Hakika ni NGANO tena ngano ya nera!
Jipumzishe na hiyooo!!!
CRAIG KELLY AMPA UJUMBE POWELL.
Huko mjini Lima, Peru, asubuhi hiyo, waziri wa mambo ya Nje Colin L. Powell alikuwa ndiyo kwanza ameanza kupata kifungua kinywa na rais mpya Alejandro Toledo. Powell alikuwa anahudhuria mkutano wa nchi za umoja wa Nchi za Amerika. .Alikuwa na mategemeo ya mawasiliano mema na mawaziri wa nchi za nje au viongozi 34 wa nchi 35 za eneo hilo.Cuba ilikuwa haikukaribishwa, Toledo alikuwa anasisitiza kuhusu mgao wa soko wa nguo kutoka Marekani . Alitaka kuondolewa kwa kodi katika pamba ya hadhi ya juu ambayo alidai isingeweza kushindanishwa na pamba ya hadhi ya chini iliyokuwa inazalishwa katika mataifa ya kusini ya Marekani ambayo ilikuwa inataka pawepo mgao huo katika soko.
Ghafla mlango ukafunguliwa na Craig Kelly, msaidizi mtendaji wa Powell, aliingia haraka akiwa na ujumbe uliokuwa umeandikwa katika kipande cha karatasi kilichokuwa kimechanwa kutoka katika kitabu cha kumbukumbu .Ndege mbili zimejibamiza katika kituo cha Biashara cha kimataifa. Ndege mbili, si tukio la ajali, Powell alitambua .ujumbe wa pili ulisema kwamba ndege hizo zilikuwa ni za injini ya "jet" .Powell akafikiri, nilazima niende nyumbani. Hata kama kimetokea nini, hali ilikuwa ni mbaya mno kwake kuendelea kukaa katika mkutano wa mawaziri wa mamboya nje mjini Peru. "Hebu tayarisha ndege, alimwambia Kelly, Nenda kawaambie tunasubiri". Ingechukua kiasi cha saa moja kuitayarisha ndege, hivyo Powell aliueleza mkutano huo.
Mawaziri wengine walitoa hotuba za kumpa pole. Powell alizungumza kwa ufupi, akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa pole zao na kuahidi kwamba Marekani inachukua hatua mara moja "Mkasa mkubwa sana umeikumba nchi yangu," alisema "Lakini….lazima mfahamu kwamba Amerika itapambana na wakosaji watafikishwa mbele ya haki. Mfahamu kwamba pamoja na siku hii kuwa mbaya kwetu, nilazima tutashinda kwani sisi ni taifa lenye nguvu na linalo jiamini duniani' Wajumbe wengine walisimama nakupiga makofi. Mara tu baada ya ndege kuondoka Powell alifahamu kwamba asingezungumza na mtu yeyote kwavile vyombo vyake vya mawasiliano vilikuwa vimeunganishwa na mfumo wa mawasiliano nchini Marekani ambao ulikuwa umejaa habari mbalimbali za ma wasiliano.
Bila yasimu au barua pepe, alikuwa ni sawa na mtu ambaye hakuwa na nchi. Baada ya dakika kadhaa alikwenda mbele ya ndege kupiga mawasiliano ya radio. Hiyo ilimaanisha mawasiliano hayo hayakuwa na usalama. Alimpata Richard L Armitage, naibu waziri wa mambo ya nje na rafiki yake mkubwa, walizungumza mara kadha, lakini mazungumzo ya maana hayakuwezekana. Armitage ambaye alihitimu chuo cha jeshi la maji mwaka 1967 alikuwa ametumikia jeshi mara nne nchini Vietnam na baadaye akawa Naibu waziri wa ulinzi katika utawala wa Reagan. Alikuwa ni mtu mwenye kupenda kusema ukweli mwenye tambo kubwa na kifua kipana ambaye hakupenda kuzungumzia diplomasia yenye kujificha.
Hata kabla hawajawa wakuu wa wizara ya mambo ya nje Powell na Armitage walikuwa wakizungumza mara kadhaa kila siku. "Mtu huyu ninamwamini kuhusu uhai wangu, watoto wangu, hadhi yangu, kila kitu ambacho ninacho," alikuwa akisema Powell kuhusiana na Armitage. Katika mambo yote ambayo Powell alikuwa anayachukia, ni kushindwa kuchukua hatua yoyote wakati wa tatizo ndilo jambo lililokuwa linashika nafasi ya kwanza. Jambo kuu katika upangaji wa sera za usalama wa taifa, na timu ya Ikulu au ya usalama wa taifa ingetaka kuweka msimamo gani katika upangaji wa sera kulikuwa kuna utaratibu wa kipekee katika nyakati za matukio makubwa. Hali ya migogoro ndiyo ilitoa fursa ya kuwepo hatari kubwa zaidi na fursa kubwa zaidi za utendaji wa kazi. Ni mmarekani wa kwanza mweusi kuweka historia ya kuhudumu katika ngazi za juu za utawala wa Marekani.
