Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kipande cha hotuba ya Kikwete...
Ndugu Wananchi;
Waislamu nao wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yo yote ya maana. Waislamu wananyanyaswa katika nchi yao, wanakamatwa ovyo, hawapewi fursa sawa na kwamba Serikali inawapendelea Wakristo. Wanasema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo. Mimi binafsi wananishutumu kuwa napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama vile harambee za kujenga Makanisa na shule za Makanisa. Naambiwa kuwa mwepesi kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Masheikh wanapofariki. Ipo Misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova.
Lazima mzee wetu Mohamed Said atakuwa anaswali kwenye hiyo misikiti.
 
Nguruvi3
Suruali inakupwaya hiyo ndugu yangu,hebu pandisha juu kidogo,hawa jamaa zako wanaokupigia makofi eti ya kwamba una ubavu wa kupambana na Mohamed Said hawakutakii mema,wanakudhalilisha tuh,

Ubavu wa kukunja ngumi na Moh Said wewe huna,historia hii ishaandikwa na wenye kujisimamia wenyewe kifikra wameuona uhalisia..

Pole sana jamaa yangu..
 
Last edited by a moderator:
Imekuaje mkawa maskini wakati mlielimika? au nanyi mlipitia madrasa na kuishia kunywa gahwa na kashata vibarazani!
kweli huna uwezo wa kufikiri! pole sana kijana. Achana na hilo zee lako chimvi labda utaweza kufikiri kwa kujitemea!
 
Wanaelezwa historia yenye heshima kubwa na iliyofichwa wao hawataki kubali na mwishowe wameishia kukejeli na kukosoa bila mashiko,

Ni khiyari yao kuamini au kutoamin,kukubali ama kutokubali,,

Watu wenye hekima zao wanasema ukimuona mtoto kabebwa mgongoni na ubebeo yeye ananyoosha miguu ujue hataki tena masuala ya kubebwa hata umweleze jambo gani,,

Hakuna wa kuwalazimisha ila tunaamini upande wa pili wa shillingi umefahamika..
 
Bahati nzuri nimebahatika kukisoma hiki kitabu cha ndugu yangu Mohammed Said the life and times of Abdulwahid, Uamuzi wa Busara na vitabu kadhaa vya brother Said i suggest watu wasome sio tu kumuattack. wengi wanajua tu kumuatack na inaonesha dhahiri hawajasoma kitabu chake..
brother Said ameandika kisomi bila kumuatack mtu yoyote wala dini bali amonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi gani njia mbalimbali zilitumika kudidimiza wengine.
mnaomuattack brother Said someni kitabu cha padri J.Silvanus kanisa katoliki na siasa za tanzania 1954-1985 utagundua kuwa brother Said yeye ni miongoni tu mwa waliojitolea kusema kweli kosa lake kubwa kawasemea kweli waislamu, ukisoma kitabu cha Silvanus utanielewa kwa nini nimesema kosa la brother Said.
ifike kipind tukubali madhifu ambayo yamewahi tokea na kujitahidi kujenga a better tomorrow,
aliyoandika brother said ni sehemu tu kwa yatakayo andikwa huko mbele na tukumbuke kitabu kama maisha na nyakati za Abdulwaheed ni cha mwaka 1997 sidhani kama Marehemu aliweza au alipata muda wa kukubali au kukanusha yaliyomo ktk kitabu hicho.
Tukumbuke tu maneno haya yalipata kusemwa na Wole Soyinka
"TISHIO KUBWA KWA UHURU NI UKOSEFU WA UKOSOAJI.VITABU NA MAANDISHI NI TISHIO KWA WALE WOTE WANAOTAKA KUUFICHA NA KUUZIKA UKWELI"
 
Bahati nzuri nimebahatika kukisoma hiki kitabu cha ndugu yangu Mohammed Said the life and times of Abdulwahid, Uamuzi wa Busara na vitabu kadhaa vya brother Said i suggest watu wasome sio tu kumuattack. wengi wanajua tu kumuatack na inaonesha dhahiri hawajasoma kitabu chake..
brother Said ameandika kisomi bila kumuatack mtu yoyote wala dini bali amonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi gani njia mbalimbali zilitumika kudidimiza wengine.
mnaomuattack brother Said someni kitabu cha padri J.Silvanus kanisa katoliki na siasa za tanzania 1954-1985 utagundua kuwa brother Said yeye ni miongoni tu mwa waliojitolea kusema kweli kosa lake kubwa kawasemea kweli waislamu, ukisoma kitabu cha Silvanus utanielewa kwa nini nimesema kosa la brother Said.
ifike kipind tukubali madhifu ambayo yamewahi tokea na kujitahidi kujenga a better tomorrow,
aliyoandika brother said ni sehemu tu kwa yatakayo andikwa huko mbele na tukumbuke kitabu kama maisha na nyakati za Abdulwaheed ni cha mwaka 1997 sidhani kama Marehemu aliweza au alipata muda wa kukubali au kukanusha yaliyomo ktk kitabu hicho.
Tukumbuke tu maneno haya yalipata kusemwa na Wole Soyinka
"TISHIO KUBWA KWA UHURU NI UKOSEFU WA UKOSOAJI.VITABU NA MAANDISHI NI TISHIO KWA WALE WOTE WANAOTAKA KUUFICHA NA KUUZIKA UKWELI"

Kama watu wengine hawakupata nafasi ya kutetea vitabu ni bahati mbaya sana tu. Ila maadam yuko hai huyu bwana atafanya vema kukitetea kitabu chake hapa.
 
Mzee Mwanakijiji,

Sijui kama unahifadhi kumbukumbuku ya maandiko yako.

Kupitia huu uzi uliandika kuwa Mohamed Said na Prof Njozi wapo tofauti Prof Njozi yeye hana chuki na Nyerere chuki yake ni CCM.

Leo tena unatuambia Mohamed Said na Prof Njozi wapo pamoja na mfadhili wao ndiyo walioanzisha madai ya Waislam kudhulumiwa. Unajidanganya sana unapenda sana kutumia fikra zako kwenye masuala ya Waislam bila kufanya utafiti.

Narudia tena kukwambia Mohamed Said, Prof Njozi, ndani ya Misikiti ni maamuma tu kama mimi kuna Masheikh wakubwa ndiyo viongozi unawaogopa sana hawa jamaa aisee!

Dhulma dhidi ya Uislam zipo wazi toka miaka ya 1962 siyo leo kama unavyofikiri wewe kuna Masheikh wengi wamefungwa jela wewe ili unaweza kuliona dogo sababu alikuhusu na ukaona siyo dhulma.

Kuna Masheikh wamepelekwa jela hata siasa hawazifahamu.

Hawa hapa Sheikh Al Amin Maftah, Sheikh Suleiman Masudi Manoji, Sheikh Jumanne Bias, Sheikh Nurdin Hussein, Sheikh Shariff Hussein Badawiy, Sheikh Ali Migeyo, Sheikh Adulkarim Adulwahid, Sheikh Matar, Sheikh Shariff Adnan.
Ritz,

Naomba msaada wako, mpaka mtu kuitwa sheikh anapitia vigezo gani? Na sababu kubwa nimemsikia mzee mo said akimuita sheikh, Bilal waikela na huyu yuko hai je? Ni sheikh kweli? Au? tafadhali naomba mwongozo wako. Na usheikh unapatikanaje?
 
