Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

, Uislam ni dini ya mwenyezi mungu. Uislam hauna miliki au hati miliki isipokuwa kwa muumini. Baru baru aliwahi kusema si kila mwislam ni muumini lakini kila muumini ni mwislam. Uislam unasimama katika amani, haki na ukweli.

Uislam si ushabiki na Uislam umesisitiza katika kutafuta maarifa. Maarifa yaweza kupatikana hadi China. Maarifa si ushabiki, ni utambuzi na ufahamu. Kila anayekwenda kinyume na mafunzo ya Allah anamhalifisha Mwenyezi Mungu.

Uislam hauzui kusema au kukubali ukweli. Na hakika hiyo ni moja ya hidaya ya mwenyezi mungu kwa waja wake.
Hakika yule anayesimama katika ukweli basi atakuwa ameiona nuru na atakuwa miongoni mwa waja wema.

Mohamed Said akisema, yule mwenye elimu ana bahri, hivyo usichoke kujifunza na wala usijizuie kujifunza.
Kujifunza kunahitaji ustahamilivu hekima na busara. Hasira, jwazba na unyonge ni silaha mbaya unapokuwa katika kujifunza. Jifunze kila kilichopo katika mazingira yako, kiwe ndani ya msikiti, kanisa, sinagogi au Jamatini.

Basi tumuombe mwenyezi akunusuru na hasira na matusi, ili sote tuwe waja wake.
Mimi nimekusamehe kwasababu hakika hakuna mtimilifu miongoni mwetu wanadamu.

Masalaam, msalimie Ahli na nduguzo.

Nguruvi kwahaya maneno nimekubali uko vizuri :yo::yo::yo: na wewe naomba ukubali mzee MS yuko vizuri hata kama umeona kuna makosa kwenye historia yake yeye ni binadamu kwasababu kitabu chake si msahafu ninacho kushauri huu mnakasha tuendenao kwa ustaarabu bila madharau kwasababu ziko pande mbili hapa lakini kunaupande ambao unadharau upande mwingine eti kwasababu wanasoma madrasa hilo sio jambo lilotuleta kwenye huu mnakasha kwahiyo respect ni kitu muhimu sana sawa mkubwa[/QUOTE]

Nifurahishwa sana na maungamo haya. Binafsi nimeshawahi kuungama kuwa ni afadhali nimsome Sheikh Said kuliko kusoma Annur (ingawa Sheik Said hakupenda kauli yangu ya kumtenganisha yeye na Annur).
Hapa sikuikataa kazi nzima ya Sheikh Said, tatizo lake ni pale anapounganisha matatizo ya Waislamu na kudai tatizo la yote ni Nyerere na Ukristo wake na Wakristo!
Najiuliza hivi, kwa nini Waislamu wengi linapitokea tatizo kwenye Uislamu basi sababu au Mchawi wao ni Ukristo? Bila shaka haya ndio matokeo ya "elimu" inayotolewa kwa umma wa Waislamu nchini na Wahadhiri wengi na Sheikh hujiingiza humo kwa makusudi. Hatoi suluhisho ila kunogesha chuki za kidini!
 
Hiki kitabu ndio kimenifikia leo kikiwa miongoni mwa vile vitabu nilivyokuwa nimeagiza; kingine ni Tanganyika Under German Rule... Kumbe kina Kleist hawakusahauliwa na historia... wametajwa sehemu nyingi tu...

Duh! Miaka yote hiyo hukupata kuwasoma waakina Kleist wakitajwa "sehemu nyingi" mpaka leo hii ulipopata hicho kitabu tena kwa kushauriwa na huyo huyo unayompiga vita?
 
Jamani nilikuwa likizo kidogo, naona mnakasha bado unaendelea. Mohamed, si sahihi kusema kuwa waislamu walileta uhuru wa Tanganyika. Waislamu walianzisha harakati za kupigania uhuru katika eneo la pwani, hasa jiji la Dar-es- Salaam, hilo ni sahihi. Wakamwamini Julius Nyerere kuongoza harakati hizo, hilo pia ni sahihi. Lakini mizizi ya harakati ilienea nchi nzima hata katika maeneo ambayo waislamu si wengi. Lakini wewe unataka kutuaminisha kuwa ni waislamu pekee ndio waliopigania uhuru wa nchi hii, na kumalizia kwa kibwagizo kuwa baadaye wakabaguliwa. Nitarudi tena baadaye, ngoja ni "catch up" kidogo. Rafiki yangu Ritz yuko wapi?
Ritz kapewa likizo atarudi baada ya likizo
 
Duh! Miaka yote hiyo hukupata kuwasoma waakina Kleist wakitajwa "sehemu nyingi" mpaka leo hii ulipopata hicho kitabu tena kwa kushauriwa na huyo huyo unayompiga vita?
You have missed the point mr. Kudadeki. Mohamed Said alitaka kutuaminisha kuwa bila yeye akina Kleist wangesahaulika katika historia.
 
