Tunaomba huo upande wa pili,but lest you forget,kabla hata ya arusha,dar es salaam grapevine ilikuwa inamzungumzia sana huyu mtu kwa tabia zake
Son...
Unanipa mtihani.
Grapevine ina mengi na ni hulka ya binadamu kupenda kusikia yale yanayosisimua.
Ndiyo maana leo unaona magazeti ya udaku yanashamiri.
Sheikh Kassim alikuwa sheikh kijana sana na alivunja zile taratibu za usheikh kama
zilivyozoeleka za kuwa ''conservative'' nk.
Ilikuwa jambo la kawaida sana kumkuta Sheikh Kassim kakaa kona ya Mkunguni na
Lumumba anatia stori na vijana wenzake wa umri wake.
Jambo ambalo masheikh kama walivyozoeleka wasingeweza kuthubutu kulifanya.
Au unaweza kumkuta Sheikh Kassim kavaa kanzu tupu bila kofia wala juba anatembea
mjini nk.
Lakini kubwa juu ya hayo Sheikh Kassim alikuwa na maadui wa siri katika jamii ya Kiislam.
Haya utayaona katika ''excerpts'' kutoka pp yangu Insha Allah.
Baada ya kusema haya nitakuomba usinirejeshe katika ''grapevine'' bali soma kile ambacho
naamini hukuwa unakijua.