Nenda Chadema kaangalie wabunge wa viti maalum kama ukukuta Wakirsto watupu.

Kuna wabunge wa 3 kutoka zanzibar na wengine wengi tu waislam we ni muongo na ni mnafiki sana unachuki sana na cdm, kwa taalifa yako hakuna chama kilichochanganya viongozi wake wa juu kama cdm.
 
Nimesoma maandiko ya ndugu yangu Mohamed Said aliyoyaweka katika kitabu chake akiitacho Historia ya Uhuru upande wa Pili,
Katika maandishi yake ameonyesha wazi kulazimisha dunia iamini kuwa waislamu wamedhulumiwa katika historia ya Uhuru wa nchi hii,
Katika matakwa yake Mohamed Said anataka historia ya Uhuru ingetazama itikadi za kidini kwanza kabla ya kusimamia maudhui halisi ambayo ni Uhuru,

Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,

Hajajishughulisha kuutazama utawala wa Kiingereza wala kuutazama upya utawala wa Kijerumani ambao ndio uliosimika misingi ya utawala na mifumo mingi ambayo leo tunaitumia! Mjerumani mfumo wake wa utawala kwa ASILI ni wa kikristu na kwa Tanganyika walisimama hivyo bila kutetereka! (Yaani mfumo kristu 100%)

Akaja Muingereza na yeye mfumo wa utawala wake wa ASILI ni wakikristu!

Imenilazimu kitabu cha bwana Mohamed Said kiitwacho "Maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968" (Historia ya uhuru iliyofichwa ya upande pili) kukiita ni NGANO za masika.

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.



Elimu,

Woga



Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/71954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)

Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kwenda UNO iligharimiwa kwakiasi kikubwa na shirika la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa Kasisi Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni boss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.


Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta

Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?

Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru?

Nitaeleza kwakifupi tu:

Mwalimu Nyerere baada ya kukabidhiwa mamlaka kamili ya kushika dola na Malkia wa Uingereza alianza mageuzi ya kubadili mfumo huo kristu hasa mwanzoni mwa 1962 na juuhudi zilishika kasi zaidi mwanzoni mwa 1964 baada ya kuunganisha nchi ya Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Tanzania!

Juhudi hizi zilikwenda taratibu na kwa ufanisi wa hali ya juu kwakupitia hatua kadhaa ambazo ni pamoja na, kutaifisha huduma za kijamii zote zilizokuwa chini ya makanisa, kuanzisha sera ya elimu ya msingi kuwa ni ya LAAZIMA kwa watanzania wote nk, Kumbuka Mjerumani amekaa zaidi ya karne tatu akitumia mfumo kristu kutawala, Muingereza nae akalowea karne kadhaa akitawala kwa mfumo huohuo, Lakini ndani ya miongo miwili tu ya utawala wa Mwalimu Nyerere huku nchi ikitoka kwenye dimbwi la ukoloni aliweza kubadili sura na mfumo huo wa kikoloni na kuwa wawatanzania wote bila kujali dini, kabila rangi au kanda.

Naomba nimfungue macho na akili rasmi Mzee Mohamed Said huyu mpigania Dini kwa mgongo wa Uhuru wa nchi hii.
Nitaeleza kwa kifupi tu yale anayoyalilia Mohamed Said juu ya WAZEE wake.


Ukweli nikuwa kuanzia mwaka 1955 kulianza kuibuka mlengo tofauti kwa baadhi ya washarika wa ukombozi ndani ya TANU,
Hasa hasa mlengo huo ulikuwa ni kuweka itikadi ya DINI mbele, yaani iwe ndio tiketi halisi yakupigania uhuru na sio Utanganyika wao, na baada tu ya kupata uhuru, baadhi ya wazee waliokuwa beba kwa bega na Mwalimu katika harakati za kudai uhuru WALIASI rasmi sera ya Mwalimu nakuanza kuendesha vita ya chini kwa chini yakumpindua Mwalimu chini DINI.

Mwalimu Nyerere kwakutumia falsafa na malengo yake ya tangu akiwa Shule ya Tabora, Chuo kikuu Makerere na pale Scotland akiwa sambamba na wanaukombozi wasomi wenzie waliweza kuanzisha mfumo stahiki wa kufuta UDINI, UKABILA, Rangi, Ukanda na kisha Waliamua kuwafanya Watanganyika kuwa kitu KIMOJA.

Sasa mgogoro ulikuja kwa WAASI, kwakuwa hawakukubaliana na sera za Serikali mpya ya Mwalimu, wakaziidisha vurugu kwakushawishi makundi kadhaa ya kiroho yaenzi uasi huo, hilo lilipelekea serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi yao ambapo mwaka 1962 katika kiwango cha juu cha hekima za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na waambata wake, waliamua kuanzisha sheria ya kumuweka mtu kizuizini.

Sheria hii ilikuwa na mafaa kwa waasi kwani ililinda hadhi zao licha yakuwa waasi waliostahili vifungo vya maisha au kunyongwa kama ilivyokuwa destuli ya viongozi wengi wa dunia ya pili.
Mashehe wengi walitiwa kizuizini na wengine kufukuzwa nchini na makasisi wengi kupewa onyo kali.
Ifahamike kuwa hilo halikuwakumba mashehe tu kwani uasi huo ulikuwa hata kwa makasisi waliotaka itikadi zao ipewe kipaumbele zaidi na serikali ya Mwalimu Nyerere.

Kazi aliyofanya mzee Nyerere ni kubwa na alikumbana na vikwazo vingi sana kutoka kwa wakatoliki, rejea kitabu cha Van Bergen kuna barua nzito ya Mwalimu Nyerere kwenye faharasi ya 15 kwenda kwa makasisi wa kikatoliki akiwatolea karipio kuu kwakukwamisha juhudi zake, katika hii hakuchukua karne kadhaa kuumaliza mfumo uliodumu kwa mvua na mvua.

Japokuwa hakumaliza chembe za mfumo huu lakini kwangu naona ni zaidi ya 98% alimaliza, palipobaki ni mimi, wewe na wale ndio wenye dhamana ya kumalizia.

Uthabiti na tunu aliyoifanya Mzee Nyerere inathibitishwa kwa Hotuba yake ya tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Mzee Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilikuwa thabiti na yenye kuvuta nyoyo za waungwa, Baba wa Taifa Mzee Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wakiwemo Bin Amir ambae Mohamed Said anamlilia, wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Mzee Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisemakuwa "upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake":

Inakera kuona wewe Mohamed unarudisha nyuma juhudi za wanaukombozi wetu na kupandikiza chuki miongoni mwa dini hizi mbili!
Faida unayopata ni ndogo na niyakwako tu kuliko hatari inayolikumba taifa hivi leo!
Sipingi kusahihisha historia ya nchi hasa kama kuna mema yaliyoachwa lakini kupotosha na kuchochea kunatulazimisha tuhoji mamlamla za usalama wa nchi zimelala wapi? Leo mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Mohamed Said anataka kutuaminisha kuwa Wanamapinduzi hawa wa Zanzibar waliwadhulumu waislamu wa Zanzibar na kuweka mfumo kristu anaodai upo au mfumo huo upo kwa Tanganyika tu?!


