Haaa! hapa ndipo nasema matatizo ya waislam mara nyingi baadhi yao huyakuza bila sababu za msingi.
Tumesikia kuhusu taasisi za kiislam kufanyiwa hujuma. Tumeuliza je, WML !
Watu wamekimbia hawataki kabisa kuliongelea hilo kwasababu wanajua kulikuwa na uchafu nyuma yake.
Wanakimbia ukweli ili kutafuta mahali pa kunyooshea vidole.
Tumesikia wakitajwa akina Commonwelath, world church council n.k.
Hili la Wolrd Muslim linafunikwa funikwa kwasbabu linahusu uhalifu na uharmia ndani ya wanaonung'unika
Ni kwa mtazamo huo huo Gombesugu naye anapatwa na mshangao wa barabara kuitwa Kibaki.
Mwaka jana tukiwa na mnakasha na Mohamed, alisema barabara ya Mshume Kiyate imerudishwa baada ya waislam kulalamika.Akamtuhumu sana Nyerere kwa kufuta majina kama ya Kiyate na akina Bibi Titi Mohamed.
Leo Gombesugu naye anatafuta mahali pa kujishikiza kwasababu Nyerere keshafariki.
Hii barabara imejadiliwa na baraza la madiwani wa Kinondoni, Jiji na mkoa.
Aliyekuwepo katika kutoa hadhi hiyo ni pamoja na Rais Kikwete, Meya wa Jiji, Meya wa Mnaisapaa ya Kinondoni n.k.
Hatukuwahi kusikia mzee yoyote wa Dar es Salaam akisimama kupinga. Hatukuwahi kusikia taasisi yoyote ikisimama kohoji.Kwa maneno mengine wakazi wote wa Dar es Salaama akiwemo Mohamed Said walikubaliana na hili.
Ninachokifikiria hapa sijui nani atabeba lawama maana nikiangalia kwa haraka haraka hakuna mkono wa mfumo na Nyerere hayupo tena.Mtego zaidi ni kutambua kuwa mkazi wa pwani ndugu JK anayeijua historia ya Pwani ndiye aliyekabidhi.
Hili ni tatizo la wakazi wa Dar es Slaama kama basi ni tatizo!
Sasa hebu njooni na hadithi za kuunga unga ili tujue nani amefanya nini na kwanini.
Acheni mambo haya jamani, jamii ina matatizo mengi sana ya kushughulikia. Majungu na fitna havitasaidia kabisa.
Tatizo likiwa ndani ya nyumba yako unachukua hatua na si kusimama na kuangalia jirani kapika nini ili iwe sababu!
NB
***Mohamed, WML bado lina utata, tusipoliongelea basi itabidi tufute habari za EAMWS katika maandiko yetu** ha ha ha
Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3,
I must admit that sometimes when I read your comments I get bit depressed. But still both of you have my
utmost respect for your contributions in here.
Ile "
habari ya Mwai Kibaki" kupewa jina la mtaa/barabara hapo Mzizima,mimi niliitaja sababu iliniumiza moyo kwa uzalendo na wala si
udini,
u-wana mjini au
u-Dar Es Salaam. Nastaajabu yale
maelezo marefu na
dhana yalihusu nini!? Lakini haina neno, tuendelee na mnakasha.
Huyo
Mwai Kibaki, wala sifa zozote za kuwa kiongozi mwadilifu au alofata uadilifu. Na hii ni kabla ya kuingia madarakani na mpaka kesho. Nafikiri mtakumbuka vitimbi vyao vingi enzi zao za
u-playboy na akina
D. Moi,
Baraka H.
Obama Snr na wengineo wengi pale
Nairobi!? Mwai Kibaki hana
credibility ya maana pahala pengi saana duniani,na hata huko kwao
Kenya.
Scandals zake na "udhalim" ni nyingi mno na
unatisha saana.Hata self discipline yake na
dignity yake binafsi ni utata mtupu!? Tuyaache hayo maana si yetu!
Ndo maana nilipostaajabu na kujiuliza hivi hao "
viongozi wetu" na
Serikali walitumia
criteria na kufata taratibu, vipengele vipi mpaka walipoamua kumtunuku hiyo "
zawadi"!? Lakini naona wenzangu hapo hamkuona
uzalendo wangu bali
udini tu!?ahaha!! Viongozi wengi wageni kama vile
Patrice Lumumba,
Augustino Neto,
Ngouabi na wengineo nawakubali saana,lakini huyo
Mwai Kibaki nafikiri ni
Taifa/Nchi yetu kuzidi kujivunjia heshima tu.
Mag3:
Ile
idea yako ya kuleta
mada juu ya mada,nafikiri ni nzuri mno. Lakini nachelea isijeleta
tafrani na songombingo, na kuzidisha "
mtafaruku wa Juma Mbaruku". Nahisi la muhimu tuumalize huu ulopo hapa kwanza kabla hatuja tambukia pengine. Lakini hii shauri tu,nafikiri mtoa
mada/shutuma Yericko Nyerere nae pia ashauriwe ili atujuze yakini yake!?
Ahsanta kwa kunisikiliza huo uchechefu wangu.
CC:
Ritz,
Ami,
JokaKuu,
Jasusi,
Kadogoo,
Boko haram,
Sheikh Mohamed Said,
THE BIG SHOW,
Nyambala,
mfumo,
wimbi la mbele