Akiwa na umri wa miaka 64 katika kipindi cha mgogoro Powell alikuwa tayari amekaa katika viti vitatu vya chumba cha dharura vya Ikulu ambavyo ni mshauri wa kitaifa kwa Rais Regan kwa muda wa mwaka mmoja, kisha akawa mwenyekiti wa Muungano wa Wanadhimu kwa Rais Bush wa kwanza wakati wa vita vya Ghuba, na wakati mgogoro alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje kwa rais George W. Bush. Ripoti nyingine ilifuata ikisema kwamba makao makuu ya jeshi yalikuwa yameshambuliwa, na kulikuwa na ripoti na uvumi usioaminika kwamba kulikuwa na ndege nyingine zikiruka kila mahali.
Powell alianza kuandika notisi kwa ajili ya matumizi yake, aliandika hivi, "Watu wangu watakuwa na majukumu gani"? Je, ulimwengu na Marekani zitajibu vipi tukio hili? Je, hali itakuwa vipi kwa Umoja wa Mataifa? Je, Umoja wa kujihami wa NATO? Je, nitaanzaje kuwaita watu mbali mbali wakusanyike? Masaa saba kutowasiliana na mtu yeyote yalionekana kama miaka isiyohesabika kwa mtu huyo ambaye angekuwa mkuu wa majeshi. Mnamo 1995, miaka miwili Powell akiwa amestaafu kutoka jeshini, alikuwa amefikiria kugombea urais. Aliandika kitabu cha simulizi ya maisha yake kiitwacho My America Journey (Safari yangu ya Amerika) ambacho kilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika idara ya mauzo.
Alikuwa amejichimbia katika siasa za Marekani akiwa katika kiwango cha makadirio ya juu kiumaarufu ambacho uteuzi wa chama cha Repblican ulikuwa ni wa kutaka aseme tu, na urais alikuwa karibu sana kuufikia. Armitage alikuwa amekipinga kitu hicho kwa nguvu "hapana haja. "Achana nacho" alimshauri rafiki yake huyo, "sidhani kama uko tayari kwa kitu kama hicho". Shughuli ya kuendesha kampeni ni jambo ambalo Powell alikuwa halipendi, "inajumuisha kila kitu kibaya unachoweza kukifikiria." Powell alikuwa anapenda mipango iliyotayarishwa vyema utaratibu mwema wenye kuweza kutabirika, na kiwango cha uhakika jambo ambalo halikuwa ni sehemu ya siasa za haraka haraka za Marekani.
Ilikuwa inafahamika wazi kwamba mkewe, Alma, alikuwa hapendi jaribio hilo kugombea nafasi hizo. Kilichokuwa siri ni kwamba Alma alikuwa amemwambia wazi kwamba iwapo angegombea urais angemwacha. "Ukigombea tu naondoka", alisema. Alma alikuwa anaogopa kwamba (mumewe) angeshambuliwa au kupingwa risasi. Mumewe kugombea urais, "akishinda" na yeye kuwa mke wa rais ni mambo ambayomwanamke huyo alikuwa hayataki maishani mwake."Itabidi uyafanye mambo hayo peke yako," alisema. Baada ya Bush kushinda uteuzi wa kugombea urais wa chama cha Repblican mwaka 2000, Powell alisaini makubaliano ya kutoa msaada, lakini Karl Rove aligundua kwamba kampeni hiyo ilikuwa ifanye juu chini kumwezesha aonekane katika tukio lolote sambamba na Bush. Karibu wafuasi wote muhimu wa Repblican walikubaliana kwamba chaguo la kugombea urais siyo Powell.
Watu wake walitaka kufahamu ni nani mwingine ambaye angekuwepo kwenye tukio muhimu la chama hicho, kitu gani kingesemwa, nani wangehudhuria, na lengo la kisiasa lilikuwa nini. Yote haya yalikuwa yamepangwa kuelekeza mgawanyiko dhidi ya Powell na si Bush. Isitoshe ni nyenzo za kumweka Bush katika siasa za mlengo wa kati na baadaye akawa ndiye chaguo kuu la kuwa waziri wa mambo ya nje iwapo Bush angechaguliwa kuwa rais. Katika sura ya nchi zaidi kulikuwa na hisia kubwa kuwa walifahamu kuwa walikuwa wanachagua timu si Bush na makamu mgombea mwenza wake, Waziri wa ulinzi wa zamani Dick Cheney, pia Powell. Wakati mahakama kuu ilipomtangaza Bush kuwa mshindi kwa kura 537 katika mkanganyiko wa uchaguzi huko Florida washauri wa Powell walikuwa na imani kwamba bosi wao alikuwa amesaidia kwa kiwango kikubwa sana katika ushindi huo.
