Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hoja za Mag3 zimekuwa mwiba mchungu sioni majibu kama kawaida

Nishazoea sasa nabaki kuwasoma tu hapa Nguruvi,Mwanakijiji,Mag3 et al wanavyoshusha nondo
 
<br />
<br />
Mkuu ni zaidi ya hoja zenye nguvu za Mwanakijiji zinazo msumbua

Kuna kitu hataki kukikubali kuhusu Mwanakijiji...

Soma katikati ya mistari majibu yake mengi kwa Mwanakijiji utaelewa hasa pale anapobanwa

Tunaendelea kusoma na tunaona nani anaetoka jasho hapa

Rapheri,
Sina uwezo wa kukuzuia kufikiri utakavyo.

Mimi napenda majadiliano na jinsi mshindani
anavyokuwa mkali kwa maswali ndivyo mimi
ninapofurahi.

Mpiganaji miereka hupenda mshindani ambae
atamtoa jasho si yule nyolinyoli.

Mimi niko ulingoni nakikirika vipi niogope kuanguka?
Ila nisichokiweza ni matusi.

Hapa hakuna wa kunitisha hata kidogo.

Paper na vitabu nilivyoandika viko hapa mnasoma na
kuchangia.

Uzi umefurtu ada.
Tuna wasikizaji 115,000 and counting...

Hapa sizungumzi na hao uliowataja hao ni wachache.
Akili yangu ipo kwa hawa laki na zaidi.

Unataka uthibitisho upi?
 
Alhaj Mwamwindi aliua Desemba/1971 na mapema June/1972 kesi ilikuwa imekwishamalizika...Ni vipi kesi hii ya mauaji iliyohitaji uchunguzi wa muda mrefu iliendeshwa kihara haraka namna hiyo?Ni kweli kwamba Mwalimu alitia saini adhabu ya kifo kwa sababu tu kifo kilimuhusu rafiki yake?Mbona alikawia na hatimaye kumuacha huru Mama Liundi ambaye aliuawa watoto wake wawili kwa kuwatilia sumu kwenye chakula?(wakati hukumu ya mahakama ilikuwa ni adhabu ya kifo?)..Huyu baba wa taifa kama wanavyo muita dah ngoja ni nyamaze kiukweli huyu mzee alikuwa dikteta wakisiri siri.
Kitu gani kilikuwa ugomvi wa Mwamwindi na Dkt Kleruu?
 
Ndugu zangu wana jf, Nimefarijika kuona mada hii imeangaza sehemu nyingi duniani na inaendelea kuwaangazia wengi zaidi, Juzi niliombwa namba na mdau mmoja akajitambulisha kuwa yeye ni mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha California nchini Marekani. Jana akanipigia simu, na tukaongea mengi sana, lakini kubwa zaidi akasema yeye amesoma kitabu cha Maisha na nyakati za Abdul Sykes kilichoandikwa na Mohamed Said ambacho ndicho nilichokipinga katika uzi huu na kuweka ukweli halisi japo kwakifupi tu. Akasema zaidi kuwa yeye alikuwa ni muhanga wa kitabu hicho kwani aliamini habari za Mohamed kwa asilimia fulani lakini kuna mambo yalikuwa yakimtatiza mpaka alipobahatika kusoma uzi huu. Anazidi kusema kuwa amewaambia baadhi ya wanafunzi wake waufuatilie kwaukaribu uzi huu, kwakuwa unamengi mazuri na mapya kwao kwa historia ya harakati za ukombozi afrika. Hii ni heshima kubwa kwa jf na uongozi wake mzima kwakuendelea kuulinda mjadala huu mpaka hapa ulipofika, Nawaomba Mods muendelee kuulinda hivyohivyo kwa mafaa ya historia ya nchi yetu, na ikiwezekana ubadilisheni rangi iwe nyekundu kuonyesha ni zaidi ya STICKY THREAD tulizozizoea.
 