Katika kitabu chake bwana Mohamedi ametoa shutuma nyingi sana kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo ya eti Mwalimu katika hotuba yake ya kuaga taifa alitamka wazi kuwa hamjui ABDUL SYKES, Inashangaza sana kwani Mohamed Said anajua wazi ameudanganya umma na kudhihaki wanaukombozi wetu.

Ilikujiridhisha ndugu zangu wadau pitieni sehemu ya Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kuaga taifa tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam,




‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAWA

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA?
Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

WAZEE NA MSIMAMO

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

WAINGEREZA WAONGO

Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.


Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

TWAININGI AMEKWISHA

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."’



Mohamed Said kuwa mkweli, waambie ukweli watanzania (waislamu) kuwa umetumia mgongo wa Uislamu na Hayati Abdul Sykes, kwakumkashifu na kumdhihaki Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuwasafisha wazee wako walioasi serikali mpya ya Mwalimu ambapo ndipo madhila hayo wakayapata.

Juzi nimemuuliza maswali katika mjadala flani hapa, lakini majibu yake yamenifanya nijiridhishe kuwa Mohamed Said ni muhaini na mchochezi mkubwa wa nchi hii, Ameudhihaki Uislamu nchini na duniani kote,

Nilimuuliza hivi:


Naomba unijibu maswali haya kwaufasaha mwanazuoni Mohamed Said:

1) Uliathirika vipi kwa baadhi ya wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kutokuwemo kwao katika histori ya nchi hii kama unavyodai?

2) Taifa na waislamu waliathirika vipi kwa baadhi ya wazee unaodai wewe walipigania uhuru wa nchi hii na hawamo katika historia?

3) Ulijuaje kuwa wazee hao walipigania uhuru ilihali hawapo katika historia stahiki ya nchi hii?

4) Unaposema historia ya uhuru wa nchi hii haiwakumbuki ama haiwatambui, ulitaka wakumbukwe katika maandishi ya vitabu au katika nyaraka za serikali za historia ya uhuru wetu?

5) Unatambua kuwa historia ya nchi yoyote ile duniani huwa wapi?

6) Upeo wako umegota kwenye historia ya waislamu wa Tanganyika na Nyerere tu, au historia ya waslamu duniani kote? Kama ndivyo, je matatizo ya waislamu wa Nigeria, Somalia, Sudani, nk Nyerere ndiye kayapeleka?

7) Je ulichokiandika ni historia ya Uhuru wa Tanganyika au ni historia ya baadhi ya Waislamu wa Tanganyika na mapito yao kisiasa?

8) Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?

9) Je ni kweli Mohamed Said huwajui na huwatambui wale wazee 17 waliosimama kidete kudai uhuru wa nchi yetu? Je wote walikuwa wakrstu?

Naomba majibu ili tujenge hoja mpya yamjadala huu kwa mafaa ya taifa letu!






Lakini maswali mengine yamsingi yaliulizwa na wadau wengi kama Nguruvi3, Mwanakijiji na moja ya maswali yaliyonivutia ni hapa hapa chini:


By adolay:


Ninakuuliza somalia na nyerere kwasababu waislam wa somalia wanamatatizo makubwa ya kijamii, kisiasa, kieliemu, afya nk

Nani mchawi maana hapa kwetu kwa mujibu wa hadithi zako ni Nyerere. (Tunaongelea matatizo ya waislamu na wanaowahujumu)

Watanzania (Waislam, wakristu pia wa imani zingine na wasio amini) wanamatatizo aghalabu si makubwa kama ya wasomali.

1. Kwanini useme waislam wa Tanzania ni hujuma za nyerere na kwanini wasiwe waislam wa somalia? kunatofauti ya uislam wa somalia na ule wa tanzania?

2. Je katika historia yako ufahamu wako umegota Tanzania kwa hayati JK Nyerere peke yake? kama ndivyo nini ubora na ufahamu wako kujisifu mwanahistoria makini kama sio mbabaishaji?

Tafadhali rejea maswali kutushawishi kwamba wewe ni mkweli na kashifa zako dhidi ya Nyerere ni uwongo na majungu.

Tuanze na Somalia, nataka usome swali uelewe ujibu kama nilivyouliza sio kuniwekea hadithi za maandishi zisizoakisi maudhui ya swali.

1. Nani amewahujumu/aliwahujumu wasomali na uislamu wa somalia mpaka wamefikia hapa walipo je? ni nyerere

2. Ni mfumogani unatumika katika kuitawala somalia kiasi kwamba wamefika hapo walipo ilituutupie lawama

a) Mfumo kristo ndiyo maana wamefika hapo walipo

b) Mfumo islam, mahakama ya kadhi nk

c) hufahamu nakama hufahamu nini mtazamo wako.

Ninakuuliza maswali haya lengo nikutaka kuujuwa ukweli wa pengine Nyerere huyu pia yupo somalia, afghanistan, pakistani, lebanon, syria, libya nk nakwamba machafuko yote yanayoendelea huko ni hujuma za Nyerere na mfumo kristo kama unavyowapotosha watanzania na kuwachochea!

Naomba majibu ya maswali yangu hapo juu kuthibitisha kwamba wewe sio mchochezi na mchonganishi wa waislamu na wakristo kwa kubuni vitu visivokuwepo.

Mohamed Said, baada ya utangulizi huo narejerea maswali yangu ya jana kwa ufafanuzi. Angalizo jibu maswali kama yalivyoulizwa na sio siasa au funika kombe mwanaharamu apite kwa nukuu za maandishi zisizobeba maana wala majibu ya hayo maswali




MAJIBU YA MOHAMED SAID:

quote_icon.png
By Mohamed Said

Umeingiza mambo mengi sana.
Kuna Zanzibar, elimu ya Waislam, matokeo mabaya ya shule za Kiislam, kuchinja.

Itakuwa tabu kufanya mjadala uliokuwa hauna mwelekeo ulionyooka.

Lakini kwa mukhtasari ukitaka historia ya Zanzibar na maendeleo yake itabidi tuanza kwa kuvamiwa
kwa Zanzibar na jeshi mamluki la Wamakonde kutoka Kipumbwi wakifadhiliwa na utawala wa Nyerere.

Kuanzia hapa tutaingia katika tatizo la Muungano na kwa nini leo Wazanzibari wanadai nchi yao.

Kuhusu elimu ya Waislam itatubidi tuje katika njama za Nyerere kuhujumu chuo kikuu cha Kiislam
kilichokuwa kijengwe Dar es Salaam mwaka 1968 na jinsi alivyotumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS
na kuunda taasisi kibaraka BAKWATA.

