Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Hakuna tukio muhimu katika historia ya Harakati za uhuru wa Tanganyika kama azimio la Mkutano mkuu wa TANU Tabora mwaka 1958 kushiriki katika uchaguzi wa kura tatu...azimio ambalo lilipitishwa kwa kupigiwa kura na wajumbe 60 kutoka majimbo yote ya Tanganyika. Kati ya kura hizo kura 60 zilizopigwa ni wajumbe 37 waliounga mkono azimio lililokuja kujulikana kama "decision of wisdom" na wajumbe 23 walipinga! Ni azimio hili lililomfanya Zuberi Mtemvu, publicity secretary wa TANU makao makuu, kuhama TANU na kuanzisha chama chake cha African Congress.
Pia ni mkutano huu wa Tabora uliowachagua wajumbe wanne kwenye baraza la LEGCO katika uchaguzi mwaka huo huo wa 1958. Hawa wajumbe walichaguliwa kuwawakilisha Watanganyika wenzao kwa uwezo na sifa zao na katu hawakuchaguliwa kwa misingi ya dini zao...Wajumbe hao ni;
Ni huo huo mwaka 1958, ndipo shaka na manung'uniko yalianza kujitokeza mioyoni mwa baadhi ya wana TANU, hasa wale wa dini ya Kiislaam kuwa Kanisa linaanza kuiteka TANU ambao ndio msingi wa madai ya Mohamed Said. ILI kukabiliana na hali hiyo chama cha Kiislaam, AMNUT, kikiongozwa na Chamwenyewe kilianzishwa kama LUKU dhidi ya spidi ya TANU. Ajabu ni kwamba mpaka kufikia hapo, kwa nini Abdulwahid Sykes, kiongozi asiye na mfanowe katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika, hatumsikii? Ni nani huyo, wakati huo, alizima ama kuficha habari/historia za wazee wake Mohamed Said wa Gerezani, Kipata na Kariakoo? Mohamed Said ni masalia tu ya AMNUT.
- Julius Nyerere - Jimbo la Mashariki na makao makuu ya TANU.
- Solomon Eliufoo - Jimbo la Kaskazini
- John Mwakangale - Jimbo la Kusini
- Chief Abdalla Fundikira - Jimbo la Magharibi
Kwa namna yoyote mtu anayejaribu kuwaweka kwenye mizani sawa Mwalimu Julius Nyerere na watu kama hao wazee wa Gerezani ni wa kupuuzwa. Somo tunalopata hapa ni kuwa kuna watu walianza kuwabagua Watanganyika wenzao wasio wa dini yao toka kabla ya uhuru na hata baada ya kukataliwa waliendeleza harakati zao hata baada ya uhuru...ni hawa Mohamed Said anawalilia na kujaribu kuwakweza na sisi wengine tunamkatalia kata kata. Ndio maana msimamo wangu kwake haubadiliki wala hauyumbi, Mohamed Said ni mchochezi na mtu hatari ambaye kama serikali isingekuwa dhaifu, angeshashughulikiwa zamani. Lakini masikini Tanganyika, mbegu aliyoipanda imeanza kuwazaa akina Ilunga, Ponda na Uamsho na bado!
5. Lawi Sijaona
6. Poul Bomani
7. George Kahama
8. John Ketto
Funguka zaidi hapo wanajamvi wakusome na mimi takuja na mpini kuhusu hawa uliowataja na hawa wengine ulikuwa umewasahu nimekuongezea.