Kwani wewe hujui ya kwamba wa kwanza kuanza kujenga pande mbili katika mnakasha huu ni nyinyi??
Mmesahau kuwa ni nyinyi ndio wa kwanza kumwambia Moh Said anaoga na watoto wadogo,ya kwamba hawa ni walamba buti wa Moh Sadi,na kwamba hawa ni wafuasi wa Moh Said kisa tuh wameonekana kukubaliana na Moh Said katika mnakasha huu??
Sasa kipi kinachhokushangaza Moh Said akisema nyie na sie??,hopless blocks..

THE FIFTH ESCAPE ROUTE..

The fith escape route;

inasemaa,,inasema..

The fifth escape route is to frighten people away fom discussing the Muslims question by making it a political taboo.
To raise it is to threaten our country's peace and security..!,,yes,to threaten peace & security together with country's prosperity,,,"afanalekii !!"
Th
is strategy is of little value because Muslims have never been known to be peace - and -order fanatics,who regard human life so precious and peace so valuable,as to be brought at the price of servitude.
To them peace and order do not constitute an ultimate value,to be held dear irrespective of what they preserve.In any case,trying to scare away a debt collector,is not a reliable way of attaining peace,even of mind.
Wanywa kahawa tuna msemo unaosema ya kwamba "DAWA YA JINO NI KUNG'OA",,'DAWA YA DENI NI KULIPA",,

"A bad tooth has to be removed and replaced,but a debt has to be paid"

Waanzilishi wa "sisi na nyie" ni nyinyi..

The Big Show,

Salaam,Al Akhiy.

Wallahi nakupongeza kwa umahiri wako uso mfano. Tangia weekend nilikua nakusoma na kukufuatilia kwa makini minyambulisho na maporomoko ya bayana zako hususan kwenye hii "The Escape Route".
Ama kwa hakika ume-summarize hizi tafran zoote za huu mnakasha, tena kwa ustadi na utuvu wa kina kama dasturi yako.
Hata huu mnakasha umekua dhaifu sasa kwayo ulonena,ilobaki hapa sasa ni wingi wa fadhaa na ile "inadi ya mbwa koko".

Mola takulipa fadhila zako pamoja na Maalim wetu Sheikh Mohammed Said Insha Allah.

Ahsanta.
 
You have missed the point mr. Kudadeki. Mohamed Said alitaka kutuaminisha kuwa bila yeye akina Kleist wangesahaulika katika historia.
Mohamed Said anataka historia ya TANU ifananishwe na historia ya familia ya Sykes:
- AA ihusishwe moja kwamoja na SYKES;
-TAA itundikwe shingoni mwa KLEIST;
-TANU ni mali ya ABDULWAHID;

Kwa mtindo huu historia inarejeshwa mahala pake. Mwalimu ahusishwe na CCM ile ya 1977 angalau!
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli hii ndiyo turufu ya Mohamed Said,

Bahati mbaya sana kwake nikuwa anapingana na fact za historia na kukumbatia hisia zake tu,

Hapa tunamkatalia kuwa aliwazalo sio uhalisia wake.
 
Last edited by a moderator:
Mnakasha umejaa vitishoo!!
Mara....list this...list that...nitakupuuza...nitaku-nini sijui aaah!!

Hii ni ishara ya kuishiwa hoja.

Hili ndilo lina nifanya nami niishie kusoma tu, hoja zimekuwa repetitive hakuna mpya. Same quotes and evidance ndizo zinarudiwa rudiwa. Hoja zenye mashiko hakuna tena. Hakuna nguvu ya hoja bali ni ubabe tu yaani hoja ya nguvu. Mjadala umekuwa "your wrong am right and there is nothing you can do about it." I just want to see where will this thread take us.
 
gombesugu, how much I wish the above was true for, had it been so, the kind of discussion currently taking place in this thread, would never have seen the light of day. Kama nilivyosema mwanzo kuhusu post yako ya kwanza kabisa, mimi Mag3 niliipokea kwa moyo usio na doa and my greatest expectation was for you to be for real! Ungekuwa umeufuatilia huu mnakasha kwa umakini na ukomavu kama huu uliouonesha hapo juu, hungekuwa na shaka lolote kujua sisi wengine tunatetea nini na tunapinga nini.

Kwetu wengine tuliozaliwa 1940s, huko kunikuta humu mtandaoni tu, kungefawafanya vijana wanaonitupia maneno ya kejeli wajiulize mara mbili mbili. Ni wazee wangapi wa rika yangu walioshuhudia mathalani computer zikiundergo metamorphosis kutoka zilizojaza nyumba nzima hadi sasa zinaweza kuwekwa kwenye mifuko ya shati. Ni wazee wangapi waliopata bahati ya si kuziona tu bali kufanya nazo kazi when computers were anything but user friendly...nakueleza haya ili uelewe kitu kimoja, hiyo historia anayojaribu kusimulia Mohamed Said, wengine tuliiishi, we lived it na kwa rehema za Muumba bado tupo.