Vipi shule za Waislam hazifanyi vyema inabidi tuje katika hujma ya NECTA kwa wanafunzi wa Kiislam na
tuupitie waraka wa marehemu Prof. Malima kuhusu yale aliyoyakuta Wizara ya Elimu mwaka 1987.

Wizara ya Elimu na NECTA vimegeuzwa vigango vya kanisa.

Kubwa zaidi ni kuwa Waislam kwa muda mrefu hatukuruhusiwa kujioganaizi nje ya BAKWATA kibaraka
wa serikali.

Makanisa mnaendelea kwa kupendelewa na serikali iliyojaza watendaji Wakristo sisi tungepewa hayo
mabilioni ya MoU kati ya Makanisa na Serikali tusingekuwa kama hivi.

Yapo mengi sasa chagua tuanze na lipi katika hayo hapu juu niliyokugusia.

Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.
Kwenye ghetto hakuna maji wala misala sasa watu wafanyeje?

Mnatusimanga kwa hospitali mnazoendesha kwa hela ya kodi ya serikali kodi inayolipwa na raia
wote.

Tunabanwa na mfumokristo kisha mnatulaumu hatuna maendeleo







Mohamed said

katika pita pita zangu nimekutana na post yako hii ya tare 4 January 2013 #914

Umeongelea kunyanyaswa kwa waislamu katika elimu ni njama ya JK Nyerere - Elimu ya somalia ipo taabani sana na Nyerere hayupo huko

Nakwamba Nyerere alitumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS - lakini ghilba wala uongo wa nyerere haupo Somali na inateketea vibaya

Necta imegeuka vigango vya kanisa - Somalia haina vigango vya makanisa katika taasisi zake hususani elimu lakini ipo taabani

Serikali imejaza wakristo kwa upendeleo na kuwaacha waislam - Somalia serikali takribani yote ni waislam hakuna maendeleo

Wakristo
wanawasimanga kwa hospitali zilizo jengwa kwa kodi ya watanzania- wasomali pia wanatoa na kukusanya kodi hakuna afya bora, elem wala siasa safi!

Waislamu wanabanwa na
mfumo kristo
- Somalia kuna mfumogani unaowabana wasiendelee



habari? yako Bwana ADOYA najalibu kupitia mjadala wenu na mohamed nimzuri kwa lengo la kujenga lakini maswali ya wasomali ni kumtoa nje ya mada.
hivi una jua kwamba 1992 wamarekani waliburuzwa kwenye mitaa ya mogadishu hakukua na matatizo haya unayo yaona pale hila kwa sababu mataifa ya maghalibi khasa AMERICA hile somalia ni HORN of AFRICA ukikamata ni nzuri kwa military base ndio kwa maana yamewafika haya unayoyaona HATA SISI KAMA TUTAKATAA MASILAI FURANI YA AMERICA BASI YATATUFIKA YA WASOMALI,,

Tangu mwaka 1992 wasomalia walianza kupata mazila america walitumia kila hila pamoja ya kupandikiza makundi ya kigaidi ndani ya somalia.mpaka serikali ya somalia hikapinduliwa na wanaoitwa wa babe wavita ambao wanafadhiliwa na AMERICA.wakitumia sera za mabeberu wote ya divide and rule. makundi mbali mbali ya kaanzishwa chini ya koooo mbalimbali za kisomali zenye uchu ya utawala.na wengine wakijalibu kuhikomboa somalia kutoka kwenye mzozo au vita hiyo iliyo leta wasomalia wengi Tanzania nA SEHEMU NYINGINE DUNIANI.


1997..mwaka huu wasomali waliochoshwa na vita na mapingano Viongozi wakimira,wakoo na kidini wakaona nibora kukaa chini na kuangalia kwanini wauane wao kwa wao ? wakapata jibu ni kule kungawanyika kwao nini kitawarudisha pamoja? wakapata jibu ni dini yao kumbuka somalia 100% waislam. wakakubaliana wote wawechini ya kaulimbiu ya umoja wa kiislamu,ndipo hikaanzishwa mahakama ya kislam..

1999-mpaka kufikia mwaka huu hakukua na shida kwa mahakama zakislamu kuwaludisha wasomalia katika umoja wao kwani kundi moja tu ndio lililokataa kujiunga na mahkama za kislamu nalo ni wababe wa kivita.linalofadhiliwa na America vita hikawa ni vibaraka wa America ambao ni THE LORD of War na wa somalia chini ya uongozi wa mahakama za kiislam Wakati huu eneo dogo tu ndio lilokua navita ambalo wababewakivita walikua wana tawala.

2000-mahakama za kiislamu hili chukua eneo lote la somalia na somalia hikawa chini ya utawala wa kiislamu na wasomali wote wakawa kitu kimoja taifa moja na wale wilokuanje wakimbizi wakaanza kurudi somaria Historia INAONENESHA hakuna kipindi ambacho wasomalia waliludi somalia na wageni kwenda somalia kama kipindi hiki cha 1999- 2001.

2001-RAIS wa AMERICA wakati huo GEORGE BUSH akatangaza kuamba kona ya AFRICA inakaliwa na Magaidi na wao hawapati usingizi kwa sababu magaidi wana shikilia sehemu furani duniani vikaanza vikwazo somalia. vikifwatia na vita kali baina ya wasomalia na VIBARAKA WENGINE ETHOPIA...kwa masilahi ya marekani droon zikatumika

2003-ETHOPIA wanaingia somalia wakisaidiwa na America wasomali wanapambana na wavamizi kwako wewe ni kosa hilo
ajabu kweli hii kutete Taifa lako nikosa???

2004 somalia haikaliki tena mahakama za kiislamu zina angushwa na baazi ya viongozi wao wanakamatwa baadhi yao wana kubali matakwa ya AMERICA wanaachwa hai na waliobaki na msimamo wao wana uwawa.

2004-2005 AL-SHABAB tafsiri hisio rasmi(vijana shupavu) Inazaliwa baadhi ya viongozi vijana waliobaki wanabakia na msimamo usioteteleka zidi ya wavamizi wote walioingia somalia kwa masilahi ya marekani

2004-2005-Burundi ,Rwanda Uganda zinaingia Somalia kwa masilahi ya marekani

2010-Kenya inaingia kwa masilahi ya marekani

WASOMALI MATATIZO YAO NI KWA SABABU YA UZALENDO WAO.KWA NCHI YAO

MWISHO
 
Said, nadhani kuna mambo ambayo ima hujayaona, hayaelewi au yamefunikwa na ''mapenzi''
Wenyewe wanasema ukipenda chongo utaita kengengeza.
Hebu tuvunje vunje hii habari yako ili tuone wapi ambapo hatupo pamoja

Said Mago;6039464]Bahati nzuri nimebahatika kukisoma hiki kitabu cha ndugu yangu Mohammed Said the life and times of Abdulwahid, Uamuzi wa Busara na vitabu kadhaa vya brother Said i suggest watu wasome sio tu kumuattack. wengi wanajua tu kumuatack na inaonesha dhahiri hawajasoma kitabu chake..
Hapa unafanya makosa ya kuhisi bila ukweli.
Mimi nimesoma nakala za mwanzo kabisa za vitabu vyake kwa lugha zote. Najua na wengi pia walisoma.