Katika miezi yake ya kwanza akiwa waziri wa mambo ya nje Powell alikuwa hajaliziba pengo la uhusiano wake na Bush ambalo halikuwafanya wawe karibu zaidi kama alivyokuwa na uhusiano wa karibu na watu wengine. Kulikuwa na pengo kati ya watu hao wenye kuunganishwa na maelewano ya kirafiki. Bush na Powell walikuwa wanataniana wakiwa na watu wengine lakini walifanya hivyo mara chache sana wakiwa wawili. Rove alihisi kwamba Powell alikuwa anajidukiza mno kisiasa na kuendesha shughuli zake nje ya cheo chake. "Lazima ufahamu siku zote kwamba vyote hivi ni siasa na mimi ndiye nitaushinda mchezo huu wa kisiasa," Rove alimwambia kwa faragha Powell. Kila mara Powell alipokuwa katika mandhari ya mbele kuhusiana na suala fulani na kuonekana kuwa ndiyo sura ya utawala, shughuli za kisiasa na mawasiliano huko Ikulu zilihakikisha zina mweka pembeni mwa mandhari na mwanga wa kisiasa.
Rove na Karen P. Hughes mkurugenzi wa muda mrefu wa mawasiliano wa Bush ambaye wakati huo alikuwa ni mshauri Ikulu waliamua nani miongoni mwa viongozi angetokea katika kipindi cha mazungumzo cha jumapili kipindi maarufu cha televisheni kuhusu habari za jioni na asubuhi. Iwapo Ikuluisingetoa taarifa kupendekeza kwamba akubali mwaliko wa kutokea kwenyekipindi hicho Powell alikuwa anafahamu utaratibu mzima. Aliwaambiawatayarishaji wa kipindi hicho. Mnamo Aprili 2001 wakati ndege moja ya ujasusi wa kijeshi ya Marekani aina ya EP-3E ilipokingamwa na ndege za kivita katika pwani ya China, ikalazimishwa na serikali ya China kutua na kukamatwa mateka wote 24 waliokuwa katika ndege hiyo. Ikulu ilikuwa imedhamiria kuona kwamba Bush hajihusishi na suala hilo ili rais huyo asionekane kuwa mzungumzaji katika mgogoro huo.
Ilikuwa ni kama vile hapakuwepo na mgogoro wa mateka, hii ilikuwa ni kwa kutia maanani jinsi mgogoro wa mateka huko Iran ulivyomdhoofisha Rais Carter na jinsi mgogoro wa mateka huko Lebanon ulivyokuja kumwathiri Rais Reagan katikati ya miaka ya 1980. Suala hilo lilipelekwa kwa Powell ambaye alifanikisha kuachiliwa kwa mateka hao baada ya siku 11. Ulikuwa ni ushindi mkubwa lakini hata hivyo, Ikulu haikutaka atokee kwenye televisheni kupata sifa alizostahili. Powell na Armitage walikuwa wanataniana na kusema kwamba Powell alikuwa amewekwa katika kisanduku cha barafu au kwenye friji ambapo alikuwa anatumiwa tu wakati akitakiwa. Muda mfupi kabla ya mashambulizi ya September 11, jarida la times lilikuwa limeandika habari moja kuu kuhusiana na Powell ikiwa na kichwa cha habari "Umekwenda wapi Colin Powell"? Habari hiyo ilisema kwamba alikuwa akiacha nyoyo zikiwa kwenye kina kirefu kuhusiana na sera mbali mbali na kuonekana kuwa amemezwa na watu wenye msimamo mkali katika utawala uliokuwa madarakani.
Habari hiyo ilitoa changamoto kubwa kwa Ikulu ambako maofisa kadhaa walikuwa wamewashikilia waandishi kuthibitisha kwamba Powell alikuwa akifanya kazi kama kawaida wakati mwingine akiwa amekata tama.mara nyingi akifanya kazi kwa upweke akiwa amejikita pembeni na utawala huo mpya. Rove akiwa miongoni mwa maofisa hao alikuwa akisema chini chini kwamba alikuwa anahisi Powell alikuwa ameteleza sehemu fulani na kwamba ilikuwa si kawaida kumwona akiwa katika hali isiyoonyesha furaha akiwa na Rais.
Kutoka katika kitabu kiitwacho "
Vita Dhidi ya Ugaidi"
Na Yericko Nyerere