Hiyo ndio maana gombesugu, nina ujeuri wa kuita koleo kwa jina lake...a spade deserves to be called by its name...I have had the priviledge of witnessing most of it! Nilitaka tu kuweka hili sawa...tuendelee na mjadala.

Thanks Mag3; Gombesugu, fikiria hivi, tulipigana na Idd Amin ile vita ya Uganda kama Tanzanians. Nobody cared askari aliyepigana ni kabila gani au dini gani. Kesho akija "mwanahistoria" na kuandika jinsi ambavyo "wakurya" waliokomboa uganda au bukoba kutoenziwa utamwelewa? kesho mwingine anaandika jinsi mchango wa "freemasons" walivyopigana kulikomboa daraja la Mto kagera katika jeshi hilohilo haujathaminiwa; wewe utamwelewa vipi? Mwisho ya yote ukimpa swali DOGO kabisa; SASA? Hana jibu. Wazee waliompenda na kumchagua Nyerere akiwa na miezi Dar hawakujali wao ni Sunni au Shia au Freemason an Protestants. Hivi kesho nikivalia hilo kidedea na kusema wote waliomnunulia baiskeli walikuwa ni wa jumuiya ya Qadiriya utanielewa? Hapo ndipo ukiongozwa na chuki ALWAYS utafanya blunders kwenye vission.
 
Gombesugu, umejitahidi sana kujificha katika pazia. Tulikwambia kuwa ni suala la muda true color zitajitokeza na sasa zimejitokeza. Bandiko lako hili hukuwa na sababu ya kutumia neno mtu au watu. Hili umemlenga Nguruvi3.
Mimi nipo na Mohamed siku nyingi na moja kati ya mambo hayanisumbui ni kudharauliwa, kutukanwa au kudhalilishwa.
Mambo hayo hayanisumbui kwasababu kama kuna mtu mmoja ananielewa si tatiziki na 10 wasionielewa Hili ni kosa lile lile la kila mara. ''baadhi yetu akina nani? Hivi akitokea kaka yako hakubaliana na Mohamed huyo ni ''baadhi yetu'' au inakuwaje.
Nadhani kama umesoma vizuri kuhusu Mohamed, dhima ya andiko lake ni chuki, farki, tashtiti n.k. Kama unachukia chuki basi Mohamed hafai kuwa ''baadhi yetu''. Kwanini ndugu yangu usisimame katika ukweli?Hapa tuna uelewa tofauti na ni vema tukasadiana. Endapo kuna kitu kimefanyika kisayansi, methodically basi tunakuomba sana utusaidie. Na hapa nitakuuliza kitu kimoja. Je, upo tayari nikuwekee habari ya Mohamed utuelezee kisayansi ili utusaidie kitaalauma na ki-uwanazuoni kuonyesha chuki na dhalili anazofanyiwa?
Kama utakuwa tayari nifahamishe.Si kweli, labda kama unamuongelea Mohamed. Mohamed anajulikana jamvini kwa kauli za ''sina ujuzi'', nimekusoma, tuendelee na darsa, hilo tuliache kwanza, inasemekana, andika kitabu, nimekwenda ulaya, nimekula na wazungu n.k. katika kukimbia hoja.
Mfano, mumekomalia Makerere, nimeweka mnakasha niliokuwa nao na Mohamed,si hoja imekwisha!
Nimewauliza kwani harakati ni kitu gani hakuna aliyeeleza, hoja ikaisha. Nafahamu unachukia sana hoja za Mohamed kubomolewa lakini spade iitwe spade na siyo big spoon.Ukweli ni sehemu ya dini na imani kwa waumini.

Wala usiseme jamaa sema Nguruvi3. Nimeweka hoja hiyo kwasababu imesemwa kuwa waislam hata walisoma wananyijmwa nafasi. Nikasema basi kama yupo Zoologist ajitokeze maana kuna shirika '(siyo mimi linahitaji mtu)Katika kufanya spinning zile zile za Ritz nawe umeniwekea maneno. Hilo sijali kwasababu kumbu kumbu zipo.
Narudia kama kuna Zoologist ajitokeze, kama hakuna shirika hilo hilo linatafuta local epidemiologist hasa mwenye background ya vetenary. Kama hakuna basi hapo ndipo mahali pa kuanzia kwanza kujiuliza kwanini? Nimesema waislam specifi kwasababu ndio wenye malalamiko ya kupea nafasi za menial job hata kama ni qualified kama alivyosema Mohamed.Nimeongeza Epidemiology na zaidi kama yupo mtu wa Eng-Agric aliye na utaalamu katika combine harvester naye pia ajitokeze na qualification zake tusaidiane.And respectful Muslims to add on.
Hapo juu umelalamika sana kuhusu matusi, kwa bahati mbaya na hili nakusamehe umerudia kile kile usichokitaka.