Unakosea unaposema kumu-attack. Hakuna wa kumuattack Mohamed eti kwasababu yeye ni Mohamed na in fact hakuna hata mtu anayeattack vitabu vyake. Kinyume chake watu wanatumia akili zao kutathmini na kutafakuri kama kile wanachokiona au kukisoma ni sahihi.

Mohamed anaweka hoja zake, zile zenye utata ima zinafafanuliwa, zinawekwa sawa au anaulizwa atoe utata. Pengine ungesema watu wana attack hoja zake ningeweza kukubaliana nawe kwasababu katika fikra mtu anatakiwa afanye hivyo si kwa vitabu hata katika fikra zake mwenyewe.

Kwa msingi huo wewe umeandika ukiwa na dhana tayari kuwa anakuwa attacked.
Hapo hutatenda wema kwa wale walisoma na kuelewa na si kulewa vitabu vyake.

Lakini pia lazima utambue kuwa mtu anaye attack hoja ana strong background ya kufanya hivyo na hiyo ni kwa yule tu aliyesoma vitabu vyake akiwa na akili timamu.
brother Said ameandika kisomi bila kumuatack mtu yoyote wala dini bali amonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi gani njia mbalimbali zilitumika kudidimiza wengine.
Hapa tayari umeshajiaminisha kuwa kile alichokisema ni sahihi.
Hakuna namna ya kukusaidia kuona vinginevyo ila kukutakia heri na fanaka.

Hizo njia alizoonyesha pengine utupe mfano mmoja tu unaodhani ameonyesha na kuwa ''attacked'' unfair.
Yeye mwenyewe ameshindwa kufanya hivyo pengine wewe unaweza kutusaidia.

Hatari inayokukabili ni kuangalia mambo kwa mapenzi na si kwa ukweli.
Ipo siku Mohamed atakuambia Rais wa kwanza wa Tanganyika alikuwa Oliver Tambo kabla hajahamia Africa kusini kuendeleza mapambano dhidi ya makaburu.

Kwavile utakuwa na hofu ya ku-attack hoja hiyo huku ukiwa na lundo la mahaba itabidi uamini hivyo. Atakayekuambia si kweli huyo attakuwa ame attack Vitabu vya bro Mohamed, ame attack imani yako ya uislam, ame attack mapenzi yako kwa vitabu vyake na ame attack fikra zilizofungwa na atahitajika kusoma tena vitabu vya Mohamed. Kama atakuwa hajakufur na kuwa kafir sijui atakuwa na bahati kiasi gani.

Wasomaji wajiulize, mathalan, Mohamed anaposema Warioba hakuwahi kujulikana nchini kabla ya uteuzi wake kuwa waziri mkuu, akatokea mtu na kuonyesha bila kificho kuwa alikuwa anajulikana na Mohamed akakubali sasa hapo tatizo lipo wapi? Kwamba kueleza usahihi ndio ku attack.

Mohamed, kaweka takwimu, wana JF wakazipitia na kumwambia zina tatizo.
Mohamed akakubali kuwa zina matatizo makubwa sasa hapo tatizo lipo wapi?

Mohamed kaonyesha Nyerere alivyokuwa na chuki na waislam, akapewa nafasi ya kueleza chuki, badala yake akamuelezea Nyerere kama mtu mkarimu sana kwa waislam, sasa hapo tatizo lipo wapi?

Mo kasema John Garang alikuwa mkristo, mtu mmoja kasema ni kweli lakini pia alikuwa mwanafunzi wa UDSM, hapo kuna tatizo lipi?

Mo, kaeleza AA iliundwa na K.Sykes, akatokea mtu na kusema ndiyo Sykes ni mmoja wa waanzilishi lakini mkutano wa kuanzisha chama ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola ambaye alikuwa Rais wa chama na Ramadhani Ali akiwa makamu, Sykes katibu, hivi hapo kuna tatizo gani?

Mo, kaandika kuhusu EAMWS akaulizwa, eh kama Nyerere aliiua je kule Mombasa ilipoanzia aliyeiua ni nani, alikuwa Kenyata au mtu gani? Hakujibu sasa kosa ni la nani yule atakaye ufafanuzi au yule asiyeweza kufafanua.

Orodha hiyo ni ndefu, sijui mwenzetu Said ulikuwa na ushauri gani!
Kwamba ilikuwa bora kukaa kimya tu na kuamini Kawawa alikuwa makamu wa Rais 1988, juzi juzi tu hata wewe ukiwa umeshazaliwa.Endapo hilo hukuona kama kosa, je yele yaliyoelezwa wakati baba yako hajazaliwa unadhani yana usahihi gani?

Na mwisho mbona Mohamed kaeleza kuhusu marehem bibi yake binti Mluguru na jinsi togwa lilivyotamu wakati wa jua hasa ukiangalia wachezaji wa Yanga wakiwa uwanjani au ukiwa unanyolewa na mwingereza pale chini ya ukwaju n.k. hakuna aliye ''mua attack'' Hivi Said, tukae kimya tukiambiwa Rais wa TANU alikuwa Abdul Sykes! real. Eti tukisema tuna attack si Mo tu bali imani nzima ya Uislam!!

Said tuonee huruma muungwana! Tukienda madukani inflation inatuliza, hospitali hakuna dawa, tukirudi nyumbani mgomo wa walimu, tukivuka bara bara dala dala zinanyemelea roho zetu, tukiingia JF Mo anatusubiri kutupiga kamba za ubongo, please tuone huruma Said Mago.
 
Bahati nzuri nimebahatika kukisoma hiki kitabu cha ndugu yangu Mohammed Said the life and times of Abdulwahid, Uamuzi wa Busara na vitabu kadhaa vya brother Said i suggest watu wasome sio tu kumuattack. wengi wanajua tu kumuatack na inaonesha dhahiri hawajasoma kitabu chake..
brother Said ameandika kisomi bila kumuatack mtu yoyote wala dini bali amonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi gani njia mbalimbali zilitumika kudidimiza wengine.
mnaomuattack brother Said someni kitabu cha padri J.Silvanus kanisa katoliki na siasa za tanzania 1954-1985 utagundua kuwa brother Said yeye ni miongoni tu mwa waliojitolea kusema kweli kosa lake kubwa kawasemea kweli waislamu, ukisoma kitabu cha Silvanus utanielewa kwa nini nimesema kosa la brother Said.
ifike kipind tukubali madhifu ambayo yamewahi tokea na kujitahidi kujenga a better tomorrow,
aliyoandika brother said ni sehemu tu kwa yatakayo andikwa huko mbele na tukumbuke kitabu kama maisha na nyakati za Abdulwaheed ni cha mwaka 1997 sidhani kama Marehemu aliweza au alipata muda wa kukubali au kukanusha yaliyomo ktk kitabu hicho.
Tukumbuke tu maneno haya yalipata kusemwa na Wole Soyinka
"TISHIO KUBWA KWA UHURU NI UKOSEFU WA UKOSOAJI.VITABU NA MAANDISHI NI TISHIO KWA WALE WOTE WANAOTAKA KUUFICHA NA KUUZIKA UKWELI"
Said Mago, kwa kuwa hii ni posti yako ya kwanza kwenye huu mjadala, nitakuomba uzingatie mambo kadhaa kabla ya kukurupuka kwani yaonesha wazi kwamba huu mjadala umeudandia tu na hujaupitia toka mwanzo wake. Huyu Mohamed Said wengine tumeanza naye mbali sana na si hivyo tu tuko baadhi yetu hata umri tunamzidi kwa kiasi kikubwa tu. Yawezekana kwako anaonekana mzee wa busara lakini kwangu na naamini kwa Watanzania walio wengi Waislaam, Wakristo na wasio na dini, wakwe kwa waume, wazee kwa vijana, wa makabila yote zaidi ya mia moja hamsini, Mohamed Said ni zaidi ya mchochezi na mdini, ni mtu wa fitina.

