Ritz,Kinshansa 1974.Ali ulingoni na Foreman.Daktari wa Ali Dk. Pacheco anamwambia Ali unasikia jamaa wa Foreman wanamuhimiza akumalize duru ya tatu?Ali akajibu akasema, ''Kuanzia hapo nitamchukua Foreman kwenye nchi hajapata kufika. Mimi huyu nampiga.''Dk. Pacheco akamwambia basi fanya haraka hili jambo lishe.
Ritz,Mimi naujua uwezo wa hawa jamaa.Wanachokijua ni kuuliza maswali ya ubabaishaji kwa kuwa wamejaa hasira.
Katika raundi za mwanzo mashabiki wa Ali walionekana kuwa na fadhaa hasa ikizingatiwa kuwa wakati Ali anaingia ulingoni wengi walikuwa wakiimba ''Ali bumuyee, Ali Bumayee''
Mohamed hili la magazeti ya Africa Events umelileta wewe na si mara ya kwanza au ya pili. Kila mara umejinasibu kuwa magazeti yalichomwa moto kwa makala yako moja.
Nikakuambia kuwa wakati huo nilikuwa nasoma magazeti hayo ya Africa Events na Afirca Now na yalizuiliwa kwa nyakati fulani yote si kwasababu ya makala zako bali makala zilizoonekana kupinga usoshaliti na hasa kuichukulia Tanzania kama mfano. Wakati hayo yakiendelea magazeti kutoka nchi za mashariki yaliendelea kuingia.
Katika magazeti yaliyonisadia sana kuelewa siasa za Nigeria ni pamoja na hayo mawili kwasababu yalikuwa na ushabiki mkubwa sana wa siasa za Nigeria.
Tumekuuliza kuwa mwaka 1988 ndio mwaka yalipopigwa marufuku? Ukasema ndio. Ukweli ni kuwa magazeti hayo yalianza kuzuiliwa kuuzwa nchini kabla ya hapo.
Tukauliza tena nani aliyapiga marufuku, ukasema CCM kupitia Mayanja Kiwanuka.
Tukauliza CCM kama chama iliwezaje kupiga marufuku bila kuiagiza serikali ya CCM? Ukaleta kejeli na matusi.
Ndipo tukasema huna jibu na ukakubali nimeelekeza swali langu mahali pasipo husika ambako ni wewe.
Soma ile post ambayo nimeweka rekodi sawa utaona kuwa hakuna jibu la maana zaidi ya ngonjera na vituko vinavyoshabihiana na hivyo. Hata kwenye ngano ulishatoka.
Kwahiyo hatuna hasira, tunauonyesha ulimwengu kuwa Mohamed anaandika kwa kuficha ficha hisia zake ili auchanganye ulimwengu. Mwanakijiji kaonyesha vizuri sana katika ufafanuzi wa generalization yako.
Hadi ulipobanwa sehem muhimu leo ndio kwa mara ya kwanza umeandika ''yakaondolewa katika news stand'' tena si stands. Yawezekana yaliondolewa katika news stand ya Narung'ombe kwa kukosa wasomaji wewe ukadhani ni kwa makala yako vingnevyo yangekuwa yameondolewa katika stands.
Lengo lako lilikuwa kujenga mazingira ya kumtuhumu Nyerere ambaye ni marehemu lakini mwenyezi mungu ni wa haki kakunyooshea kidole! kama alivyokunyooshea kidole kwa kumsingizia marehem Kawawa.
Mo,hili la Africa events lifike mwisho kama la namba za mitihani, ni ushauri tu wa wewe kujisetiri.