Gombesugu, Uislam ni dini ya mwenyezi mungu. Uislam hauna miliki au hati miliki isipokuwa kwa muumini. Baru baru aliwahi kusema si kila mwislam ni muumini lakini kila muumini ni mwislam. Uislam unasimama katika amani, haki na ukweli.

Uislam si ushabiki na Uislam umesisitiza katika kutafuta maarifa. Maarifa yaweza kupatikana hadi China. Maarifa si ushabiki, ni utambuzi na ufahamu. Kila anayekwenda kinyume na mafunzo ya Allah anamhalifisha Mwenyezi Mungu.

Uislam hauzui kusema au kukubali ukweli. Na hakika hiyo ni moja ya hidaya ya mwenyezi mungu kwa waja wake.
Hakika yule anayesimama katika ukweli basi atakuwa ameiona nuru na atakuwa miongoni mwa waja wema.

Mohamed Said akisema, yule mwenye elimu ana bahri, hivyo usichoke kujifunza na wala usijizuie kujifunza.
Kujifunza kunahitaji ustahamilivu hekima na busara. Hasira, jwazba na unyonge ni silaha mbaya unapokuwa katika kujifunza. Jifunze kila kilichopo katika mazingira yako, kiwe ndani ya msikiti, kanisa, sinagogi au Jamatini.

Basi tumuombe mwenyezi akunusuru na hasira na matusi, ili sote tuwe waja wake.
Mimi nimekusamehe kwasababu hakika hakuna mtimilifu miongoni mwetu wanadamu.

Masalaam, msalimie Ahli na nduguzo.

Muheshimiwa Nguruvi3,

I'm quite impressed with your brain power to try comprehend what Islam is and its teaching and who Muslims are.

Ahsanta kwa kunijuza jitihada zako za kujaribu kuwasaidia kwa kuwatafutia ajira/vibarua waIslam hapo Tanganyika.

Nashukuru pia kwa kunisamehe kwa kuhisi kwako kuwa maelekezo yangu ya awali yalikua na "elements" za hasira na kashfa dhidi yako.

Ile habari ya kunitaka mimi nikiandike upya kitabu cha Sheikh Mohammed Said "kwa njia ya kisayansi" ili kifahamike uzuri,ahsanta kwa kunipa cheo hicho japo ni kikubwa mno dhidi yangu. Kama utarejea kwenye bayana yangu ya awali kwa Sheikh Mohammed Said nalieleza uchechefu wangu na ku-declare kuwa nipo kwa kujifunza!

Pia nachelea isijekua ile habari ya Rais wenu Bw W. Mkapa,alipotuamrisha ati tumwandikie madai na dhiki zetu "kwa njia ya kisayansi". Tulipomaliza na kumkabidhi akatujibu, ati yeye binafsi hana uwezo wa kuyashughulikia na Serikali haiyamudu maana ni "magumu mno na ni ya kiHistoria". I have never come across the most ridiculous comment made by a sitting President my entire life!!

Kuhusu yule Alhaj Rukara wa WML,nilikufahamu maswali yako kwa Sheikh Mohammed Said,japo naye kwa ustaarabu alikujibu kuwa hazijui "zile habari".
Nafikiri kwa upande mwingine inalazim tuwasamehe hawa ndugu zetu wa kirundi na kinyaRwanda maana yaelekea ndio "dasturi na mazoea" yao, kuwa makwao pakitulia basi hurejea.
Nafikiri unakumbuka habari ya Prof. Silas Lwakabamba wa UDSM baadae KIST na sasa hivi ni mmojawapo wa watu wa karibu saana na Kagame na ana cheo/mamlaka nyeti pale Kigali-Rwanda.
Tujitahidi na kujiepusha kidogo kuwa selective tunapotoa mifano. Huyo Lwakabamba naye vitimbi na ghilba zake haitofautiani kabisa na shutuma na madai ulotoa dhidi ya Alhaj Rukara na labda kupita. Alikua ni kama "James Bond" fulani hivi. Shughuli nyingi nyeti alizowahi kutumwa na Serikali na Consultancy kadhaa alikua akizipitisha kwanza kwa Kagame na Rwanda tangia yupo pale UDSM. Huyu ni mkristo mzuri tu kama alivyokua Alhaj Rukara ni mu-Islam mzuri pia. Nafikiri hatuna haja ya kufungua mnakasha mwingine ati kujadili na kupeana definitions za Gaidi,Mchochezi,mwanaharakati au Jasusi!?

