Vitabu vyote nilivyoagiza vimefika; ninacho vya John Iliffe (vyote vitatu); ninavyo na vingine. Ninapitia si kwa sababu sikuwa najua lakini nilitaka nisome kama alivyosoma Mohammed Said na kuona kama nafikia hitimisho lile lile. NInachokiona alichofanya Mohammed Said ni kupotosha historia ya harakati za Uhuru wa Tanganyika. Ameipotosha mno kiasi kwamba kweli inawezekana inabidi mtu aandike kusahihisha upotofu huo.
Muheshimiwa Mwanakijiji,
Nashukuru kwa kutujuza marejeo ya ile likizo yako fupi,na matokeo ya ufuatiliaji wa vile vitabu. Nikubalie fursa ya kukuuliza maswali kiduchu japo kwa uchechefu wangu.
Naona sasa unajaribu kukubaliana nami,kuwa pana umuhimu wa kutunga kitabu na kumjibu au kumkosoa kimaandishi Sheikh Mohammed Said.
Hapa jamvini tumeonyeshwa nakala ya mojawapo ya vitabu vyako. Nimeipenda ile picha ilomo kwenye jarida.
Muheshimiwa Mwanakijiji,nafikiri unakumbuka awali niliwahi kukuuliza kuhusu zile harakati zako za kuandika kitabu kuhusu Bwana Rostam Aziz.
Jibu lako lilikua fupi mno hasa ukizingatia maswali/swali nilokuuliza. Ulinijibu kwa mtindo wa kuniuliza swali mie muulizaji.
"Je huyo Rostam Aziz bado yumo madarakani? Na unafikiri hizo nyadhifa aliziacha kwa ridhaa yake mwenyewe?"
Kama sijakosea ulijibu/uliuliza hivyo ili kuashiria kuwa uwezo wako fulani wa uandishi /kimaandishi ulisaidia kumuondoa Muheshimiwa yule kwenye nyadhifa alokua nazo.
Ama kwa hakika,kwa yeyote mwenye fikra na maarifa ya ufuatiliaji wa mambo,basi atajua yakuwa tuhuma na shutuma zilizokuwa zinamkabili Rostam Aziz na zilizopo sasa dhidi ya Sheikh Mohammed Said juwezi linganisha hata chembe.
Nina maana tuhuma mnazompa Sheikh Mohammed Said kama ni kubwa pita kiasi (kama ni za kweli).
Hasa ukizingatia kuwa wewe binafsi umedai kuwa Sheikh Mohammed Said ni member wa Muslim Brotherhood,mchochezi,ana mipango ya kuleta Shariah Law hapo Tanzania,anahatarisha amani na usalama wa nchi na wananchi wake kwa kuchochea vurugu za kidini na mengineyo kadhaa.
Ama kwa hakika hizi ni tuhuma nzito pita kiasi.
Muheshimiwa Mwanakijiji,niliwahi kukuuliza kama haya mambo/tuhuma dhidi ya Sheikh Mohammed Said ni ya kweli; mbona Serikali na vyombo vyoote vya usalama katika awamu za marais tafauti hapo nchini zimekua kimya hawakuliona hilo?
Pia nilihoji na kumtupia lawama Bwana Nyerere kwa ukimya wake mpaka anafariki kwa kutofafanua ukweli wa suala hilo. Sababu shutuma hizi nzito mfano wake wa karibu ni kama kutaka kufanza uhaini hapo nchini. Ndo maana pia niliwahi kusema yakuwa Nyerere hakuwa kiongozi mwadilifu na mwenye mapenzi kwa nchi yake kama tunavyoambiwa na kukumbushwa kila kukicha. Na kama angekuwa basi kuna maswali kadhaa ambayo niliuliza kwako awali. Japo ulistaajabu kwanini nikulaumu wewe binafsi na Nyerere.
Nahisi utakubaliana na mimi kuwa kama ni kweli hizo shutuma ulotoa dhidi ya Sheikh Mohammed Said,kama wewe binafsi uliweza kuzifuatilia,kuziona na kuzijua kwa miaka mingi saana huko nyuma,basi lazim tukubali kuwa Nyerere nae pia alizijua tena labda kwa kina zaidi yako.
Narejea tena kwanini Nyerere hakumjibu Sheikh Mohammed Said au kumdharau tu, lakini angetoa ufafanuzi japo kiduchu kwa wananchi wake au labda "kumshughulikia" kama walivyoshughulikiwa watuhumiwa wengi tu hapo nchini tangia "enzi za Mwalimu" mpaka sasa? Mimi binafsi bado naamini kama Nyerere angelifanza hivyo basi kwa kiasi fulani ingetuepusha mno hapa tulipo leo na hili "janga" la Sheikh Mohammed Said, na pia angekua ameinusuru kwa kiasi kikubwa nchi yake na wanachi wake vipenzi.
Najua hapo awali kuna "manyangumi wa hoja",walipazwa saana na kustaajabu pasi kiasi ati kwanini Nyerere amjibu Sheikh Mohammed Said ambae ni "mtu mdogo mno" kwa kulimnganisha na Nyerere? "Hao jamaa" walitakiwa wafahamu yawezekana Sheikh Mohammed Said ni mtu dhalili mbele ya Bwana Nyerere,lakini kina cha lile swali langu ilikua tafauti na muangalio/mtazamo wao,na hasha sikuwa katika kulinganisha baina ya Nyerere na Sheikh Mohammed Said kwenye maana walohisi wao.
