Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
hii ni alfu ulela ya gerezani.bila Nyerere uhuru ungechelewa kwa miaka 10 na ushee
Son...
Mie sibishani tena kuhusu mambo haya.
Yeshachusha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hii ni alfu ulela ya gerezani.bila Nyerere uhuru ungechelewa kwa miaka 10 na ushee
Mohamed,
Hujajibu swali. Waislamu walitujengea shule za kutuelimisha? Umesoma shule ya misheni. Hizi harakati za kupigania uhuru tumeshiriki sote. Umefaidi matunda ya mfumokristo, lakini hilo mpaka sasa hutaki kukiri. Have some humility, my brother.
Jasusi,
Wazee wangu wamepigania uhuru wa nchi hii.
Kitabu changu shahidi.
Kanisa limefaidi juhudi za wazee wetu na linaendelea
kufaidi hadi leo.
Jasusi,
Wazee wangu wamepigania uhuru wa nchi hii.
Kitabu changu shahidi.
Kanisa limefaidi juhudi za wazee wetu na linaendelea
kufaidi hadi leo.
Lakini umesoma St. Joseph na si Shaaban Robert.
umekosea taaluma,ulitakiwa kuwa prof wa linguistics specilising in swahili
Hivo?...Je kitu gani kiliwashinda wazee wako kutwaa madaraka baada juhudi zao kufanikiwa na uhuru kupatikana? Huyo aliyekuja kuwatilia mchanga kwenye kitumbua alitokea wapi tena!Wazee wangu wamepigania uhuru wa nchi hii.
Kitabu chako hakina hadhi wala uhalali wa kuwa shahidi, je ulikuwapo? FYI kitabu chako is just a figment of your own imagination kilichojaa hisia zilizotawaliwa na chuki za kidini.Kitabu changu shahidi.
You can not get any lower than this...umechanganyikiwa. Ulianza kwa kudai ni wazee wako ndio walipigania uhuru wa nchi hii, sasa hili la wazee wetu linatokea wapi?Kanisa limefaidi juhudi za wazee wetu na linaendelea kufaidi hadi leo.
Wanajamvi, Hapa ndipo tunasema kila siku kuwa historia ya Mohamed hailengi kueleza nini kilitokea wakati wa kupigania uhuru. Lengo kubwa ni kujenga kwanza mazingira fulani.Son...
Mbona Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele
katika kupigania uhuru lakini matunda mnafaidi nyie
peke yenu?Nanyi wezi wa fadhila?
Son...
Umekosea.
Nimefanya vizuri sana kwenye Kiingereza.
Kiswahili sihitaji kusoma.
Nimezaliwanacho.
kuzaliwanacho sio hoja,any tom,dick and harry maadam amazaliwa dar irrespective of where parents come from amezaliwa nacho
Which is not true!Son of Alaska
Ni mmanyema tu ndio akizaliwa Dsm anakuwa amezaliwa na kiswahili. Na kumbuka mmanyema lazima awe muislam. Mohamed Said once said "alhamdullilah, sijawahi kuona mmanyema mkristo"
Which is not true!
Wild Card,
Hakuna tatizo.
Kila mtu ana haki ya kuisomesha historia yake apendavyo.
Sisi historia ya TANU kama tuijuavyo haianzi na Nyerere.
Hapana haja ya kugombana kwa hili.
Kivukoni wameandika historia yao na mimi nimeandika ya wazee
wangu ambayo inakwenda nyuma hadi mwaka 1929 ilipoasisiwa
African Asociation.
Son...
Mbona Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele
katika kupigania uhuru lakini matunda mnafaidi nyie
peke yenu?
Nanyi wezi wa fadhila?
Mwanakijiji,
Hayo aliyoongoea Nyerere unaamini kuwa ni kweli?
naomba ufafanue maana ya (Unahatibu kujwepa kilichodhahiri...) ni kiswahili au lugha gani hii? wewe uliandika hivyo!
Mohamed,Jasusi,
Uzi huu una mengi sana.
Sijakwambia kingine.
Nimesoma Lutheran Primary School.
Jioni nakwenda chuoni.