Mohamed Said, akisaidiwa na Mwalimu wake kutoka Pakistani, Malik na vijana wachache wa wakati huo waliokubali kurubuniwa kirahisi kama Prof. Hamza Njozi, Dr. Ramadhani Dau na wengine kadhaa walikaa kitako na kutunga hadithi. Hiyo hadithi ilijengwa katika misingi ya uongo na ulaghai na iliweza kudumu tu kwa sababu walengwa wake hawakuwa tayari kuhoji uhalali na ukweli wake. Leo hii nuru inaanza kuchomoka, giza hiloo linapiga bye bye kwani toka lini giza na mwanga zikachangia sinia? Ukweli unapogonga hodi, uongo uko mashakani na salama yake ni kuaga mapema.

  • Mimi Mag3 niliwahi kumsihi sana Mohamed Said achutame ili huko baadaye atakapoathirika watoto wasishuhudie aibu yake.
  • Nguruvi3 aliwahi kumwonya asipende kuogelea mtoni pamoja na watoto kwani hataweza kutakata kutokana na maji kuchafuliwa.
  • Mwanakijiji alimtahadharisha kuhusu kuwawekea marehemu maneno mdomoni na badala yake ajitahidi kuwahoji wahusika wakingali hai.
  • jasusi alimkanya kutokuwanukuu vibaya waandishi kwani vitabu vipo na asipoangalia vitakuja kumuumbua kwani dunia ni ndogo.
  • Ngongo alimshangaa kwa nini anaangalia kila kitu kwa macho ya kidini na kumwomba ajaribu kuwa mkweli kwa nafsi yake.
  • Nyambala amemkemea tabia yake ya kutunga na kuleta madai ya uongo hapa jamvini lakini masikini wapi, kalewa porojo.
  • sweke, Pasco, Gwalihenzi na wengine, wameshauri, wametahadharisha, wameonya, lakini mmm!...
Kweli, tumejitahidi lakini kama kawaida na kwa upofu na chuki zilizomjaa rohoni hakutusikiliza na badala yake akaamua kuendelea kuoga mtoni na watoto. Ni kweli wako waliokubali awapake na wao uchafu nao wanaona fahari kufanana na yeye lakini nasema na kusisitiza, ni vipofu wachache. Nina hakika kuwa Watanzania kwa umoja wao uliojengeka kwa kipindi kirefu hawatakubali kurubuniwa kirahisi kama anavyodhani na badala yake iko siku atawekwa kitimoto na washiriki wake wote wajibu kwa nini walitaka kulivuruga taifa. Hakuna Mfumokristo...ni zimwi walilojiundia wenyewe ndani ya mioyo yao na sasa wakae kutafunwa nalo.

Mimi yaliyofanyika miaka ya 1940s mpaka tunapata uhuru niliyaishi na kuyashuhudia, sikusubiri kuhadithiwa na watu wenye donge rohoni. Nilipoingia Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, Mohamed Said hata mlango wa shule alikuwa hajauona...nimekuta Sindbad Night Club, nimekuta Sombrero Night Club, nimekuta Banda beach, nimekuta Metropole Night Club, nimekupa Gateways Night Club, nimekuta Anatoglu Hall, nimekuta Afrika Hotel original ikitazamana na Lutheran Church kivukoni...maandamano ya kupinga National Service nilikuwapo, mkutano wa kuunga mkono Azimio la Arusha nilihudhuria, jamani wengine tumetoka mbali!

Said Mago, ni kweli umesoma hicho kitabu cha kivukoni? Sisi tumesoma vyote, vya mohamed Said na hicho, na ukweli ni kwamba wengi anaodai wamesahauliwa wametajwa ndani ya kitabu hicho. Kinachogomba ni Mohamed Said kujaribu kupotosha dhana kuwa ni Waislaam ndio waliopigania uhuru wa nchi hii, tena si Waislaam Watanganyika bali wakuja Wazulu, Wamanyema na Wanubi! Huku ni kuwadhalilisha wazee wetu...kumbuka hawa waliletwa Tanganyika na Mjerumani kama mamluki katika jeshi la Kijerumani kupigana dhidi ya Watanganyika. Kwanza Wazulu wenyewe mwanzoni hawakuwa Waislaam mpaka baada ya kuoleana na Wamanyema, je upo mpaka hapo?
 
Sijui kama ulipata nafasi ya kumsikiliza raisi Jakaya Kikwete kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi March 2013, ametoa majibu kuhusu mfumo wako kristo kwamba ni uwongo tu! na kwamba miskiti mitatu ya dar mumemuombea dua yeye Jk afe!
Mfumokristo ni dhana ya kufikirika ambayo haipo, ila kundi fulani la MS na wafuasi wake wanasema lipo.

Huko nyuma aliko toka kabla ya kuuawa watumishi wa Mungu niliwahi muuliza MS, Hivi hao anawaita wazee wake walipigania uhuru wa Tanganyika kama waislam au Watanganyika, majibu niliyopewa yalikuwa ya kejeli kupita maelezo lkn sasas kadli siku zinavyosonga mbele. Naona kumbe hicho kitabu chake kinamakosa mengi sana ya kihistoria ambayo yanatakiwa yahaririwe kama atataka muhusika.

Hainiingia akilini yeye kuandika kuwa Sinde Warioba, eti alikuwa hajulikani, Hivi MS anataka kutuambia kuwa yeye alipokuwa anaandika hiyo historia alikuwa hajui kuwa Warioba tayari alishafikia kiwango cha jaji katika utumishi wa mahakama, si hilo tu anataka kutuambia kuwa wakati yeye anaandika alikuwa hajui kuwa Jaji Warioba aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivi ni kweli MS alikuwa hajui kuwa Jaji Warioba aliwahi kuwa Waziri wa Sheria katika nchi hii.

