Tatizo ni kuwa kwa mtu anayedai kuandika kisomi inasikitisha kuwa uliamini kila ulichoambiwa na wazee wako na wala hukutumia akili zako au utaalamu wako kuhoji ukweli wake, usahii wake au hata uwezekano wa yote mawili. Kwa vile wazee walikupigisha stori wewe ukachukulia kama absolute truths... without questioning or applying critical method of reasoning. Ndio maana mwalimu wako wa Mantiq ingeliwezekana angecharazwa viboko hadharani kwa kutokuandaa kuwa a critical thinker...
Ndio maana katika articles aliyotuma niliyosema ina matundu Mohamed amejicontradict sana. Kwabahati mbaya file limekuwa corrupted, nitaliweka tena mstari kwa mstari.
Kwa ufupi, Mohamed anasema Nyerere alikuwa ''stranger'' Dar es Salaam na kwa wapiga kura.Hakunjua Sykes labda kama alimsikia katika maongezi ya Mwapachu Uingereza.
Halafu anasema Nyerere alikutana na Denis, Kasella Bantu na Dosa Azizi katika national conference mwaka 1947.
Maana yake alisikia habari za Sykes kutoka kwa Aziz mwaka 1947 na si wakati akiwa Uingereza.
Akasema Nyerere alipopewa uongozi ndio ukawa mwanzo wa Political career. Amesahau kuwa aliashaanza mwaka 1947 alipokuatana na watu katika mkutano mkuu, alipokuwa Makerere n.k.
Akasema Phombeah alimpigia kampeni lakini hakukuwa na ulazima kwasababu wazee wake walishaamua awe kiongozi.
Cha kushangaza ni pale aliposema kura zilipigwa kwa kunyosha mikono. ''Inasemekana'' Nyerere alishinda kwa kura moja, wengine wanasema hakushinda kama alivyomkariri Dosa.
Sasa kama kura zilikuwa za kunyoosha mikono kwanini matokeo yake yajulikane kwa watu wawili watu na si washiriki wote katika mkutano ule wa wazi.
Akamnanga Nyerere kuwa alikuwa mzuri wa debate lakini si siasa kama Sykes. Sasa Nyerere alikuwa anafanya debate za shule au za kisiasa na kama ni hivyo kwanini wazee waliamua kumpa uongozi tena kwa kumuomba mara mbili.
Akasema hivi mikutano ya TAA ilikuwa inafanyika kwa Sykes,hapo ndipo mahali ambapo Nationalist walikutana.
Hapa alikuwa na maana uwepo wa Nyerere ulileta Nationalist na si waislam. Halafu akajisahau na kusema Nyerere alipokuwa anaaga mwaka 1985 aliwaita waislam exclusive, yaani mkutano ule ulikuwa si wa wazee wa Dar es Salaam au Nationalist bali waislam. Amesahau kuwa Nyerere alipokuwa na jambo aliongea na taifa kwa kupitia wazee wa Dar.
Article nzima ina back and forth kwasababu tu alisimuliwa na wazee tofauti tofauti na hakuchukua initiative za kuhakiki habari bali kuongozwa na ushabiki. Nitaiweka tena ili wasioamini kuwa hii ni simulizi na si tafiti waone.