Unajua Mzee unaweza kabisa kuandika 'historia' ya Wazee wako; lakini kwa wewe kuiandika hakuifanyi kuwa iwe ni kweli hata urudie mara ngapi kuwa ni 'kweli'. Historia inakuwa kweli kwa sababu inaweza kushuhudiwa hivyo na matukio. KUendelea kuwadanganya hawa vijana kuwa TANU haikuanza 1954 na kuwa haikuanza na "Nyerere" ni ulaghadi wa hhoja. NI sawasawa na kusema Muungano wa Tanzania haukuanza 1954 kwa sababu tu wazo la kuunganishha nchhi za Afrika ya Mashariki lilikuwepo toka miaka ya hamsini!
Historia - na ulinukuu maneno ya Sykes huko nyuma - akisema TANU iliasisiwa 1954. Umeng'ang'ania kusema kuwa tuanzie kwenye kuasisiwa AA huko nyuma na hata uwepo wa wazo hilo kwa Sykes akiwa Burma. Sawa; kwanini usirudi nyuma hadi mwanzo wa kuumbwa ulimwengu?
Historia ya TANU kama chama cha siasa imeanza na Nyerere; sasa hii si kumpa sifa Nyerere au kumtukuza Nyerere bali ni kuwa wakweli wa HIstoria. Kusema kuwa Tanzania ilianza 1964 si kukataa kuwa huko nyuma akukuwepo na Tanganyika au Nchi ya Watu wa Zanzibar! NI kuwa mkweli tu wa historia. Vita ya Kagera ilianza 1978 sasa hii ni kweli; lakini 'chokochhoko' za Idi Amin hazikuanza 1978!
TANU ni zao la vyama vilivyokuwepo nyuma yake na ni matokeo ya mawazo yaliyokuwepo kabla yake. Historia yake imetanguliwa na historia ya vyama vingine kabla yake. Hivyo, kuisoma historia ya TANU ni kusoma historia ya political development in Tanganyika na katika kufanyahivyo mtu ni lazima asome historia ya AA, TAA na vyama vya wafanyakazi na vyama vingine vya kikabila. Mwanzo wa TANU basi siyo zao la AA peke yake kama unavyotaka watu waamini; ni zao la vyama vya kikabila (tribal associations), vyama vya wafanyakazi na vyama vya maslahi ya Waafrika (AA kikiwemo).
Unajitaidi kulazimisha ionakena kuwa TANU ilitokana na AA peke yake na kuwa kulikuwa na mstari ulionyoka ambao haukuwa na kitu kingine toka AA => TANU. Hii si kweli. Na tukisoma historia kidogo tunaweza kusema pasi ya shaka kuwa TANU ni zao pia la kile chama cha wanafunzi wa Kitanganyika kule Makerere. Nyerere alisema hivi katika ile hhotuba yake ya 1985:
Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere Chuo Kikuu nikiwa mwanafunzi.
Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.
Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?
Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia nikiwa Makerere akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).
Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.
Je siyo kweli kuwa Nyerere alikuwa tayari na wazo la kuanzisha chama siasa kabla hajakutana na kina Sykes miaka kadhaa mbele? Well.. jibu lipo - ndio alikuwa nalo. Tena wazo lake tunaweza kusema was more developed than Syke's. Nyerere alifikiria kuanzisha chama cha kitaifa cha kupigania uhuru. Lakini siyo tu alifikiria yeye na wenzake walianzisha chama - utaona kuwa hasemi kuwa yeye ndiye aliyeanzisha na hhadi leo sijui kama kuna watu wamewai kuuliza ni kina "nani walisahauliwa" kule Makerere maana nayo ni historia iliyotangulia TANU.
Lakini kinachokuudhi wewe na kinakufanya uwe na roho ya korosho ni ukweli kuwa Nyerere alikuwa mwanasiasa aliyesimama kifikra kabla ya kukutana na kina Sykes. Mawazo yake juu ya hatima ya Watanganyika yalikuwa mbali mno kuliko vijana wengi wa zama zake. Kitu hiki kina kukera na unajaribu kumfanya Nyerere mgeni wa siasa. Nyerere ambaye tayari aliingia TAA na kushika nafasi ya uongozi kabla ya kuja DAR anakukera. Kama kungekuwa na uwezo wa kufuta historia ya Nyerere nje ya Dar mngeweza kufuta lakini kwa vile hamuwezi mnajaribu kupuuzia.