Hebu MS naomba unisaidie wewe unaposema mtu huyu anajulikana katika ulingo wa siasa huwa unamaanisha mtu huyo awe ameshika nafasi zipi hasa kisiasa. Naomba majibu sio yale ya nimekusoma
 
Hongera sana bwana Mohamed kwa uchambuzi wako katika hili swala. Kila anapoingia kiongozi (Rais) muislamu hawa wakristo hawishi kumsakama kwa maneno ili aonekane kwa watanzania kuwa hafai, Angalia enzi za Al-hajj Mwinyi na sasa Dr kikwete, Hawaishi kutoa miongozo ya uchaguzi, kauli nzito nzito kwa kiongozi mkuu wa nchi. Mbona wkt wa Ben Mkapa hawakutoa muongozo wa uchaguzi, Wala kauli wanazotoa hivi sasa?! Wanatuchokoza na tumeambiwa (Waislamu) tusianze mpk tuchokozwe!!
 
Katika kile kinachoitwa madai ya waislam hasa kuhusu elimu, zipo tuhuma kuwa wanafunzi wakristo walichukuliwa kupelekwa maeneo yenye waislam na viwango vidogo vya ufaulu.
Hili linaonekana kuwa ni dhulma kwa kuliangalia kama linavyoletwa.

Kinachowashindwa watu kuelewa ni kuwa mfumo wa kugawa nafasi uliletwa makusudi ili angalau kuwepo na uwiano katika makundi na jamii tofauti ambazo zilionekana kuwa nyuma.
Huko nyuma mtihani wa taifa ulikuwa unaangalia kiwango cha ufaulu bila kuangalia mtu anatoka eneo gani.

Kuna nyakati ambapo mkoa mmoja au miwili iliweza kutoa wanafunzi wengi kwenda sekondari pengine kuliko mikoa 10 kwa pamoja. Ilionekana maeneo yasiokuwa na fursa yaliendelea kuwa nyuma. Hii ni pamoja na mikoa ya pwani.

Utaratibu wa nafasi kimikoa ulilenga kupeleka fursa kwa kila mkoa. Ndipo hata viwango vya ufaulu vikawekwa kutokana na ushindani. Mfano, mkoa uliamua kiwango cha ufaulu ili kutimiza namba waliopewa na elimu taifa.
Kama ni wanafunzi 300 basi hata aliyepata 30 lakini akawa ndani ya 300 alikwenda sekondari.

Kwa namna fulani ilionekana kama uonevu kwa baadhi ya mikoa.
Fikiria mkoa ambao kuna mwanafunzi alipata 60 na kuachwa lakini wapo wanafunzi waliopata 45 na kuendelea na masomo.Kwahiyo si kweli kuwa utaratibu huo ulilenga kuhujumu zaidi ya kusaidia.

Kilichotokea ni kuwa wanafunzi kutoka mikoa yenye ushindani walihamia kule kwenye viwango duni.
Hili halikufanywa na serikali bali mwamko wa watu katika jamii zilizoona mbali.
Hapa nadiriki kusema kwa mkoa kama Kilimanjaro, Bukoba na ile ya kanda ya ziwa hii waliifaya sana kuhamishia wanafunzi pwani.

Nimeona kwa macho yangu mkoa kama wa Tanga mwanafunzi akitolewa ili akaolewe na wa kiume kuacha shule kwa ajili ya biashara za kuangalia viunga vya minazi. Narudia nimeona kwa macho yangu na akili nikiwa mtu mzima.

Swali linakuja, kwanini basi mikoa ya pwani ilikuwa na viwango duni?
Je, tatizo ni wale wenye viwango vikubwa kuhamia huko au tatizo ni wenyeji kutothamini elimu na kuwa na viwango duni. Mimi nadhani hakuna anayepaswa kutete uzembe kuwa katika dunia ya sasa basi kila kitu kitakuja katika silver plate.

Nawapongeza wazazi walioona fursa hiyo na nawalaumu wale waliodhani ni vema kuishi na viwango duni.
Tatizo si wahamiaji, tatizo ni wenyeji ambao hawakuwa na mwamko.

Mfano, Kilwa shule imefungwa kwasababu hakuna wanafunzi. Kama shule hiyo ingekuwa na wanafunzi waliohamia 50 pengine isingefungwa na hao ndio wangepata fursa iliyopo na ambayo haitumiwi vema na wenyeji.

Si kweli kuwa wakristo walipeleka watoto huko, hili lilihusu kila mtu mwenye uelewa na mwamko bila kujali imani yake.
Hakuna mwislam aliyeiona fursa hiyo akaiachia eti kwasababu wale wenyeji ni waislam na hivyo walipaswa kuachiwa nafasi hizo. Kama ingekuwa ni rahisi hivyo basi tusingeona rushwa katika taasisi za kiislam katika mambo hayo hayo ya elimu.

Hao wanaosema huo ni mfumo wanasahau kuwa nafasi zinazotolewa na mashirika mbali mbali kwa waislam zimekuwa zintumiwa kwa njia ya ''know who'' na wala si vinginevyo.

Matokeo yake wamechaguliwa vijana walioishia katika biashara za unga huko Uturuki na kwingineko na wala hawajarudi kusaidi jamii zao.

Vipi leo ionekane dhulma wakati ndani ya taasisi za kiislam kuna dhulma na wanajamvi wanaoshahdidia hoja hii mfu wanajua kuwa hilo lipo na linatendeka?

Hoja hii ya nafasi kwa maeneo na wahamiaji kuchukua fursa ni mfu na wala haina mashiko.
Hoja imejengwa ili kuendelea kuwapumbaza watu badala ya kuwaeleza ukweli wa dunia ya leo ya ushindani.

Hakuna anayefanikiwa kwa kudhani jina lake ni sehemu ya Resume. Ni lazima watu waambiwe ukweli hata kama unauma
Ningeshauri taasisi na wasomi wa kiislam wazame katika chimbuko la tatizo na sikutafuta band aid.
 
Kuna mahali nimesoma kuhusu shule za serikali. Kama kawaida imejengwa hoja dhaifu sana na imegusa hata kule watu wasikojua kuwa wengine walishiriki kwa macho na akili zao.

Zimetajwa shule zilizojengwa kwa misaada ya serikali zikatajwa shule kama Ruvu, Kibiti na nyingine za miaka ya 70 kama ilivyosemwa.

Zimerushwa tuhuma kuwa asilimia 80 ya wanafunzi na wafanyakazi wa maeneo hayo ni wakristo.
Sijui asilimia hiyo ilipatikanje kwasababu kuu mbili.

Wafanyakazi wa kawaida wanapatikana kutoka katika eneo husika. Hawa ni kama wapishi madereva na wengine (auxilliary)
Wafanyakazi wa taaluma kama walimu wanapatikana kwa sifa za vyeti vyao.

Zimetajwa shule katika mpangilio ambao unazua maswali kuliko majibu.
Nadhani mwandishi wa habari hiyo hafahamu shule hizo zilijengwa kwa utaratibu gani na zilitumika vipi.

Nimpe kionjo kidogo. Shule za Ruvu, Kilosa, Ifakara na Kibiti zilijengwa kwa msaada kutoka Cuba.
Ukienda katika shule hizo kila kitu ni ''copy' ya kingine.
Shule hizi zilikuwa za mchepuo wa Kilimo.