Mohamed Said, nilini utaacha visingizio vya kitoto kukwepa hoja? Mwana kijiji amekuja na hoja nyingi sana nzito ambazo zilikuacha mtupu! na kwakuwa hukuwa na majibu muafaka ukaamua kuingia chaka. Onesha wapi Mwanakijiji alipotumia lugha ya matusi dhidi yako! Mwanakijiji ni muungwana sana katika kutoa mawazo yake. Kuna wakati watwana wako akina Ami, Biko Haram, Zomba na THE BIG SHOW wamekuwa wakimpolomoshea matusi Mwanakijiji katika jitihada za kukunusuru wewe, lakini Mohamed Saidi hukuwakemea zaidi ya kuwapongeza tu! Wacha uzandiki mzee wewe.
Unayosema si kweli.
Angalia sehemu ambapo Mwanakijiji alibaki mtupu kweli si kama sifa unazotoa kibubusa.Mwenyewe hakurudi kujibu.
Ikiwa wewe utakuwa na jawabu kumsaidia lete.
 
the Vatican City's capacity to enter into relations with other states is difficult to asses.
too much emotions ndo zinakucloud hata kuchambua na kuelewa.Hapo juu umequote uchambuzi wa some lawyers ambao wao wametoa maoni yao. Wewe ukamaliza hapo ndo conclusion kwako. Kuna shida sana
 
Ndugu zangu wana jf, Nimefarijika kuona mada hii imeangaza sehemu nyingi duniani na inaendelea kuwaangazia wengi zaidi, Juzi niliombwa namba na mdau mmoja akajitambulisha kuwa yeye ni mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha California nchini Marekani. Jana akanipigia simu, na tukaongea mengi sana, lakini kubwa zaidi akasema yeye amesoma kitabu cha Maisha na nyakati za Abdul Sykes kilichoandikwa na Mohamed Said ambacho ndicho nilichokipinga katika uzi huu na kuweka ukweli halisi japo kwakifupi tu. Akasema zaidi kuwa yeye alikuwa ni muhanga wa kitabu hicho kwani aliamini habari za Mohamed kwa asilimia fulani lakini kuna mambo yalikuwa yakimtatiza mpaka alipobahatika kusoma uzi huu. Anazidi kusema kuwa amewaambia baadhi ya wanafunzi wake waufuatilie kwaukaribu uzi huu, kwakuwa unamengi mazuri na mapya kwao kwa historia ya harakati za ukombozi afrika. Hii ni heshima kubwa kwa jf na uongozi wake mzima kwakuendelea kuulinda mjadala huu mpaka hapa ulipofika, Nawaomba Mods muendelee kuulinda hivyohivyo kwa mafaa ya historia ya nchi yetu, na ikiwezekana ubadilisheni rangi iwe nyekundu kuonyesha ni zaidi ya STICKY THREAD tulizozizoea.
Huyo Profesa ni mpuuzi tu kama wewe.Yaani huu mjadala umemvutia kwa kusoma hata huu uongo wako!
Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,.
Nikwambie basi!. Na mimi jana nilipigiwa simu na profesa mwengine wa UK akaniambia Yes nimeona mchango wa waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.Endeleeni kuwakaba koo hao watu wa mfumo kristo wanaokusudia kufuta ukweli ulioandikwa na Mohammed Said.
Umeona Yerico!.
 
Wanajamvi huyu Mohamed Said ni mtu wa kuogopa kama ukimwi. Huko nyuma aliwakana Cecil Matola, Dr Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Nyerere kama Maraisi waasisi wa AA mwaka 1929, TAA mwaka 1950 na TANU mwaka 1954 huku akiwamwagia sifa makatibu wao Kleist Sykes na baadaye mwanaye Abdulwahid Sykes. Sasa shuhudieni hapa anavyomweka kando Balozi Christopher Tumbo katika harakati za Tanganyika Railway African Union (TRAU) na kummwagia sifa babu yake Salum Abdala kama Mwenyekiti muasisi na aliyeongoza mgomo wa Wafanyakazi wa Reli mwaka 1960. Namnukuu;