Mifano ni mingi tu kuanzia misimamo ya kina Reagan na Thatcher dhidi ya Mandela kipindi kile mpaka leo tunafikia baina ya wa-Afrika wenyewe kwa wenyewe! Kwa hiyo yawezekana kabisa kuwa; huyo umuonae wewe ni gaidi,mwanaharakati hatari na mchochezi,wengine wanamuona mpigania haki na ni mkombozi wao!! Kwa ufupi huyo Prof. Silas Lwakabamba mnyaRwanda,ambae miaka mingi baadhi ya jamaa walikua wakiamini kuwa ni mzalendo halisi,mkristo mtakatifu na msomi mahiri, "sisi wengine" tulishajua madhila na ujasusi wake dhidi ya nchi yetu. Japo kwa bahati mbaya kelele zetu zoote wakti huo zilipuuzwa kwa kuitwa wadini!?

Kwahiyo nakufahamu "kiasi" juu ya kilio chako dhidi ya Alhaj Rukara.

Tafadhali tuendelee na mnakasha ili tusiende nje ya mada/shutuma alizoleta Yericko Nyerere. Punguza kumbana Sheikh Mohammed kuhusu hilo suala la Alhaj Rukara na WML,na kishasema haijui hiyo habari.

Ahsanta kwa kunisikiza uchechefu wangu na nakutakia siku njema mTanzania mwenzangu.
 
[/COLOR]Nguruvi kwahaya maneno nimekubali uko vizuri :yo::yo::yo: na wewe naomba ukubali mzee MS yuko vizuri hata kama umeona kuna makosa kwenye historia yake yeye ni binadamu kwasababu kitabu chake si msahafu ninacho kushauri huu mnakasha tuendenao kwa ustaarabu bila madharau kwasababu ziko pande mbili hapa lakini kunaupande ambao unadharau upande mwingine eti kwasababu wanasoma madrasa hilo sio jambo lilotuleta kwenye huu mnakasha kwahiyo respect ni kitu muhimu sana sawa mkubwa
Nifurahishwa sana na maungamo haya. Binafsi nimeshawahi kuungama kuwa ni afadhali nimsome Sheikh Said kuliko kusoma Annur (ingawa Sheik Said hakupenda kauli yangu ya kumtenganisha yeye na Annur).
Hapa sikuikataa kazi nzima ya Sheikh Said, tatizo lake ni pale anapounganisha matatizo ya Waislamu na kudai tatizo la yote ni Nyerere na Ukristo wake na Wakristo!
Najiuliza hivi, kwa nini Waislamu wengi linapitokea tatizo kwenye Uislamu basi sababu au Mchawi wao ni Ukristo? Bila shaka haya ndio matokeo ya "elimu" inayotolewa kwa umma wa Waislamu nchini na Wahadhiri wengi na Sheikh hujiingiza humo kwa makusudi. Hatoi suluhisho ila kunogesha chuki za kidini![/QUOTE]

Wimana; U have hit a very central point. Mzee MS lazima apewe heshima kama scholar na efforts zake za kuandika kitabu lazima tumpe Hi-5 (japo Kadogoo ataniungurumia kuwa Hi-5 ni ya kikafiri!!!!!) That said, lazima pia apewe heshima nyingine kwa kutambua kuwa sio lazima wote tukubaliane naye (myself included). Na hii ni desturi ya scholars. Ipo siku atahitaji pengine kuandika another work, nakwambia zile criticisms za kina Mag3, Nguruvi, wewe, nk ndio zitamsaidia sio sifa za wapambe.
 
Thanks Mag3; Gombesugu, fikiria hivi, tulipigana na Idd Amin ile vita ya Uganda kama Tanzanians. Nobody cared askari aliyepigana ni kabila gani au dini gani. Kesho akija "mwanahistoria" na kuandika jinsi ambavyo "wakurya" waliokomboa uganda au bukoba kutoenziwa utamwelewa? kesho mwingine anaandika jinsi mchango wa "freemasons" walivyopigana kulikomboa daraja la Mto kagera katika jeshi hilohilo haujathaminiwa; wewe utamwelewa vipi? Mwisho ya yote ukimpa swali DOGO kabisa; SASA? Hana jibu. Wazee waliompenda na kumchagua Nyerere akiwa na miezi Dar hawakujali wao ni Sunni au Shia au Freemason an Protestants. Hivi kesho nikivalia hilo kidedea na kusema wote waliomnunulia baiskeli walikuwa ni wa jumuiya ya Qadiriya utanielewa? Hapo ndipo ukiongozwa na chuki ALWAYS utafanya blunders kwenye vission.
well said, well done!
Mimi nimeona Wakurya wakidanganya umri ili waende Kagera! Nimeona kwa macho.
Nimeona matajiri wakitoa ng'ombe kwa ajili ya chakula cha wanajeshi, mabasi yakitolewa kupeleka wapiganaji.

Kule barabara ya 10 na 11 sikuona hamasa kama nilizoziona Tarime, Kyabakari, Nyamongo n.k. lakini haina maana hawakwepo Wabondei au wasambaa.