Utaratibu wa kuchagua wanafunzi kuingia katika shule hizi uligawanywa kwa kanda.
Katika kanda hizo ninakumbuka shule ya Kibiti ilikuwa inachukua kanda ya mashariki(Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara).

Kwa wale waliopitia Ruvu zama hizo nadhani watakuwa wanamkumbuka rafiki yangu Mjale na kule Ifakara Matimbwi.
Si kweli kuwa shule hizo zilichukua randomly, na hii ilifanywa makusudi kuhakikisha kuwa kila kanda inafaidika na msaada huo wa Cuba.Wazee waliokuwa wizara ya elimu na walioshiriki katika kuratibu haya waje hapa waniambie kama si kweli.

Sasa kama kuna kanda iliyokuwa imezembea wakaingia watu wengine, nani wa kulaumiwa?
Hivi kwanini umlaumu mtoto wa kiislam aliyesoma Ikizu akafaulu vizuri.

Kama mwanafunzi alitokea Mkuranga akaenda kusoma Peramiho na akafaulu, tatizo ni huyu aliyekwenda kule au wale wa kule waliozembea kutumia fursa!

Siku zote huwa nasema ni lazima wasomi watumie usomi wao kutafuta suluhu ya tatizo.
Ni jambo baya sana kutafuta suluhu kwa kutafuta visingizio. Tatizo liangaliwe kwa kina na wala si kwa ushabiki.

Mohamed alitoa mfano mzuri sana. Alisema sheikh Kassim alipokuja Dar alikuwa ''mshamba'' maana alishuka kwenye dau na hakujua anaelekea wapi hata baba yake kumfuata.

Alichokifanya ni kwenda kufundishwa ilm na baba yake kumkuta akiwa na maalim. Alipokuja Dar aliwakuta watu wa kariakoo wapo pale, yeye akatumia fursa hiyo na leo anamwandika kama mtu maarufu.

Huyu si alitumia fursa kutoka Bagamoyo! sasa kwanini alaumiwe yeye kuja kuchukua ilm wakati watu wa kariakoo walikuwa na fursa hiyo bila kupanda dau na hawakuitumia.

Vipi leo mwananchi aone Kilwa wanafunzi hawataki shule na yeye kuitumia fursa hiyo kwa watoto wake ionekane kama dhulma. Dhulma iko wapi? Kwanini mtu ajidhulum halafu aseme kadhulimiwa?

Narudia mfano huu kila siku, shule ya Hassan Mwinyi miaka miwili iliyopita ilikuwa na wanfunzi 250 na walim wawili.
Hapa nani anamdhulumu mwenzake! Hivi hapa si kujidhulumu kweli.

Kule mkuranga mwalimu Mkuu mmoja, akisafiri kiranja wake anakuwa makamu mkuu wa shule.
Haya ndiyo ameneo tunaambiwa walidhulumiwa kwa kuleta watoto kutoka nje. Haa! hapa kunadhulma gani jamani! nisaidieni wanajamvi.

Halafu mwl Mbwambo hasemwi kuwa ni shujaa! Walimu wangapi wa mkuranga wamekimbia maeneo hayo.
Nani anadhulumu hapa?

Kunakitu nadhani sikielewi kwasababu kila nikisoma hoja naona zingine kama gurudumu.
Hata nikijaribu kuzichongea miguu na mikono ya miti, hazisimami na wala hazina utetezi.Zinakosa mashiko.
 
Nimeona kwa macho yangu mkoa kama wa Tanga mwanafunzi akitolewa ili akaolewe na wa kiume kuacha shule kwa ajili ya biashara za kuangalia viunga vya minazi. Narudia nimeona kwa macho yangu na akili nikiwa mtu mzima..
Ukianza kuhojiwa kuhusu haya "matukio" utaanza kutoa mapovu na bado utataka tukuamini!

Kama umedanganya kwenye haya mangapi huko nyuma utakuwa umetudanganya?! hufai kujihusisha na Historia ya Tanzania umefeli!
 
Hongera sana bwana Mohamed kwa uchambuzi wako katika hili swala. Kila anapoingia kiongozi (Rais) muislamu hawa wakristo hawishi kumsakama kwa maneno ili aonekane kwa watanzania kuwa hafai, Angalia enzi za Al-hajj Mwinyi na sasa Dr kikwete, Hawaishi kutoa miongozo ya uchaguzi, kauli nzito nzito kwa kiongozi mkuu wa nchi. Mbona wkt wa Ben Mkapa hawakutoa muongozo wa uchaguzi, Wala kauli wanazotoa hivi sasa?! Wanatuchokoza na tumeambiwa (Waislamu) tusianze mpk tuchokozwe!!

Ni kweli mkuu hawa wapo kidini zaidi juu ya uislam na anachofanya muislam wao wanapinga hata kama kinaukweli
 
Hongera sana bwana Mohamed kwa uchambuzi wako katika hili swala. Kila anapoingia kiongozi (Rais) muislamu hawa wakristo hawishi kumsakama kwa maneno ili aonekane kwa watanzania kuwa hafai, Angalia enzi za Al-hajj Mwinyi na sasa Dr kikwete, Hawaishi kutoa miongozo ya uchaguzi, kauli nzito nzito kwa kiongozi mkuu wa nchi. Mbona wkt wa Ben Mkapa hawakutoa muongozo wa uchaguzi, Wala kauli wanazotoa hivi sasa?! Wanatuchokoza na tumeambiwa (Waislamu) tusianze mpk tuchokozwe!!
Hizi ni porojo za kwenye mihadhara ya mjinga mwenzenu Mohamed Said ambaye daima kila kitu anakiangalia kwa jicho la uislam! hizo ni fikra mfu na zinaendeshwa na watu wapuuzi kama wewe na hilo zee lako puuzi Mohamed. Mtu mwenye akili timamu ataiangalia serikali kama taasisina sio kama Kikwete. Na kwa ujinga wenu huo ndio maana mnaishia kushinda miskitini kuombea dua ati watu wafe! pumbavu zenu, mtakufa wenyewe kabla ya hao mnaowaombea wafe.
 
Hongera sana bwana Mohamed kwa uchambuzi wako katika hili swala. Kila anapoingia kiongozi (Rais) muislamu hawa wakristo hawishi kumsakama kwa maneno ili aonekane kwa watanzania kuwa hafai, Angalia enzi za Al-hajj Mwinyi na sasa Dr kikwete, Hawaishi kutoa miongozo ya uchaguzi, kauli nzito nzito kwa kiongozi mkuu wa nchi. Mbona wkt wa Ben Mkapa hawakutoa muongozo wa uchaguzi, Wala kauli wanazotoa hivi sasa?! Wanatuchokoza na tumeambiwa (Waislamu) tusianze mpk tuchokozwe!!

nani anamsakama kati ya wale wanaotokoa nyaraka za kishauri na wanaokaa kuomba duwa na kusoma itkafu ili MUMUUWE?
 
Back
Top Bottom