Sasa yatubidi tujiulize, hii simulizi ni ya kweli au imetiwa chumvi. Wanajamvi hebu linganisheni hii na ripoti ya mgomo wa TRAU mwaka 1959/1960, mwaka moja kabla ya uhuru. Je "star" wa huu mgomo alikuwa nani? Hapa chini nanukuu kutoka kwa wakoloni wenyewe;

Wanajamvi, yako mengi ningeweza kuyaandika hapa lakini nawaomba mjiulize tu kwamba katika vyama vya wafanyakazi popote duniani, nani ni mtendaji mkuu? Juzi juzi hapa tumemshuhudia Nicholas Mgaya akiandamwa na serikali kuhusu mgomo wa wafanyakazi (ingawa mpaka sasa wameweza kumnyamazisha) lakini wangapi wanamjua mwenyekiti wake? Mohamed Said kama kawaida anamtukuza babu yake na kumpa sifa zoote huku akimweka kando aliyekuwa Katibu na Mtendaji Mkuu wa TRAU, kulikoni?

Je viongozi wakuu wa vyama vya wafanyakazi walioitikisa dunia na kuleta mapinduzi kama Lech Walesa wa solidarity Poland, nani alimjua aliyekuwa mwenyekiti wake? Kwa vyama vya wafanyakazi katibu wake ndiye mtendaji mkuu au hata hili huyu mzushi mkubwa Mohamed Said anayedai amezunguka dunia nzima halijui? Jamani tukubaliane huyu mchochezi ama kwa makusudi au kwa hila, lengo la kumwaga ngano zake ni kuleta machafuko ya kidini nchini na amini usiamini, hata Waislaam wengi hawamuungi mkono.

Mag3, nilipomaliza tu kusoma maandiko yako nikamkumbuka, huyu jamaa
" In 1989 he became the Secretary-General of the Zimbabwe Congress of Trade Unions"

This guy is now a prime minister, hivi kwa nini hawakumpa hii nafasi mwenyekiti?
 
Huyo Profesa ni mpuuzi tu kama wewe.Yaani huu mjadala umemvutia kwa kusoma hata huu uongo wako!

Nikwambie basi!. Na mimi jana nilipigiwa simu na profesa mwengine wa UK akaniambia Yes nimeona mchango wa waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.Endeleeni kuwakaba koo hao watu wa mfumo kristo wanaokusudia kufuta ukweli ulioandikwa na Mohammed Said.
Umeona Yerico!.

Uongo wa hapo ni nini?

Je umesoma kitabu cha Mohamed Said kiitwacho maisha na nyakati za Abdul Sykes nilichokipinga katika uzi huu?
 
Mohamed Said,

Naam, tuendelee na darsa, Kuna ukweli gani kuhusu Kanisa Katoliki kutoa mchango wa fedha kugharimikia Mkutano wa Bakwata? kwa lengo gani? Ule mkutano wa pili uliofanyika Diamond Jubilee mwaka 1991 na kuwafukuza viongozi wa Bakwata Kinondoni ulifanikiwa?
 
Mwanakijiji,

Kwani nilichomueleza Geeky ni kitu gani? Holy See ndio na wanamahusiano ya kidiplomasia na nchi mbali mbali duniani na sio Vatican. Ila tatizo lililopo ni kuwa kuwa Holy See sio nchi ni taasisi ya wakatoliki duniani. That is why it is controversial issue na baadhi ya nchi zimekataa kuwa na uhusiano wao wa kidiplomasia kwa kuhofia nchi zao zinaweza kuwa matatizoni kwa kuendekeza udini kwa kuipendelea dini moja na kuacha nyengine hazina uhusiano wa kidiplomasia na na serikali.

This is silly; hivi unajua Upapa (Papacy) ndio una historia ndefu zaidi ya kuwa na mahusiano ya kidiplomasia duniani? Of course kile kinachoitwa "Ubalozi wa Vatican" kimsingi ni ubalozi wa Holy See na ndio maana officially mwakilishi wa Holy See haitwi "Balozi wa Vatican" (japo unofficially ndivyo anavyoitwa) bali huitwa 'Papal Nuncio'.