Sasa akitokea mtu aka single out Wakurya na kuandika historia ya vita ya Kagera kwa kutumia Wakurya tu na kisha kusema ndiyo historia ya vita ya Kagera na kwamba huo ni ukweli, inafikirisha sana.

Kwa wanajamvi, tunathamini mchango wa kila mtu lakini basi mchango wa mtu fulani usitumike kumdhalilisha mwingine.
Uhuru wa Tanganyika ni nyumba ya matofali na kwamba kila tofali lilikuwa na nafasi yake muhimu na isemwe hivyo.
Hapa ndipo watu hawaelewi na kuishia katika ''nyie na sisi''

Hatuwezi kuwa na taifa la nyie na sisi. Rwanda hawakuweza, Bosnia hawakuweza, Nigeria ni matatizo tupu n.k.
Hata pale walipo akina ''sisi'' kama Somalia bado wamegawanyika kwamba Wasengeli wanasema sisi, wabaidoa wanasema nyie. Mtoto amezaliwa na sasa ni askari hakuna muafaka. Jamani, huko ndiko mnataka tuelekee?

Kama ndiko, basi tuelewesheni nani mshindi wa maeneo hayo!
 
JOKAKUU:
Hakuna Muislamu asiezingatia elimu! huna tafiti yoyote uliyoifanya ila ni hisia zako tu! kama dai lako la Waislamu wa Machame wanazingatia elimu kuliko wenzao wa pwani toa ushahidi hapa kuonesha ni wangapi wenye nyadhifa Serikalini au wamepata ajira ktk idara mbalimbali za Serikali, Mashirika ya umma nk!

Mimi Mama angu ni Mmachame na Machame naijua vema! Waislamu wa Machame kiboko cha Mfumo kristo hakikuwaacha nyuma! baadhi yao wameokolewa kwa kurithi vihamba na mashamba yenye Migomba ya ndizi, matunda na kahawa! na hulka waliyonayo ya biashara pia imesaidia kuinua kidogo hali yao ya maisha kwa baadhi yao tu wala sio wote!
Sasa ukija na taarifa kama hiyo isiyofanyiwa utafiti utakuwa bado hujasaidia jamii yetu kuepuka madhara ya mfumo kristo!

Kadogoo
,

..acha ubishi ndugu yangu, Waislamu wa Machame, Usangi, Kagera, wanazingatia elimu kuliko wenzao walioko Pwani na Kusini.
 
Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3,

I must admit that sometimes when I read your comments I get bit depressed. But still both of you have my utmost respect for your contributions in here.

Ile "habari ya Mwai Kibaki" kupewa jina la mtaa/barabara hapo Mzizima,mimi niliitaja sababu iliniumiza moyo kwa uzalendo na wala si udini,u-wana mjini au u-Dar Es Salaam. Nastaajabu yale maelezo marefu na dhana yalihusu nini!? Lakini haina neno, tuendelee na mnakasha.

gombesugu,

..hauko peke yako ktk hilo.

..wana Jamii Forums wengi walitoa maoni wakilaumu barabara kubwa D'Salaam kupewa jina Mwai Kibaki.

..kuna viongozi wazito na marafiki wa kweli wa Tanzania hawajapewa heshima kama aliyopewa Kibaki.

..hapa nazungumzia viongozi kama Mzee Kenneth Kaunda. Linganisha barabara ya Kaunda na ile ya Mwai Kibaki.
 
Last edited by a moderator:
The Big Show,

Salaam,Al Akhiy.

Wallahi nakupongeza kwa umahiri wako uso mfano. Tangia weekend nilikua nakusoma na kukufuatilia kwa makini minyambulisho na maporomoko ya bayana zako hususan kwenye hii "The Escape Route".
Ama kwa hakika ume-summarize hizi tafran zoote za huu mnakasha, tena kwa ustadi na utuvu wa kina kama dasturi yako.
Hata huu mnakasha umekua dhaifu sasa kwayo ulonena,ilobaki hapa sasa ni wingi wa fadhaa na ile "inadi ya mbwa koko".

Mola takulipa fadhila zako pamoja na Maalim wetu Sheikh Mohammed Said Insha Allah.

Ahsanta.

Waleykhum Salaam gombesugu a.k.a THE GREAT THINKER..
Hao ndio walitaka kuutia Utaifa wetu kwenye mashaka,sisi tunaurudisha..
Ajabu Twashangaa Twaitwa wachochezi..
Ila umma unaelewa mbivu na mbichi..
 
Last edited by a moderator:
well said, well done!
Mimi nimeona Wakurya wakidanganya umri ili waende Kagera! Nimeona kwa macho.
Nimeona matajiri wakitoa ng'ombe kwa ajili ya chakula cha wanajeshi, mabasi yakitolewa kupeleka wapiganaji.

