizo si sahihi kwa sababu serikali tangu 1967 haijaweka kipengele cha dini katika sensa yoyote ile baada ya hiyo.
Viongozi wa Kiislamu wakaonesha takwimu mbali mbali zilizopo katika maandiko na tovuti mbalimbali na kuitaka idara ya takwimu kwa kuwa inaonekana takwimu hizi za idadi ya wakristo na waislamu zinahitajika nchini na kimataifa, basi katika dodoso la sensa mwaka huu kipengele hicho kiwekwe.
Mkurugenzi wa Idara ya takwimu akasema serikali ilikiondoa kipengele hicho mwaka 1967 kwa ajili ya kuleta umoja wa kitaifa kwa hiyo haiwezi kukiweka. Waislamu walipinga hoja hiyo kwa kusema hakuna ushahidi wowote kwamba umoja wa kitaifa utatoweka kwa kuweka kipengele cha dini na kuna nchi nyingi tu duniani zinatoa takwimu za sensa kwa mujibu wa dini na wala amani haijatoweka.
Mfano Uingereza, India, Kenya, Ethiopia, Uganda, Malawi n.k. Kinachohatarisha amani si kuweka kipengele cha dini katika dodoso la sensa bali hizi takwimu za uongo kwamba watu fulani ni wengi kuliko wengine wakati hakuna sensa iliyofanyika kuhusu suala hili.
Katika mkutano huo wa White Sands, viongozi wa Kikristo wote waliunga mkono kutokuwekwa kipengele cha dini katika sensa. Waislamu walipohoji kama kuna hatari ya kuvunjika umoja wa kitaifa, mbona dodoso la sensa lina kipengele cha makanisa na misikiti? Kama kujua majumba hayo ya ibada hakuvunji umoja wa kitaifa, iweje kujua wafanya ibada au wenye kujinasibisha na majaumba hayo ya ibada kuvunje umoja wa kitaifa? Hakukuwa na majibu bali idara ya takwimu ikashikilia msimamo wake.
Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Dar es Salaam.
Baada ya mkutano wa viongozi wa dini na idara ya takwimu White Sands Hotel, na baada ya kuona msimamo wa serikali ni kutokuweka kipengele che dini, viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wakakutana jijini Dar es Salaam tarehe 29 Juni, 2012 kujadili suala hili. Katika mkutano huo, umauzi ulifikiwa kuiandikia idar aya takwimu ombi rasmi la kuitaka iweke kipengele cha dini katika dodoso la sensa la sivyo waislamu hawatoshiriki. Jumuiya na Taasisi ziliandika barua hiyo tarehe 4 Juni, 2012 iliyosainiwa na viongozi wa Mumuiya na Taasisi za Kiislamu isipokuwa Bakwata na zilitoa hadi tarehe 20 Juni, 2012 idara hiyo iwe imefanya hivyo laa sivyo waislamu watasusia zoezi la sensa mwaka huu.
Mkutano wa Dodoma tarehe 11 Juni, 2012
Wakati tukisubiri majibu ya barua yetu kwenda idara ya takwimu, tukapata mwaliko wa idara hiyo tarehe 8 Juni, 2012 kwenda Dodoma kuhudhuria semina ya siku moja ya viongozi wa dini juu ya masuala ya sensa .
Katika semina hiyo, waislamu wakalileta tena suala hili mbele ya idara ya takwimu na likajadiliwa na pande tatu wakristo, waislamu na serikali. Msimamo wa viongozi wa kikristo na serikali ukawa kama siku ya mkutano wa White Sands Hotel kwamba serikali haitoweka kipengele cha dini. Baada ya waislamu kutoa hoja zisizojibika, TBC1 ikalazimika kukanusha tena takwimu walizozitoa kama moja ya juhudi za kuwafanya waislamu waache msimamo wao.
Hatimaye viongozi wa idara ya takwimu wakakubali kuchukua maoni ya waislamu na kuahidi kuyafanyia kazi. Lakini wakati akifunga semina hiyo, Waziri Ofisi ya Rais Sera na Uhusiano Mhe.Stephen Wasira, alitoa msimamo wa serikali kwamba serikali haiwezi kuweka kipengele cha dini kwa sababu haipangi maendeleo kwa kipengele cha dini!!!Huku waislamu wakijua kuwepo kwa MoU kati ya Makanisa na Serikali, serikali kupanga mipango ya maeneo ya ibada, makaburi n.k. kwa dini mbali mbali Waislamu walipotaka kuhoji, waziri alikataa na kuwaambia kama ninyi hamkuelewa somo wenzenu (wakristo) wameelewa, kauli ya kejeli kwa masheikh na viongozi wa Kiislamu waliohudhuria pale.
Viongozi wa Kiisalamu waliohudhuria semina hiyo jioni ya siku hiyo wakakaa na kuandika barua ya pamoja kwa idara ya takwimu kupinga msimamo huo wa serikali na kauli za kejeli za Mhe. Wasira kwa viongozi wa Kiislamu. Barua hiyo ikasainiwa na viongozi wote wa wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu waliohudhuria semina hiyo ambao wanafikia 31 wakiwemo Bakwata.
Mkutano wa pili wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Dar es Salaam 13 Juni, 2012
Baada kurejea Dar es Salaam, masheikh na viongozi wa Jumuiya na Taasisi mbali mbali za Kiislamu walipokea taarifa ya wajumbe waliokwenda Dodoma na kuijadili ambapo paliamuliwa itolewe Press Release kwa vyomboo vya habari kusisitiza msimamo wa kutokushiriki sensa kwa kuwa serikali imepuuza madai ya waislamu pasina hoja za msingi.
Press Conference ikafanyika Makao makuu ya Bakwata Kinondoni na likatoka tamko rasmi la waislamu
kwamba hawatoshiriki sensa ya mwaka 2012 hadi yafuatayo yafanyike;-
1. Kipengelel cha dini kiwekwe katika dodoso la sensa.
2. Kuwepo na uangalizi wa pamoja kati ya waislamu na wakristo kwa kuwa tayari kila upande
unadai wao ni wengi kuliko upende mwingine..