Sasa, hakuna tatizo hata kidogo kwa nchi kuwa na mahusiano ya kibalozi na Taasisi; tuna mahusiano ya namna hiyo na taasisi za Umoja wa Mataifa na hata Umoja wa Mataifa ni taasisi lakini ina mabalozi wake na nchi zina mabalozi pale. Taasisi ya OIC ni mojawapo ya taasisi ambazo japo ni ya Waislamu inaruusu nchi kuwa na wawakililishi (Marekani ina balozi wake OIC). Ndio maana sisi wengine tunaamini Tanzania inatakiwa ianzishe uhusiano wa kibalozi na OIC (nililisema hili tangu 2007) na wala halina shida. Tayari Tanzania ina mahusiano na Aga Khan (Taasisi ya Kiislamu ikiongozwa na Imam) ambao wanapewa Kinga nchini zile zile za Kibalozi (rejea makubaliano ya Mkapa na Aga Khan).

Kwa hiyo hakuna hhoja dhidi ya Vatican City kama nchi au Holy See kama Serikali ya Papa.
 
Kanyoosha kitu gani? Sijakuelewa au Holy See nayo ni nchi???? Naona mnakosa hoja mnabakia na mitambo ya kijinga nileteeni hoja za msingi na sio kuzunguka mbuyu. Nasubiri.

Mdondoaji wakati mwingine unazungumza kama mtu mwenye dalili za usomi lakini wakati mwingine hisia zako zinakufanya uonekane kama mtu ambaye alipita nje ya majengo ya shule. Jadili hoja kama unaweza kama huwezi usilete viroja. Utu uzima huja na wajibu.
 
Mzee Mohammed Said, Assalaam alayka warahmatullah, mzee wangu basically the truth imekuwa-exposed and we really thank tumeijua, hawana hoja zaidi ya kupiga lwange sasa wale walokupinga, ni dhahiri wameanza kuja na defensive arguments, ashamed of themselves, jazak Allah kheyr mzee wetu.
 
Nguruvi,Mimi nikuandikie wewe matusi!Sijapata kutukana mimi ndugu yangu.Unachanganya mambo sana kaka.Nimesema ametumwa kueleza mfumokristo.Wewe unaingiza mengine katika kauli yangu.Ndipo hukuambia mara nyingi.Hamaki imekutangulia sana.Hamaki inavuruga tafakuri.Usipende kughadhibika hapa ni barzani ni majadilianohakuna cha zaidi.Mwisho.Hiki kitu cha kudhani kuwa sisi hatuko pamoja kitakupeni shida sana.Waislam ninapokutajia ujue ni majority.La ikiwa unapenda kujifariji kuwa BAKWATA wana watu mimi siwezikuzuia.
Mzee ms, Kwahiyo bakwata wanawanyama?
 
JokaKuu,

Ni ngumu kutenganisha Uislam na harakati ya TANU kwa Dar es Salaam labda maeneo mengine.

Masheikh karibia wote ndiyo walikuwa wanaongoza harakati za AA. TAA, TANU, mjini Dar es Salaam Nyerere mwenye amekiri ilo kwenye hotuba yake ya kuaga.

Ukimtaja Sheikh Takadir, Mufti Hassan Bin Amir, Sheikh Bilal Waikela, Sheikh Ramia, umetaja TAA, TANU.
Ritz,

..tuko pamoja ktk mtizamo wako kuhusu harakati za TANU kwa eneo la D'Salaam.

..nilichokuwa nazungumzia mimi ni hoja za Mohamed Said anapodai kwamba baada ya uhuru dola iliwashughulikia watu wa dini moja tu, tena dini yake yeye.

..kwa mtizamo wangu, mkono wa dola haukuwa na huruma kwa watu wa dini moja, huku ukikandamiza dini nyingine. ndiyo maana unaona babu yake Mohamed alitiwa kizuizini akatoka, wakati katibu wake, Christopher Kassanga Tumbo, ambaye alikuwa Mkristo, alizuiliwa kwao Sikonge hata baada ya Mwalimu kuondoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohammed Said, Assalaam alayka warahmatullah, mzee wangu basically the truth imekuwa-exposed and we really thank tumeijua, hawana hoja zaidi ya kupiga lwange sasa wale walokupinga, ni dhahiri wameanza kuja na defensive arguments, ashamed of themselves, jazak Allah kheyr mzee wetu.