Kule barabara ya 10 na 11 sikuona hamasa kama nilizoziona Tarime, Kyabakari, Nyamongo n.k. lakini haina maana hawakwepo Wabondei au wasambaa.

Sasa akitokea mtu aka single out Wakurya na kuandika historia ya vita ya Kagera kwa kutumia Wakurya tu na kisha kusema ndiyo historia ya vita ya Kagera na kwamba huo ni ukweli, inafikirisha sana.

Kwa wanajamvi, tunathamini mchango wa kila mtu lakini basi mchango wa mtu fulani usitumike kumdhalilisha mwingine.
Uhuru wa Tanganyika ni nyumba ya matofali na kwamba kila tofali lilikuwa na nafasi yake muhimu na isemwe hivyo.
Hapa ndipo watu hawaelewi na kuishia katika ''nyie na sisi''

Hatuwezi kuwa na taifa la nyie na sisi. Rwanda hawakuweza, Bosnia hawakuweza, Nigeria ni matatizo tupu n.k.
Hata pale walipo akina ''sisi'' kama Somalia bado wamegawanyika kwamba Wasengeli wanasema sisi, wabaidoa wanasema nyie. Mtoto amezaliwa na sasa ni askari hakuna muafaka. Jamani, huko ndiko mnataka tuelekee?

Kama ndiko, basi tuelewesheni nani mshindi wa maeneo hayo!

Alaa..!
yan umetoa well said na well done juu..??
kwa lipi sasa?angesema Rits au Ami maneno hayo bila shaka ungewaita Wanywa kahawa..
double standards at its best level..!!
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Mnakashaumejaa vitishoo!!
Mara....list this...list that...nitakupuuza...nitaku-nini sijui aaah!!

Hii ni ishara ya kuishiwa hoja.
MzeeSaid, hizo kambi mbili ni zipi? Na una hakika gani kuwa wanaokubali hoja zakowote ni kambi "SISI" na wasiokubali hoja zako ni kambu"NYIE"?

Kwa hizo "fitna" zako sio ajabu kuwa mihadhara kuhusu vitabu vyakounafanyiaga Misikitini ambako kambi ya "NYIE' hawawezi kuingia na kuulizaili kukupa changamoto, na kwenye redio (bila shaka ni ile iliyofungiwa) ambayohadhira ni ile ambayo haina Waandishi wenye kuzingatia weledi wa Tasnia yahabaru.
Kwani wewe hujui ya kwamba wa kwanza kuanza kujenga pande mbilikatika mnakasha huu ni nyinyi??
Mmesahau kuwa ni nyinyi ndio wa kwanza kumwambia Moh Said anaoga na watotowadogo,ya kwamba hawa ni walamba buti wa Moh Sadi,na kwamba hawa ni wafuasi waMoh Said kisa tuh wameonekana kukubaliana na Moh Said katika mnakasha huu??
Sasa kipi kinachhokushangaza Moh Said akisema nyie na sie??,hopless blocks..
.....................................

Waanzilishi wa "sisi na nyie" ni nyinyi..

Ami :violin:
 
gombesugu,

[/B]..hauko peke yako ktk hilo.

..wana Jamii Forums wengi walitoa maoni wakilaumu barabara kubwa D'Salaam kupewa jina Mwai Kibaki.

..kuna viongozi wazito na marafiki wa kweli wa Tanzania hawajapewa heshima kama aliyopewa Kibaki.

..hapa nazungumzia viongozi kama Mzee Kenneth Kaunda. Linganisha barabara ya Kaunda na ile ya Mwai Kibaki.

Hili binafsi naliona kama ni tatizo la kiitifaki na weledi wa watawala wetu tu.
 
Last edited by a moderator:
Muheshimiwa Nguruvi3,

I'm quite impressed with your brain power to try comprehend what Islam is and its teaching and who Muslims are.

Ahsanta kwa kunijuza jitihada zako za kujaribu kuwasaidia kwa kuwatafutia ajira/vibarua waIslam hapo Tanganyika.

Nashukuru pia kwa kunisamehe kwa kuhisi kwako kuwa maelekezo yangu ya awali yalikua na "elements" za hasira na kashfa dhidi yako.

Ile habari ya kunitaka mimi nikiandike upya kitabu cha Sheikh Mohammed Said "kwa njia ya kisayansi" ili kifahamike uzuri,ahsanta kwa kunipa cheo hicho japo ni kikubwa mno dhidi yangu. Kama utarejea kwenye bayana yangu ya awali kwa Sheikh Mohammed Said nalieleza uchechefu wangu na ku-declare kuwa nipo kwa kujifunza!

Pia nachelea isijekua ile habari ya Rais wenu Bw W. Mkapa,alipotuamrisha ati tumwandikie madai na dhiki zetu "kwa njia ya kisayansi". Tulipomaliza na kumkabidhi akatujibu, ati yeye binafsi hana uwezo wa kuyashughulikia na Serikali haiyamudu maana ni "magumu mno na ni ya kiHistoria". I have never come across the most ridiculous comment made by a sitting President my entire life!!