Nyerere aliandika msimamo wake wa kisiasa kuhusu masuala mbalimbali kabla ya kwenda masomoni Uingereza na hata kabla ya Makerere. Nyerere alikuwa kiongozi wa shule yake alipokuwa Tabora. Na kuna kisa kinasimuliwa katika "We Must Run While They Walk" jinsi alivyojaribu kutetea wengine. Nyerere huyu huyu alikuwa na uhusiano mzuri na Waislamu wengi tu kabla ya kuja Dar na hata baada ya kuja Dar. Waislamu wa Dar hawakuwa wa kwanza katika maisha ya Nyerere. Na kile ambacho unakisimulia vizuri kwenye kitabu chako jinsi Nyerere alivyopendwa na Waislamu hakikuja kwa sababu ya hisani ya watu wa Dar. Nyerere alishajenga maoni juu ya wananchi wenzake na alishawazoea Waislamu kabla ya kukutana na wale wa Dar. Waislamu wa Dar wamejikuta wanavuna wasichopanda wao. Nyerere aliwaamini si kwa sababu iliyoko hewani; aliwaamini na wao walimuamini kwa sababu alkuwa mkweli kwao.
Kama kiongozi ni uongo kudhani unaweza kupendwa na kila mtu. NI kujidanganya kudhani kuwa katika maisha ya uongozi basi waliokuwa marafiki leo wataendelea kuwa marafiki kesho! Wapo wengi ambmao walikuwa marafiki zake ambao baadaye waligeuka maaudi wa serikali yake na hili halikuangalia dini wala mkoa! Umewaaminisha watu kwa miaka kumi na tano kuwa 'it was about religion' but history stand innocent of such an accusation. Umejaribu kuwafitinisha Waislamu kwa kupandikiza chuki isiyo na sababu dhhidi ya ndugu zao Wakristu.
Leo maskini wa Mungu wapo vijana wanamchukia Nyerere, wanawachukia Wakristu, wanachukia Kanisa (wameambiwa na Mohammed Said kwua Kanisa lilitangaza Uislamu ni adui yake Tanzania!). Maskini wa Mungu vijana hawa (na labda wazee pia) wanatembea wakiwa na shuku dhdii ya ndugu zao Wakristu. WAkienda maofisini wakikosa kazi "ni kwa sababu ni Muislamu" wanasema; wanaenda wakikamatwa na polisi wanasema "kwa sababu ni Muislamu"; wakienda na kunyimwa mkoppo benki wanasema 'kwa sababu ni Muislamu'.
Leo hii mtendaji Mkristu hatakiwi kumwajibisha mtumishi Muislamu kwa sababu akifanya hivyo ataonekana anatekeleza "mfumo". Leo mtendaji Muislamu na Mkristu wakigombania ajira, anayetakiwa kupewa ni Muislamu kwani ukimpa Mkristu watalia " mfumo".
Imefika mahali sasa tumeanza kutengeneza tabia kama ya baadhi ya ndugu zetu Wamarekani Weusi ambao kila wanakopita wanaona 'racism'. Kwa sisi ambao ni weusi lakini tusiopitia mfumo wa maisha yao wakati mwingine inashangaza! Mtu kasimamishwa na polisi analia "racism'; mtu kashindwa mtihani analia 'racism'. Wamekuwa ni manabii wa kulilia racism! Watoto wetu na vijana wetu wa Kiislamu wamekubali hizi porojo (kuziita ngano ni kuzipa sifa kwani ngano ina matumizi muhimu tu!). Wamekubali kuwa wao wananyanyaswa, wamekubali kuwa wanadhulumiwa; wamekubali kuwa wanatengwa; wamekubali kuwa wao hawawezi kufanikiwa katika nchi yao!
Kinachoshangaza ni kuwa wanaosema 'dhulma' wao ndio wamefanikiwa! Waulize kina Dau, Njozi, na hata Mohammed Said wajumbe wa kilio cha "Mfumo Kristu". Wao wanakula na kusaza; hakuna hata mmoja wao aliyewahi kusema ameonewa kwa sababu ni Muislamu lakini haweshi kuwaambia vijana wetu hadaa hii! Na maskini tunaweza kuona humu jinsi makundi ya vijana na labda wazee wakikubali porojo hizi bila kuzihoji na wakiamini kabisa kuwa wao ni duni mbele ya Wakristu huku wakihofia jinamizi lisilokuwapo la Mfumo Kristu!
Wenyewe wanasema wanasimulia historia ya 'wazee wao'!