DJ L,

Waleikum Salaam Warahamatullah Wabarakatu.

Ahsante sana ndugu yangu.
Hii historia ilifutwa kabisa na haikutakiwa ijulikane.

Ndiyo kisa tunapata tabu leo kwa kuulizwa maswali
kwa mambo yaliyofanyika na watu ambao walikuwapo.

Leo wazee wetu wanazungumza kutoka kwenye makaburi
yao walikolala...

Akina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir,
Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Abdu
Sykes, Idd Tulio, Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Mshume Kiyate,
Bi Shariffa bint Mzee, Bi Titi Mohamed, Bi Tatu bint Mzee,
Mama Bint Maalim, Bi Dharura Bint Abdulrahman, Yusuf
Chembera, SalumMpunga, Ali Mnjewale, Suleiman Masoud
Mnonji, Yusuf Olotu...majina huwezi kuyamaliza na kila jina
lina jambo kubwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ndiyo maana kuna maneno haya kakiita kitabu changu...
''The Untold Story of the Muslim Struggle Against British
Colonialism...

Kisa ambacho hakikupata kuelezwa popote...
 
Algeria,Egypt,Chad,Morocco, Iran,Pakistan, Iraq nk ni nchi zenye waislam wengi lakini zina uhusiano na Holy Sea...unaweza labda ukatutajia hizo nchi zilizokataa kuwa na uhusiano na Holy Sea kwa sababu ulizozitaja?


Unadhani basi ataweza; muulize tu akupe kati ya nchi zote duniani ni ngapi zina mahusiano na Papa na zile ambazo hazina? Maana hata ambazo hazina zina mahusiano ya aina fulani. Labda nijibu mwenyewe; kuna nchi 15 hivi ambazo hazina uhusiano wowote wa kidiplomasia na Holy See. Hizi ni:

Afghanistan, Bhutan, Brunei, Comoros, Laos, the Maldives, Mauritania, Myanmar, North Korea, Oman, the People's Republic of China, Saudi Arabia, Somalia, Tuvalu and Vietnam

Kutoka Wikipedia: Rangi ya kijani ni nchiz ote ambazo zina uhusiano wa kibalozi na Holy See (ambazo hazina controversy ambayo ndugu yetu Mdondoaji anasema ipo)

800px-Vatican_relations.svg.png


Kitu ambacho nimeelewa baada ya kumsoma mara kwa mara ni kuwa anafikiria au anaamini kuwa Tanzania inayo "Ubalozi wa Vatican City State" na sisi wengine tumechangia kumfanya aamini hivyo kwa kusisitiza unchi wa Vatican City State. To put record state ni Holy See ambayo mkuu wake ni Papa na ambayo ni serikali ya Papa (Mkuu wa Kanisa Katoliki) ambayo Tanzania na nchi nyingine zina mahusiano nayo. Sasa, ikumbukwe kwamba kuwa kiongozi wa dini fulani siyo kigezo cha kutokuwa na uhusiano wa kidiplomasia nimetoa mfano wa Aga Khan (ambaye ni Imam Mkuu wa madhehebu ya Ismailiya duniani - sawa na Papa kama mkuu wa Dhehebu Katoliki Duniani). Aga Khan kupitia taasisi yake ya AKDN ina mahusiano ya kibalozi na baadhi ya nchi na kupewa kinga za kibalozi (mfano ni huu wa Tanzania).

Holy See inafanya kazi kutokea Vatican City na hivyo mara nyingi watu (kama mimi) tunazungumzia uhusiano na Vatican kama vile mtuakizungumzia uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na Riyadh au Tanzania na Tehran. Tukisema ubalozi wa Washington DC, tunajua tunazungumzia ni nchi gani au wanamwakilisha nani. Hii hata siyo issue sijui kwanini bado inasumbua watu.
 
Back
Top Bottom