Kuhusu yule Alhaj Rukara wa WML,nilikufahamu maswali yako kwa Sheikh Mohammed Said,japo naye kwa ustaarabu alikujibu kuwa hazijui "zile habari".
Nafikiri kwa upande mwingine inalazim tuwasamehe hawa ndugu zetu wa kirundi na kinyaRwanda maana yaelekea ndio "dasturi na mazoea" yao, kuwa makwao pakitulia basi hurejea.
Nafikiri unakumbuka habari ya Prof. Silas Lwakabamba wa UDSM baadae KIST na sasa hivi ni mmojawapo wa watu wa karibu saana na Kagame na ana cheo/mamlaka nyeti pale Kigali-Rwanda.
Tujitahidi na kujiepusha kidogo kuwa selective tunapotoa mifano. Huyo Lwakabamba naye vitimbi na ghilba zake haitofautiani kabisa na shutuma na madai ulotoa dhidi ya Alhaj Rukara na labda kupita. Alikua ni kama "James Bond" fulani hivi. Shughuli nyingi nyeti alizowahi kutumwa na Serikali na Consultancy kadhaa alikua akizipitisha kwanza kwa Kagame na Rwanda tangia yupo pale UDSM. Huyu ni mkristo mzuri tu kama alivyokua Alhaj Rukara ni mu-Islam mzuri pia. Nafikiri hatuna haja ya kufungua mnakasha mwingine ati kujadili na kupeana definitions za Gaidi,Mchochezi,mwanaharakati au Jasusi!?

Mifano ni mingi tu kuanzia misimamo ya kina Reagan na Thatcher dhidi ya Mandela kipindi kile mpaka leo tunafikia baina ya wa-Afrika wenyewe kwa wenyewe! Kwa hiyo yawezekana kabisa kuwa; huyo umuonae wewe ni gaidi,mwanaharakati hatari na mchochezi,wengine wanamuona mpigania haki na ni mkombozi wao!! Kwa ufupi huyo Prof. Silas Lwakabamba mnyaRwanda,ambae miaka mingi baadhi ya jamaa walikua wakiamini kuwa ni mzalendo halisi,mkristo mtakatifu na msomi mahiri, "sisi wengine" tulishajua madhila na ujasusi wake dhidi ya nchi yetu. Japo kwa bahati mbaya kelele zetu zoote wakti huo zilipuuzwa kwa kuitwa wadini!?

Kwahiyo nakufahamu "kiasi" juu ya kilio chako dhidi ya Alhaj Rukara.

Tafadhali tuendelee na mnakasha ili tusiende nje ya mada/shutuma alizoleta Yericko Nyerere. Punguza kumbana Sheikh Mohammed kuhusu hilo suala la Alhaj Rukara na WML,na kishasema haijui hiyo habari.

Ahsanta kwa kunisikiza uchechefu wangu na nakutakia siku njema mTanzania mwenzangu.

Gombe sugu kumbe na wewe ni muokoteza hoja kama Said, hahaha unamfahamu Lwakabamba lakini? Huyu aliwapa maisha wabongo pale Kist kuanzia malekchara, tvutorial assistants mpaka workshop instructors wa dini na makabila mbalimbali leo analinganishwa na huyo Rukala? ama kweli hili somo lenu la udini halina aibu.

Kuna kit nakisoma btn the lines, shule si mchezo bana yaani leo waliokuwa wa mjini kama nukuu lukuki za mchchezi said wanalamika kuonewa n a kudhulumiwa na mijitu isiyostaarabika kutoka bara hahahahahaha!!!!! Kweli waliosema elimu ufunguo wa maisha they were very right.
 
Kadogoo
,

..acha ubishi ndugu yangu, Waislamu wa Machame, Usangi, Kagera, wanazingatia elimu kuliko wenzao walioko Pwani na Kusini.

Ahsante Jokakuu; Mi napenda sana input ya Kadogoo. Hii ni kwa sababu sio mbali na pale kwao wana shule safi ya Mudio Islamic, inafanya vizuri sana. Ukija kwa watani zake hapa Same upareni wana Kirinjiko, inafanya nayo vizuri. Lakini hapa JF eti Kadogoo naye anawapa "company" jamaa kusikitika jinsi ambavyo wamebanwa mbavu na Mfumo Kristo hata shule hawana. Hiyo ni kuzingatia kuwa kwao Kadogoo wamezungukwa na wasio Waislamu!!!! Hata Kadogoo akatae, lakini presence ya Wakiristo wengi jirani na wao imewafanya wachacharike kielimu wakati "washikaji" wanalia na Mkapa majukwaani.
 
Back
Top Bottom