Bila ya kurejea mengi nilowahi kukuuliza kwenye bayana yangu ya awali.
Muheshimiwa Mwanakijiji,umedai mara kadhaa kuwa ulishaiona hii hatari ya kina Sheikh Mohammed Said,Prof. Njozi,Dr. Dau na WARSHA miaka mingi saana ilopita.
Sasa inakuwaje hukuweza/hukutaka kutumia umahiri wa kalamu yako,ambayo kwa hakika ni kali mno kama ulivyotujuza jinsi ilivyomnyofoa Bwana Rostam Aziz nyadhifa zake, na ungewashughulikia Sheikh Mohammed Said na wenzie? Hasa ukitilia maanani kama ulivyodai yakuwa,ulikua unawajua hatari na madhara yao kwa nchi na ulikua unawafuatilia kwa miaka mingi?
Nafikiri huyu Rostam Aziz allibuka miaka sio mingi sana kwenye ulingo wa siasa. Au alianza "vitimbi vyake" kabla ya Sheikh Mohammed Said,WARSHA na wenzie?
Muheshimiwa Mwanakijiji,hivi kweli leo hii ndo wewe unaanza kuuona huo umuhimu wa kumjibu kimaandishi Sheikh Mohammed Said ili kuepusha hilo "janga" kwa nchi yetu? Wakati ulidai kuwa ulikua unawafuatilia hawa watu/kikundi na kujua hatari zao takriban miaka thelathini ilopita ndugu yangu?
Huo muda woote ulotumia kwa ufanisi dhidi ya Rostam Aziz(kitu ambacho inanilazim nikupe pongezi za dhati) na kuandika hizo riwaya za mahaba,huoni kuwa uliupoteza badala ya kushughulika na lile "hatari/janga" dhidi ya nchi toka kwa Sheikh Mohammed Said na wenzie? Kama uliweza kushughulika na habari za Rostam Aziz ambae amekuja baadae na issue yake haiwezi kabisa kulinganisha na uzito wa "janga/shutuma" za kina Sheikh Mohammed Said,na pia umekua na muda pia na muda wa kutosha kuandika vitabu vyako binafsi vya riwaya. Sasa huoni kuwa hapa yawezekana ulitoa kipaumbele kushughulika na mambo mepesi kuliko yale yenye hatari dhidi ya nchi yako?
Kama uliweza ku-priortise habari za Rostam Aziz,ambazo nina hakika nazo zilihitaji ufuatiliaji wako wa kina na pia ulipata muda wa kutunga hadithi za mahaba,na kuliwacha suala la kina Sheikh Mohammed Said/WARSHA,sasa huoni hapa sisi wengine tunapata tafsiri tafauti,ya kuwa hiyo hatari na janga unaloona linasababishwa na Sheikh Mohammed Said ni hadithi tu za kufikirika toka kwako na kikundi chako kwa sababu mzijuazo nyinyi wenyewe? Au utakubaliana na mimi yakuwa, Sheikh Mohammed Said ni kinyume na ujumbe wa mada hii unavyomtuhumu,na labda pana khitilafu za kisomi/kiuandishi baina yenu na zaweza kumalizwa kitaaluma tu, kama ambavyo unavyohisi sasa hivi kuwa ipo haja ya Sheikh Mohammed Said kujibiwa kimaandishi?
Zile lawama zangu dhidi yako binafsi, kwenye ile bayana yangu ya awali naziacha palepale. Muheshimiwa Mwanakijiji nafikiri wewe ndie mtu pekee hapa ulodai kuwajua,kuwafuatilia kwa karibu na kugundua hatari yao kubwa dhidi ya Taifa hili takriban miaka thelathini ilopita(hawa kina Dr. Dau.Prof. Njozi,Sheikh Mohammed Said na WARSHA).
Muheshimiwa Mwanakijiji,hivi ndugu yangu wewe binafsi kwa mtazamo wako unakubaliana na mawazo ya baadhi ya wanajamvi hapa,watanzania kadhaa pamoja na Serikali hapo kuwa Waislam wana matatizo na dhiki kadhaa za kihistoria na inalazim Serikali iwatengee sikio japo la upande mmoja kujua kinachowasibu?
Sijui kama unakubaliana na ile kauli ya Bwana W. Mkapa ya kuthibitisha na kuwa wengi kati ya Waislam wana matatizo na dhiki zilizosababishwa na kurithiwa toka kwa wakoloni?
Unakubaliana na mimi kuwa Sheikh Mohammed Said alipoandika Historia ya Tanu/Tanganyika, hakuwa na madhumuni potofu au kukusudia uchochezi kama mnavyodai bali labda ni khitilafu kiduchu na dhahama tu za kitaaluma na kiuandishi na pia hakukusudia nia dhalili dhidi ya nchi yake na wananchi wenzie.
Nashukuru, na niwie radhi kama kuna masuala nimekuuliza tena. Najaribu kuangalia kama mpaka hapa mnakasha ulipofikia labda kuna majambo umeyaona na umepata kubadili fikra zako japo kiduchu.
Ahsanta.